The Radar Scandal: Investigation & Progress

huyu jamaa sikutegemea kwani tuulize sisi wafanyakazi wa TANESCo jinsi tunavyotesaka,Kafukuza watu kwa vikesi vya kijinga yaani kaweka record ya kufukuza watu TANESCO.sasa kumbe naye Mungu alikuwa anamuandalia upeo KUBENEA.Jamaa anatisha sana kwa kujifanya msafi,maskini yaliwakuta wafanyaazi wa TANESCO walofukzwa ni wengi sana kwa vikesi vya kijinga
 

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Hosea katika hili hakutoa siri, bali utaratibu wa wenzetu hata huko kwao ni kuwajulisha wahusika kwamba wanataka kuwapekua na kuwahoji na mwenyeji wa wageni hao toka SFO ni ofisi ya Hosea (si Hosea binafsi) ambayo ililazimika kufanya mawasiliano na Chenge na Dk. Rashid. Chenge wakati huo alikuwa katika ziara ya Rais lakini aliarifiwa na rais alijulishwa na wote (Chenge na JK) wakaridhia kuendelea kwa uchunguzi huo. Sasa kusema Hosea alitoa siri, sijui ni siri gani. Hose tuendelee kumuuliza ama kumtaka ajisahihishe kuhusu suala la Richmond na kwa ukimya huu wa serikali, ina maana alipata baraka zote za juu katika kutoa taarifa ile ya Richmond, na ndio maana hata JK atajiona mkosefu kama atamtimua Hosea kwa kosa la Richmond, ambalo kwa nafasi ya PCB (si PCCB) walikua hawana meno kama ilivyo sasa PCCB. Makosa yametoka nadhani matano (PCB Act) hadi 24 (PCCCB Act), na hivyo sasa tutaipima taasisi hiyo na sheria mpya
 
N wananchi kuwakumbatia mafisadi

Nakubali kuwa hata wananchi wanamchango wao katika hili. lakini usisahau kuwa political parties are the driving forces behind politics. Nchi yetu haina watu wenye mwamko. Namaanisha kuwa wananchi wengi ni "apolitica" na vyama vya siasa havijafanya kazi ya kutosha kuwafahamisha maovu wanayotendewa na CCM na wao kuja na sera mbadala ambazo zinaeleweka. If you ask me, bado tuko katika mfumo wa chama kimoja "defacto" kwani vyama vya upinzani bado ni vichanga. Hope umeelewa argument yangu.
 
Huyu bwana kwa historia yake, asingepewa u-CEO pale TANESCO.

Connection yake na kufilisika kwa benki ya Meridian Biao ilikuwa tosha kabisa kumweka mbali na utumishi wa umma.
 
WanaJF naomba munisaidie swali hili: Hivi ule mradi mpya wa umeme wa Watsila unaozalisha Mega Watt 100 pale Ubungo unamilikiwa na nani vile??!!
 

Hawa wahalifu ni lini watapelekwa kortini? Haya ndio majambazi yanayokwiba mchana kweupe...
 


Unashangaza mkuu kwa hayo maneno yako niliyoyawekea rangi nyekundu. Kama huoni kosa la pccb kwenye kashifa ya richmond basi hilo ni tatizo lako binafsi la kushindwa kukonect the dotts. Kosa la pccb ni kusema uongo juu ya mchakato mzima wa jinsi richmond ilivyojipatia ushindi wa tenda ya kufua umeme wa mega watt 100, pamoja na uhalali na uwezo wa kiufundi wa kampuni hiyo!
 
Nchi yetu imekwisha, mimi ni muda mrefu sasa nimekuwa nikiamini, tatizo la Tanzania ni hawa wenzetu walioko kwenye vyeo vya kati serikalini na kwenye mashirika.

Vita ni kubwa kuliko tunavyodhani, labda aje kiongozi mwingine ambaye ataweza kuwang'oa wote.

Mkuu Halisi, toka lini mtuhumiwa anaambiwa kuna watu wanakuja kukupekua? Kama Hoasea na JK walitoa siri, ina maana na wao ni wahusika kwenye kuihujumu nchi yetu.

Labda ifike siku mtu atwangwe risasi, ndio hawa jamaa watakoma kutuibia.

Inasikitisha sana wakurugenzi wanaolipwa mishahara ya zaidi ya 20M kwa mwezi bado wanaingia kwenye wizi wa kijinga hivyo. 20M kwa Tanzania unaweza kuanzisha biashara yoyote na baadaye ukawa bilionea kwa biashara halali kabisa, kwanini uingie kwenye wizi? Shame on them, inabidi na yeye aende na maji.
 


Tana wameshindwa hata kwenda 'kubalance' stori kwa mtuhumiwa. Si haki na ni kinyume na maadili ya uandishi
 

Mtanzania,

Ninakubaliana na wewe kabisa. Yaani hao watu kwenye vyeo hawana hata sifa moja ya kuwa viongozi. Hawana uwezo ki akili, hawana huruma, hawana lolote.

Na cha kushangaza bado wako madarakani.
 
Fisadi, fisadi, fisadi,
Wa Tz Sasa tuseme hapana kwa hawa mafisadi. kwani wana nini? Elimu? nani asiyekuwa na hiyo elimu? tunataka uadilifu na kujali wanyonge sio u-Dk wala U-Professor. Wangefisadi vihiyo tungesema hawana elimu sasa mafisadi wakubwa ni ma-Dk na Maprofessor.

Hicho chama kinachowakingia kifua, kipigwe chini. Hao wanaobweka kuwa chama kilichopo ni safi 'tuwapime kwa mizani yetu na ufahamu wetu' je ni kwa nini wanatetea uozo?

Hahahah Siku zao zinahesabika
 

Wamekalia Vyombo vya dola, halafu wanaongoza mabwege. Ila wasio lijua ni kwamba vyombo vya kisasa vitawaumbua tu, muda wao umefika.

Kukipiga chini hicho chama inahitajika plan mkuu. Kumbuka aliposhindwa Mrema aliposema kukibomoa kirejareja? That's what we need. Kila mtu atangaze yuko tayari kuanza mapambano akimshirikisha kila aliye karibu nae. Ili ikifika 2010 watu wengi wawe na mwamko na waondekane na ubwege. 2010 si mbali.
 
Tana wameshindwa hata kwenda 'kubalance' stori kwa mtuhumiwa. Si haki na ni kinyume na maadili ya uandishi


Give me a break!
Mtuhumiwa yupi, FISADI Idris? Kwanini useme "si haki na ni kinyume na maadili ya uandishi". Mahakama ingemhukumu bila kusikiliza hadithi yake ningekuelewa.



.
 
Yupo mmoja tu! Johnson Mwanyika........ aliwapa challenge waandishi wa habari na wameshindwa kumpata na dosari.

This says more about the press in Tanzania than Mr. Mwanyika's integrity.

Kumbuka,

Man is conceived in sin and born in corruption and he passeth from the stink of the didie to the stench of the shroud -- Willie Stark in All the King's Men

Tangu lini tuna waandishi wa habari Tanzania? Waandishi wenyewe ndiyo hawa wanaoiharibu habari nzuri kwa kushindwa hata kuweka sentensi moja kuwa "tulipojaribu kupata maelezo kutoka kwa Dr. Rashid alikataa kusema chochote". Mpita Njia I am with you, hata kama the details are intact Kubenea alitakiwa kumtafuta mtuhumiwa, this is a cardinal rule of not only journalism, but also all principles founded in fairness.
 
This says more about the press in Tanzania than Mr. Mwanyika's integrity.

Kumbuka,



Tangu lini tuna waandishi wa habari Tanzania?

Kuhani....no wait, he an investigator....freelance investigator that is....
 
Swahiba wa Kikwete ahusishwa na rada
Dk. Rashidi aliteuliwa na Rais Kikwete Novemba 2006 kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mwaka mmoja baadaye, Dk. Rashid aliandika barua ya kujiuzulu lakini rais alimkatalia kujiuzulu

Ukitaka kuwa karibu na kisura basi ujue kuzitafuta kifisadi au ujue kulinda mafisadi. Matatizo yote na longo longo zote zinamlenga mkuu wa kaya. Kweli tumempata Raisi (cheap)
 
Ingawa mchakato wa ununuzi wa rada ulianza mwaka 1992, kufuatana na rekodi za SFO, mkataba ulikamilika mwaka 1999. Wakati huo Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Hey,wakuu JF zingatieni muda haswa dhambi ya ununuzi wa radar ilipoanzia,kama sikosei ni mwaka ule ambao MZEE WA RUKSA akiwa mbioni kuachia ngazi.Si jambo la busara hata punje kumsakama Mr.Clean,JMK na wenzake bila kumjadili na huyu mzee,ametusababishia matatizo mengi sana hapa Tz hadi leo hii ni vigumu kuyapatia ufumbuzi.

Au vipi?
 

Mzee Ruksa aliitema issue ya Radar baada ya Mwalimu kumkalia pabaya, na kwa kuwa hakupata support ya UK. Hiyo issue iliibuka tena wakati wa Mr. Clean (read Chenge as AG) kimya kimya na kuikamilisha baada ya Mwalimu kutututoka.
 

Unaposema uchanga ni uchanga wa nini, wa KUIBA PESA ZA WANANCHI?. Tanganyika wakati inapata uhuru mwaka 1961 chama gani kilikuwa kimekomaa kuongoza?. Hizi ni Lugha za kutetea Ulaji wa Kifisadi, Tanzania ya Leo si ya mwaka 1961, Kuna watu wanamipango mizuri na mawazo mbadala ya kuendeleza nchi. Hakuna Chama chenye nyota Tano za kuongoza nchi na kingine moja. Vyote ni vyama vya siasa vyenye lengo la kuchukua uongozi wa nchi. Kwa taarifa yako UPINZANI kuna watu makini na pengine kupita hata wale wa CCM ambao wengi wao ni MABUBU kwa kuogopa kupoteza ulaji.
 
...Tz tumekwisha hivi tutapona na hii kasi ya mafisadi??? Kwa kweli this is too much. Lakini haya mambo kuwa kila siku watu wanaibuliwa kwa tuhuma za ufisadi then mambo yanaishia hewani ndio inawapa kiburi ukizingatia hata huto tujisenti twao wanaendelea kujipoza tu!!!!!!Kazi ipo wandugu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…