- Wakuu ahsanteni sana kwa hii response, Tanzania tumetokewa na nini hasa? I mean tumefikaje hapa jamani ambapo hakuna wa kumuamini? Mimi sasa nimefikia mahali mtu akitaka kunikopa na ni rafiki yangu wa karibu, kama anataka 100, nitampa 50 na kumuomba asinirudishie ili tuendelee na urafiki wetu maana nikimdai tutavunja urafiki.
- Kweli kiongozi mkubwa wa taifa anatafuta risiti za uongo ili akadai hela za wananchi, na huku akijua wazi kuwa anachokifanya ni uizi? Unajua tumefikia mahali huu sasa nationally ya kutafuta risiti yamekubalika kuwa ni tabia ya kawaida tu kwa sisi wafanyakazi wa serikali yetu, wakubwa kwa wadogo bila hata ya aibu kidogo!
- Hatuwezi kuaminiana tena, hatuwezi hata kujali time maana tutatafuta sababu za hapa na pale na kudai tulikuwa na shughuli zilizotufanya tuchelewe kumbe ni uongo uongo usio na mfano. Ninakumbuka nilipokuwa nchi moja majuu, ilikuwa mbongo ukitaka kununua tiketi ya ndege, mhindi mmoja alikuwa na tiketi za cheap kwa hiyo wabongo wengi tulikuwa tunajimwaga huko, sasa hata yule Mhindi alishatushitukia I mean mbongo anapiga simu kuwa anaondoka Jumapili kumbe hata hela hana anategemea kupata Ijumaa jioni, atamzungusha Mhindi mpaka mwisho ataanza kujizungusha mwenyewe, matokeo safari hakuna analaumu Mhindi kumbe ni uongo tu umemzidi!
- Unajua ninashukuru sana kwa wale wote mliolichukulia hili suala on a serious note, wakuu sisi tunao-deal na wabongo kila siku kwa kweli hamjui how bad this thing are, sasa ninajiuliza kama sisi wenyewe kwa wenyewe ni hivi mazishi mazishi hawa viongozi wetu itakuwaje na wako kwenye nafasi na wanaziona hela ziko nje nje?
Wakuuu solution nini hasa na hili tatizo na sisi wabongo? Tumefikaje hapa? Hili taifa letu litakombolewa na nani hasa jamani kama sisi wenyewe ndio hivi hivi? Something ni lazima kifanyike jamani ama sivyo tutacheza mzunguko mpaka mwisho wa dunia ndugu zangu! Unajua yanakatisha tamaa sana huko uongozi wa juu, maana tulisema wakiingia wapya na hasa vijana mambo yatabadilika, kumbe sasa ndio worse kuliko zamani, ni nini hasa sisi na hiii special Tanzania's character?
Ahsante Wakuu!