LordJustice1
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 2,263
- 533
Jamani ni mimi nina usingizi au, I see nothing new kwenye taarifa hizi, labda kuandijwa kwa Kiswahili tuu!.
Hizi taarifa zitaendelea kuwa mpya hadi tutakapomwona "Mzee wa Vijisenti" kizimbani!
Jamani ni mimi nina usingizi au, I see nothing new kwenye taarifa hizi, labda kuandijwa kwa Kiswahili tuu!.
Chenge ni mwanasheria na ali exploit hilo, watu walikuwa hawajui nguvu ya DPP?Yule hana haja ya kutoa sababu akifuta kesi.Na Chenge kwa kutumia uelewa wake, karata yake aliyopewa kwenye mtandao ya ku call a shot baada ya ushindi wa JK ili kupigiana mapande ya fadhila, aliitumia kupachika mtu wake sehemu nyeti, ndo bongo hiyo.Brother Mwanakijiji, usiumize kichwa bure! FELESHI KAMWE HAWEZI KUMSHITAKI CHENGE, ANALIPA FADHILA! Hata akilazimishwa yuko tayari kujiuzulu alimradi mzee wake hasimamishwi kizimbani!
Eliezer Feleshi amevunja rekodi kuwa DPP wa kwanza, si Tanzania tu bali Afrika ya Mashariki, kushika wadhifa huo mkubwa akiwa na umri mdogo chini ya miaka 40 na akiwa na uzoefu mdogo katika uongozi na katika taaluma ya sheria. Uteuzi wake uliacha vinywa wazi miongoni mwa wanasheria wote nchini maana Feleshi hana sifa ya pekee kuweza kuwaruka mawakili waandamizi lukuki walio katika wizara ya sheria. Aliyewezesha yote haya kufanyika si mwingine ni Andrew Chenge. Alijua alichokuwa anafanya: alikuwa anawekeza kwa kijana mdogo, Msukuma mwenzake na ndugu yake kiukoo akijua kuwa siku moja atasimama kidete kulipa fadhila kwake! Sasa yanaonekana: faili la Chenge litazungushwa wee mpaka Waswahili msahau kuhusu majambo ya mzee wa vijisenti.
Ndiyo maana nasema, Mzee Mwanakijiji achana na hoja nzito unazotaka kuingiza kwenye suala hili: hapa hakuna jurisprudence ni WIZI MTUPU!!!
Ndugu yangu nashangaa hata wabunge wanazungumza kwa jaziba kama kweli wako serious lakini mbona hakuna wa kuleta mswada bungeni wa kuomba fedha zetu zilizo kwapuliwa zirudishwe????Ndugu utaumia bure na uchungu wa nchi hii watu walishachoka maendeleo ya jumla(nchi) wanaangalia binafsi zaidi. Na kwa hao mafisadi wanaitwa WAJANJA WACHACHE kama vile mwizi ni mjanja badala ya kuwaita wajinga na majizi. Inauma sana tena sana ndugu zangu wazalendo.