The Radar Scam: Chenge & Rashid...

The Radar Scam: Chenge & Rashid...

Jamani nilisisitiza kuwa SFO wamefanya uchunguzi kwa sababu kwa sheria ya Uingereza, kamisheni hairuhusiwi kuzidi 10%. Mkosaji wao mkuu ni BAE kwa nini alifanya biashara na TZ na kulipa kamisheni kubwa zaidi ya asilimia 10%.

Sheria za Tanzania hazijaweka ukomo wa kamisheni. Hivyo Vithlani bado hana hatia kutoza kamisheni ya asilimia 40% na hata mashitaka aliyofunguliwa sio wizi bali kutosema ukweli kwa PCCB.

Waingereza ndio wanamshupalia Chenge. Mimi naamini UWT wanajua kila kitu. Kuna uwezekano mkubwa mgawo ulifika mpaka kwa Mkulu wa Magogoni ndio maana serikali yetu sio haifanyi lolote, bali haitafanya lolote zaidi ya kumwacha Mzee wa Vijisenti astaafu ubunge mwakani na kuachwa akajipumzikie kwa amani na kujilia vijisenti vyake kwa taratibu kama anavyolindwa Mzee wa Kiwira.

Kwa mujibu wa tuhuma zote 9 za SFO, hakuna yenye criminal liabilty kwa viwango vya serikali yetu, not at least for now.

IBARA MOJAWAPO KATIKA uKURASA WA NANE WA BARUA YA SFO UNASEMA HIVI " It appears tha in breach of Tanzanian law. the Public Leadership Code of Ethics Act 1995 ("Ethics Act") Chenge has not disclosed asets held in Jersey on the appropriate register. Under the Ethics Act as Attorney General fell within the category of persons obliged to disclose his worldwide assets annually, on a public register. The SFO has been informed by the PCCB that Chenge has failed to declare any assets on the relevant register.

Wakuu wangu kama mwaka 2008, PCCB iliaiarifu SFO kuwa Chenge kavunja maadili ya uongozi kwa mujibu wa sheria za Tanzania, sasa ni PCCB ipi tena inayomsafisha Chenge huyo huyo?

Hivi ni kweli kwamba hakuna makosa yoyote ya jinai mtumishi wa ngazi ya juu ya serikali kukutikana na fedha nyingi kiasi hicho? Je fedha hizo zimelipiwa kodi kweli? Je kukwepa kodi sio kosa la jinai?.

Mimi nafikiri wakati wa kulalamika umekwisha/ watanzania wnye uchungu tuchukue hatua mara moja, ikikumbukwa na uchungu wa kuibiwa kura zetu ni lazima tufanye kitu ili mafisadi hawa wajue sio rahisi kuwaharishia watanzania uharo kama wapendavyo baada ya kutuibia fedha, raslimali na kura.

Wadau toeni mawazo tufanye nini ili kutuma ujumbe kwa mafisadi?
 
SFO watoa tuhuma tisa dhidi ya Chenge

2009-02-09 10:07:58
Na Mwandishi Wetu

Makachero wa Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) wa Uingereza waliokuwa wanachunguza tuhuma za mlungula uliotolewa kwa aliyekuwa Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Andrew Chenge, ili kuruhusu ununuzi wa rada ya bei mbaya, wamejenga tuhuma kuu tisa ambazo zinaweza kumfikisha mwanasiasa huyo kizimbani.

Tuhuma hizo zimo kwenye ripoti ya SFO ambayo vyombo vya kisheria vya serikali ya Tanzania vilikabidhiwa tangu Machi mwaka jana, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Chenge na mshirika wake wa karibu katika sakata hili, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk Idriss Rashidi.

Tuhuma ambazo zimetajwa na SFO dhidi ya watuhumiwa hao wawili, wakiwa ni miongoni mwa watuhumiwa 10 wanaochunguzwa katika kashfa ya rada iliyoigharimu Tanzania Dola za Marekani milioni 40, ni kwamba Chenge na Dk Rashidi walikuwa ni watu muhimu katika kufikiwa kwa mkataba wa ununuzi wa rada hiyo iliyouzwa kwa serikali na shirika la kuuza vifaa vya kijeshi la Uingereza, BAE System.

Mbili, Chenge anatajwa kuwa karibu na wakala wa kampuni ya Siemens Plessey System (SPS) iliyokuwa ikisukuma mpango huo, Sailesh Vithlani na kwamba ukaribu wao ulijitokeza wazi wakati wa kumalizia makubaliano ya mkataba wa ununuzi wa rada hiyo.

Tatu, SFO wanadai kwamba uhusiano wa karibu kati ya Chenge na Vithlani ulikuja katika kipindi ambacho wakala huyo, (Vithlani) anadaiwa kuwaeleza wafanyakazi wa SPS kuwa alikuwa na makubaliano ya zamani na mapya, makubaliano hayo katika mawasiliano yao yalimaanisha rushwa.

Nne, makachero hao wanamtuhumu Chenge kuwa alifanya maamnuzi mengi ya kisheria ambayo yalionekana wazi kwa jinsi mkataba wa malipo ulivyofikiwa katika ununuzi wa rada hiyo.

Tano, SFO pia wanatuhumu kwamba maamuzi hayo kwa vyovyote vile yanaonyesha kwamba hayakuzingatia maslahi ya Tanzania katika ununuzi wa rada hiyo.

Kwa maana hiyo kulikuwa na kitu kilichomfanya Chenge asiweke maslahi ya taifa mbele katika kutoa maoni hayo ya kisheria ambayo yalichukuliwa katika kufikia maamuzi ya mkataba wa kununua rada.

Sita, makachero hao wanaunganisha matukio hayo hapo juu na mmiminiko wa ghafla wa fedha kwenye akaunti ya Chenge kisiwani Jersey zikitokea Frankfurt.

Saba, Chenge anatuhumiwa na makachero hao kwamba ili kuficha kujulikana kwa fedha hizo, alianzisha kampuni ya Franton ambayo inamiliki akaunti hiyo, lakini pia akaibua anwani mjini London ambayo ilitumika kwa mawasiliano, kuficha kuonekana kwake moja kwa moja katika miliki ya fedha hizo.

Nane, SFO wanamtuhumu Chenge kwamba kutokana na ujanjaujanja wa kuficha vyanzo vya fedha hizo, benki hiyo iliamua kuvunja mahusiano naye kama mteja kwa kuwa hakuwa tayari kutoa maelezo ya kina juu ya fedha hizo.

Tisa, makachero wanatuhumu kwamba malipo ya Dola za Marekani 600,000 kwa Rashidi yanaonyesha kwamba hakuwa mpokeaji pekee wa rushwa kutoka kwa BAE System, ila ni mtu muhimu katika kuisambaza kwa kuwa watuhumiwa hao wawili (Chenge na Rashidi) walikuwa watu muhimu katika ununuzi wa rada hiyo.

Tuhuma hizi dhidi ya Chenge zinajulikana kwa vyombo vya kisheria vya nchi, lakini hadi sasa hakuna hata chombo kimoja cha kiserikali kimefungua kinywa kueleza hatma ya uchunguzi wa mwanasiasa huyo.

Chenge mara kadhaa amekanusha kuchukua rushwa ya rada, na alisema fedha alizojiwekea benki kisiwani Jersey ni vijisenti, lakini mara mbili ametoa kauli za kutatanisha juu ya vyanzo wa Dola za Marekani milioni 1.5 katika akaunti yake akieleza ni malipo yake halali kwa kazi za uanasheria lakini mara nyingine akasema ni urithi na akiba ya familia.

Katika fedha hizo alidai mkewe anamiliki asilimia 25.

SFO wamekuwa wanachunguza sakata la rada kwa miaka mitatu sasa, na kuna kila dalili imekuwa ikipewa ushirikiano na serikali tofauti na Kenya ambako walitangaza wiki iliyopita kufunga uchunguzi wa wizi wa Aglo Leaseing kutokana na kutokuwapo kwa dalili za kufungua mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo.

Hadi sasa ni Vithlani pekee amefunguliwa mashitaka rasmi mahakamani kutokana na kashfa ya rada, lakini wakati mashitaka hayo yanawasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mshitakiwa hakuwapo na tangu wakati huo anasakwa kuja kujibu mashitaka yake.

SOURCE: Nipashe

Pumbafu!!!!!!!!!!!!!! hiyo kampuni ndio Chenge aliwaambia waandishi wa habari ni NGO ya watoto yatima? anataka kutugeuza watanzania wote ni wajinga sio?
 
Shiling katika mshahara wa Waziri wa Utumishi Hawa Gasia Haikutoka, Lakini Tatizo la serikali la kutomshitaki Chenge na Dokta Idris Rashid Ambao kwa mjibu wa barua ya mkuu wa Serious Fraud Office ( SFO ) iliyotumwa kwa mwansheria mkuu wa serikali ya Tanzania katka Ununuzi wa Rada.Je watanzania wametendewa haki kweli?.
 
Always chini ya utawala wa CCM watz wasitegemee kutendewa haki kabisa. Kwani hivi sasa kunaushahidi mwingi tu wa wazi jinsi watz wanavyohujumiwa na sirikali ya chama tawala; kama kuuza wanyama, kuiba madini, na mauaji ya wananchi yanayofanywa na vyombo vya dola vya chama tawala.
 
Hapa mbaya sio Chenge ni CCM na serikali yake. Inaonyesha kati ya vigogo wote kila mtu ana mradi wake. Benno Ndulu naye atakwapua pesa nyingi halafu atatulia
 
Juni 21, 2002 Waziri wetu wa Fedha wa wakati ule, Basil Pesambili Mramba, katika kauli iliyoonekana kutowakilisha maslahi ya Taifa, alitamka Bungeni maneno yafuatayo ambayo itawachukua Watanzania muda mrefu kuyasahau: "Tunakataa kuambiwa mambo yakufanya hata kama sisi ni masikini … Wanawezaje kuwa na ujasiri wa kutuambia kwamba rada hiyo ni aghali sana kwetu?... Tuko tayari kula majani, na kama wanataka, waache kutupa misaada yao".

Kuonyesha kwamba hoja za wananchi hazikuwa na uzito kwake, Mramba, kwa wakati tofauti, alisema: "Baadhi ya watu wanaokota okota maneno baa na kuyafanya wimbo rada … rada … rada kwa kujisumbua; hawajui kwamba Serikali ya Uingereza imekwishatoa leseni ya kuiuzia Tanzania rada; na kinachotokea Uingerza sasa ni mgogoro ndani ya Serikali ya huko ambayo wanataka kuuleta katika Serikali ya Tanzania".
 
Taifa letu lina Taasisi kedekede na sheria zinazoweza kushughulikia karibia kila jambo hapa nchini bila haja ya kuundwa kwa kamati za ziada au kuundwa sheria nyingine kuweza kushughulikia matukio makubwa ya kifisadi yaliyotukumba na yanayoendelea kulikumba Taifa letu. Tatizo viongozi wa taasisi hizi muhimu ni mafisadi wao wenyewe au facilitator wa huo ufisadi. Sijui tutasema mangapi kwenye Taifa hili "lililopiga kambi kwenye bonde la kashfa?" Inasikitisha sana kuona DPP akikaa kimya au "kubutua mpira" kwenda pahala pengine na kupoteza muda, alimradi tu anawalinda anaofahamiana nao!! Analipwa pesa kibao kwa kodi zetu, analindwa na kupatiwa haki zote kama kiongozi muhimu, lakini uzalendo kwa Taifa na mali yake ni ZERO!! 🙁
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Siri zafichuka ufisadi wa rada
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 01 December 2011 20:47 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

dk-hoseah-top.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Dk Edward Hoseah

SERIKALI YADAIWA KUZUIA UCHUNGUZI WA VIGOGO
Mwandishi Wetu
KASHFA nyingine imeikumba Serikali ya Tanzania, kufuatia tuhuma kwamba ina mkakati maalumu kuzuia watuhumiwa wa ufisadi wa rada kufikishwa mahakamani.Taarifa za mtandao wa Wikileaks ambao umekuwa ukifichua siri za kidiplomasia na ufisadi duniani, umeibua tuhuma hizo mpya kwa Serikali na kwamba hicho ndicho kikwazo cha watuhumiwa husika kutofikishwa mahakamani.Taarifa ya mtandao huo uliyosambazwa jana imeeleza kuwa mpango huo, ndio ulioathiri jitihada za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Clare Shot kuzuia Tanzania kuuziwa rada hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao huo, juhudi za Shot zilijumuisha kuinyima Tanzania misaada inayofikia Paundi 35 Milioni kutokana na kununua rada hiyo kwa bei ya kuruka.

"Pamoja na shinikizo hilo, juhudi za Shot zilishindwa kabisa kuzuia ununuzi wa rada hiyo ambayo thamani yake ilikuwa Paundi 28 Milioni kutoka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza," ulisema mtandao huo na kuendelea:

"Suala hilio si jipya. Gazeti la The Guardian la Uingereza liliwahi kutoa ripoti yake ya uchunguzi wake kuhusu uuzwaji wa rada hiyo ambao ulimsababishia pia Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Tony Blair kuamuru kikosi chake cha kuchunguza makosa makubwa (SFO) kuingilia kati na kuchunguza namna BAE ilivyohusika."

Ilichobaini Wikileaks ni kwamba viongozi wa Serikali ya Tanzania ilikuwa ikifanya juhudi za kuficha kasoro zote zilizokuwa katika mpango wa ununuzi wa rada hiyo.

Hata kwa upande wake, mtu mahususi aliyetakiwa kushughulikia kashfa hiyo kwa kufanya uchunguzi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Dk Edward Hoseah alinukuliwa akimweleza Afisa wa Ubalozi wa Marekani nchini kwamba aliwahi kutishiwa kuuawa mara kadhaa na kukumbushwa kwa ujumbe wa maneno kila siku.

Mara kadhaa, kutokana na kashfa hiyo ya rushwa, Serikali ya Uingereza na ya Tanzania ziliingia katika mvutano.

BAE Systems ni kampuni kubwa ya uuzaji wa vifaa vya ulinzi ambayo iwapo ingefungiwa kufanya biashara yake kungekuwa na athari kubwa kwa Uingereza.

Suala la uchunguzi wa aina yoyote ambao ungemweka matatani Rais wa zamani, Benjamin Mkapa na washirika wake wa karibu (kwa mujibu wa Wikileaks) lilikuwa ni gumu kuweza kufanyika.

Ulisema baada ya kumalizika kwa kipindi cha ukimya bila kushughulikiwa kwa kashfa hiyo, suala la kutafuta ufumbuzi lilionekana kuwa muhimu kwa nchi zote mbili, lakini kasoro kubwa ni pale kila aliyehusika katika kashfa hiyo ya BAE nchini Uingereza na Tanzania kukwepa kuchunguzwa.

Hata hivyo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Tonny Blair alifanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba SFO wanafanya uchunguzi na kama ikiwezekana BAE ifungiwe kufanya kazi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Kwa upande wake, Tanzania ilikuwa ikilaumiwa kwa kufanya juhudi za kutetea ununuzi huo na hata kumtisha Mkurugenzi wa Takukuru kumtaka aachane na suala hilo.

Dk Hosseah
Jana Dk Hosea hakupatikana kuzungumzia taarifa hiyo, lakini akizungumzia tuhuma za kufichua siri ya Rais Kikwete kupitia mtandao huo Desemba 20 mwaka jana, alikiri kupata vitisho vinavyohatarisha maisha yake kutokana na mapambano yake dhidi ya rushwa.

Dk Hoseah alisema hayo alipotakiwa kuzungumzia madai ya mtandao huo wa Wikileaks kuhusu kauli yake na Afisa wa Ubalozi wa Marekani kwamba kiongozi huyo wa nchi, asingependa vigogo Serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Mtandao huo pia ulidai kuwa mkuu huyo wa Takukuru ameshindwa kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika na kashfa ya rada kwa sababu anahofia usalama wake.

Mbali na hofu hiyo, mtandao huo ulieleza kuwa Dk Hoseah alipewa maelekezo maalumu na Rais Kikwete kutoshughulikia kesi za rushwa zinazowahusu vigogo katika Serikali yake na hasa marais waliomtangulia.

The Guardian lilitoa taarifa hiyo likiunukuu mtandao wa habari wa WikiLeaks uliojizolea umaarufu duniani kwa kutoa habari za kiuchunguzi hasa baada ya mwasisi wake, Julian Paul Assange, kutiwa matatani
Akijibu hoja hizo mwaka jana, Dk Hoseah alisema ni kawaida kwake kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kila mwaka na kujadiliana nao mambo mengi kuhusu Tanzania, lakini hakumbuki kuzungumza naye mambo hayo.

Alisema mabalozi ni wadau wakubwa katika bajeti ya Tanzania na hivyo huwa wanakutana kila mwaka kujadili mambo mbalimbali ya kuhusu kusaidia bajeti ya Serikali.

“Mimi huwa nakutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kwa sababu wao ni wadau katika mradi wa ‘government budget support’ (Mpango wa kusaidia bajeti ya Serikali), hivyo hilo sio tatizo,” alisema Dk Hoseah.

“Msimamo wangu ni kwamba mapambao dhidi ya ufisadi ni endelevu hadi hapo tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili,” alisema Dk Hosea na kukiri:

“Vitisho vipo vingi tu, kutoka kwa watu wanaotuhumiwa, lakini si hata ninyi waandishi mnamwagiwa ‘tindikali’ katika mapambano yenu, hivyo hivyo hata mimi napata vitisho.”

Alisisitiza kuwa pamoja na vitisho hivyo, hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya rushwa na ufisadi.

“I’m a Tanzanian, I will die in Tanzania, it is my country’ (mimi ni Mtanzania, nitakufa Tanzania, ni nchi yangu), siwezi kuhama nchi kwa vitisho vya watu wachache wanaotuhumiwa kwa ufisadi na rushwa,” alisisitiza Dk Hoseah.

“Hilo la kwamba nafikiria kuhama nchi wametia chumvi si unajua magazeti? Sijafikiria kuhama nchi licha ya vitisho, mimi naona ni changamoto na jambo la kawaida katika mapambano,” aliongeza Dk Hoseah.

Kuhusu Rais Kikwete kukwamisha mapambano ya ufisadi kama alivyonukuliwa na gazeti hilo la The Guardian, Dk Hoseah alipiga chenga kulijibu badala yake akaeleza:

“Ili umpeleke mtu mahakamani si lazima umtuhumu na kumfanyia uchunguzi? Lakini pia lazima tujenge utamaduni wa kuwaheshimu viongozi wetu.”

Siku hiyo, Takukuru ilituma taarifa iliyoeleza kuwa Dk Hoseah alishangazwa na Ofisa wa Ubalozi wa Marekani kumnukuu vibaya huku akisema hajui ana lengo gani.

Katika taarifa hiyo, Dk Hoseah alikiri kukutana na ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani ofisini kwake Julai mwaka 2007, lakini akasema ripoti ya mazungumzo yao aliyoipeleka nchini kwake imechakachuliwa.

“Kwa mfano haikutokea katika mazungumzo yetu kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete hakutaka kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake, kuwashitaki vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama ilivyodaiwa na Ubalozi wa Marekani,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na idara ya mahusiano ya Takukuru.

“Nilichosema ni kwamba Rais hayuko tayari kuruhusu kushitakiwa kwa vigogo wa Serikali au mtu mwengine yeyote kwa tuhuma za uvumi au kwa ushahidi dhaifu, kwa sababu kufanya hivyo, Serikali itakuwa hatarini kwa kulipa gharama kubwa ya fidia ikiwa mtuhumiwa huyo atashinda kesi mahakamani,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza.

Kuhusu hofu ya maisha yangu, nakumbuka niliulizwa na Ubalozi wa Marekani kwamba je, naogopea maisha yangu au la, nikiwa Mkuu wa Takukuru? Na jibu langu lilikuwa rahisi kwamba ‘bila ya shaka’ unapopambana na wakubwa na matajiri kama hao wanaotuhumiwa unapaswa kuwa makini na maisha yako.

Lakini hata siku moja sikusema kwamba napanga kuhama nchi kwa sababu maisha yangu yapo hatarini. Ni mshangao kuona kwa mara nyengine ofisa wa Ubalozi wa Marekani ananinukuu mimi vibaya au nje ya mada na sielewi kabisa lengo lao lilikuwa nini.”

Alsema rekodi yake, akiwa Mkuu wa Takukuru iko wazi kabisa wakati wowote anapokuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa yeyote wa ufisadi hawaogopi lolote isipokuwa ni kumburuza mahakamani bila ya kujali cheo chake.

Bunge la Uingereza
Taarifa ya mtandao huo imekuja siku moja tangu Bunge la Uingereza liitake Serikali ya Tanzania kuwafikisha mahakamani watu wote walioshiriki mchakato wa ununuzi wa rada na kuingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.

Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo lilisema lingependa kuona watu wote walioshiriki kwenye mchakato wa ununuzi wa rada hiyo, wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa juzi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), ilieleza kuwa wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali, watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.

Wito huo wa wabunge wa Uingereza umekuja wakati tayari Kampuni ya BAE System, iliyoiuzia Tanzania rada hiyo, ikikubali kuwa kulikuwa na kasoro katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo na hivyo kuirudishia Tanzania Dola za Marekani 46 milioni kama fidia. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Jamani ni mimi nina usingizi au, I see nothing new kwenye taarifa hizi, labda kuandijwa kwa Kiswahili tuu!.
 
Walishasema hili jambo limeshamalizwa, wakasahau wakaja na madai uchunguzi unaendelea, kwa uroho wakasahau yote wakaenda London kudai chenchi
Natamani nipate uwezo wa kuwatia kibiriti hawa wapuuzi wanaoitwa viongozi wa ccm
 
hii na ile ya Jairo ni moja ya matendo ya serikali, tofauti ni moja Jairo aliwatukana wabunge kwa kiburi ama la angekuwa anakula bata mpaka sasa
 
So WIKI LEAKS is back on front pages?

typical blast from the past...
 
dk-hoseah-top.jpg

Ya Jairo yametelekezwa ambayo ni moto uliolipuka bungeni, sasa haya ya Nzee Nkapa nachelea kusema ndo maana unaona Nkapa anavyomkingia Kikwete kifua kwa nguvu zote kwa vile yu kivuli kwake asivuliwe nguo hadharani.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Njemba imeshaona kwamba Kikwete hajamgusa kwa miaka zaidi ya sita sasa pamoja na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wake mbali mbali alioufanya akiwa madarakani na inajua fika kama akifagilia kuondolewa kwa msanii Kikwete kama Mwenyekiti wa Magamba basi Mwenyekiti mpya anaweza kuamua kumuanika na hivyo Mkapa kuadhirika zaidi katika umma wa Watanzania, hivyo ndio maana anampigia debe la nguvu abaki kama Mwenyekiti wa Magamba. Waswahili walisema, zimwi likujualo....... Mkapa ameamua kuweka mbele maslahi yake badala ya yale ya nchi na chama chao cha magamba.
 
Viongozi legelege wanaunda serikali legelege, Ni vema watanzania tukasimama imara kupambana na mafisadi hawa.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Siri zafichuka ufisadi wa rada
[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 01 December 2011 20:47
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
dk-hoseah-top.jpg Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Dk Edward Hoseah

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

SERIKALI YADAIWA KUZUIA UCHUNGUZI WA VIGOGO
Mwandishi Wetu
KASHFA nyingine imeikumba Serikali ya Tanzania, kufuatia tuhuma kwamba ina mkakati maalumu kuzuia watuhumiwa wa ufisadi wa rada kufikishwa mahakamani.Taarifa za mtandao wa Wikileaks ambao umekuwa ukifichua siri za kidiplomasia na ufisadi duniani, umeibua tuhuma hizo mpya kwa Serikali na kwamba hicho ndicho kikwazo cha watuhumiwa husika kutofikishwa mahakamani.Taarifa ya mtandao huo uliyosambazwa jana imeeleza kuwa mpango huo, ndio ulioathiri jitihada za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Clare Shot kuzuia Tanzania kuuziwa rada hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao huo, juhudi za Shot zilijumuisha kuinyima Tanzania misaada inayofikia Paundi 35 Milioni kutokana na kununua rada hiyo kwa bei ya kuruka.

"Pamoja na shinikizo hilo, juhudi za Shot zilishindwa kabisa kuzuia ununuzi wa rada hiyo ambayo thamani yake ilikuwa Paundi 28 Milioni kutoka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza," ulisema mtandao huo na kuendelea:

"Suala hilio si jipya. Gazeti la The Guardian la Uingereza liliwahi kutoa ripoti yake ya uchunguzi wake kuhusu uuzwaji wa rada hiyo ambao ulimsababishia pia Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Tony Blair kuamuru kikosi chake cha kuchunguza makosa makubwa (SFO) kuingilia kati na kuchunguza namna BAE ilivyohusika."

Ilichobaini Wikileaks ni kwamba viongozi wa Serikali ya Tanzania ilikuwa ikifanya juhudi za kuficha kasoro zote zilizokuwa katika mpango wa ununuzi wa rada hiyo.

Hata kwa upande wake, mtu mahususi aliyetakiwa kushughulikia kashfa hiyo kwa kufanya uchunguzi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Dk Edward Hoseah alinukuliwa akimweleza Afisa wa Ubalozi wa Marekani nchini kwamba aliwahi kutishiwa kuuawa mara kadhaa na kukumbushwa kwa ujumbe wa maneno kila siku.

Mara kadhaa, kutokana na kashfa hiyo ya rushwa, Serikali ya Uingereza na ya Tanzania ziliingia katika mvutano.

BAE Systems ni kampuni kubwa ya uuzaji wa vifaa vya ulinzi ambayo iwapo ingefungiwa kufanya biashara yake kungekuwa na athari kubwa kwa Uingereza.

Suala la uchunguzi wa aina yoyote ambao ungemweka matatani Rais wa zamani, Benjamin Mkapa na washirika wake wa karibu (kwa mujibu wa Wikileaks) lilikuwa ni gumu kuweza kufanyika.

Ulisema baada ya kumalizika kwa kipindi cha ukimya bila kushughulikiwa kwa kashfa hiyo, suala la kutafuta ufumbuzi lilionekana kuwa muhimu kwa nchi zote mbili, lakini kasoro kubwa ni pale kila aliyehusika katika kashfa hiyo ya BAE nchini Uingereza na Tanzania kukwepa kuchunguzwa.

Hata hivyo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Tonny Blair alifanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba SFO wanafanya uchunguzi na kama ikiwezekana BAE ifungiwe kufanya kazi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Kwa upande wake, Tanzania ilikuwa ikilaumiwa kwa kufanya juhudi za kutetea ununuzi huo na hata kumtisha Mkurugenzi wa Takukuru kumtaka aachane na suala hilo.

Dk Hosseah
Jana Dk Hosea hakupatikana kuzungumzia taarifa hiyo, lakini akizungumzia tuhuma za kufichua siri ya Rais Kikwete kupitia mtandao huo Desemba 20 mwaka jana, alikiri kupata vitisho vinavyohatarisha maisha yake kutokana na mapambano yake dhidi ya rushwa.

Dk Hoseah alisema hayo alipotakiwa kuzungumzia madai ya mtandao huo wa Wikileaks kuhusu kauli yake na Afisa wa Ubalozi wa Marekani kwamba kiongozi huyo wa nchi, asingependa vigogo Serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Mtandao huo pia ulidai kuwa mkuu huyo wa Takukuru ameshindwa kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika na kashfa ya rada kwa sababu anahofia usalama wake.

Mbali na hofu hiyo, mtandao huo ulieleza kuwa Dk Hoseah alipewa maelekezo maalumu na Rais Kikwete kutoshughulikia kesi za rushwa zinazowahusu vigogo katika Serikali yake na hasa marais waliomtangulia.

The Guardian lilitoa taarifa hiyo likiunukuu mtandao wa habari wa WikiLeaks uliojizolea umaarufu duniani kwa kutoa habari za kiuchunguzi hasa baada ya mwasisi wake, Julian Paul Assange, kutiwa matatani
Akijibu hoja hizo mwaka jana, Dk Hoseah alisema ni kawaida kwake kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kila mwaka na kujadiliana nao mambo mengi kuhusu Tanzania, lakini hakumbuki kuzungumza naye mambo hayo.

Alisema mabalozi ni wadau wakubwa katika bajeti ya Tanzania na hivyo huwa wanakutana kila mwaka kujadili mambo mbalimbali ya kuhusu kusaidia bajeti ya Serikali.

“Mimi huwa nakutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kwa sababu wao ni wadau katika mradi wa ‘government budget support’ (Mpango wa kusaidia bajeti ya Serikali), hivyo hilo sio tatizo,” alisema Dk Hoseah.

“Msimamo wangu ni kwamba mapambao dhidi ya ufisadi ni endelevu hadi hapo tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili,” alisema Dk Hosea na kukiri:

“Vitisho vipo vingi tu, kutoka kwa watu wanaotuhumiwa, lakini si hata ninyi waandishi mnamwagiwa ‘tindikali’ katika mapambano yenu, hivyo hivyo hata mimi napata vitisho.”

Alisisitiza kuwa pamoja na vitisho hivyo, hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya rushwa na ufisadi.

“I’m a Tanzanian, I will die in Tanzania, it is my country’ (mimi ni Mtanzania, nitakufa Tanzania, ni nchi yangu), siwezi kuhama nchi kwa vitisho vya watu wachache wanaotuhumiwa kwa ufisadi na rushwa,” alisisitiza Dk Hoseah.

“Hilo la kwamba nafikiria kuhama nchi wametia chumvi si unajua magazeti? Sijafikiria kuhama nchi licha ya vitisho, mimi naona ni changamoto na jambo la kawaida katika mapambano,” aliongeza Dk Hoseah.

Kuhusu Rais Kikwete kukwamisha mapambano ya ufisadi kama alivyonukuliwa na gazeti hilo la The Guardian, Dk Hoseah alipiga chenga kulijibu badala yake akaeleza:

“Ili umpeleke mtu mahakamani si lazima umtuhumu na kumfanyia uchunguzi? Lakini pia lazima tujenge utamaduni wa kuwaheshimu viongozi wetu.”

Siku hiyo, Takukuru ilituma taarifa iliyoeleza kuwa Dk Hoseah alishangazwa na Ofisa wa Ubalozi wa Marekani kumnukuu vibaya huku akisema hajui ana lengo gani.

Katika taarifa hiyo, Dk Hoseah alikiri kukutana na ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani ofisini kwake Julai mwaka 2007, lakini akasema ripoti ya mazungumzo yao aliyoipeleka nchini kwake imechakachuliwa.

“Kwa mfano haikutokea katika mazungumzo yetu kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete hakutaka kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake, kuwashitaki vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama ilivyodaiwa na Ubalozi wa Marekani,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na idara ya mahusiano ya Takukuru.

“Nilichosema ni kwamba Rais hayuko tayari kuruhusu kushitakiwa kwa vigogo wa Serikali au mtu mwengine yeyote kwa tuhuma za uvumi au kwa ushahidi dhaifu, kwa sababu kufanya hivyo, Serikali itakuwa hatarini kwa kulipa gharama kubwa ya fidia ikiwa mtuhumiwa huyo atashinda kesi mahakamani,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza.

Kuhusu hofu ya maisha yangu, nakumbuka niliulizwa na Ubalozi wa Marekani kwamba je, naogopea maisha yangu au la, nikiwa Mkuu wa Takukuru? Na jibu langu lilikuwa rahisi kwamba ‘bila ya shaka’ unapopambana na wakubwa na matajiri kama hao wanaotuhumiwa unapaswa kuwa makini na maisha yako.

Lakini hata siku moja sikusema kwamba napanga kuhama nchi kwa sababu maisha yangu yapo hatarini. Ni mshangao kuona kwa mara nyengine ofisa wa Ubalozi wa Marekani ananinukuu mimi vibaya au nje ya mada na sielewi kabisa lengo lao lilikuwa nini.”

Alsema rekodi yake, akiwa Mkuu wa Takukuru iko wazi kabisa wakati wowote anapokuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa yeyote wa ufisadi hawaogopi lolote isipokuwa ni kumburuza mahakamani bila ya kujali cheo chake.

Bunge la Uingereza
Taarifa ya mtandao huo imekuja siku moja tangu Bunge la Uingereza liitake Serikali ya Tanzania kuwafikisha mahakamani watu wote walioshiriki mchakato wa ununuzi wa rada na kuingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.

Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo lilisema lingependa kuona watu wote walioshiriki kwenye mchakato wa ununuzi wa rada hiyo, wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa juzi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), ilieleza kuwa wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali, watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.

Wito huo wa wabunge wa Uingereza umekuja wakati tayari Kampuni ya BAE System, iliyoiuzia Tanzania rada hiyo, ikikubali kuwa kulikuwa na kasoro katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo na hivyo kuirudishia Tanzania Dola za Marekani 46 milioni kama fidia.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Chanzo: Siri zafichuka ufisadi wa rada
 
Dr Hossea na Dr Kikwete wanapaswa kunyoosha maelezo katika hili. Hivi bado tunaendelea kuamini katika kusamehe "7 mara 70?"
 
Back
Top Bottom