The Radar Scam: Chenge & Rashid...

Radar deal`s top 10

2009-02-08 11:28:27
By Staff Writer

After nearly three years of investigation, the UK`s Serious Fraud Office has implicated at least 10 top officials in Tanzania and Britain in the trumped up radar deal that cost the country $40m, The Guardian on Sunday can reveal.

The SFO has evidence that the officials were involved in the key negotiation stages that led Tanzania to purchase the military radar at an inflated price.

The top ten include former Attorney General Andrew Chenge, Sailesh Pragji Vithlani, Tanil Kumar Chandulal Somaiya, and Dr Idriss Rashidi.

Other players from the UK are Michael Peter Rouse, Sir Richard Harry Evans, Michael John Turner, Julia Adgridge and two senior officials from the British Aero Space Engineering (BAE System), the arms dealer that manufactured the radar.

It is believed that there are still more names from the previous regime that were part of the team that pocketed $12m in kickbacks from the deal.

According to reliable sources inside the SFO, the kickbacks were paid to Tanzania`s top officials in advance to move the negotiation process along smoothly.

Chenge`s role
The UK investigators believe the former Minister for Infrastructure Chenge was just `a conduit` through which the radar billions were distributed to selected top government officials whose decisions were crucial to the deal.

The SFO established that Chenge received $1.5m (2.1bn/-) from the deal through a slush fund he set up in the UK island of Jersey.

According to a draft report written by the UK`s Serious Fraud Office and seen by The Guardian on Sunday, Chenge received payments through six credit transfers between June 19, 1997, and April 17, 1998, while he was serving as Attorney General.

The billions were paid to account No.59662999 owned by Franton Investment Limited through Bank Code No 204505 of Barclays Bank Plc, according to the draft report, a final version of which has reportedly already been sent to the Director of Public Prosecutions.

The SFO has established that Chenge owns Franton Investment, a registered company that appears to have been established primarily to enable the transfer of the dirty money.

According to information provided by the Jersey Authority, the $1.5m was transferred from a Frankfurt branch of Barclays Bank to Chenge`s account at a Jersey branch.

But aside from the money Chenge pocketed himself, he also used the Franton account to dish out the money to others involved in the radar deal.

For example, the SFO established that on September 20, 1999, Chenge personally authorised the transfer of $1.2m from the Franton account to Royal Bank of Scotland International in Jersey.

In May 1998, Chenge also authorised the transfer of $600,000 to an account owned and operated by Langley Investments Ltd. The account was officially operated by former Central Bank Governor Dr Idrissa Rashidi.

Rashidi is currently the managing director of the troubled Tanzania Electric Supply Company Ltd (Tanesco).

The SFO report concluded that both Rashidi and Chenge were key figures in the corrupt radar deal, but they were acting with the full support of top officials from the third phase regime.

Hiding the facts
Details made available to The Guardian on Sunday show that Chenge, alarmed by the possibility of being detected, directed his financial advisors abroad not to use his Tanzania address for any correspondence concerning the offshore bank account.

``Instead Chenge asked his financial advisors to send all documentation to C/o 11 Sid Mouth Road, London this is the current address for JO Humbros used during their communication with Chenge,`` reads part of the SFO investigation report, compiled by lawyer Mathew Cowie.

The London address was the subject of a search operation conducted on March 26, last year.

Mr Fat from Tanzania
The SFO investigation established that, to avoid being caught, the facilitators of the radar deal gave Vithlani the codename `Mr Fat`, while any mention of bribing or corruption was replaced with the euphemism `commitments`.

``I had an extensive discussion with our friend and I have this morning had a meeting with the AG to go through outstanding contractual issues,`` reads part of the fax message from a Mr Simpkins confiscated by SFO investigators early last year.

``The fat man having, as I stipulated, now resolved all the issues, is keen to sign an addendum to his agreement and argues he has a lot of commitments to a lot of old and new players as the project has taken considerable period to effect.``

``In addition he has stated to achieve the above compromises, new promises have had to have been made,`` the fax reads.

Again in September 1997, Simpkins wrote a fax message to a BAE official using more code language. ``Also over the weekend our fat friend has been working to resolve the outstanding commercial issues,`` he wrote.

``This morning he informed me that all issues are now resolved as follows: They [the government] have accepted English Law with arbitration in London.``

Registered a front company in Panama
In what is believed to have been a tactic to obscure the deal`s corruption, Vithlani and his partners registered a front company in Panama called Envers Trading Co Ltd.

The company, according to SFO records, received $8m in kickbacks between 2000 and 2005.

The payments came from Red Diamond Trading Co Ltd a front company of BAE System until December 2005 when it was terminated at a settlement of $3.36m.

In 1999 BAE System, through Red Diamond, registered in the British Virgin Islands and entered into an agreement with Envers Trading Co.

The Panamanian company was identified as a consultant working in Tanzania, which acted for Siemens Plessey System (SPS) in 1992/93 when the government was considering purchasing the radar for $88m.

SPS was acquired by BAE System in 1995, according to available details.

UK investigators have established that Tanil Somaiya and Vithlani held a power of attorney over Envers for six years, until December 2006.

Somaiya had earlier told the SFO that he wasn`t involved directly in the radar deal, but that everything had been under the control of his partner, Vithlani.

SOURCE: Sunday Observer
 
SFO watoa tuhuma tisa dhidi ya Chenge

2009-02-09 10:07:58
Na Mwandishi Wetu


Makachero wa Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) wa Uingereza waliokuwa wanachunguza tuhuma za mlungula uliotolewa kwa aliyekuwa Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Andrew Chenge, ili kuruhusu ununuzi wa rada ya bei mbaya, wamejenga tuhuma kuu tisa ambazo zinaweza kumfikisha mwanasiasa huyo kizimbani.

Tuhuma hizo zimo kwenye ripoti ya SFO ambayo vyombo vya kisheria vya serikali ya Tanzania vilikabidhiwa tangu Machi mwaka jana, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Chenge na mshirika wake wa karibu katika sakata hili, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk Idriss Rashidi.

Tuhuma ambazo zimetajwa na SFO dhidi ya watuhumiwa hao wawili, wakiwa ni miongoni mwa watuhumiwa 10 wanaochunguzwa katika kashfa ya rada iliyoigharimu Tanzania Dola za Marekani milioni 40, ni kwamba Chenge na Dk Rashidi walikuwa ni watu muhimu katika kufikiwa kwa mkataba wa ununuzi wa rada hiyo iliyouzwa kwa serikali na shirika la kuuza vifaa vya kijeshi la Uingereza, BAE System.

Mbili, Chenge anatajwa kuwa karibu na wakala wa kampuni ya Siemens Plessey System (SPS) iliyokuwa ikisukuma mpango huo, Sailesh Vithlani na kwamba ukaribu wao ulijitokeza wazi wakati wa kumalizia makubaliano ya mkataba wa ununuzi wa rada hiyo.

Tatu, SFO wanadai kwamba uhusiano wa karibu kati ya Chenge na Vithlani ulikuja katika kipindi ambacho wakala huyo, (Vithlani) anadaiwa kuwaeleza wafanyakazi wa SPS kuwa alikuwa na makubaliano ya zamani na mapya, makubaliano hayo katika mawasiliano yao yalimaanisha rushwa.

Nne, makachero hao wanamtuhumu Chenge kuwa alifanya maamnuzi mengi ya kisheria ambayo yalionekana wazi kwa jinsi mkataba wa malipo ulivyofikiwa katika ununuzi wa rada hiyo.

Tano, SFO pia wanatuhumu kwamba maamuzi hayo kwa vyovyote vile yanaonyesha kwamba hayakuzingatia maslahi ya Tanzania katika ununuzi wa rada hiyo.

Kwa maana hiyo kulikuwa na kitu kilichomfanya Chenge asiweke maslahi ya taifa mbele katika kutoa maoni hayo ya kisheria ambayo yalichukuliwa katika kufikia maamuzi ya mkataba wa kununua rada.

Sita, makachero hao wanaunganisha matukio hayo hapo juu na mmiminiko wa ghafla wa fedha kwenye akaunti ya Chenge kisiwani Jersey zikitokea Frankfurt.

Saba, Chenge anatuhumiwa na makachero hao kwamba ili kuficha kujulikana kwa fedha hizo, alianzisha kampuni ya Franton ambayo inamiliki akaunti hiyo, lakini pia akaibua anwani mjini London ambayo ilitumika kwa mawasiliano, kuficha kuonekana kwake moja kwa moja katika miliki ya fedha hizo.

Nane, SFO wanamtuhumu Chenge kwamba kutokana na ujanjaujanja wa kuficha vyanzo vya fedha hizo, benki hiyo iliamua kuvunja mahusiano naye kama mteja kwa kuwa hakuwa tayari kutoa maelezo ya kina juu ya fedha hizo.

Tisa, makachero wanatuhumu kwamba malipo ya Dola za Marekani 600,000 kwa Rashidi yanaonyesha kwamba hakuwa mpokeaji pekee wa rushwa kutoka kwa BAE System, ila ni mtu muhimu katika kuisambaza kwa kuwa watuhumiwa hao wawili (Chenge na Rashidi) walikuwa watu muhimu katika ununuzi wa rada hiyo.

Tuhuma hizi dhidi ya Chenge zinajulikana kwa vyombo vya kisheria vya nchi, lakini hadi sasa hakuna hata chombo kimoja cha kiserikali kimefungua kinywa kueleza hatma ya uchunguzi wa mwanasiasa huyo.

Chenge mara kadhaa amekanusha kuchukua rushwa ya rada, na alisema fedha alizojiwekea benki kisiwani Jersey ni vijisenti, lakini mara mbili ametoa kauli za kutatanisha juu ya vyanzo wa Dola za Marekani milioni 1.5 katika akaunti yake akieleza ni malipo yake halali kwa kazi za uanasheria lakini mara nyingine akasema ni urithi na akiba ya familia.

Katika fedha hizo alidai mkewe anamiliki asilimia 25.

SFO wamekuwa wanachunguza sakata la rada kwa miaka mitatu sasa, na kuna kila dalili imekuwa ikipewa ushirikiano na serikali tofauti na Kenya ambako walitangaza wiki iliyopita kufunga uchunguzi wa wizi wa Aglo Leaseing kutokana na kutokuwapo kwa dalili za kufungua mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo.

Hadi sasa ni Vithlani pekee amefunguliwa mashitaka rasmi mahakamani kutokana na kashfa ya rada, lakini wakati mashitaka hayo yanawasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mshitakiwa hakuwapo na tangu wakati huo anasakwa kuja kujibu mashitaka yake.

SOURCE: Nipashe
 
Jamani nilisisitiza kuwa SFO wamefanya uchunguzi kwa sababu kwa sheria ya Uingereza, kamisheni hairuhusiwi kuzidi 10%. Mkosaji wao mkuu ni BAE kwa nini alifanya biashara na TZ na kulipa kamisheni kubwa zaidi ya asilimia 10%.

Sheria za Tanzania hazijaweka ukomo wa kamisheni. Hivyo Vithlani bado hana hatia kutoza kamisheni ya asilimia 40% na hata mashitaka aliyofunguliwa sio wizi bali kutosema ukweli kwa PCCB.

Waingereza ndio wanamshupalia Chenge. Mimi naamini UWT wanajua kila kitu. Kuna uwezekano mkubwa mgawo ulifika mpaka kwa Mkulu wa Magogoni ndio maana serikali yetu sio haifanyi lolote, bali haitafanya lolote zaidi ya kumwacha Mzee wa Vijisenti astaafu ubunge mwakani na kuachwa akajipumzikie kwa amani na kujilia vijisenti vyake kwa taratibu kama anavyolindwa Mzee wa Kiwira.

Kwa mujibu wa tuhuma zote 9 za SFO, hakuna yenye criminal liabilty kwa viwango vya serikali yetu, not at least for now.
 
DPP returns radar case file to PCCB
THIS DAY

THE Director of Public Prosecutions (DPP), Eliezer Feleshi, has opted to withhold his mandatory consent for the prosecution of suspects implicated in ongoing corruption investigations related to the $41m (approx. 52bn/-) military radar transaction scandal, it has been learnt.

Instead, the DPP has now instructed the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) to continue with its investigation into the circumstances surrounding the deal, and seek consent afresh after gathering sufficient evidence.

This development follows the Bureau’s move last year to seek the DPP’s permission to prosecute suspects already earmarked in the course of its investigation into the 2002 deal.


However, the DPP has yet to give the consent requested, directing the government’s anti-corruption watchdog to dig deeper.

In a written response to questions sent by THISDAY about the status of the long-running radar deal probe, the PCCB confirmed that the DPP has returned the case file to the investigators with instructions that more work be done on it.

Said PCCB: ’’We would like to inform you that the investigation file on these (radar corruption) allegations was sent to the Director of Public Prosecutions, who then returned the file to us for further investigations.’’

Under the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Act of 2007, the Bureau is required to get a written consent from the DPP before prosecuting graft cases.


The legislation empowers PCCB, ’’subject to the directions of the Director of Public Prosecutions, [to] prosecute offences under this Act and other offences involving corruption’’.

According to a newly-released report compiled by the Prime Minister’s Office (PMO) detailing the implementation of various Government pledges made in Parliament during 2007/08, the PCCB has already concluded its investigation into the radar transaction.

But it now appears that DPP Feleshi is not satisfied with the Bureau’s work on the case so far.

At least four prominent Tanzanian personalities have so far been named as the main targets of an ongoing international investigation into the scandal.

Those being probed by the UK’s Serious Fraud Office (SFO) include ex-attorney general Andrew Chenge, former Bank of Tanzania governor Dr Idris Rashidi, and prominent local businessmen Tanil Somaiya and Shailesh Vithlani.

The SFO investigation into the scandalous radar deal has been proceeding parallel to that of the home-based PCCB, but it has yet to be established if any or all of the four named individuals are also on the Bureau’s own radar of suspects.

Vithlani has already been formally charged by local authorities before a Dar es Salaam court, but only for allegedly committing perjury and lying to an investigating officer in connection to the radar deal.

With an international arrest warrant hanging over his head, he is reported to have long since skipped the country, and is presently hiding out in Switzerland.


Otherwise, no charges directly related to corruption in the radar deal have so far been brought by PCCB or any other agency against any suspect implicated in the scandal.
 
The current DPP is closely linked to one of the prime suspects in the radar scandal; no wonder he has been very reluctant to give a go ahead to the anti-corruption bureau to go ahead and prosecute Andrew chenge and Idris Rasshid inspite of the glaring evidence against the suspects gathered by the British SFO.

In the same manner the DPP is also dragging his feet to prosecute Richmond culprits Karamagi & co. inspite of all the incriminating evidence so far gathered. It is widely believed that the DPP'S independence is being eroded by his weakness in taking orders fron senior members of the executive branch, this type of conduct does not aurgur well with the conduct of good governance!!

Let justice be done and not seem to be done if at all we have to salvage this country from the MAFIA.
 
Hapa yanachezwa mazingaombwe tu kutaka kutuonnyesha Watanzania kwamba DPP na vingunge wa PCCB wanafanya kazi zao kumbe hakuna lolote lile bali ni usanii tu. Tayari kuna ushahidi wa kutosha kwamba Mzee wa Vijisenti aliwekewa zaidi ya shilingi bilioni kwenye bank account yake ya nje naye akaweka kwenye Bank account ambayo nayo iko nje $600,000 ya Idrissa Rashid ambaye ni Managing Director wa TANESCO. Huu ni ushahidi wa kutosha kabisa kuwaweka rumande hawa Wazee wa vijisenti na kuanza kuwahoji kuhusu hivyo vijisenti walivyowekewa kwenye bank accounts zao.

Tutachoendelea kukiona ni kutupiana mpira kati ya DPP na PCCB huku siku zinayoyoma na ikikaribia uchaguzi Chenge atakamatwa na kuwekwa rumande kwa siku chache na kufunguliwa mashtaka. Kesi itapigwa kalenda na baada ya uchaguzi wa 2010 tutaambiwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Chenge au Idrissa Rashid!! Ndiyo Bongo yetu hiyo itajengwa na wenye moyo na kuliwa na mafisadi.
 
sheria nyingine ni za kijinga kweli...(ninamaanisha neno hilo).

a. Kama PCCB ina wanasheria na wanasheria hao wanaamini kuwa wana ushahidi wa kutosha kushinda kesi mahakamani kwanini wasiweze kwenda mahakamani na kuona huko kesi itakavyokwenda. Kisheria ambacho wangetakiwa kufanya ni kutoa taarifa tu kwa DPP ya hatua wanayoenda kuichukua na kuweka muda kuwa endapo DPP hatopinga ndani ya siku 21 basi wao PCCM wataendelea.

b. Endapo DPP hatotaka kuendelea na kesi hiyo basi yeye mwenyewe asubiri kesi ifunguliwe mahakamani na baadaye atumie nulli prosequi kufuta hiyo kesi.

c. Kwa kuilazimisha PCCB kupata kibali toka kwa DPP tunachosema ni kuwa taasisi hiyo siyo huru kabisa kama inavyodhaniwa. PCCB, iwe na uwezo wa kufungua mashtaka yenyewe bila kibali cha DPP vinginevyo, DPP ndiye apewe kesi zote za PCCB kuziprosecute baada ya PCCB kukamilisha uchunguzi wao. Haya mambo ya kuzungusha faili moja utadhani mchezo wa hiki na hoko hayana tija wala mpango!
 
sheria nyingine ni za kijinga kweli...(ninamaanisha neno hilo).

a. Kama PCCB ina wanasheria na wanasheria hao wanaamini kuwa wana ushahidi wa kutosha kushinda kesi mahakamani kwanini wasiweze kwenda mahakamani na kuona huko kesi itakavyokwenda. Kisheria ambacho wangetakiwa kufanya ni kutoa taarifa tu kwa DPP ya hatua wanayoenda kuichukua na kuweka muda kuwa endapo DPP hatopinga ndani ya siku 21 basi wao PCCM wataendelea.

b. Endapo DPP hatotaka kuendelea na kesi hiyo basi yeye mwenyewe asubiri kesi ifunguliwe mahakamani na baadaye atumie nulli prosequi kufuta hiyo kesi.

c. Kwa kuilazimisha PCCB kupata kibali toka kwa DPP tunachosema ni kuwa taasisi hiyo siyo huru kabisa kama inavyodhaniwa. PCCB, iwe na uwezo wa kufungua mashtaka yenyewe bila kibali cha DPP vinginevyo, DPP ndiye apewe kesi zote za PCCB kuziprosecute baada ya PCCB kukamilisha uchunguzi wao. Haya mambo ya kuzungusha faili moja utadhani mchezo wa hiki na hoko hayana tija wala mpango!

Brother Mwanakijiji, usiumize kichwa bure! FELESHI KAMWE HAWEZI KUMSHITAKI CHENGE, ANALIPA FADHILA! Hata akilazimishwa yuko tayari kujiuzulu alimradi mzee wake hasimamishwi kizimbani!

Eliezer Feleshi amevunja rekodi kuwa DPP wa kwanza, si Tanzania tu bali Afrika ya Mashariki, kushika wadhifa huo mkubwa akiwa na umri mdogo chini ya miaka 40 na akiwa na uzoefu mdogo katika uongozi na katika taaluma ya sheria. Uteuzi wake uliacha vinywa wazi miongoni mwa wanasheria wote nchini maana Feleshi hana sifa ya pekee kuweza kuwaruka mawakili waandamizi lukuki walio katika wizara ya sheria. Aliyewezesha yote haya kufanyika si mwingine ni Andrew Chenge. Alijua alichokuwa anafanya: alikuwa anawekeza kwa kijana mdogo, Msukuma mwenzake na ndugu yake kiukoo akijua kuwa siku moja atasimama kidete kulipa fadhila kwake! Sasa yanaonekana: faili la Chenge litazungushwa wee mpaka Waswahili msahau kuhusu majambo ya mzee wa vijisenti.

Ndiyo maana nasema, Mzee Mwanakijiji achana na hoja nzito unazotaka kuingiza kwenye suala hili: hapa hakuna jurisprudence ni WIZI MTUPU!!!
 
Inawezekana DPP anataka majina mengine yawemo zaidi ya hayo 4 ya jamaa wa SFO! Otherwise hakuna justification yoyote kwamba ushahidi bado! Hata mtoto mdogo anajua kwamba Chenge na Idrissa wamekula mlungula hapo!
 
Totally confused!

Ok kama DPP hajaridhika na kazi yz PCCB, hao supspects siwakamatwe now na kufikishwa kwanza mahakamani kwa ushahidi uliopo, then kazi ya kutafuta ushahidi zaidi iendelee wakiwa under custody!
 
Inawezekana DPP anataka majina mengine yawemo zaidi ya hayo 4 ya jamaa wa SFO! Otherwise hakuna justification yoyote kwamba ushahidi bado! Hata mtoto mdogo anajua kwamba Chenge na Idrissa wamekula mlungula hapo!

Unajua NJ issue ya Radar ukiifuatilia sana unafika mpaka kwa JK maana alikuwa Waziri wa fedha 1994 hadi 1995. Kwa hiyo kama Waziri wa fedha alijua mipango ya matumizi ya serikali kwa kipindi hicho kama Mramba alivyojua masuala ya ndege ya Rais. Kwa hiyo JK analijua hili deal na alijua waliohusika. Lakini bado akawateua kwenye nafasi mbalimbali. Sasa kama Rais kawateua unategemea PCCB na DPP watafanya nini?? Wizi Mtupu.
 
Katika nchi ambazo uongozi wake unachukia rushwa kwa dhati kama vile Ruanda ya Kagame, hivi leo hii Andrew chenge, Idris Rashid na swahiba wao Somaia[ Licha ya kuwapa CCM 400mill] wangekuwa Keko kama si Ukonga!! Kwa bahati mbaya sana viongozi wetu hapa Bongo wao ni washiriki wa hawa jamaa katika kuiibia nchi yao!!

Kama huamini ninachosema hebu wewe nenda kijiji kinachoitwa MSOGA huko Chalinze ukaone ujenzi unaoendelea na ufananishe na umasikini wa nchi hii!!

Uongozi wa nchi yetu ni wizi mtupu na ndio maana wote wezi kama wakina Idris Rashid bado wako kazini!! Katika nchi yeyote inayofuata utawala bora huyu jamaa na wengine kama yeye wangekuwa hawako kazini lakini kwa sisi wadanganyika bado jamaa wanadunda mpaka lyamba!!

Mungu tuonee huruma tutelemshie muujiza!!
 
Tujikumbushe ya rada, tusijesahau

Mwandishi Wetu Machi 25, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

SASA imedhihirika kwamba Mkataba wa Ununuzi wa Rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems, uligubikwa na rushwa kubwa, kwa mujibu wa Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya nchini Uingereza – Serious Fraud Office (SFO).

Wapelelezi wa ofisi hiyo juu ya mkataba wa ununuzi wa chombo hicho kwa Sh. bilioni 40 wamekuwa wakipeleleza kampuni hiyo na washukiwa wanane, wakiwamo Waingereza wanne - Sir Richard Harry Evans (67), Michael Peter Rouse (61), Michael John Turner (61), John Aldridge (52), na Watanzania watatu (majina tunayo, umri miaka 63, 44 na 45).

Katika taarifa yao ya awali ya Machi 2008, walisema: "Kuna kila sababu kuamini kwamba watu wote hao na Kampuni ya BAE Systems walitenda makosa ya rushwa katika ununuzi wa rada hiyo".

Wakibainisha jinsi sehemu ya mavuno ya rushwa hiyo yalivyogawanywa kupitia benki mbili za kigeni, kati ya Juni 19, 1997 na April 17, 1998, taarifa hiyo inasema hivi kuhusu Wa/Mtanzania hao/huyo: "SFO inahitimisha kwamba kuna kila sababu na kwa ushahidi tosha kwamba kwa kufanya hivyo (watu/mtu hao/huyo) alikuwa akiuweka uchumi wa Tanzania hatarini".

Ni dhahiri pia kuwa Serikali inawajua watu hao nao wanajijua; na ingekuwa kwa Nchi Zilizoendelea, zenye kuheshimu dhana ya kuwajibika, wangekuwa wameachia ngazi zamani kuponya nyuso zao. Lakini si kwa Mtanzania, ambaye kwake wizi, ubadhirifu na ufisadi ni ushujaa wa kupokelewa kwa kutandikiwa zulia jekundu.

Ningekuwa mimi ndiye Rais, ningewashauri watu hao kuachia ngazi kiungwana ili kutoipaka tope serikali yangu. Ningekuwa mimi ndimi mshukiwa, nafsi yangu ingenisuta na kujiuzulu sawia. Huu ndio uungwana; huu ndio ustaarabu wa binadamu, wa kuweka mbele maslahi ya walio wengi, tofauti na wanyama kama Nyang'au, wanaoweka maslahi binafsi mbele kwa maana ya "Rule of the Jungle"- Kanuni za mwituni". Na haya yanapotokea, tuliowaweka kusimamia serikali, wako wapi?. Au wametusahau kwa kujichongea mzinga wa asali?

Tabia ya kikundi cha viongozi wachache ya kulishwa asali kidogo na wawekezaji kwa kutumia mamluki wa ndani, ili kutetea manunuzi na uwekezaji usio na maslahi kwa taifa, inaendelea kuitafuna nchi. Tumejionea hili kwa mradi wa IPTL, ununuzi wa ndege mbovu ya Rais, mbuga za wanyama (Ortello), Richmond, mikataba ya madini na sasa Dowans, bila kusahau sakata hili la Ununuzi wa Rada.

Miradi yote hii imethibitika kuwa bomu la maangamizi kwa Taifa kiuchumi na kijamii. Na kwa nguvu ya fedha ya kifisadi, imeweza kuingiza "wateule" Bungeni, Chama tawala, Taasisi nyeti za serikali na serikali kuu. Ndiyo maana kero za wananchi hazipati majibu kutokana na jeuri za kifisadi, eti kwamba "dua la kuku halimpati mwewe".


Ungekuwa mmoja wa waliotetea ununuzi wa rada na ndege ya Rais kwa maneno makali ya kutunisha mishipa ya shingo; kisha unagundua kwamba kwa kufanya hivyo uliudanganya umma, ungefanyaje? Ungekuwa na ujasiri tena kusimama kadamnasini, macho makavu, na kuusalimia umma unaoteseka kiuchumi kwa ulaghai wako?.

Rais Richard Nixon wa Marekani, kwa ustaarabu, alijiuzulu urais kwa kashfa ya Watergate. Naye Waziri Mkuu wa Israeli, amejiuzulu hivi karibuni kwa kashfa ya rushwa; wengi walipita njia ulimwenguni, kwa ustaarabu wao; wewe je? Utetezi wa matusi kwa kujificha ndani ya mbawa za chama kinalisaidia nini Taifa lako?.

Rushwa ya mtu mmoja ni mbaya vya kutosha, lakini Serikali nzima inapohusishwa na rushwa kwa matendo ya wachache ndani yake wasioguswa, kwa sababu tu wanaonekana kukipenda chama tawala kuliko Taifa, hili si jambo la kufumbia macho.

Tuangalie mfano wa sakata la rada. Wakati hoja ya utapeli wa mkataba huo ilipoibuliwa na wapinzani, Naibu Waziri wa Fedha, Abdulsalaam Issa Khatibu; Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mark Mwandosya na Mkurugenzi Mkuu wa Kurugenzi ya Usafiri wa Anga, Margareth Munyangi, ndio waliokuwa wa kwanza kutetea mradi huo wakisema: "Rais hawezi kudiriki kamwe kuacha usalama wa wasafiri wa ndege, mikononi mwa bahati nasibu".


Hakuna aliyekuwa akipinga hili, bali kilichopingwa ni bei kubwa na ubora hafifu wa kifaa hicho mtumba, kwa sababu tayari jumuiya za kimataifa na Waziri Clare Short wa Uingereza, walikwishaonya na kuitahadharisha Serikali juu ya ulaghai wa dili hilo. Kwa nini hawakuamka kwa tahadhari hiyo?

Naye Rais Benjamin William Mkapa, kwa kuambukizwa na watu waliomzunguka, na pengine kwa kutumia Chama, akiwa ziarani Mbeya alitetea ufisadi huo akisema: "Wanaoikosoa Serikali si tu wanaibeza Serikali na Chama chake, bali wanawabeza Watanzania waliokipatia Chama cha Mapinduzi mamlaka ya kutawala kwa wingi wa kura (bila kujali zilivyopatikana) ili kiweze kutekeleza ilani na sera sahihi, zenye kulenga kumletea maendeleo mwananchi….. Hao ni vipofu na viziwi".

Baada ya kuthibitika kwamba ndege ya Rais na rada aliyokuwa akitetea ni mabomu na kikwazo kwa maendeleo ya mwananchi; kati ya yeye na hao aliowaita eti ni vipofu na viziwi, ni yupi aliyekuwa akiwabeza Watanzania?.

Tangu mwanzo, Baraza la Mawaziri la Uingereza lilikuwa limegawanyika juu ya Uingerza kuiuzia Tanzania ndege mbovu, licha ya kwamba zoezi zima lilikuwa la udanganyifu. Waziri wa Fedha, Gordon Brown (sasa ni PM) na Mama Clare Short, Waziri wa Ushirikiano na Misaada ya Kimataifa, Mashirika ya Oxfam, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Shirika la Kimataifa la Usalama wa Anga (ICAO), Jane's Air Traffic Control na wengine, wote waliweza kubainisha mapema juu ya udanganyifu wa mkataba huo, kiasi kwamba Benki ya Dunia ikatishia kuzuia misaada kwa Tanzania.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, alijua yote haya; lakini aliishinikiza Kabineti yake imruhusu kutoa kibali cha mauzo kwa BAE Systems ili kuokoa ajira za Waingereza 280 wa Kampuni hiyo, iliyopo katika kisiwa cha Isle of Weight, ili Chama chake kisipoteze ushindi katika jimbo lililohusika. Rais Mkapa alipeleka salaam kwa Blair, kumshukuru kwa kuweza kuifanya Serikali yake iidhinishe mauzo ya mtambo huo mbovu chini ya mkataba wa kitapeli.

Juni 21, 2002 Waziri wetu wa Fedha wa wakati ule, Basil Pesambili Mramba, katika kauli iliyoonekana kutowakilisha maslahi ya Taifa, alitamka Bungeni maneno yafuatayo ambayo itawachukua Watanzania muda mrefu kuyasahau: "Tunakataa kuambiwa mambo yakufanya hata kama sisi ni masikini … Wanawezaje kuwa na ujasiri wa kutuambia kwamba rada hiyo ni aghali sana kwetu?... Tuko tayari kula majani, na kama wanataka, waache kutupa misaada yao".

Kuonyesha kwamba hoja za wananchi hazikuwa na uzito kwake, Mramba, kwa wakati tofauti, alisema: "Baadhi ya watu wanaokota okota maneno baa na kuyafanya wimbo rada … rada … rada kwa kujisumbua; hawajui kwamba Serikali ya Uingereza imekwishatoa leseni ya kuiuzia Tanzania rada; na kinachotokea Uingerza sasa ni mgogoro ndani ya Serikali ya huko ambayo wanataka kuuleta katika Serikali ya Tanzania".


Mramba na wenzake waliilewa vizuri Kampuni ya BAE Systems na malengo yake; kwani wakati huo ilikuwa imekumbwa na kashfa ya madai ya kutoa rushwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, baada ya nchi hiyo kutiliana sahihi mkataba wa kampuni hiyo kuiuzia silaha za kijeshi. Na kufuatia upelelezi wa SFO, kama inavyofanya hapa kwetu kwa sakata la rada, ilibainika kuwa BAE Systems, iliweka Pauni za Kingereza milioni saba katika Akaunti ya Mifuko (Trusts) huko Jersey, katika Visiwa vya Channel, na kutokana na uchunguzi zilimilikiwa na Waziri huyo.

Baada ya kuonekana mambo yanamwendea vibaya, Waziri huyo aliutema mfupa, akalipa Pauni milioni sita kwa mamlaka za utawala wa visiwa hivyo kama fidia ya usumbufu walioupata kutokana na upelelezi huo, na kwa maelewano ya kusimamishwa kwa upelelezi.

Kwa kufanya hivyo, inaweza kutafsiriwa kuwa, ama Waziri huyo alikuwa anautema mlungula kwa nafsi yake kumsuta, au naye alikuwa anatoa rushwa ili upelelezi usitishwe.

Hakuna shaka yoyote sasa kwamba wabeba mikoba ya ufisadi wa rada ya Tanzania, wanafahamika kwa mujibu wa taarifa ya SFO kwamba: "There is every reasonable cause to believe that all the above named persons and Company have committed offences of corruption …. The SFO concludes to believe that in taking this stance….. (name/s) was putting the economic interest of Tanzania at risk", ni maneno ambayo tafsiri yake tumeitoa hapo mwanzo.

Je, kwa taarifa hii ya SFO, wahusika wa kashfa ya rada nao sasa wanaweza kuitema milungula kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar; au watazuia wasiwajibishwe, au Sheria kuchukua mkondo wake, kwa nguvu ya fedha walizo nazo? Hivi ni mpaka SFO waje Tanzania ndipo tubaini vitendo vya ufisadi vyenye kuangamiza uchumi wa nchi yetu?

Hii inadhihirisha aina ya viongozi tulio nao, ambao Shaaban Robert anawaelezea kwa maneno yafuatayo:

"Ni waledi wa kusema, watu wa leo,
Bali hawana huruma, katika moyo,
Tamthili ya Wanyama mfano wao,
Kisha waweza kuuma, sumu wanayo,
Mungu nilinde nao wanyama, wala wenzao.

Kwa mazingira yetu ya sasa, Shaaban Robert hakosei anaposema tumepungukiwa hekima na heshima, kwamba heri wanyama, ndege na wadudu:

Serikali za wanyama, na ndege au wadudu,
Ndani zina taadhima, kama kwamba maabudu,
Na watu wenye hekima, siku hizi hawamudu,
Madaraka na heshima, heri mnyama na dudu,
Na mambo haya si mema, watu wanayahusudu;
Hizi husemwa ni zama, za watu kufa kibudu,
Kufa wangali wazima, na nguvu za kusujudu,
Na maudhi na hasama, kwa kashata na ladu.
 
Duuu.....mimi nashindwa hata kuanza kujadili maana serikali hatabakia mtu yeyote maana kashfa. Ziko kama 15 ivi sasahata JK anatakiwa ajiuzulu haraka...kwa kweli ni balaa sana na aibu watu wamo tuu...JK unafanya nini?unatuuuzia sura??kuwa jasiri japo kidogo tu,ni aibu jamani...hadi tunaikiria kukufuru kutaka mapinduzi maana watu hao hao. Wanatufanya wenginewote wapumbavu alaaa
 
Report ya SFO ya Uingereza kuhusu scandal ya radar hii hapa. Waoneni mapapa wa ufisadi wa TZ.
 

Attachments

  • Mafisadi wa radar TZ.zip
    638.3 KB · Views: 141
swali langu ni kuwa tuhuma dhidi ya Chenge na Dr. Idris ni kubwa mno. Ni kubwa kiasi cha kutisha. Sasa kinachongojewa ni nini?

Hivi SFO wakisema hawawashtaki na sisi tusiwashtaki?

Kwanini tusiamue kufuta tu makosa yote ya nyuma tuanze na ukurasa mpya?

Mzee Mwanakijiji,
Mramba alisota rumande siku kadhaa na akakosa hata harusi ya mwanae, Mwakalebela , Mungai,wanakesi mahakamini, Lihumba amefungwa miaka miwili. Why not Chenge?

Tanajenga nchi gani ambayo sheria zake ni kwa watu fulani tu. Tunaweza kuanza upya iwapo watu watakili makosa yao na kukakaa pembeni.
Wakati wananchi walianza kusahau haya masakata ya rada, Chenge anaibuka na kutaka usipika.

Bibilia inasema wote tumenda dhambi. Tutahukumiwa kwa kuto kutubu. Change hajatubu na anakataa andai yeye ni safi na TAKAKUU inamsafisha. Maanayake katuona mabwege, na akipewa uspika tutaona ya filauni.

 
TAKUKRU ni kichaka cha mafisadi maana anayeongoza ni kama hivyo tena wnakura rushwa hao kuzidi police maana rusha yao sio ndogo, tukirudi kwenye topic yaani SFO wajinga harafu wale waindi waliokimbia nchi nao hawahusiki sasa, uozo mara 70
 
[/COLOR]Mzee Mwanakijiji,
Mramba alisota rumande siku kadhaa na akakosa hata harusi ya mwanae, Mwakalebela , Mungai,wanakesi mahakamini, Lihumba amefungwa miaka miwili. Why not Chenge?

Tanajenga nchi gani ambayo sheria zake ni kwa watu fulani tu. Tunaweza kuanza upya iwapo watu watakili makosa yao na kukakaa pembeni.
Wakati wananchi walianza kusahau haya masakata ya rada, Chenge anaibuka na kutaka usipika.

Bibilia inasema wote tumenda dhambi. Tutahukumiwa kwa kuto kutubu. Change hajatubu na anakataa andai yeye ni safi na TAKAKUU inamsafisha. Maanayake katuona mabwege, na akipewa uspika tutaona ya filauni.


Tumejenga nchi ambayo sheria zinafanya kazi kwa wanyonge tu. Wenye nguvu na pesa wanahaki ya kufanya makosa na sheria zinakpindishwa, we have been there. Ditopile alifanya hivyo na akapeta. sasa wako wengine wanapata. wewe iba kuku ukione cha mtema kuni.
 
Back
Top Bottom