The new Landrove Defender

Hahah daah i hope wangepitia huku wakajipatia free consultation(majina ya bureeee) ya magari yao.

Kuna ka-nissan nakapendaga,hua naiona imekaa fresh afu kitu VQ35 na bei reasonable ila sasa jina lake ndo lina nipaga changamoto inaitwa Nissan Fairlady z,hio 'fairlady' (ingawa najua ina definition nyingi ) lkn hua ni kisanga.
Kale kagari ni ka racing...kapo vizuri ila hilo jina hata mimi halinivutii
 
Mkuu, unajua gari kadri linavyokuwa sophisticated saana na umeme, linakuwa less reliable, na uwezo wa kudumu muda mrefu unapungua. Hata resale value yake kwenye used markets inashuka. Range Rover ikiwa mpya inazidi Defender bei mara mbili au zaidi. Ila kwenye used market Defender ina bei kubwa hata 3 times ya Range Rover. Leo hii ukiangalia Defender ya 1990s ina bei kubwa kuliko Range Rover ya 2000s. Wajuzi wa Range Rovers wanakwambia huwa wanazitumia zikiwa kwenye warrant tu. By the time zimetoka kwenye warrant wanaziuza, maana maintenance cost inakuwa kubwa mno, kila mara linazingua, na cost ya repair inakuwa kubwa. Ila kina Defender wa zamani ambao ni very mechanical, bado wanatesa tu.

Hizi sophisications hata bmw zimeshawakumba, zimeifanya hata depreciation za bmw 7 series kua ni balaa,resale value yake ni aibu.
 
Hizi sophisications zimeifanya hata depreciation za bmw 7 series kua ni balaa,resale value yake ni aibu.
Saana. Maana its obvious mnunuzi wa kwanza ni tajiri, na anaweza kumudu gharama, na linakuwa bado kwenye warrant. Sasa linapokuwa used, maana yake tunanunua watu wa kawaida ambao kipato ni cha kawaida,na hailiko kwenye warrant, parts ni bei balaa, mafundi wa kitaa hawaliwezi mpaka ulipeleke kwa dealer. Unafikiri bei itabaki juu kweli?

Ila angalia mnyama wa 91 na kilometa kibao ila cheki bei yake ilivyo
70 series.PNG
 
Hahah daah i hope wangepitia huku wakajipatia free consultation(majina ya bureeee) ya magari yao.

Kuna ka-nissan nakapendaga,hua naiona imekaa fresh afu kitu VQ35 na bei reasonable ila sasa jina lake ndo lina nipaga changamoto inaitwa Nissan Fairlady z,hio 'fairlady' (ingawa najua ina definition nyingi ) lkn hua ni kisanga.
tena kwenye hili hata Lady Rover ingependeza zaidi!
 
Gari almost zote mpya zina umeme na teknolojia kubwa sana.

Nadhani ndio maana hata ile ya mwanzo wameamua kuachana nayo.

G Wagon wamebaki na muundo uleule ila humo ndani wamejaza umeme wa kufa mtu.
Systems za Umeme zinawork kwa efficiency kubwa kuliko system za mechanical. Ndo maana makampuni mengi wanazipiga chini saiv...

Sasa ufundi magari utahitaji shule ya maana na siyo kukariri
 
Saana. Maana its obvious mnunuzi wa kwanza ni tajiri, na anaweza kumudu gharama, na linakuwa bado kwenye warrant. Sasa linapokuwa used, maana yake tunanunua watu wa kawaida ambao kipato ni cha kawaida,na hailiko kwenye warrant, parts ni bei balaa, mafundi wa kitaa hawaliwezi mpaka ulipeleke kwa dealer. Unafikiri bei itabaki juu kweli?

Ila angalia mnyama wa 91 na kilometa kibao ila cheki bei yake ilivyo
View attachment 1206164
Naam hapo ndipo watajua the power of simplicity mkuu,hicho chuma hakina mambo mengi chenyewe kinagonga kazi mwanzo mwisho.

What do you think mkuu,miaka mingi ijayo do you think hiki chuma 70's series kitakuja kua collector cars/vintage?
 
Siyo kubana mafuta tu.... ila inaongeza efficiench nzima ya gari.
Uwezekano huo ni mkubwa sana....sasa hivi umeme mwingi ili kubana mafuta lakini kuhakikisha nguvu ya kutosha ilihali mafuta yanayotumika ni kidogo...
Pia suala la mazingira
 
UK wao wanapendelea Manual trans. na statistics zinaonyesha manual to auto ratio ni 5:1 respectively.

Americans wanapendelea Autos though North America mostly ni wazee wa manual.

Europe nchi kama(Germany,italy,France) manual ndo mpango mzima.

Always kutakua na cars kwa ma car enthusiast wazee wa DIY hao manual trans is preferred.

Kama dunia ita adopt electric cars per se then hapo existence ya manual itakua shughuli.


System za manual nazo zitakuja kufutwa ni swala la muda tu...
 
Muulize alokuwa na Frelander ya mwaka gani?
CX othiambo cairo
Mkuu Freelander imetutesa . Propeller shaft tu ilileta shida na hazipatikani. Imebidi ki cancel miguu ya nyuma na sasa tunaitumia kwa kuvutia mbele . Magari ya land rover ni mazuri tatizo spare mpaka uagize . Kutembea yanatembea tena ni mababe barabarani. Shida ikiua spare parts
 
sijazungumzia LC au Nissan Patrol... nmezungumzia Landrover defender 110
Ooh .ok....
Lakini hata hizo 110 kwa sasa ni lulu...
Trust me, 110 will exist in the next 30 years...Kuna maduka hapa Arusha naona wanauza body parts zake kama milango, mashavu ...ukinunua unaenda tu kupulizia rangi unayotaka ndinga inakuwa mpya....
Kwa sasa 110, tutaiona kama ndiyo 109 a.k.a Mando....
 
Tengenezeni na nyie defenders zenu za kitanganyika.

Sio kulia lia tu ooh gari baya liko softi!

Viwanda vyenu vya kitanganyika vinazalisha maembe tu?
 
Back
Top Bottom