Mercedes Benz C Class Full Electric yazinduliwa!

Mercedes Benz C Class Full Electric yazinduliwa!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
33,665
Reaction score
97,418
Mercedes Benz wamezindua C Class with EQ Technology, ambayo ni sedan ya umeme tu. (Haina maana kwamba C Class ya ICE imekufa, hapana, ipo)!
IMG_7815.jpeg

C Class with EQ Technology Mercedes waliiteaser mwaka jana walivokua wanazindua GLC with EQ Technology, ila officially imezinduliwa jana tar 20 April.
IMG_7816.jpeg

Kwa sasa wamezindua version moja tu, C400 4MATIC with EQ Technology, inayokuja na motor mbili, AWD, 480 hp, na battery ya 94 kWh itakupa kilometa 800.
IMG_7818.jpeg

Kama kaka yake GLC, hii sedan inakuja na grille ya LED, hii mkiguswa na bodaboda tu msiba, na pia ina three-pointed star logo inayowaka.
IMG_7819.jpeg

Ndani kuna hyper screen ya inch 39, heated and massage seats, mziki mnene, panoramic roof, na mengine mengi.
 
Yeah. Ila SUV S Class (GLS) ni kubwa sana, kama ki minivan fulani hivi.

Ile na BMW X7 kuwa nayo inabidi uwe na familia kubwa.
Mimi mpenzi wa Sedan, labda familia ndio itaforce 2nd car iwe Minivan. Sijawahi penda SUV. Nazitamani tu kwa macho ila kuzimiliki sijawahi penda.

Kwa Mercedes, C Class naonaga perfect size. E Class na S naona kubwa sana. Sijui ata mtu uaishije nayo hapa Dar.

Kwa BM, 3 Series perfect. 5 na 7 hapana aisee.

Sasa ayo ma X7 dah ova tank, sijui utaliendeshaje mjini kulia bajaji kushoto boda.
 
Watengenezaji wa umeme wame fail kutengeneza mfumo wa gari kuji charge jinsi linavyotembea
Wamejaribu kiasi chake ila kufanikiwa 100% bado. Kwamba ukishachaji ndio iwe mazima sidhani. Law ya conservation ya energy inakataa.

Kuna magari yana solar pannel juu. Ila contribution yake ni ndogo sana. Ndio maana unaona sio trend.

EV zote zina regenerative brakes. Ukifunga brakes, energy inayotakiwa ipotee inaenda kuchaji battery. Kwahiyo kiasi flani inarudi.
 
Hapo ndio mwarabu ataendelea kutambua. Uwezekano wa ma bus ya umeme kusafiri safari ndefu ni mdogo. Otherwise waendelee kufanya utafiti wa magari ya kutumia nishati ya MAJI maana NASIKIA ukivunja bond ya Hydrogen na oxygen zinazounda MAJI zinatoa energy kubwa sana
 
Watengenezaji wa umeme wame fail kutengeneza mfumo wa gari kuji charge jinsi linavyotembea
A matter of time tu. Watapaswa kuwa na motor kwa ajili ya kufua umeme,Battery kwa ajili ya kusukuma gari, wheels(mbazo tayari zipo kwa ajili ya kuzungusha motor inayo fua umeme unaotunzwa kwenye battery na baadae kusambazwa kwenye gari watu hawajalala. + Teknolojia nyingine ambayo sijaitaja hapo

Nimeandika kirahisi tu ila kwa hao wataalamu naamini hawatashindwa jambo
 
Uwezekano wa ma bus ya umeme kusafiri safari ndefu ni mdogo
Kwa jinsi teknolojia inavyokua inawezekana kwa sasa wataalamu wengi focus ni kwenye gari ndogo, BRT buses na fully electric trucks

Mfano mwezi huu China wamezindua fully electric container ship ina uwezo wa kubeba container 700. Ikiwa full charge inaenda hadi 500km

Leo CATL wamezindua sodium battery, kuijaza full charge ni dk 6 tu, single charge range ni 1,500km

Kama kuna heavy duty fully electric trucks kama Sany zinapiga kazi kwa masaa mengi naamini kwenye basi za masafa coaches inawezekana

Hizi innovations zinatupa picha kuwa muda si mrefu tutaona mabasi ya masafa ya umeme barabarani

Kwa sasa full electric long distances coaches zipo zinaenda hadi 500km
 
Mercedes Benz wamezindua C Class with EQ Technology, ambayo ni sedan ya umeme tu. (Haina maana kwamba C Class ya ICE imekufa, hapana, ipo)!
View attachment 3577041
C Class with EQ Technology Mercedes waliiteaser mwaka jana walivokua wanazindua GLC with EQ Technology, ila officially imezinduliwa jana tar 20 April.
View attachment 3577042
Kwa sasa wamezindua version moja tu, C400 4MATIC with EQ Technology, inayokuja na motor mbili, AWD, 480 hp, na battery ya 94 kWh itakupa kilometa 800.
View attachment 3577044
Kama kaka yake GLC, hii sedan inakuja na grille ya LED, hii mkiguswa na bodaboda tu msiba, na pia ina three-pointed star logo inayowaka.
View attachment 3577045
Ndani kuna hyper screen ya inch 39, heated and massage seats, mziki mnene, panoramic roof, na mengine mengi.
Hii ina muonekano mzuri zaidi kuliko ile sedan iliyopo sokoni sasa hivi.
 
Japo ukiweza kununua hiyo swala la umeme kwako sio changamoto ila naomba kuuliza.
Ikiwa gari inakupa kilomita 900, je utatakiwa kuchaji battery zako kwa muda Gani, kwa units ngapi za umeme na ambazo zitagharimu sh ngapi?
 
BYD walishatoa mwaka Jana gari kama hii ...kwangu Mimi naona huku ulimwengu wa magari ya umeme haya makampuni ya ulaya watachemka tu
 
Back
Top Bottom