DU ASANTESalaamu Kaka Mshana !...
Naomba nijibu maswali haya kadri uwezavyo japo ni mengi.... samahani lakini.
1.Pesa (Sarafu) za kale zina mahusiano gani na mambo ya kichawi.... kazi yake ni nini hasa?.UKALE WAKE NA ASILI YAKE ZILITENGENEZWA NA MANUIZI
2.Je ni kweli mtu anaweza kuwekewa kinga ya mwili kumzuia kutodhurika na baya lolote lile litakalopangwa juu yake?. ZIPO KINGA ZA KIMILA NA KISHIRIKINA
3.Mchawi anaweza kuwa na vitu hivi viwili "uchawi na Imani ya Kiroho" je kama anaweza kuwa navyo anavitumia vipi?. SIO MCHAWI TU WENGI WAKO HIVYO KWA MUNGU KIDOGO KWA SHETANI KIDOGO
4.Waganga wanapokupa masharti pale unapoenda kuhitaji msaada wao huwa haiwezekani mtu kutatuliwa tatizo lake bila kupewa masharti?. NI SAWA NA KUPEWA DAWA HALAFU USIZINGATIE MASHARTI
5. Unaweza kuona dalili gani ukatambua kuwa unatumiwa kichawi?. HAKUNA DALILI RASMI MPAKA KITU KIENDELEE KUKUTOKEA MARA NYINGI
6. Je wachawi wa Mataifa mbalimbali wakikutana hutumia lugha gani kwenye mawasiliano yao?. VITENDO
7. Ikitokea mtu anataka kukudhuru wewe kwa uchawi utatumia njia ya uchawi kumdhibiti au utatumia imani?. MAPAMBANO YA KIROHO HUPAMBANA KIROHO SOMETIMES NI MPAKA UWE NA KINGA AMA NGUVU FULANI
8. Je leo hii akija mtu kwako anahitaji msaada na kweli ukaona yupo kwenye tatizo kubwa (ulimwengu wa giza ) utakuwa tayari kumsaidia?. KWA UWEZO WANGU NITAFANYA HIVYO
9. Mshana uliwahi kujaribu kutumia usafiri wowote wa kichawi na kama bado je unaweza kunielezea kidogo hatari ya usafiri wowote wa kichawi na mwendo wake?. NAOMBA HILI NISILIJIBU
10. Mchawi anapoamua kumchezea mtu huwa anatafuta mtu anaemjua au yeyote?. HIYO NI MICHEZO YA WANGA MCHAWI ANAKUDHURU KABISA HATA KAMA HAKUJUI
11. Mtu anaweza kurithishwa uchawi akiwa na umri gani, (kwa mtoto na mtu mzima). INATEGEMEA WENGINE HURITHISHWA KATIKA UMRI MDOGO KABISA
12. Je wachawi wenyewe huwa wanaogopa nani ( tukiacha watu wa kiroho). WACHAWI WENZAO WA DARAJA LA JUU
13. Ni sehemu gani uchawi hauwezi kuingia (au unaingia kwa shida sana) KWA WATU WALIOMSHIKA MUNGU VIZURI.
14. Kuna tofauti gani pale mchawi anapomchezea mtu aliyejikinga na dawa na yule ambaye hajajikinga?. HUMKWEPA MWENYE KINGA
15. Kuna Pesa mtu anaweza kuwa nazo ndani ila hazitumii kichawi pesa hizi huwa zina matumizi gani?. HULKA BINAFSI SOMETIMES UBAHILI
Mwisho......... Karibu Mashana Nakungojea kwa majibu yako Muruaaaaaaaa
Ni siri ya wale jamaa mimi sifahamuKipi kinafanyika hadi ninaona hivyo kumbe sivyo?
Mchawi anakudhuru mwanga anakuchezea tuEheeeH.. kumbe kuna tofauti kati ya mchawi na mwanga(wanga)..!
Hapana ila nilishawahi kufika mpaka eneo la kuondokeaSwali lingine:
Mshana ulishawahi kupanda ungo? Inawezekanaje kauongo kadogo wanakaa watu wa 5.
Brother Mshana acha Siasa bana, can't you mention specific sources?Kutoka vyanzo mbalimbali
Refer vitabu vya dini! But si kila kitu Mungu anaruhusuUchawi ulitoka wapi? Au ulitokana na nini? Ni kweli mtu hawezi kurogwa mpaka Mungu mwenyewe aruhusu?
Mmh hizo mimi huwa nazisikia tu niwe mkweliMkuu mshana jr Heshima kwako!
Kuna kipindi nimefanya kazi katika mazingira fulani hapa Tanzania. Wakazi wa maeneo ya huku huwa wanatumia njia za kishirikina kuadhibiana pale unapomfanyia jambobambalo sio la kiungwana, hasa kutumiana Radi wakati wa mvua. Nilijaribu kudadisi kwa wazee wa jamii ya huku. Ila wakadai kwamba Radi hizi lazima umtumie mtu ambae mna uhusiano wa damu. Naomba ufafanuzi kidogo kuhusu njia hii ya ushirikina kama unaifahamu.
Mmh ila hapa si chit chatUna dawa ya kutakatisha vyeti feki? Kama unayo msaidie Bashite
Mkuu halafu mshana anafanana na mbwiga Mbwiguke (MZARAMO) wa Clouds Media.Asante mshana jr
Nakupongeza kwa kutuonesha picha yako halisi.
Wengi tulidhani kwa mambo unayoyajua basi utakuwa mzee au mbabu fulani.
Kumbe ndo kwanza unatafuta mchumba.
Safi sana mheshimiwa
Mshana Jr
Kwa kututhamini
Naposti
Tafadhali fanya hivyoKuna somo la machale takutag
Yeah maranyingi viwanja vya vya mpiraHaha eti eneo la kuondokea. Kwa hiyo kuna viwanja maalumu kama ilivyo JNIA?
Ni masharti gani kupanda ungo? Mbona baadhi huwa wanadondoka wanakuwa wamekosea nini?
[emoji23] [emoji15] [emoji12] [emoji115] [emoji781] [emoji779]Mkuu halafu mshana anafanana na mbwiga Mbwiguke (MZARAMO) wa Clouds Media.
Tafuta hii post no 93
Tofauti ya viini macho/mazingaombwe na uchawi ni ipi?Ule si uchawi ni mazingaombwe na viini macho na wengi huingizwa mkenge kuwa ni uchawi