The Interview: mshana Jr.

Uchawi ni dunia ya kiza na dunia ina usiku na mchana! Kila kinachotokea upande mmoja ni replica ya upande wa pili
Dhana ya uchawi na mambo yake yote vinatumiwa na kada zote katika maisha kuanzia viongozi wa dini wanasiasa mpaka vibaka
 
Asante mshana jr

Nakupongeza kwa kutuonesha picha yako halisi.
Wengi tulidhani kwa mambo unayoyajua basi utakuwa mzee au mbabu fulani.

Kumbe ndo kwanza unatafuta mchumba.
Safi sana mheshimiwa
Mshana Jr
Kwa kututhamini

Naposti
 
Kabla ya yote mkuu vipi una hirizi la kujikinga?maana hayo makombora yatakayokuja hata yale ya korea kaskazini hayaoni
 
OK asante sorry nimejibu kwa ufupi
 
jr mi swali ni hili?je kama huamini kuna uchawi tena ikatokea ukamtukana mchawi je anaweza kukuloga na ukadhurika kwa manuizo yake?pili, je kama uchawi kweli unafanya kazi kwanini trump asimshushe hata busha kim jung ili dogo apate heshima?
Uchawi una miiko taratibu na masharti yake! Hawa wa kawaida unaeza kutukana na asikufanye chochote ila kuna namba hazichezewi asilani
Trump siwezi kumzungumzia kwakuwa sijui mtazamo wake kwenye uchawi
 
Mshana
1.Kuna uhusiano gani kati ya maisha ya mtu na nyota?
2.mtu anaweza kumuibia mwazake nyota?
3.Zipi ni dalili au njia za kujua kama nyota yako ipo au vibaka walisha ikwapua?
4.Je nyota iliyo ibwa yaweza kurudishwa kwa mhusika? how?
 
Kuhusu mabangili ya shaba:kuna mtu alinambia kuwa yanazuia mapepo pia ni kinga kwa mfano kutochukuliwa pesa na wazee wa chuma ulete,hii imekaaje?
Inategemea na bangili na manuizi iliyofanyiwa japo kuna baadhi zina material yanayovutia ama kupingana na dunia zote mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…