The Interview: mshana Jr.

Kwako mshana, nina maswali kadhaa hapa.

1. Ni kitu gani haswa unajutia maishani.?
2. Elimu yako ya mambo ya kiroho imekusaidiaje wewe binafsi na watu wanaokuzunguka.?
3. Je ushawahi kupata woga.? Ilikuwa ni wakati gani na nini kilipelekea wewe kuogopa.?
4. Haya unayoshare nasi jukwaani, je familia yako inajua kuwa unajua.? Wanakuchukuliaje juu ya hilo.?

5. Umeshawahi kuona visivyooneka kwa macho ya kawaida.? Vipoje.?
6. Nakumbuka katika thread mojawapo inayozungumzia budhist college, ulsema kuwa ushawahi shuhudia kafara ya mtu toka kwa waabudu shetani, na ulipewa offer ya kujiunga nao. Je ulifikia nao wapi.?

Tuanze na hayo kisha nitarejea na mengine ninayohitaji kujua toka kwako.
 
Mkuu mshana hivi uchawi una nafasi gani katika maendeleo ya mwanadamu?(Asilimia kubwa ya watu wanaamini, Mali & Utajiri unapatikana kwa njia zisizo halali,mfano utapeli,uchawai n.k) Na hata matapeli,Majambazi n.k wanatumia sana uchawi hili kutimiza Malengo yao.
Je kuna ukweli upi kuhusu hili jambo mkuu.
 
jr mi swali ni hili?je kama huamini kuna uchawi tena ikatokea ukamtukana mchawi je anaweza kukuloga na ukadhurika kwa manuizo yake?pili, je kama uchawi kweli unafanya kazi kwanini trump asimshushe hata busha kim jung ili dogo apate heshima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…