The Daring and Bold Magufuli

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Kama kuna kitu cha wazi ambacho ni funzo kubwa kwetu Watanzania katika miaka minne hii ya Awamu ya Tano na "Utawala" (maksudi kabisa badala ya kutumia uongozi) wa Magufuli ni UTHUBUTU!

Uthubutu, ni uwezo wa kufanya mambo bila kuwa na kigugumizi au kujishuku. Ni kufanya mambo, kusimamia unaloliamini bila kujali au bila woga. Sasa kwa Magufuli ambaye tulijua akiwa waziri alikuwa ni mchapakazi mpaka kuitwa bulldozer, ilimaanisha alifanya mambo jinsi alivyoona ni sawa kwa nafasi yake na sasa kwa kupata Urais n kuwa Rais wa Jamhuri, basi Ari, Kasi na Nguvu zake za kuwa Bulldozer na uthubutu zimeongezeka maradufu.

Uthubutu si lazima tuutazame kwa matokeo chanya pekee, hata matokeo hasi yanaweza kutokea kutokana na mtu kuwa na uthubutu, kudhamiria na kufanya lile alilokusidia.

Rais Magufuli ametusaidia sana kutuonyesha kwa vitendo, na si semi, kauli au porojo kuwa kwenye nia pana njia.

Naam, kuna maamuzi mengi yaliyotokana na Uthubutu huu yameleta maswali mengi na hata matokeo ya "uthubutu" kuonekana kama hatua ambazo zilikosa weledi, busara, uhakika au hata hekima. Lakini cha msingi kwa andiko langu hili si kukosoa au kusifia mafanikio au kushindwa kwa maamuzi aliyoyafanya, la hasha... naangalia silika ya kibinadamu ya kuwa na uthubutu, Daring!

Nakumbuka miaka 10 ya Rais Kikwete, uongozi au utawala wake ulionekana umepwaya kwa kukosa Uthubuu wa ukali na kusimamia mambo yafanyike, bila kujali matokeo. Nakumbuka mgombea wa Urais 2015 Bwana Lowassa alinukuliwa mara kadhaa akisema Tanzania inahitaji mtu mwenye kufanya maamuzi magumu, na Watanzania ule u-soft soft wa awamu ya nne, ulitufanya tutake kupata mtu "Dikteta" kauli na nadharia ambazo kwa umoja wa Kitaifa bila hata chembe ya tofauti za kisiasa ai itikadi, ilikuwa ni "natural" kukubali uhitaji wa kuwa na Rais Mkali, Dikteta!

Magufuli kathibitisha katika uanadamu kuwa Uthubutu si jambo la kusadikika, bali li jambo la kweli, lina uhai na kila mtu akikusudia na kujiamini, anaweza kuwa na Uthubutu!

Nikiiangalia Tanzania ilipo leo hii, miaka 58 tangu tupate Uhuru ambapo bado tuko kwenye hatua za mwanzo za kujaribu kupiga vita Ujinga, Umasikini, Maradhi, Unyonge na Utegemezi (UUMUU)pamoja na kutamka kwa vinywa vyetu mahitaji ya maendeleo ya taifa kuwa ni Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, sifa, hulka na wajihi wa kuwa na Uthubutu bado ni mchanga sana na ndio chimbuko la kukosa kujiamini, kuwa wanyonge na waoga kufanya maamuzi magumu.

Kuna dhana na falsafa inayosema fanya jambo, lisipozaa matunda chanya au uliyotegemea-matokeo hasi yanakupa fursa kurudia mchakato na kujifunza pale ulipokosea na kurudia jambo kwa ubora na umakini zaidi. Cha msingi ni kujiamini na kuwa na uthububu wa kufanya mambo.

Sasa kwa Tanzania yetu ya leo "Ya Magufuli" ya "MATAGA" na "CCM Mpya" utegemezi wa mwenye kujiamini na mwenye kuthubutu kumebakia kuegemea na kumtegemea mtu mmoja, Rais Magufuli. Wengine wote wamekaa kando wakishangilia na kusifia lakini hawana Uthubutu wa kwao wa kujitegemea na kwa nafsi zao bila kutegemea na kuzengea Uthubutu wa magufuli ambao sasa umeambatana na mamlaka na dhama kubwa kama Rais wa nchi.

Tumeshuhudia watendaji wa Serikali na Wanasiasa ambao wana majukumu ya kuongoza nchi, wakigeuka kuwa Wanyapara, wasiojiamini, wakitegemea sana UDola wa Kimamlaka na zaidi turufu yao kubwa ni kusema "maagizo kutoka juu" wakimaanisha ni maelekezo na maagizo ya Magufuli, wakikimbilia kuutegemea Uthubutu wa Magufuli kama ngao na nguzo.

Nasi wananchi ambao hatuna mamlaka au dhamana ya kiuongozi au madaraka, nasi tumekaa kando kwa unyonge au kuachia kila kitu kifanywe na kuamini na kutegemea "ah Magufuli ni kiboko".

Leo haki ya mwananchi inakanyagwa na kupuuzwa, tunakosa Uthubutu wa kudai haki na kusimama imara kukataa kuburuzwa. Ndio kuna hofu na mazingira ya kutishiana ambayo yanatufanya kukosa kujiamini, lakini kwa nini hatumtazami Magufuli yule aliyekuwa Waziri ambaye alisimama na kupata alichotaka na kudhamiria mpaka tukamsifia kwa ujenzi wa miundo mbinu Tanzania?

Nimesema awali, Uthubutu si lazima uzae matoke chanya (ambayo yanaweza kuwa ni mtazamo wa mtu, kikundi au wa aina moja au nyingine) au matendo yanayotikana na Uthubutu yapokelewe kwa mikono miwili na kila mtu. Lakini laiti kama kila mmoja wetu kwa miaka 58 tangu tupate Uhuru wetu tungekuwa na utashi, uimara, ujeuri, kujiamini na uthubutu hata kwa asilimia 50% a uthubutu wa Magufuli, si ajabu Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye maendeleo yake ya uchumi, kupanuka na kukomaa kwa haki za watu na yote ambayo tunanung'unikia leo, si ajabu yasingekuwa manung'uniko au kero za kutukosesha raha.

Nikiangalia na kupima Uthubutu wa Magufuli, kuna mengi kafanya (kutenda si lazima kuwe ni sifa ya kufanikiwa jambo) kwa kuamua. Ama ni kutoa maagizo, kuamrisha na kusimamia kikafanyika bila kujali matokeo (consequences or final result) au kuangalia hisia za watu. Mfano, aliazimia kupanuliwa kwa barabara, kukafanyika ubomoaji ili kupisha upanuzi wa barabara hata njia ya reli ya SGR. Hakusubiri majadiliano ingawa yawezekana kukawa na gharama kubwa kwa maamuzi hayo hasa pale penye malalamiko ya fidia.

Akaamua kununua ndege kwa fedha taslimu, zimenunuliwa ndege 5 kwa mkupuo tena kwa fedha taslimu bila kuwa na ukiritimba ambao Serikali na ATCL walifanya kwa miaka 20 kabla ya Magufuli kuboresha au kuwezesha Shirika la ndege kuwa na ndege za kutosha (wengi mtakumbuka ndege za Mattaka). Akasitisha mazoea ya kusafirisafiri ya viongozi na watendaji wa Serikali bila kujali kama kulikuwa na umuhimu wa uwepo na uwakilishi wetu au la, lakini amri yake ilisikilizwa kwa kuwa alisema atatumbua. Leo tumeona Chato inajengwa kwa kasi kubwa; iwe ni maagizo, amri au watu "kujituma" kuhakikisha Chato inakuwa na hadhi kubwa na sasa inageuka kuwa kivutio cha biashara na utalii. Akasema kufanyike uhakiki wa vyeti, wa wafanyakazi wa Serikali, nayo yakatimia. Akasema lazima kila mtu apate stakabadhi akinunua bidhaa ili Serikali ipate mapato... leo kila mtu anahangaika kuwa na stakabadhi! Akasema lazima tuhamie Dodoma, iwe kumekamilika au la, watu wakahamia Dodoma, wengine ofisi ziko kwenye vibanda na wanakaa vyumba vya kupanga.. lakini Serikali imehamia Dodoma.

Sasa najiuliza, sisi kilitushinda nini miaka yote kufanya maamuzi kama haya?ni kigugumizi gani kilitushika kwa muda mrefu kufanya mambo na kuwa na uthubutu, bila kuwa na woga au kujiumauma? kwa nini tuliamini hatuna uwezo wa kufanya mambo kwa hiari lakini tunafanya sasa kwa kuamrishwa na ni sawa na kwamaba tunachapwa mijeledi, tunazinduka na kufanya?

Leo nina uhakika Magufuli akisema tunarasimisha Katiba ya Wananchi iliyotokana na Rasimu ya Warioba, litafanyika bila kupingwa au miguno. Sheria kadhaa na miswaada imepelekwa bungeni na "Chama tawala" ama kwa woga, unafiki au labda ukweli halisi kimepigia kura na kupitisha kila kilichopelekwa na Serikali ya awamu ya tano. Rais Magufuli leo akisema ni marufuku kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa, hakuna atakayebisha.

Sasa ni rahisi kusema yeye ana mamlaka makubwa na anatumia cheo chake, lakini ukweli unabakia kuwa anayafanya kutokana na Uthubutu, daring.. hata kama mara nyingine ni kiholela (reckless) au ni kishari (mercilessly), but he gets shit done regardless.

Je sisi wote tungeanza kujiamini na kuanza kuwa na uthubutu bila woga kufanya mambo tunayoamini ni haki yetu kikatiba, ni wajibu wetu kusimama kuyapigania. Iwe ni nyumbani, makazini, kwenye masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiuzalishaji na kila jambo, uwe ni mfanyakazi, mwajiri, mfanyabiashara, mwanasiasa.. tukiwa wote na uthubutu, na tukafanya maamuzi kwa umakini lakini tukisimama imara kwa uthubutu, basi Tanzania ya Viwanda na Gurudumu letu la maendelo litapiga hatua kubwa na za haraka sana.

Lakini tukiendelea kwua Wategemezi wa magufuli, siku anaondoka tutarudi kule kule, kukwama matopeni na hata kuwa na mawazo potofu ambayo yanajengwa sasa hivi kusema tunahitaji Magufuli akae zaidi ya muda ulioko kwenye katiba.

Namshukuru sana kwa kutuonyesha Uthubutu, tuungane, tusimame imara tufanye mambo kwa uthubutu kupata haki zetu na maedneleo ya kweli na endelevu.

Ahsante Rais Magufuli kwa kutufundisha Uthubutu! Daring, Boldness.. Get Shit Done attitude!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mkuu, ni vema tukajadili hoja tukapingana na kukubaliana, I mean agree or agree to disagree without insinuation or words construe.

Hoja zikiwa nzito kuna option ya kuiacha lakini ni jambo baya sana kumwekea mtu maneno.
Tena unasema ''unaposema'' ukiwa na uhakika nilisema hayo.

Tadhali onyesha katika bandiko langu lolote ndani ya JF nililowahi kutumia neno Bulldozer

Pili, naomba waonyeshe wasomaji wapi nilipotumia neno 'Magufuli' katika mjadala huu

Tukiliweka hili sawa tutaendelea na mjadala wetu mzuri tu.
Title ya thread inahusu Magufuli; kwa hiyo hata kama hukusema neno Magufuli, the context is clear. Chanzo kikubwa cha upande huu wa mjadala tunakoelekea ni pale nilipo-question mchangiaji mmoja aliyesema ana weaken institutions na alichota fedha za hazina kujenga Uwanja kijijini kwao Chato bila kibali cha Bunge. Wewe umekuwa unachangia upande huo huo wa kussuport hilo. Ni kwa vile huwa sipendi kutumia majibu ya generalization, ndiyo maana ninapokujibu wewe ninakuaddress wewe tu bila kuhusisha wengine walio upande wako, kwa hiyo ndiyo maana sikusema kuwa "Mnaposema" bali nilisema "Unaposema." Ingawa hujaandika neno kwa neno kama nilivyo paraphrase kwenye conclusion hiyo, context ya michango yako ilikuwa hivyo kuhusu institutions. Upande wa Bunge ulifikia kusema kuwa Spika ni member wa NEC na hata hiyo post niliyoquote hapo inarudia hilo hilo "Inadvertently unatusaidia kuonyesha umuhimu wa taasisi imara, na jinsi gani Bunge letu lime deteriorate kama sikuwa defunct"

Nyuma huko nilikuambia kuwa Bunge lilikuwa hivyo siku zote tangu Uhuru, wewe ukasema hapana ni wakati wa utawala huu tu.

Kama unakana kuwa huo siyo mtazamo wako, na serikali ya sasa haijaweaken Bunge, basi ni vizuri, kwani ina maana kuwa tunakubaliana sasa kuwa ni kweli Bunge lina matatizo makubwa sana kiutendaji, lakini hayasababishwi na Magufuli..
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32464455, member: 348"]
Title ya thread inahusu Magufuli; kwa hiyo hata kama hukusema neno Magufuli, the context is clear.
Mkuu soma nilivyo approach mada
"Nguruvi3, post: 32333488, member: 24272"]
Mkuu Rev

Hii mada ni ngumu kidogo kutokana na tafsiri ya maneno daring and bold
Kwa kiswahili ulinganifu wa maneno hayo unaweza kuwa '' Ujasiri na uthubutu''

Ujasiri ni kitu tofauti na uthubutu.
Ujasiri una sifa zake, kwamba, unatenda jambo bila kujali hali iliyopo (consequences)
Ujasiri unaongozwa na hisa (emotion) na mara nyingi hutokea katika udharura

Uthubutu una sifa ya kutenda kwa kupanga ( planning) na nidhamu (discipline)
Uthubutu huzingatia hali ya wakati na matokeo yawe chanya au hasi

Rais Mandela alipotoka gerezani wafuasi wa Inkhoto Weswizwe walimuomba mapanga na mikuki ili Afrika kusini itakapoondokana na utawala wa kibaguzi walipe kisasi.

Kwa hisia (emotion) Mandela aliwaambia ''kama hicho ndicho wanachotaka yupo tayari kutokuwa kiongozi wao'' . Alipinga pale pale na kwa hisia kali, alikuwa JASIRI

Rais Mandelea alijua hali iliyotokea inahitaji uthubutu kukubaliana nayo

Akapanga (plan) tume ya maridhiano na suluhu (reconciliation and truth commission)
Akasukuma mbele mchakato wa kuandika katiba ya Afrika kusini baada ya ubaguzi

Mandela alitambua, bila uthubutu huo hali ya baadaye akiondoka itakuwa mbaya sana
Lakini pia alikuwa jasiri wa kukabiliana na Inkhoto Weswize bila kujali matokeo yake ikiwa atakuwa popular au unpolular.

Mandela alitambua ipo siku ataondoka, hakutaka kufanya Uthubutu ''single handedly ''
Alitambua uthubutu mzuri ni ule wa mfumo ambao hata baada ya kifo chake bado upo

Rais Kikwete alijaribu Uthubutu wa kutupa katiba mpya ili tujenge mfumo mpya wa kujitawala
Uthubutu wake ulikosa sifa ya kupanga(plan) na nidhamu(discipline) ukageuka kuwa Ujasiri

Kwavile ulikuwa ujasiri tu, nguvu yake ilipokutana na ''uthubutu wa wahafidhina wa CCM''
Kwahiyo inabidi usome alichoandika mtu, siyo kutafsiri kwa mtazamo wako. Ni hatari
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32464455, member: 348"]Chanzo kikubwa cha upande huu wa mjadala tunakoelekea ni pale nilipo-question mchangiaji mmoja aliyesema ana weaken institutions na alichota fedha za hazina kujenga Uwanja kijijini kwao Chato bila kibali cha Bunge. Wewe umekuwa unachangia upande huo huo wa kussuport hilo.
Kama uli question mimi nilionyesha kwa uwazi kwanini kuna wanao doubt. Hoja yangu ilikuwa moja, kwamba, kulikuwa na tatizo kuanzia mwanzo jambo ulilokubaliana nami kwamba neno Geita ni tatizo

Tofuatisha kati ya kujenga hoja na ku support. Mimi najenga hoja hata kama hutakubaliana nazo. Kwa njia hiyo sote tunaona ''blind spot''.
Ni kwa vile huwa sipendi kutumia majibu ya generalization, ndiyo maana ninapokujibu wewe ninakuaddress wewe tu bila kuhusisha wengine walio upande wako, kwa hiyo ndiyo maana sikusema kuwa "Mnaposema" bali nilisema "Unaposema."
Watu wangapi wanajua hupendi generalization? Mtu aliyesoma bandiko lako bila kupitia huko nyuma angeelewaje kuwa sijasema maneno hayo?

Utetezi wako ni flimsy na lengo halikuwa zuri. Ilikuwa kufanya implication kwa kuweka maneno nisiyosema. Ni hatari sana na sijui kama unaelewa impact yake.
This was intentional, the best way is to say sorry!
Ingawa hujaandika neno kwa neno kama nilivyo paraphrase kwenye conclusion hiyo, context ya michango yako ilikuwa hivyo kuhusu institutions.
Unaweza kuwa na tasfiri yako ambayo tunaiheshimu. Huna haki ya kufanya tafsiri yako kuwa ni ya umma! Ni hatari sana
Kama unakana kuwa huo siyo mtazamo wako, na serikali ya sasa haijaweaken Bunge, basi ni vizuri, kwani ina maana kuwa tunakubaliana sasa kuwa ni kweli Bunge lina matatizo makubwa sana kiutendaji, lakini hayasababishwi na Magufuli..
Nani kasema ndiye anayesababisha? Unaweza kuliangalia tatizo kwa jicho la wasomaji na si kwa mtazamo wako binafsi

Kabla ya rasimu ya Warioba niliwahi kusema sana hadi kuitwa mzee wa Mfumo.
Nilisema mifumo yetu ya taasisi si imara, lakini kwasasa hali ni mbaya kuliko huko nyuma.

Uliniuliza Mahakama inashinikizwa kutoa hukumu?
Sikujibu kwasababu tunaposema udhaifu hutuangalii factor moja.

Wewe ulitaka hukumu wakati mfumo wa sheria una mambo mengi sana.
Bunge nimekuonyesha matundu ambayo umekubaliana nayo
NBS nikakuuliza, mswada wa dharura na nguvu kubwa ilikuwa ya nini? Huna jibu
Nikakuonyesha jinsi taasisi kama polisi ilivyokosa credibility na integrity, ukakubaliana nami

Hoja hapa si nani kashinda nani kashindwa bali tujifunze kwa hoja bila kuwa na vinyongo.
Tuwe honest and credible.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Kama uli question mimi nilionyesha kwa uwazi kwanini kuna wanao doubt. Hoja yangu ilikuwa moja, kwamba, kulikuwa na tatizo kuanzia mwanzo jambo ulilokubaliana nami kwamba neno Geita ni tatizo

Tofuatisha kati ya kujenga hoja na ku support. Mimi najenga hoja hata kama hutakubaliana nazo. Kwa njia hiyo sote tunaona ''blind spot''. Watu wangapi wanajua hupendi generalization? Mtu aliyesoma bandiko lako bila kupitia huko nyuma angeelewaje kuwa sijasema maneno hayo?

Utetezi wako ni flimsy na lengo halikuwa zuri. Ilikuwa kufanya implication kwa kuweka maneno nisiyosema. Ni hatari sana na sijui kama unaelewa impact yake.
This was intentional, the best way is to say sorry! Unaweza kuwa na tasfiri yako ambayo tunaiheshimu. Huna haki ya kufanya tafsiri yako kuwa ni ya umma! Ni hatari sanaNani kasema ndiye anayesababisha? Unaweza kuliangalia tatizo kwa jicho la wasomaji na si kwa mtazamo wako binafsi

Kabla ya rasimu ya Warioba niliwahi kusema sana hadi kuitwa mzee wa Mfumo.
Nilisema mifumo yetu ya taasisi si imara, lakini kwasasa hali ni mbaya kuliko huko nyuma.

Uliniuliza Mahakama inashinikizwa kutoa hukumu?
Sikujibu kwasababu tunaposema udhaifu hutuangalii factor moja.

Wewe ulitaka hukumu wakati mfumo wa sheria una mambo mengi sana.
Bunge nimekuonyesha matundu ambayo umekubaliana nayo
NBS nikakuuliza, mswada wa dharura na nguvu kubwa ilikuwa ya nini? Huna jibu
Nikakuonyesha jinsi taasisi kama polisi ilivyokosa credibility na integrity, ukakubaliana nami

Hoja hapa si nani kashinda nani kashindwa bali tujifunze kwa hoja bila kuwa na vinyongo.
Tuwe honest and credible.
Mjadala huu umeanza kukosa mwelekeo kwani sasa mjadala unaanza kuwa na lugha ambazo siyo kiwango cha platform hii.

Ngoja nikumbushe tena kuwa mimi nilianza kwa kusupport decisiveness ya uongozi wake. Nina imani kuwa kiongozi shupavu ni lazima awe decisive na unapologetic kwa mambo anayoamini. Kuna wakati tuliwahi kusema rais ni Kikwete ni dhaifu tena hapa hapa JF kwa kuwa alikuwa indecisive katika mambo mbalimbali.

Baada ya hilo la decisiveness mada ikaishia kwenye hoja mbili kuu hizi:
(a) Magufuli kachota pesa bila idhini ya bunge kwenda kujenga uwanja kwao
(b) Magufuli anajiamulia mambo peke yake kiasi kuwa anaweken institutions mbalimbali za serikali (paraphrasing) . Imefikia kuwa institutions hizo zinashinikizwa kutoa data za uwongo ili kumfurahisha yeye tu. Ninadhani hii ndiyo pia uliyotumia kusema kuwa huamini data zinazotolewa na taasisi serikali. Na vile vile kuimply kwamba hata bunge linapitisha yale mambo anayopenda yeye tu, kwa vile (I guess) Speaker ni mjumbe wa NEC.

Majibu yangu yote yako focussed kwenye hizo hoja mbili tu na nilikuwa natoa vielelezo kwa nini ninazipinga.

Sasa kama wewe ulikuwa unazungumza mambo mbali mbali hata yaliyo nje ya hoja hizo mbili, basi it is very unfortunate, mimi nilikuwa ninatafsiri majibu yako yote along hoja hizo mbili tu. I am sorry, I was too focussed.

Kwa sasa inabidi tuishie hapo
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,030
2,000
Mkuu Kichuguu na Rev. Kishoka

The trouble is, western theories on leadership are based on western societies, not african, so they can not really work and they have not worked in last 50 years.

Ninachoona kwenye serikali ya JPM ni kuwa kuna mentality ya "Tanzania lazima ipige hatua" come what may. Kuna kuna genuine willingness. Lakini inasikitisha kuona kuwa kumbe kuna watanzania wenzetu wanapenda status quo, tubaki tunasota tu.

These things like Decisiveness, Awareness, Focus, Accountability, Empathy, Confidence, Optimism, Honesty, Inspiration, are very good in theory, and can work in Sweden, Japan Norway and Denmark, where most of people have same or similar culture, beliefs, education levels, lakini huku kwetu ambako mtu anataka mshahara bila kazi, umeme bila kulipa kodi. Na tusiangalie kiongozi kwa kumuangalia rais peke yake, what about diwani, mbunge, waziri, mwenyekiti etc etc....nadhani waafrika tunatakiwa kuwa na akili ya kujua kuwa ni lazima tuwe na njia inayoweza kutuendeleza
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
NI KWANINI WANAMTUKANA NA KUMSIFIA NYERERE HAPO HAPO?

Mkuu Rev. Kishoka
Katika mjadala huu naomba nizungumzie mada yako kwa namna nyingine ambayo kwa kiasi fulani inafedhehesha

Siku hizi imekuwa ni kawaida kusikia watu wakiongelea '' Awamu' hii imejenga vituo vingi vya afya kuliko Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwa pamoja.

Ni hoja inayoonekana kuwa ''zungumzo' na imepangwa izungumzwe hivyo.

Wanozungumza hoja hii ni watu wenye ufahamu na weledi na hilo linaacha mwaswali kama wanafanya kwa kutojua au kwa kujua hasa tukizingatia weledi wa wengi wa wananchi wetu.

Ni upotoshaji uliokithiri usiozingatia takwimu wala mantiki unaolenga hadaa na si ukweli.

Rais mstaafu Mwinyi aliwahi kusema '' yeye hawezi kuvaa viatu vya Mwl Nyerere'' na akasema pia ''Kila zama na kitabu chake'' Maneno haya yana maana sana na sijui wanaoeneza uvumi wa vituo vya afya wanayakumbuka au kuyajua.

Niongelee zama za Nyerere ambaye kwa mtazamo wangu kauli za vituo vya afya ni kumtusi hadharani

Mwl akichukua madaraka ilikuwa zama yake na kitabu chake.
Mwl hakuwa katika nafasi yoyote ile inayolingana na waliomfuata, alianza kujenga msingi si kuezeka paa.

1. Idadi ya watu wakati wa Uhuru ilikuwa milioni 9. Alikuwa na Daktari wa tiba mwenye sifa hiyo mmoja.

Sijui kama alikuwa na Engineer zaidi ya wawil. Hakuwa na mwanasheria hadi kuazima mwanasheria mkuu kutoka nje.

Mwl hakuwa na watalaamu wa kada za kati na chini. Nchi ilikuwa haina vyanzo vya nishati kama mabwawa ya umeme.

Hatukuwa na mfumo wa kusambaza maji. Mwalimu hakuwa na viwanda zaidi ya mashine ndogo ndogo.

Hakuwa na chuo kikuu hata kimoja. Barabara hazipitiki wakati wa masika. Reli iliyokuwepo ni ya kati na kaskazini

Orodha ni ndefu na inaweza kujaza kurasa na kurasa ikionyesha changamoto alizoanza nazo Nyerere akiwa na watu milioni 9, Taifa changa lililopata uhuru.

Taifa lilihotaji kuwekwa pamoja ili kuwa na utangamano kuelekea maendeleo.
Watu hawajui kwamba Mwl aliteua hata madereva kuwa wakuu wa Wilaya achilia mbali taasisi nyingi.

Katika changamoto hizo Mw alikuwa aanze na ipi?Mwl aliyachukua mambo yote kwa pamoja hatua kwa hatua

2. Nyerere alikuta chanzo cha umeme cha Pangani, akajenga Nyumba ya Mungu na Kidatu ili tupate nishati ya uhakika
3. Mwalimu akaanzisha vyuo vya elimu ili kupata walimu wa kuliemisha taifa. Mtakumbuka Ngumbaru ili at least watu waweze hata kuandika majina yao.
4. Mwalimu akajenga vyuo vya chini vya afya (RMA), Medical assistant, Assistant medical office (AMO)
5. Mwl akajenga vyuo vya chini na kati vya kilimo na ufundi
6. Mwl akajenga chuo kikuu cha kwanza nchini kilichotoa viongozi wengi sana wakiwemo wa Tanzania ya leo
7. Akajenga barabara kuu za lami kama Segera-Chalinze ili kurahisha usafiri
8. Ni Nyerere peke yake aliyejenga reli hadi leo(TAZARA). Hizi zinzokarabatiwa hazijengwi upya
9. Alijenga reli ya Mruazi-Ruvu kurahisha mawasiliano ya reli nchini
10 Akajenga viwanda watu walikwenda ''shift' kama nchi zilizoendelea si kukaa Bar ikifika saa 10 Jioni kama leo
11.Mwalimu akajenga Hospitali ya rufaa na kutafuta watalaam
12. Akajenga vyuo vya ulinzi na usalama kama Monduli n.k.
13. Mwalimu alitoa elimu bure hadi kulipia wanafunzi nauli. Hiyo ndiyo elimu bure aliyotoa Mwl
14. Mipango ya usambazaji maji ilikuwa inaendelea kote nchini( Someni mipango ya maendeleo 1963, 1967 n.k.)

Orodha inaendelea na hayo hapo juu ni kwa ujumla wake tu. Tukianza kuchambua kwa undani orodha itapanuka sana

Yote haya Mwl aliyafanya katika mazingira magumu sana, akiwa na watu milioni 9, watalaam 0

Laiti Mwl asingejenga reli ya Tanga au Tazara akaelekeza nguvu katika vituo vya afya basi tungekuwa na vituo vya afya kila nyumba 10.

Lakini Mwl alikuwa anawaza, je, ajenge vituo vya afya bila watalaamu na vifaa ?
Zama zake vituo vya afya vilikuwa na magari kwa ajili ya referal ikibidi. Je, ndiyo hali iliyopo leo?

Lakini pia lazima tuangalie mambo kwa kutumia akili.
Hivi wakati wa population ya milioni 9 kulikuwa na sababu ya kuwa na vituo vya afya 300 kama leo tukiwa na 55 milioni? Rationale ya kwamba alijenga vituo vya afya vichache inatoka wapi?

Vituo vya afya havijengwi tu kwasababu ya ku score political point, vinajengwa kutokana na mahitaji.
Hitaji la vituo mwaka 1961 ni tofauti na 1970 au 1980 au 2000 au 2019 kutokana na ongezeko la watu.

Hoja kwamba Nyerere hakujenga vituo kama leo ni tusi. Watanzania wanaomuenzi Mwl kwa dhati wakemee tusi hili.

Kazi ya Mwl Nyerere ilikuwa ngumu na nzuri bila kupepesa. Kumlinganisha Mwl na kiongozi mwingine ni kumtukana

Tena Mwl akawa ''Bold and Daring'' kwa kutaifisha Hospitali za watu na shule ili kujenga Taifa la pamoja na kuondoa matabaka. Leo hatuoni kazi hiyo. Mwl hakuwa na resource za kutosha akachukua maamuzi magumu kabisa.

Nyerere alikuwa bold and daring kwa kila kigezo. Nchi hii ilipotoka na ilipo leo si vitu vya kulinganisha hata kidogo.

Kinachosikitisha wanaomtukana Mwl Nyerere kwa vituo vy fya kama ilivyo leo bila mantiki ni hao hao wanaomsifia pale wanapotaka kuungwa mkono.

Tuache kumtukana Mwl Nyerere kwa hoja laini zisizo na mashiko za vituo vya afya.

Kazi ya Mwl ilikuwa kubwa, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Acheni kabisa kulinganisha kazi za Mwl, mnamtusi
Tukianza kuweka kazi za viongozi katika mizani. tutaishia kudhalilishana bila sababu.

Anayedhani kuwa ni wakati wa kumweka Mwl katika mizani na kiongozi mwingie tafadhali aje hapa tuongee!!!
 
Waswahili wanasema: "Kizuri chajiuza, kibaya Chajitembeza!'
 
LUSAJO L.M.

Verified Member
Aug 21, 2007
248
225
Reverend,

Asante kwa kutuletea amani tena.

Magufuli ana mapungufu kadhaa katika uongozi wake lakini ni kiongozi thabiti anayejua kusimamia analoamini. Hiyo ni sifa nzuri sana. Kuwa kiongozi mzuri siyo lazima uwe unafanya yanayofurahisha wayu tu, wakati mwingine hata yale yasiyofurahisha watu mradi tu yana malengo mazuri. Zamani sana Nyerere alitoa mfano wa mgonjwa wa Malaria anayeota jua: ukilazimisha kwenda kivulini, atachukia lakini hiyo ndiyo hatua inayomsaidia mwili wake. Magufuli kwa kiasi fulani amelazimisha wagonjwa wa Malaria kwenda kivulini
Uthubutu ni jambo moja, lakini katika uongozi tunafahamu ya kwamba kila nafasi ina ukomo wake. Uthubutu unaoonyeshwa na Rais Magufuli katika mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa nchi na uelekeo wetu kama Taifa ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ambayo yatachukua si tu viongozi wenye uthubutu kufanikiwa, lakini pia muda mrefu na inawezekana kabisa kuwa kilele cha mafanikio hayo kitaonekana wakati wa vipindi vijavyo vya utawala.

Najaribu kuangalia 'continuity plan' ya uthubutu wa Mh. Magufuli na nabaki na jibu moja tu; safari ya kurudi pale tulipotoka kabla ya Magufuli. Wakati yeye anaonyesha uthubutu, asilimia kubwa ya waliomzunguka, wambao wanaandaliwa kuwa viongozi baada ya wakati wake kumalizika wamekuwa ni watu wa kutukuza tu yale yanayofanywa na Mh Rais lakini sio wafuasi wa falsafa za Jiwe.

Nani atathubutu baada ya Magufuli?
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,544
2,000
Du, nasikiwa watu sasa wana 'uthubutu' hadi wa 'kudukua' na 'kuiba' tarakilishi za DPP!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Uthubutu ni jambo moja, lakini katika uongozi tunafahamu ya kwamba kila nafasi ina ukomo wake. Uthubutu unaoonyeshwa na Rais Magufuli katika mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa nchi na uelekeo wetu kama Taifa ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ambayo yatachukua si tu viongozi wenye uthubutu kufanikiwa, lakini pia muda mrefu na inawezekana kabisa kuwa kilele cha mafanikio hayo kitaonekana wakati wa vipindi vijavyo vya utawala.

Najaribu kuangalia 'continuity plan' ya uthubutu wa Mh. Magufuli na nabaki na jibu moja tu; safari ya kurudi pale tulipotoka kabla ya Magufuli. Wakati yeye anaonyesha uthubutu, asilimia kubwa ya waliomzunguka, wambao wanaandaliwa kuwa viongozi baada ya wakati wake kumalizika wamekuwa ni watu wa kutukuza tu yale yanayofanywa na Mh Rais lakini sio wafuasi wa falsafa za Jiwe.

Nani atathubutu baada ya Magufuli?
Mafunzo mazuri duniani ni ya vitendo; historia ya mapokeo ineonyesha kuwa wazee wa zamani walikuwa wakiwapokeza watoto wao kwa kuwaonyesha jinsi ya kufanya mambo, Watoto wenye akili walirithi, na watoto wasiokuwa na akili hawakuriti; kupokewa au kutopokewa siyo jukumu la mzee, bali ni jukumu la warithi. Kupokea huwa siyo 1-1, bali ni kuchukua mazuri yote na kuboresha yale yaliyokuwa na mapungufu. Tanzania tunajua kuwa waliomfuata Nyerere hawakutaka kupokea bali walianza yao, na waliofuata nao wakaanza yao, na ikawa vivyo hivyo; historia ina heshima yake katika jamii. Iwapo kiongozi atakayefuata ataamua naye kujianzishia ya kwake kama waliomfuata Nyerere basi, tatizo siyo la kiongozi aliyetangulia bali linakuwa ni la jamii yetu sisi wenyewe kutotaka uthubutu. Katzi ya kiongozi nji kuonyesha njia, siyo kufundisha watu jinsi ya kufuata njia hiyo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom