The Daring and Bold Magufuli

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Kama kuna kitu cha wazi ambacho ni funzo kubwa kwetu Watanzania katika miaka minne hii ya Awamu ya Tano na "Utawala" (maksudi kabisa badala ya kutumia uongozi) wa Magufuli ni UTHUBUTU!

Uthubutu, ni uwezo wa kufanya mambo bila kuwa na kigugumizi au kujishuku. Ni kufanya mambo, kusimamia unaloliamini bila kujali au bila woga. Sasa kwa Magufuli ambaye tulijua akiwa waziri alikuwa ni mchapakazi mpaka kuitwa bulldozer, ilimaanisha alifanya mambo jinsi alivyoona ni sawa kwa nafasi yake na sasa kwa kupata Urais n kuwa Rais wa Jamhuri, basi Ari, Kasi na Nguvu zake za kuwa Bulldozer na uthubutu zimeongezeka maradufu.

Uthubutu si lazima tuutazame kwa matokeo chanya pekee, hata matokeo hasi yanaweza kutokea kutokana na mtu kuwa na uthubutu, kudhamiria na kufanya lile alilokusidia.

Rais Magufuli ametusaidia sana kutuonyesha kwa vitendo, na si semi, kauli au porojo kuwa kwenye nia pana njia.

Naam, kuna maamuzi mengi yaliyotokana na Uthubutu huu yameleta maswali mengi na hata matokeo ya "uthubutu" kuonekana kama hatua ambazo zilikosa weledi, busara, uhakika au hata hekima. Lakini cha msingi kwa andiko langu hili si kukosoa au kusifia mafanikio au kushindwa kwa maamuzi aliyoyafanya, la hasha... naangalia silika ya kibinadamu ya kuwa na uthubutu, Daring!

Nakumbuka miaka 10 ya Rais Kikwete, uongozi au utawala wake ulionekana umepwaya kwa kukosa Uthubuu wa ukali na kusimamia mambo yafanyike, bila kujali matokeo. Nakumbuka mgombea wa Urais 2015 Bwana Lowassa alinukuliwa mara kadhaa akisema Tanzania inahitaji mtu mwenye kufanya maamuzi magumu, na Watanzania ule u-soft soft wa awamu ya nne, ulitufanya tutake kupata mtu "Dikteta" kauli na nadharia ambazo kwa umoja wa Kitaifa bila hata chembe ya tofauti za kisiasa ai itikadi, ilikuwa ni "natural" kukubali uhitaji wa kuwa na Rais Mkali, Dikteta!

Magufuli kathibitisha katika uanadamu kuwa Uthubutu si jambo la kusadikika, bali li jambo la kweli, lina uhai na kila mtu akikusudia na kujiamini, anaweza kuwa na Uthubutu!

Nikiiangalia Tanzania ilipo leo hii, miaka 58 tangu tupate Uhuru ambapo bado tuko kwenye hatua za mwanzo za kujaribu kupiga vita Ujinga, Umasikini, Maradhi, Unyonge na Utegemezi (UUMUU)pamoja na kutamka kwa vinywa vyetu mahitaji ya maendeleo ya taifa kuwa ni Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, sifa, hulka na wajihi wa kuwa na Uthubutu bado ni mchanga sana na ndio chimbuko la kukosa kujiamini, kuwa wanyonge na waoga kufanya maamuzi magumu.

Kuna dhana na falsafa inayosema fanya jambo, lisipozaa matunda chanya au uliyotegemea-matokeo hasi yanakupa fursa kurudia mchakato na kujifunza pale ulipokosea na kurudia jambo kwa ubora na umakini zaidi. Cha msingi ni kujiamini na kuwa na uthububu wa kufanya mambo.

Sasa kwa Tanzania yetu ya leo "Ya Magufuli" ya "MATAGA" na "CCM Mpya" utegemezi wa mwenye kujiamini na mwenye kuthubutu kumebakia kuegemea na kumtegemea mtu mmoja, Rais Magufuli. Wengine wote wamekaa kando wakishangilia na kusifia lakini hawana Uthubutu wa kwao wa kujitegemea na kwa nafsi zao bila kutegemea na kuzengea Uthubutu wa magufuli ambao sasa umeambatana na mamlaka na dhama kubwa kama Rais wa nchi.

Tumeshuhudia watendaji wa Serikali na Wanasiasa ambao wana majukumu ya kuongoza nchi, wakigeuka kuwa Wanyapara, wasiojiamini, wakitegemea sana UDola wa Kimamlaka na zaidi turufu yao kubwa ni kusema "maagizo kutoka juu" wakimaanisha ni maelekezo na maagizo ya Magufuli, wakikimbilia kuutegemea Uthubutu wa Magufuli kama ngao na nguzo.

Nasi wananchi ambao hatuna mamlaka au dhamana ya kiuongozi au madaraka, nasi tumekaa kando kwa unyonge au kuachia kila kitu kifanywe na kuamini na kutegemea "ah Magufuli ni kiboko".

Leo haki ya mwananchi inakanyagwa na kupuuzwa, tunakosa Uthubutu wa kudai haki na kusimama imara kukataa kuburuzwa. Ndio kuna hofu na mazingira ya kutishiana ambayo yanatufanya kukosa kujiamini, lakini kwa nini hatumtazami Magufuli yule aliyekuwa Waziri ambaye alisimama na kupata alichotaka na kudhamiria mpaka tukamsifia kwa ujenzi wa miundo mbinu Tanzania?

Nimesema awali, Uthubutu si lazima uzae matoke chanya (ambayo yanaweza kuwa ni mtazamo wa mtu, kikundi au wa aina moja au nyingine) au matendo yanayotikana na Uthubutu yapokelewe kwa mikono miwili na kila mtu. Lakini laiti kama kila mmoja wetu kwa miaka 58 tangu tupate Uhuru wetu tungekuwa na utashi, uimara, ujeuri, kujiamini na uthubutu hata kwa asilimia 50% a uthubutu wa Magufuli, si ajabu Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye maendeleo yake ya uchumi, kupanuka na kukomaa kwa haki za watu na yote ambayo tunanung'unikia leo, si ajabu yasingekuwa manung'uniko au kero za kutukosesha raha.

Nikiangalia na kupima Uthubutu wa Magufuli, kuna mengi kafanya (kutenda si lazima kuwe ni sifa ya kufanikiwa jambo) kwa kuamua. Ama ni kutoa maagizo, kuamrisha na kusimamia kikafanyika bila kujali matokeo (consequences or final result) au kuangalia hisia za watu. Mfano, aliazimia kupanuliwa kwa barabara, kukafanyika ubomoaji ili kupisha upanuzi wa barabara hata njia ya reli ya SGR. Hakusubiri majadiliano ingawa yawezekana kukawa na gharama kubwa kwa maamuzi hayo hasa pale penye malalamiko ya fidia.

Akaamua kununua ndege kwa fedha taslimu, zimenunuliwa ndege 5 kwa mkupuo tena kwa fedha taslimu bila kuwa na ukiritimba ambao Serikali na ATCL walifanya kwa miaka 20 kabla ya Magufuli kuboresha au kuwezesha Shirika la ndege kuwa na ndege za kutosha (wengi mtakumbuka ndege za Mattaka). Akasitisha mazoea ya kusafirisafiri ya viongozi na watendaji wa Serikali bila kujali kama kulikuwa na umuhimu wa uwepo na uwakilishi wetu au la, lakini amri yake ilisikilizwa kwa kuwa alisema atatumbua. Leo tumeona Chato inajengwa kwa kasi kubwa; iwe ni maagizo, amri au watu "kujituma" kuhakikisha Chato inakuwa na hadhi kubwa na sasa inageuka kuwa kivutio cha biashara na utalii. Akasema kufanyike uhakiki wa vyeti, wa wafanyakazi wa Serikali, nayo yakatimia. Akasema lazima kila mtu apate stakabadhi akinunua bidhaa ili Serikali ipate mapato... leo kila mtu anahangaika kuwa na stakabadhi! Akasema lazima tuhamie Dodoma, iwe kumekamilika au la, watu wakahamia Dodoma, wengine ofisi ziko kwenye vibanda na wanakaa vyumba vya kupanga.. lakini Serikali imehamia Dodoma.

Sasa najiuliza, sisi kilitushinda nini miaka yote kufanya maamuzi kama haya?ni kigugumizi gani kilitushika kwa muda mrefu kufanya mambo na kuwa na uthubutu, bila kuwa na woga au kujiumauma? kwa nini tuliamini hatuna uwezo wa kufanya mambo kwa hiari lakini tunafanya sasa kwa kuamrishwa na ni sawa na kwamaba tunachapwa mijeledi, tunazinduka na kufanya?

Leo nina uhakika Magufuli akisema tunarasimisha Katiba ya Wananchi iliyotokana na Rasimu ya Warioba, litafanyika bila kupingwa au miguno. Sheria kadhaa na miswaada imepelekwa bungeni na "Chama tawala" ama kwa woga, unafiki au labda ukweli halisi kimepigia kura na kupitisha kila kilichopelekwa na Serikali ya awamu ya tano. Rais Magufuli leo akisema ni marufuku kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa, hakuna atakayebisha.

Sasa ni rahisi kusema yeye ana mamlaka makubwa na anatumia cheo chake, lakini ukweli unabakia kuwa anayafanya kutokana na Uthubutu, daring.. hata kama mara nyingine ni kiholela (reckless) au ni kishari (mercilessly), but he gets shit done regardless.

Je sisi wote tungeanza kujiamini na kuanza kuwa na uthubutu bila woga kufanya mambo tunayoamini ni haki yetu kikatiba, ni wajibu wetu kusimama kuyapigania. Iwe ni nyumbani, makazini, kwenye masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiuzalishaji na kila jambo, uwe ni mfanyakazi, mwajiri, mfanyabiashara, mwanasiasa.. tukiwa wote na uthubutu, na tukafanya maamuzi kwa umakini lakini tukisimama imara kwa uthubutu, basi Tanzania ya Viwanda na Gurudumu letu la maendelo litapiga hatua kubwa na za haraka sana.

Lakini tukiendelea kwua Wategemezi wa magufuli, siku anaondoka tutarudi kule kule, kukwama matopeni na hata kuwa na mawazo potofu ambayo yanajengwa sasa hivi kusema tunahitaji Magufuli akae zaidi ya muda ulioko kwenye katiba.

Namshukuru sana kwa kutuonyesha Uthubutu, tuungane, tusimame imara tufanye mambo kwa uthubutu kupata haki zetu na maedneleo ya kweli na endelevu.

Ahsante Rais Magufuli kwa kutufundisha Uthubutu! Daring, Boldness.. Get Shit Done attitude!
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
Sikiliza ndugu, Spika wa Bunge ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM
Sasa sijui unataka watu waeleze nini zaidi. Huwezi kutenga Bunge na serikali kwa hali ilivyo sasa.

Again tusidanganyane hapa.

Bajeti huandaliwa kulingana na Ilani ya chama inayotarishwa na wanasiasa kukidhi ahadi za uchaguzi.Wataalam wanahusika sehemu za kiuchumi lakini mwelekeo mzima wa Bajeti ya Bunge letu ni siasa tu.

Hata wenyewe husema, wanatekeleza ilani ya chama na kwamba bajeti imelenga ''Wanyonge'' .

Wataalam hutengeneza bajeti kutokana na takwimu, si hapa kwetu.Sisi ni siasa
Sikuelewi kabisa, unaweza kuwa na mahaba na serikali lakini yasikufikishe hapo

Unaamini kwa dhati kwamba bajeti inaandaliwa na Watalaam na kwamba hakuna siasa! real, seriously. Hao watalaamu ndio waliosema Geita halafu wakaja kuomba pesa bila kujua wanajenga nini na wapi. Baada ya hapo wakahamisha uwanja kitalaamu. Please Kwa hili, I rest my case.
Kwa faida ya wasomaji unachotaka kuwaaminisha ni kuwa data za kweli zinatoka serikalini.
Kwamba, watu wanaopika data leo wanageuka kuwa source.
Hivi unafikiri mswada wa takwimu, kwamba, zipatikane NBS ni bahati mbaya!
Hivi unaijua IMF!
Hawa ni habari nyingine, hawasubiri kusoma data za NBS. Hawa ndio dunia siyo NBS, Please
Hao watalaamu wetu wanaweza kuitwa na kuambiwa waseme 9%. Nani atakataa!
Nguruvi3;

When the government prepares its budget, there are a lot of variables that go into it. And Ilani ya chama is a very small part of it. First, the government has to cover its operational costs such has paying salaries of employees, maintaining government building, maintaining transportation fleets etc etc. Regardless of who's in power, the government will incur these costs.

Second, there are costs to cover development projects such as the costs to build new schools, bridges, hospitals, airports etc etc. Here's where Ilani za Chama can find the funding. The thing to remember here is the development projects always come after the government covers its operational costs and can be scrapped at any given time.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32417173, member: 348"]Halafu bajeti kuwa na siasa ndani yake ni mambo yanayofanyika duniani kote;
Thank you! you concur with me
wanasiasa wanaleta malengo yao, wataalamu wanapanga bajeti, halafu inawezekana wanasiasa wakachomekeza vitu vyao. Ndivyo ilivyo duniani kote; kwa Marekani nadhani unazijua hizo terms wanazoita pork barrel na earmarks kwa ajili hiyo.
Siyo kwamba inawezekana, ndivyo ilivyo hasa nchi zetu masikini ambapo siasa mbele uchumi baadaye

Hapo ndipo ninaposema kuwa usipoamini data za serikali basi usiamani data za institution yoyote.
Absolutely! Labda nikukumbushe kidogo
Taasisi yenyepublic trust kama Police inapokosa credibility unadhani taasisi gani itaaminiwa?

Tulipewa takwimu Mwangosi RIP alipigwa na kitu chenye ncha kali.
Video ilipotoka police walimlipua halafu wakafanya cover up
Katika kushadidi hilo Rais akawaambia Police ''msidhani wananchi ni wajinga''
Orodha inaendele kura zaidi ya 100

Mswada wa takwimu ulipelekwa kwa dharura kisa kuna shirika limetoa data likionyesha CCM inapoteza umaarufu. Hicho ndicho chanzo cha kuzuia taasisi nyingine binafsi

Baada ya hapo hakuna takwimu kutoka NBS kuhusu hali ya kisiasa. Hawaruhusiwi na wakifanya watatumbuliwa. Huwezi kuwa na taasisi kama NBS inayomilikiwa na serikali halafu ukategemea iwe huru. Hata siku moja takwimu zao siziamini, hakuna credibility kwa taasisi zetu
Sijajua motive ya serikali kupitisha sheria ya takwimu, lakini nadhani pia ilikuwa ni kudhibiti watu kutoa namba zao zisizokuwa sahihi na kuzisambaza.
Hapa unakosea, kama hujui motive basi huwezi kuongelea namba zisizo sahihi
Nimekuambia kuhusu taasisi ile ambayo kiongozi wake alizuiliwa

Motive ni rahisi, kwamba, baadhi (mimi simo) waimbe nyimbo zinazotakiwa
Na hili ni kosa kubwa sana. Hata kama akina Zitto wanapotosha, bado wataaminika kwasababu ndiyo mbadala na kwamba taasisi za umma hazina credibility
Kwahiyo kilichofanyika ni self inflicted wound

I would rather be curious with Zitto's data than NBS.
Nadhani unajua kuwa hata marekani data za uchumi hutotolewa na institution moja tu; rais anaweza azakazimeza au akazitema hiyo ni shauri yake.
Trump alikataa wakati wa Obama, Taasisi zikaendelea na mjukumu yake kwasababu zipo kwa masilahi ya Taifa na si Trump. Hadi leo kuna wakati anakubali kuna wakati anakataa, hilo haliyumbishi taasisi hizi
Tofauti na hapa kwetu, Trump au yoyote yule hawezi kufanya lolote ikiwemo kuwatimua wahusika. Hapa ndipo hoja ya taasisi huru inapokujaElewa kuwa hawana makarani wakusanya data za uchumi wa nchi kutoka kila kona ya nchi; hawatozi kodi, hawana maofisa wa forodha kujua ni nini kimeingia nchini na ni nini kimetoka nje. Hupata raw data kutoka serikalini.
Hawahitaji makarani wala ofisi, wapo na wanafanya kazi zao. Muulize Osama
Narudia tena hizi si taasisi weakened and dysfunctional kama zetu.
Ni taasisi zenye wataalamu wanaoweza kukaa Washington wakakueleza nini kimetokea Buguruni. Balozi unazoziona si vyumba vya kutoa Visa, kuna wafanyakazi wenye kazi zao
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
Mzuvendi na Kichuguu

Hizi taasisi za kimataifa na za magharibi si kama taasisi zetu hapa nyumbani
Kazi za IMF ni kubwa si uchumi tu inatumiwa katika usalama na ulinzi

Mzuvendi, hao classmate wake walitumika kama camouflage, kuna watu wanaijua nchi yetu na wapo kazini.

Kwa wale waliokuwepo, baada ya vita 1978 IMF ilieleza hali ya uchumi wa Tanzania miaka 10 inayofuata. Watu walidhani ni hadithi, walioishi nyakati hizo wanajua
Nakumbuka walisema hivi ''vitu vipo madukani kwa sasa, lakini baada ya muda hali itakuwa mbaya sana'' . Je hayakutokea?

Huwezi kufafananisha taasisi yoyote ya ndani na kazi za IMF hata kwa 10%

Baada ya shambulio la Dar na Nairobi, hakuna aliyejua nini kimetokea na nani walishiriki

Well, walikuja FBI ambao hata siku moja hawakuonekana, wakaenda kwenye nyumba hadi Bomu lililpotengenezwa. Apparently, hawakuwa na ''mwakilishi wala mkusanya data au taarifa''
Vyombo vyetu vya ndani vilibaki na mshangao tu bila kujua nini kinaendelea.

Kwahiyo mkae mkijua IMF na World Bank si wakusanya data za korosho, ni zaidi ya hapo na kwamba uchumi kwao ni security.

Hawa wanajua uchumi wa dunia miaka 2 au 3 ijayo, sisi hatujui hata ku forecast makusanyo ya TRA miezi 6 halafu mtuambie eti wanategemea data zetu, please
We are digressing now. Aren't we? We are going back to 1978. Anyway, I will put my two cents there. First of all, the economy of Tanzania was already going downward well before Uganda's war. After the war, I used to believe whatever cr@p Nyerere and his buddies put out as the status of the economy. However, as I got older and started digging the number, I came out with a different conclusion.

I can go deeper, but then I will be digressing. But let me give you a glimpse of the situation, and from there you will decide what to believe. Here's the thing. By the end of 1979, majority of free African countries were in severe recession or approaching it. Those who followed capitalism were in bad shape. So did those who followed socialism. So, the question is how could Tanzania alone recover, when the entire African continent was in economic crisis?

What was worse, the economies of developed countries such as UK and US were in recession too. The reason Reagan and Thatchter were elected was that the economies of their respective countries were soo bad. The question is how could the economy of Tanzania have recovered when the donors who help Tanzania were in recession?

To me I think the main problem was us. I think after we won the war, we became overconfident and overestimated our own capabilities. Zambia was in a better shape economically than any other country in our region. In 60s, economically it was near the Asian Tigers. If Zambia couldn't recover it, why Tanzanians thinks they have done it. What was special about us? Ujamaa?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Nguruvi3;

When the government prepares its budget, there are a lot of variables that go into it. And Ilani ya chama is a very small part of it. First, the government has to cover its operational costs such has paying salaries of employees, maintaining government building, maintaining transportation fleets etc etc. Regardless of who's in power, the government will incur these costs.

Second, there are costs to cover development projects such as the costs to build new schools, bridges, hospitals, airports etc etc. Here's where Ilani za Chama can find the funding. The thing to remember here is the development projects always come after the government covers its operational costs and can be scrapped at any given time.
Mzuvendi, I agree,however you missed a point of contentions.
Kichuguu asserts that the budget is prepared solely by the experts without any political influence. Later on he changed the position to concur with my argument. That's it

Kichuguu wants to convince the mass that Chato project leaves nothing to be desired, and that, the onus lies squarely on the shoulder of ''experts'' without political machinations.Not true!
The fact is, there was political machinations coerced the experts to act under duress
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mzuvendi na Kichuguu

Hizi taasisi za kimataifa na za magharibi si kama taasisi zetu hapa nyumbani
Kazi za IMF ni kubwa si uchumi tu inatumiwa katika usalama na ulinzi

Mzuvendi, hao classmate wake walitumika kama camouflage, kuna watu wanaijua nchi yetu na wapo kazini.

Kwa wale waliokuwepo, baada ya vita 1978 IMF ilieleza hali ya uchumi wa Tanzania miaka 10 inayofuata. Watu walidhani ni hadithi, walioishi nyakati hizo wanajua
Nakumbuka walisema hivi ''vitu vipo madukani kwa sasa, lakini baada ya muda hali itakuwa mbaya sana'' . Je hayakutokea?

Huwezi kufafananisha taasisi yoyote ya ndani na kazi za IMF hata kwa 10%

Baada ya shambulio la Dar na Nairobi, hakuna aliyejua nini kimetokea na nani walishiriki

Well, walikuja FBI ambao hata siku moja hawakuonekana, wakaenda kwenye nyumba hadi Bomu lililpotengenezwa. Apparently, hawakuwa na ''mwakilishi wala mkusanya data au taarifa''
Vyombo vyetu vya ndani vilibaki na mshangao tu bila kujua nini kinaendelea.

Kwahiyo mkae mkijua IMF na World Bank si wakusanya data za korosho, ni zaidi ya hapo na kwamba uchumi kwao ni security.

Hawa wanajua uchumi wa dunia miaka 2 au 3 ijayo, sisi hatujui hata ku forecast makusanyo ya TRA miezi 6 halafu mtuambie eti wanategemea data zetu, please
Hiyo imani yako ya kuwa IMF na World Bank wanajua uchumi ujao bila data zozote ni potofu kabisa; wanahitaji sana za uchumi za dunia nzima, na vile vile maenedleao ya kisiasa ya dunia nzima. Ni kwa vile siwezi kushusha hapa data za world bank katika excel ungeona wana data nyingi sana ambazo zote zimetoka serikalini. Forecasting ni procedure ya kawaida sana katika management ya organzaition yoyote. Hata kwenye bajeti za tanzania wanaposema serikali inategemea kukusanya mapatao kadhaa, ni kwa sababu ya forcaseting. Inawezekana kabisa kuwa forecastig iinaweza ikapatia iwapo hali ya dunia haitabadilika, au ikakosea. Economic outlook yoyote itolewayo na IMF huwa haina maana kuwa ni kweli kabisa; wakati mwingine huathiriwa na mambo ambayo hawakutegemea kwa mfano vita, au ukame, au ugunduzi wa jambo fulani linaloathiri uchumi kwa mfano ugunduzi wa mafuta au uOPEC kupandisha bei ya mafuta unilaterally.

Angalia mifano hii kuonyesha kuwa hizo forecasting zao siyo solid kama unavyodhani
1565249909908.png

1565249788839.png

Elewa kuwa IMF zilianzishwa ilianzishwa ili kudhibdi uchumi wa dunai na kuextend influence ya nchi za magharibi duniani. Kiongozi wa IMF anachaguliwa na Rais wa marekaneni halafu yule wa World bank anachaguliwa na nchi za EU.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mzuvendi, I agree,however you missed a point of contentions.
Kichuguu asserts that the budget is prepared solely by the experts without any political influence. Later on he changed the position to concur with my argument. That's it

Kichuguu wants to convince the mass that Chato project leaves nothing to be desired, and that, the onus lies squarely on the shoulder of ''experts'' without political machinations.Not true!
The fact is, there was political machinations coerced the experts to act under duress
Sasa mzee unaanza kupotosha post zangu; hivi kweli umesoma hii niliyokuweka hapo juu? Kuhus bajeti nimesema hivi

1565250800985.png

Politicians hawawezi kuforce kuwa kwa mwaka huu tukamilishe tujenge mradi fulani unaohitaji pesa ambazo nchi haina uwezo nazo halafu ukaingia kwenye bajeti kweli. Nilikuwa na rafiki zangu pale hazina mmoja alikuwa Mchumi na mwingine alikuwa CPA walikuwa wanashughulika na mambo ya bajeti full time, yaani mwaka mzima.

Kuhusu uwanja wa Chato usituumize sana kichwa; ninajua kuwa miaka kumi ijayo unaweza kuwa sawa kabisa na ule wa Mobutu kule Gbadolite. Ila ninachosema ni kuwa umejengwa kwa kuidhinishwa na Bunge siyo kuwa umejengwa kinyemela
kinyume na bajeti ya Bunge kama watu wanavyodai; I hope umesoma post yangu hii hapa hapo nyuma.

1565251046643.png
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Thank you! you concur with me
Siyo kwamba inawezekana, ndivyo ilivyo hasa nchi zetu masikini ambapo siasa mbele uchumi baadaye

Absolutely! Labda nikukumbushe kidogo
Taasisi yenyepublic trust kama Police inapokosa credibility unadhani taasisi gani itaaminiwa?

Tulipewa takwimu Mwangosi RIP alipigwa na kitu chenye ncha kali.
Video ilipotoka police walimlipua halafu wakafanya cover up
Katika kushadidi hilo Rais akawaambia Police ''msidhani wananchi ni wajinga''
Orodha inaendele kura zaidi ya 100

Mswada wa takwimu ulipelekwa kwa dharura kisa kuna shirika limetoa data likionyesha CCM inapoteza umaarufu. Hicho ndicho chanzo cha kuzuia taasisi nyingine binafsi

Baada ya hapo hakuna takwimu kutoka NBS kuhusu hali ya kisiasa. Hawaruhusiwi na wakifanya watatumbuliwa. Huwezi kuwa na taasisi kama NBS inayomilikiwa na serikali halafu ukategemea iwe huru. Hata siku moja takwimu zao siziamini, hakuna credibility kwa taasisi zetuHapa unakosea, kama hujui motive basi huwezi kuongelea namba zisizo sahihi
Nimekuambia kuhusu taasisi ile ambayo kiongozi wake alizuiliwa

Motive ni rahisi, kwamba, baadhi (mimi simo) waimbe nyimbo zinazotakiwa
Na hili ni kosa kubwa sana. Hata kama akina Zitto wanapotosha, bado wataaminika kwasababu ndiyo mbadala na kwamba taasisi za umma hazina credibility
Kwahiyo kilichofanyika ni self inflicted wound

I would rather be curious with Zitto's data than NBS. Trump alikataa wakati wa Obama, Taasisi zikaendelea na mjukumu yake kwasababu zipo kwa masilahi ya Taifa na si Trump. Hadi leo kuna wakati anakubali kuna wakati anakataa, hilo haliyumbishi taasisi hizi
Tofauti na hapa kwetu, Trump au yoyote yule hawezi kufanya lolote ikiwemo kuwatimua wahusika. Hapa ndipo hoja ya taasisi huru inapokujaHawahitaji makarani wala ofisi, wapo na wanafanya kazi zao. Muulize Osama
Narudia tena hizi si taasisi weakened and dysfunctional kama zetu.
Ni taasisi zenye wataalamu wanaoweza kukaa Washington wakakueleza nini kimetokea Buguruni. Balozi unazoziona si vyumba vya kutoa Visa, kuna wafanyakazi wenye kazi zao
Kuna mambo mawili hapa ninataka kuaddress; mengine hayana haja kwa sababu kwa kiasi kikubwa tunakubaliana.

(1) Imani ni haki ya kila raia; una haki kabisa ya kukosa imani na data za serikali, lakini elewa kuwa data zinazotumiwa na IMF pia zinatoka serikalini. Kuna mafaili makubwa sana ya excel yenye namba za kutoka sehemu mbalimbali. na wanapokuwa hawakupata ushirikiano na serikali basi wanaacha nafsi hizo wazi. Nilikuwa interested na inflation ya tanzania nikaipata kwenye faili hili; angalia kuwa nafasi ya Afghanistan kwa mwaka 2019 iko tupu, pamoja na kuwa jeshi la marekani liko kule miaka 18 sasa; vile vile nafasi za Andorra, Argentina, Tuvalu, na nchi nyingine kadhaa nilizofunika hawana data. Wangekuwa na uwezo huo wa ajabu wa kuweza kujua kila kitu kuhusu kila nchi kusingekuwa na mapengo kama hayo katika data zao

1565256079037.png

Original faili linapatikana kwenye link link hii
1565251986924.png

Bado nitaangalia data za GDP kwa vile ninataka kungalia walivyokokota GDB growth rate; kwani namba kamili zinazohitajiwa tu ni GDP ya miaka mwili inayofuatana na inflation rate pia ya miaka miwrli inayofuatana. Nikishazipata nitaangalia wao walifikiaje ile 5.2%

(2) Swala la pili ni kuwa kama unadhani data za IMF ni sahihi kabisa, basi fanya verification kwa kutumia data halisi siyo kukubali conclusion yao tu; naamini kuwa sisi ni intellectuals tusiolishwa habari kwa vijiko bali tunajilisha wenyewe. Kukisha kuwa na conclusions mbili zinazopingama ni wajibu wako kutafuta ukweli kwa kutumia raw data; mimi huchukua effort ya kusoma report zote za bajeti, na ripoti mbalimbali katika kutoa maoni yangu, na kila mara ninakupa ushahdi; usiongee kwa hisia kwa kurudia yale yale ambayo huwezi kuyaprove.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Data za dunia kuhusu GDP ikwemo Tanzania huko world bank zinapatikana kwenye faili hili la excel
1565254160511.png

Ukilifungua na kutafuta row ya Tanzania itaonekana kama ifuatavyo hapa chini

1565256206718.png

Hizo ndizo data zinazotoa picha uchumi wa Tanzania kutoka World Bank pamoja za zile za inflation nilizoweka kwenye post ya pale nyuma; je walifikiaje Annual Real GDP Growth ya 5.2% ?. Sasa hivi naona kama vile Serikali yenyewe ama ilitoa Annual Nominal GDP ya 7.0% (bila kuhusisha inflation) ambayo ilitakiwa ilitakiwa iwe 7.2% au walitumia difference ya inflationa kati ya 5.32% ya 2017 na 3.49% ya 2018 (ambao itakuwa makosa) lakini ni 1.83% ili kufikia namba yao hiyo. Swali hapa ni je formula ya World Bank hubadilika kati ya nchi na nchi kila mwaka? Ukitumia formula ile ile kwa kwa nchi nyingine na kwa miaka tofauti hupati majibu yanayofanana!!

Nimesoma ripoti ya UNCTAD hapa yenyewe inasema kwamba uchumi wa Tanzania mwaka 2018 ulikua kwa 6.8%

1565257673887.png
Kwa vile sasa tuna figures zinazokinzana, kama watu wazima itatusaidia sana iwapo tutajadili data hizi kuliko kujadili na kusimamia conclusion moja tu ya IMF. Sote tuwe fact-based na data-driven.

Nguruvi3, Rev. Kishoka, Mzuvendi, Zitto msinune na kususia; njooni mmwage nondo hapa kwa ushahidi wa data.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Mkuu Kichuguu
Awali ya yote nikushukuru kwa jitihada za kuleta takwimu kama si kutafuta
Nadhani akina Zitto Rev. Kishoka na wengine wanapita hapa na huenda wana la kusema

Kwangu sina tatizo na takwimu. Nimekuwa staunch proponent wa takwimu
Mara zote nimewashauri watu hasa wanaompinga Zitto wampinge kwa takwimu

Hata hivyo katika hii mada nakwazika kidogo kutumia data za NBS na IMF kwa ulinganifu.
Kufanya hivyo nitakuwa najenga uhalali wa kuamini taasisi nisiyoiamini ya NBS.

Nina sababu na siyo hisia. Mswada ulioipa NBS nguvu ulipelekwa kwa hati ya dharura.
Mazingira ya mswada ni baada ya takwimu ''mbaya'' kutolewana taasisi hiyo
Hayo hatukuyaona wakati wa REDET na wengine ambao ni wapiga debe wa ''upande wetu''

Pili, taasisi hii ni sehemu ya taasisi ninazosema hazipo huru na ni mkono wa kushoto....
Tatu, hakuna credibility wala integrity ya taasisi zetu hata zile nyeti kama Polisi
Nne, hivi umesahau tuliambiwa Bunge live ni kuepusha gharama, mbona kila siku kuna live

Nitaendelea na curiosity ya takwimu za akina Zitto na IMF kwa uangalifu rather than fooling myself with fake and fabricated info.

Ni fake kwasababu zinakuwa influenced and imposed

Hali hii si yangu pekee, Watanzania baadhi wapo upande huu kwasababu ya jeraha (self inflicted wound) ambalo serikali imejitia yenyewe.

Imetutoa imani halafu ikatulazimisha tutafute mbadala
Hakukuwa na sababu za kutumia nguvu, namba huongea zenyewe.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32419622, member: 348"]
Politicians hawawezi kuforce kuwa kwa mwaka huu tukamilishe tujenge mradi fulani unaohitaji pesa ambazo nchi haina uwezo nazo halafu ukaingia kwenye bajeti kweli.
Naomba urudi kwenye bajeti ya 2017/18 uone namna gani pesa zilitengwa na zilivyotolewa.

Sijui unatuelimisha vipi kwa hii hoja kwamba, wizara inaomba Bajeti halafu inapewa 40%
Kama hakukuwa na pesa, miradi tajwa ilipangwaje na kwa mtazamo gani kama si wa kisiasa!
Nilikuwa na rafiki zangu pale hazina mmoja alikuwa Mchumi na mwingine alikuwa CPA walikuwa wanashughulika na mambo ya bajeti full time, yaani mwaka mzima.
Wala hakuna tatizo na watalaam, wapo tena wengi tu. Hoja yangu ni kuwa kuna political influence kubwa kuliko utaalaam wenyewe.

Ukitaka kulijua hili, jiulize kwanini hatusikii mawaziri na wasaidizi wao wakitueleza kuhusu mafanikio na matatizo ya bajeti iliyotangulia? Sana sana utasikia mafanikio, hutaelezwa kwanini miradi abcd haikukamilika. Maana yake wanajua walichokisema hakikuwa ''practical'' ilikuwa ni sehemu ya propaganda.
Kuhusu uwanja wa Chato usituumize sana kichwa,Ila ninachosema ni kuwa umejengwa kwa kuidhinishwa na Bunge siyo kuwa umejengwa kinyemela
kinyume na bajeti ya Bunge kama watu wanavyodai; I hope umesoma post yangu hii hapa hapo nyuma.
Sina tatizo na uwanja , ninashaka na utetezi unaotolewa.
Pale ambapo mradi wa Geita unajengewa hoja kuwa ulikuwa wa mkoa wa Geita, kuna shaka

Lugha inatia shaka, hatusikii hata siku moja barabara ya Tanga. Tunachosikia ni barabara ya Tanga-Muheza, au Dar-Moshi, au Makambako-Iringa n.k.

Ninawaelewa wanaotumia neno unyemela. Haiingia akilini kwamba watalaam walipanga kujenga uwanja Geita na kuomba pesa Bungeni bila kujua uwanja huo unajengwa wapi.

Mbona hatusikii pesa zilizotengwa kwa bwawala Pwani, bali Stigler gorge?

Sijui siku hizi, zama hizo tukijiandaa na mtihani wa std 7 territorial matriculation(ndio ulikuwa mwisho) watalaam wa mambo ya pesa walitufunza neno ''misappropriation of fund''.

Niliwauliza wakanipa mfano rahisi ili nielewe kwa kiwango changu cha elimu.
Kwamba, pesa zimetolewa kununua mabomba lakini zikatumika kujenga kisima cha maji

Wakaguzi wa pesa wakiona misappropriation'' hufuatilia kuanzia mwanzo wa shughuli au mradi hadi ilipotokea wakifuatilia hadi vikao na maamuzi.
Wakaguzi wanajua ''misappropriation'' of fund is a precursor for embezzlement and corruption

Nimalizie uchechefu wangu kwa kusema tatizo si uwanja, wanaokuza suala hili ni watetezi wenye hoja dhaifu zinazotia shaka badala ya kuondoa.

Mbona tunasikia uwanja wa ndege wa musoma unakarabatiwa hatusikii pesa zilizotengwa kwa ukarabati wa uwanja wa ndege wa Mara!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mkuu Kichuguu
Awali ya yote nikushukuru kwa jitihada za kuleta takwimu kama si kutafuta
Nadhani akina Zitto Rev. Kishoka na wengine wanapita hapa na huenda wana la kusema

Kwangu sina tatizo na takwimu. Nimekuwa staunch proponent wa takwimu
Mara zote nimewashauri watu hasa wanaompinga Zitto wampinge kwa takwimu

Hata hivyo katika hii mada nakwazika kidogo kutumia data za NBS na IMF kwa ulinganifu.
Kufanya hivyo nitakuwa najenga uhalali wa kuamini taasisi nisiyoiamini ya NBS.

Nina sababu na siyo hisia. Mswada ulioipa NBS nguvu ulipelekwa kwa hati ya dharura.
Mazingira ya mswada ni baada ya takwimu ''mbaya'' kutolewana taasisi hiyo
Hayo hatukuyaona wakati wa REDET na wengine ambao ni wapiga debe wa ''upande wetu''

Pili, taasisi hii ni sehemu ya taasisi ninazosema hazipo huru na ni mkono wa kushoto....
Tatu, hakuna credibility wala integrity ya taasisi zetu hata zile nyeti kama Polisi
Nne, hivi umesahau tuliambiwa Bunge live ni kuepusha gharama, mbona kila siku kuna live

Nitaendelea na curiosity ya takwimu za akina Zitto na IMF kwa uangalifu rather than fooling myself with fake and fabricated info.

Ni fake kwasababu zinakuwa influenced and imposed

Hali hii si yangu pekee, Watanzania baadhi wapo upande huu kwasababu ya jeraha (self inflicted wound) ambalo serikali imejitia yenyewe.

Imetutoa imani halafu ikatulazimisha tutafute mbadala
Hakukuwa na sababu za kutumia nguvu, namba huongea zenyewe.
Jaribu kuwa neutral uwe unatafuta ukweli positively; ukishakuwa biased basi unaanza kushindwa kuwa objective. Kuna aina tano kuu za bias kama zionekanavyo katika snippet hii.

1565325143666.png
Unaelekea kuwa affected na Anchoring bias (unaamini kila kitu cha Zitto na IMF kwa sababu moja tu hata kama mambo yao mengine siyo ya kuaminika), Confirmation bias (Huamini taasisi za serikali kutokana na kosa moja tu hata kama sehemu nyingine hawafantyi makosa hayo tena- samaki mmoja akioza basi wameoza wote!), na Halo effect (Unakumbukia mazuri ya zamani ya Zito na IMF, kwa hiyo unaamini kuwa kila wasemalo leo ni sahihi pia hata kama siyo sahihi tena). Jikwamue kutokana na bias za namna hiyo; mimi nilikuwa shabiki sana wa Zitto wakati ule alipoibua skandali ya Buzwagi, lakini kadri muda ulivyokwenda nimegundua kuwa siyo kila asemalo lina ukweli.

Naomba urudi kwenye bajeti ya 2017/18 uone namna gani pesa zilitengwa na zilivyotolewa.

Sijui unatuelimisha vipi kwa hii hoja kwamba, wizara inaomba Bajeti halafu inapewa 40%
Kama hakukuwa na pesa, miradi tajwa ilipangwaje na kwa mtazamo gani kama si wa kisiasa!
Wala hakuna tatizo na watalaam, wapo tena wengi tu. Hoja yangu ni kuwa kuna political influence kubwa kuliko utaalaam wenyewe.

Ukitaka kulijua hili, jiulize kwanini hatusikii mawaziri na wasaidizi wao wakitueleza kuhusu mafanikio na matatizo ya bajeti iliyotangulia? Sana sana utasikia mafanikio, hutaelezwa kwanini miradi abcd haikukamilika. Maana yake wanajua walichokisema hakikuwa ''practical'' ilikuwa ni sehemu ya propaganda. Sina tatizo na uwanja , ninashaka na utetezi unaotolewa.
Pale ambapo mradi wa Geita unajengewa hoja kuwa ulikuwa wa mkoa wa Geita, kuna shaka

Lugha inatia shaka, hatusikii hata siku moja barabara ya Tanga. Tunachosikia ni barabara ya Tanga-Muheza, au Dar-Moshi, au Makambako-Iringa n.k.

Ninawaelewa wanaotumia neno unyemela. Haiingia akilini kwamba watalaam walipanga kujenga uwanja Geita na kuomba pesa Bungeni bila kujua uwanja huo unajengwa wapi.

Mbona hatusikii pesa zilizotengwa kwa bwawala Pwani, bali Stigler gorge?

Sijui siku hizi, zama hizo tukijiandaa na mtihani wa std 7 territorial matriculation watalaam wa mambo ya pesa walitufunza neno ''misappropriation of fund''.

Niliwauliza wakanipa mfano rahisi ili nielewe kwa kiwango changu cha elimu.
Kwamba, pesa zimetolewa kununua mabomba lakini zikatumika kujenga kisima cha maji

Wakaguzi wa pesa wakiona misappropriation'' hufuatilia kuanzia mwanzo wa shughuli au mradi hadi ilipotokea wakifuatilia hadi vikao na maamuzi.
Wakaguzi wanajua ''misappropriation'' of fund is a precursor for embezzlement and corruptions

Nimalizie uchechefu wangu kwa kusema tatizo si uwanja, wanaokuza suala hili ni watetezi wenye hoja dhaifu zinazotia shaka badala ya kuondoa.

Mbona tunasikia uwanja wa ndege wa musoma unakarabatiwa hatusikii pesa zilizotengwa kwa ukarabati wa uwanja wa ndege wa Mara!
Kwanza je mzee Nguruvi3 sasa unakubaliana nami kuwa uwanja ule haukujengwa kinyemela bali ulipitishwa na Bunge? Hapo ndipo mimi nimekuwa nasimamia nikiwa napinga propaganda hizi kuwa pesa zimechotwa hazina kinyemela.

Ieleweke kuwa kwenye hili la uwanja mimi siutetei kuwa ni mradi mzuri, ila ninalosema ni kuwa tusipotoshe kwamba umejengwa kinyemela; ni lazima tukubali kuwa umejewa kihalali kabisa kulingana na bajeti iliyopitishwa na bunge. Ila sasa wabunge ndio labda waawajibishwe kwa kupitisha bajeti iliyokuwa fuzzy namna ile, labda liwe fundisho katika bajeti zijazo. Ninajua jina Geita pia linasababisha confusion kidogo, kwani lina maana tatu tofauti: mkoa, wilaya na mji.

Niliwahi kufika Chato Ginnery zamani sana wa Practical Training za Faculty of Engineering UDSM; kalikuwa kamji kadogo sana ambako usafiri wake ulikuwa mgumu sana, kwani unatua kwa ndege Bukoba mjini, halafu unapanda basi kwenda Bihalamuro, na kusubiri siku moja ili kupata basi jingine la kwenda Chato ambalo lililikuwa moja tu, linaondoka asubuhi na kurudi jioni. Kusikia leo kuna uwanja wa ndege na barabara za lami tu, kweli ni shock kidogo nikijaribu kuweka picha niliyoona wakati ule.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Kichuguu:Unaelekea kuwa affected na Anchoring bias (unaamini kila kitu cha Zitto na IMF kwa sababu moja tu hata kama mambo yao mengine siyo ya kuaminika), Confirmation bias (Huamini taasisi za serikali kutokana na kosa moja tu hata kama sehemu nyingine hawafantyi makosa hayo tena- samaki mmoja akioza basi wameoza wote!), na Halo effect (Unakumbukia mazuri ya zamani ya Zito na IMF, kwa hiyo unaamini kuwa kila wasemalo leo ni sahihi pia hata kama siyo sahihi tena).
Mkuu sina ''bias'' nina choice. Nimechagua makusudi kabisa kutodurusu takwimu za NBS kwa kujua kuwa kufanya hivyo ni kujidanganya.Mkuu si unaona taasisi zetu zinavyozidi kutoa mashaka hata wale waliokuwa neutral?

Mbona nilisema wazi! Kwamba nitafuatilia data za watu kama Zitto au IMF kwa uangalifu (walk a thin line).

Nisichoweza kufanya ni kutoa benefit of doubt kwa taasisi zetu hadi zitakapokubali na kujenga utamaduni wa ''credibility and integrity''
Kichuguu, post: 32429128, member: 348"]Unakubaliana nami kuwa uwanja ule haukujengwa kinyemela bali ulipitishwa na Bunge?

Napinga propaganda hizi kuwa pesa zimechotwa hazina kinyemela.

Ila sasa wabunge ndio labda waawajibishwe kwa kupitisha bajeti iliyokuwa fuzzy namna ile, labda liwe fundisho katika bajeti zijazo.

Ninajua jina Geita pia linasababisha confusion kidogo, kwani lina maana tatu tofauti: mkoa, wilaya na mji.
Maelezo yako yote yanakuwa summarized na neno moja, Nyemela.

Nyemela kwa lugha ya Malkia ni ''surreptitiously'', jambo linalofanyika kwa siri kuhofia uhalali.

Sioni tatizo la kiwanja kujengwa popote Tanzania.

Mjadala ni kuwa wanaosema kuna Unyemela wana hoja ukizingatia maelezo yako.

Nitafafanua kuanzi mstari wako wa chini

1. Jina Geita halisababishi confusion kidogo, ndicho chanzo cha confusion.

Kwanini ukarabati wa uwanja wa Musoma usemwe ''Musoma'' na si uwanja wa Mara?
Kwanini MRI ipelekwe Hospitali ya Bombo Tanga na si Hospitali ya Tanga!

2. ''Wabunge wawajishwe kwa bajeti Fuzzy''.
Kwanini wawajishwe ikiwa lengo ni kujenga uwanja iwe Geita , Mang'ula au Kimbiji?
Wao waliambiwa uwanja unajengwa Geita, kwanini wakatae
Kwani huko Geita si Watanzania! na kwamba hawalipi kodi.

Katika vitu vinavyoangaliwa panapokuwa na '' proposal ya project'' ni specificity
Huwezi kuomba pesa za mradi wa maji Pwani.
Je, una maana ukanda wa ''pwani'' au mkoa wa Pwani au eneo la Pwani ufukweni ?

Na kama ni mkoa mradi upo wapi, kimbiji, Namanywili, Nyamato au Bigwa Mwarusembe!

3. Kwa confusion uliyosema ya neno Geita na Wabunge, pesa zilitokaje hazina?
Umesema kuna confusion na kutowajibika. Hao wanaosema ''zilichotwa'' wanakosea wapi.

Categorically i can say, the so called confusion was created deliberately for political correctness.

4. Kwamba uwanja una uhalali! well, the end justifies the means.

Kwahiyo wanaosema kuna unyemela ''surreptitious'' na kuchotwa pesa wanaweza kuwa waongo, lakini, wanaweza kuwa sahihi kwa wanaofuatilia yobi, namba na utaratibu .
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mkuu sina ''bias'' nina choice. Nimechagua makusudi kabisa kutodurusu takwimu za NBS kwa kujua kuwa kufanya hivyo ni kujidanganya.Mkuu si unaona taasisi zetu zinavyozidi kutoa mashaka hata wale waliokuwa neutral?

Mbona nilisema wazi! Kwamba nitafuatilia data za watu kama Zitto au IMF kwa uangalifu (walk a thin line).

Nisichoweza kufanya ni kutoa benefit of doubt kwa taasisi zetu hadi zitakapokubali na kujenga utamaduni wa ''credibility and integrity''Maelezo yako yote yanakuwa summarized na neno moja, Nyemela.

Nyemela kwa lugha ya Malkia ni ''surreptitiously'', jambo linalofanyika kwa siri kuhofia uhalali.

Sioni tatizo la kiwanja kujengwa popote Tanzania.

Mjadala ni kuwa wanaosema kuna Unyemela wana hoja ukizingatia maelezo yako.

Nitafafanua kuanzi mstari wako wa chini

1. Jina Geita halisababishi confusion kidogo, ndicho chanzo cha confusion.

Kwanini ukarabati wa uwanja wa Musoma usemwe ''Musoma'' na si uwanja wa Mara?
Kwanini MRI ipelekwe Hospitali ya Bombo Tanga na si Hospitali ya Tanga!

2. ''Wabunge wawajishwe kwa bajeti Fuzzy''.
Kwanini wawajishwe ikiwa lengo ni kujenga uwanja iwe Geita , Mang'ula au Kimbiji?
Wao waliambiwa uwanja unajengwa Geita, kwanini wakatae
Kwani huko Geita si Watanzania! na kwamba hawalipi kodi.

Katika vitu vinavyoangaliwa panapokuwa na '' proposal ya project'' ni specificity
Huwezi kuomba pesa za mradi wa maji Pwani.
Je, una maana ukanda wa ''pwani'' au mkoa wa Pwani au eneo la Pwani ufukweni ?

Na kama ni mkoa mradi upo wapi, kimbiji, Namanywili, Nyamato au Bigwa Mwarusembe!

3. Kwa confusion uliyosema ya neno Geita na Wabunge, pesa zilitokaje hazina?
Umesema kuna confusion na kutowajibika. Hao wanaosema ''zilichotwa'' wanakosea wapi.

Categorically i can say, the so called confusion was created deliberately for political correctness.

4. Kwamba uwanja una uhalali! well, the end justifies the means.

Kwahiyo wanaosema kuna unyemela ''surreptitious'' na kuchotwa pesa wanaweza kuwa waongo, lakini, wanaweza kuwa sahihi kwa wanaofuatilia yobi, namba na utaratibu .
Kuhusu choices, hiyo kila mtu ana haki yake ya kuamini na ninaheshimu haki hiyo, lakini data zote nilizoweka pale juu ni za World Bank ambao ndio wanatupatia pesa nyingi za miradi yetu; hao ndio wangekuwa suspicious zaidi ya taasisi yoyote kwa vile kuna pesa yao inahusika.

Kuna kitu hukizungumzii kuhusu madai ya unyemela, taarifa zilizosambaa ni kuwa pesa zilichotwa kinyemela "bila ridhaa ya bunge." Katika maelezo yako ya unyemela hapo juu unaacha kukamilisha na qualifieir ya "bila ridhaa ya bunge". Upinzani wangu kwenye hoja hapa ni kuwa kulikuwa na ridhaa ya bunge kuhusu matumizi ya fedha hizo.

Sehemu kubwa ya malalamiko yako mengine kuhusu uwanja huo ni kama nilivyomjibu Rev. Kishoka huko nyuma kuwa ni kweli bajeti ilifanywa fuzzy makusudi kuficha kitu fulani; hilo huenda halina ubishi. Lakini nisichowakubalia wote ni kule kupotosha kuwa pesa zimechotwa kinyemela bila kuidhiniswa na bunge kwani huo ni uzushi tu; pesa zile zillidhinishwa na Bunge 100%, hazikuchotwa kinyemela. Nadhani ni swala la semantics na logic tu.

Iwapo kuna mzazi haleti chakula nyumbani hadi watoto wakafa kwa njaa hawezi kushitakiwa eti aliuwa watoto wale kwa kuwapiga risasi. Ukimshitaki kuwa aliwapiga risasi, mimi nitakupinga kuwa unapotosha, ingawaje nitakuwa vile vile simtetei mzazi yule!

At least angejitokeza mbunge mmoja kuuliza uwanja huo utajengwa mji gani, na hata kutoa shilingi kwenye bajeti ile hadi apatiwe ripoti ya uhakika kujua uwanja utajengwa wapi, na mbaya zaidi kwa vile wabunge walishajuwa kuwa Geita ndiko kwao mkulu. Hawawezi kupitisha matumizi ya pesa bila kuwa na uhakika zitatumikaje. Je kama uwanja ungeenda kujengwa porini tu kusikofikika kirahisi? Je waliposikia mkoani Geita wao waliamini kuwa ni mjini Geita?

Hawa ni watu wanaotunga sheria zetu, watapitishaje sheria ambazo siyo specific namna ile? Nadhani na wewe unaelewa sana hadihti ya hukumu ya Kunyongwa kwa kamba ambayo haikuwa specific kuwa lazima mhukumiwa afe. Baada ya mhukumiwa mmoja kukwepa kifo kwa kamba kukatika kabla hajafa, ikabidi sheria inolewe tena kuwa specific kwamba lazima mhukumiwa anyongwe hadi afe.

Kwa hili la uwanja mimi ninalaumu Bunge tu, siyo serikali, kwani fedha zote za serikali zimeidhinishwa na bunge. Mbunge mmoja tu ana nguvu ya kutosha kusimamisha bajeti yote, kwa hiyo hata kama Bunge lote ni la wapiga debe tu, at least angekuwapo mmoja ambaye ni logical kiasi cha kutosha.
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
Kichuguu;

Thanks for your efforts to bring the numbers. Based on the reports, the GDP isn't that bad. However, GDP alone doesn't define the well being of the economy. So, it doesn't make sense to criticize or support the government using GDP solely. I think other indicators should come into play as well.

Take from example debts/GDP ratio. Can we add this one into the mix too. For example the government can borrow heavyly to build its infrastructures. In short term, this will boast the GDP number. However, in a long term if the national debt isn't sustainable,the economy will suffer.

So the GDP has to have some context attached to it. Otherwise, it is just a number. If Zitto says the GDP is slowing, he should be able to tell us where things go wrong. The same applies to those who support the government. They should be able to tell which sector of the economy does well and which ones don't and the reasons.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32441282, member: 348"]
World Bank ambao ndio wanatupatia pesa nyingi za miradi yetu; hao ndio wangekuwa suspicious zaidi ya taasisi yoyote kwa vile kuna pesa yao inahusika.
Nadhani walipotoa taarifa yao ilikuwa rebuttal ya taarifa ya NBS kwa maana ile ile kuwa ndio watoaji pesa hivyo waliona kuna kitu hakipo sawa kwa mtazamo wao
Kuna kitu hukizungumzii kuhusu madai ya unyemela, taarifa zilizosambaa ni kuwa pesa zilichotwa kinyemela "bila ridhaa ya bunge." Upinzani wangu kwenye hoja hapa ni kuwa kulikuwa na ridhaa ya bunge kuhusu matumizi ya fedha hizo.
Tukubali hili kwa wakati huu
Sehemu kubwa ya malalamiko yako kama nilivyomjibu Rev. Kishoka huko nyuma kuwa ni kweli bajeti ilifanywa fuzzy makusudi kuficha kitu fulani; hilo huenda halina ubishi.
Ahsante kwa hoja hii. Hapa pia ndipo panatia doa ''ridhaa''
Ridhaa ni (consent) isiyoambatana na shaka yoyote ile. Kama hapo juu umesema kuna mwelekeo wa kitu kufichwa, tayari ridhaa inapoteza maana yake. Kinachochukua nafasi ni duress. Hivyo pesa iliidhinishwa na Bunge under duress.Hii haiondoi ukweli kuwa iliidhinishwa na Bunge, na zaidi linaeleza kuwa ile ridhaa haikufanywa kwa uwazi na kujenga hoja ya ''surreptitious'' au unyemela. Kama ulivyosema kwanini kulikuwa na kificho ficho? Si ndio unyemela huo
At least angejitokeza mbunge mmoja kuuliza uwanja huo utajengwa mji gani, na hata kutoa shilingi kwenye bajeti ile hadi apatiwe ripoti ya uhakika kujua uwanja utajengwa wapi.
Hawawezi kupitisha matumizi ya pesa bila kuwa na uhakika zitatumikaje.
Je kama uwanja ungeenda kujengwa porini tu kusikofikika kirahisi?
Je waliposikia mkoani Geita wao waliamini kuwa ni mjini Geita?
Nakubaliana nawe.
Na hapa unatetea hoja yangu kuwa Bunge ni moja ya taasisi tunazosema zimepoteza uwezo
Hawa ni watu wanaotunga sheria zetu, watapitishaje sheria ambazo siyo specific namna ile?
Na siyo Bunge, serikali ilifikishaje mswada usio specific namna ile?
Kwa hili la uwanja mimi ninalaumu Bunge tu, siyo serikali, kwani fedha zote za serikali zimeidhinishwa na bunge. Mbunge mmoja tu ana nguvu ya kutosha kusimamisha bajeti yote, kwa hiyo hata kama Bunge lote ni la wapiga debe tu, at least angekuwapo mmoja ambaye ni logical kiasi cha kutosha.
Umetuelewa tunaosema ''taasisi zetu zimepoteza nguvu zake. Hoja ya kwamba tunahitaji kuimarisha taasisi zetu, kuzipa uhuru na kuzisimamia nje ya mfumo wa kisiasa zinaeleweka sasa. Bila kuwa na taasisi imara ''daring and bold'' hatuwezi kusogea.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Kichuguu;

Thanks for your efforts to bring the numbers. Based on the reports, the GDP isn't that bad. However, GDP alone doesn't define the well being of the economy. So, it doesn't make sense to criticize or support the government using GDP solely. I think other indicators should come into play as well.

Take from example debts/GDP ratio. Can we add this one into the mix too. For example the government can borrow heavyly to build its infrastructures. In short term, this will boast the GDP number. However, in a long term if the national debt isn't sustainable,the economy will suffer.

So the GDP has to have some context attached to it. Otherwise, it is just a number. If Zitto says the GDP is slowing, he should be able to tell us where things go wrong. The same applies to those who support the government. They should be able to tell which sector of the economy does well and which ones don't and the reasons.
Thanks and you see,

The reason to bring those numbers here was to clear the air so we discuss things using factual bases. They were not meant to show that the government is doing excellent, but to help thwart the disinformation being propagated to fill the ether using unsubstantiated numbers. Naturally I tend to get offended and feel that my intelligence is being insulted when people try to mislead me using cooked exam papers. AlI I want here is to talk about facts only; some facts can be good and some can be terribly bad, but not spend time on distorted snippets.

I just told my friend Nguruvi3 that if parents kill their kid by starving him, do not charge them for shooting that kid in order to sensationalize the public!, just be sincere that they starved their kid.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Nadhani walipotoa taarifa yao ilikuwa rebuttal ya taarifa ya NBS kwa maana ile ile kuwa ndio watoaji pesa hivyo waliona kuna kitu hakipo sawa kwa mtazamo wao Tukubali hili kwa wakati huu Ahsante kwa hoja hii. Hapa pia ndipo panatia doa ''ridhaa''
Ridhaa ni (consent) isiyoambatana na shaka yoyote ile. Kama hapo juu umesema kuna mwelekeo wa kitu kufichwa, tayari ridhaa inapoteza maana yake. Kinachochukua nafasi ni duress. Hivyo pesa iliidhinishwa na Bunge under duress.Hii haiondoi ukweli kuwa iliidhinishwa na Bunge, na zaidi linaeleza kuwa ile ridhaa haikufanywa kwa uwazi na kujenga hoja ya ''surreptitious'' au unyemela. Kama ulivyosema kwanini kulikuwa na kificho ficho? Si ndio unyemela huoNakubaliana nawe.
Na hapa unatetea hoja yangu kuwa Bunge ni moja ya taasisi tunazosema zimepoteza uwezo
Na siyo Bunge, serikali ilifikishaje mswada usio specific namna ile?Umetuelewa tunaosema ''taasisi zetu zimepoteza nguvu zake. Hoja ya kwamba tunahitaji kuimarisha taasisi zetu, kuzipa uhuru na kuzisimamia nje ya mfumo wa kisiasa zinaeleweka sasa. Bila kuwa na taasisi imara ''daring and bold'' hatuwezi kusogea.
Jambo moja nitakalosisitiza tena hapa ni kuwa uko biased ila hujui hilo kwa vile ni silka ya binadamu wote; huwezi kuchagua upande mmoja tu siku zote bila kujua upande wa pili ukoje halafu ukasema kuwa huko biased. Ingawa najua concern yako, bado unaweka undue burden kwa serikali kuhusu muswada wao huo wa bajeti kama vile bunge halihusiki. Mimi siyo mwanasheria wa serikali, ila nikikuambia kuwa wakati wa bajeti walikuwa bado wanamalizia feasibility study ya kuamua wapi wajenge uwanja huo kati ya Geita Mjini, Kharumwa, na Chato, na uamuzi wa mwisho ulifanyiaka baada ya bajeti kuwa imeshapitiswa utasemaje. Ilikuwa ni wajibu wa Bunge kuwa na uhakika kuwa pesa wanazoidhinisha zitakwenda wapi, siyo hiyo ya kutoa blank cheque halafu baadaye kuja kulalamika kwa hisia bila ushahidi wowote wa kisheria.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32450235, member: 348"]
Jambo moja nitakalosisitiza tena hapa ni kuwa uko biased ila hujui hilo kwa vile ni silka ya binadamu wote;
Mkuu kwa hili natambua nina choice siyo bias.
Taasisi zetu ikiwemo Bunge zina matatizo. Nikukumbushe tu, juzi kuna idara imetoa taarifa ya kumkamata mtu. Siku mbili baadaye hati ya mashtaka si ile idara bali mambo mengine
Sasa ''taasisi'' hizounawezaje kuamini wanachosema?

Nguvu iliyotumika kuipa NBS monopoly ni wazi ina msukumo fulani.
Mamlaka ya NBS inawajibika kwa serikali bila kuwajibika kwingine. Uhuru wake upo wapi?

Unakumbuka taarifa za kila mwezi za BoT? Zimeishia wapi na kwanini?

Huwezi kuchagua upande mmoja tu siku zote bila kujua upande wa pili ukoje halafu ukasema kuwa huko biased.
Hapa nimechagua upande mmoja kwasababu hakuna upande wa pili. Unalinganisha vitu vinavyowiana, kwangu upande mmoja siwezi kuupa uhalali.

Unaweka undue burden kwa serikali kuhusu muswada wao huo wa bajeti kama vile bunge halihusiki.
Hapana, nimetenga maeneo mawili serikali na Bunge.
Kama mswada uliwakilishwa ni wazi ulipitia ngazi zote na wataalam waliuangalia wakiwemo classmate wa Mzuvendi wanaoandaa Bajeti. Haiingii akilini kwamba hakuna aliyeona tatizo la specificity kwa project kama ile. Ni wazi kilichofanyika kilikuwa na hila unayoita confusion.

Kwa upande wa Bunge, ninapenda sana mchango wako. Inadvertently unatusaidia kuonyesha umuhimu wa taasisi imara, na jinsi gani Bunge letu lime deteriorate kama sikuwa defunct
Umesema hapa chini
Mimi siyo mwanasheria wa serikali, ila nikikuambia kuwa wakati wa bajeti walikuwa bado wanamalizia feasibility study ya kuamua wapi wajenge uwanja huo kati ya Geita Mjini, Kharumwa, na Chato, na uamuzi wa mwisho ulifanyiaka baada ya bajeti kuwa imeshapitiswa utasemaje. Ilikuwa ni wajibu wa Bunge kuwa na uhakika kuwa pesa wanazoidhinisha zitakwenda wapi, siyo hiyo ya kutoa blank cheque halafu baadaye kuja kulalamika kwa hisia bila ushahidi wowote wa kisheria.
Ni kweli, Bunge halikutimiza wajibu wake kwasababu zile zile,taasisi iliyopoteza nguvu zake katika kusimamia serikali.

Hili la bunge kwa upande wako ni ''shoot oneself in the foot''.
Huko nyuma umechangia mada hii ukisema hatuhitaji vikao, maamuzi mazuri ni ya kiongozi na kwamba kiongozi awe ''daring and bold''. Kwa mtazamo wako huo, ili kiongozi aweze kufanya maamuzi inabidi kusiwe na kikwazo . Mkuu huoni tatizo la bunge lilivyo ''drop the ball''

Wengine tunaamini katika taasisi imara, Rev. Kishoka akauliza ''checks and balances'' ipo wapi ikiwa taasisi kama Bunge inatenda kama ilivyotokea?

We're on the same page, kinachotutofautisha ni ''cherry and pick''.
The process was flawed ab initio, and that has given the critics the leverage and legitimacy to raise genuine concern, for simple reason ''Huwezi kusema nguruwe ni haramu lakini mchuzi wake ni halali''
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mkuu kwa hili natambua nina choice siyo bias.
Taasisi zetu ikiwemo Bunge zina matatizo. Nikukumbushe tu, juzi kuna idara imetoa taarifa ya kumkamata mtu. Siku mbili baadaye hati ya mashtaka si ile idara bali mambo mengine
Sasa ''taasisi'' hizounawezaje kuamini wanachosema?

Nguvu iliyotumika kuipa NBS monopoly ni wazi ina msukumo fulani.
Mamlaka ya NBS inawajibika kwa serikali bila kuwajibika kwingine. Uhuru wake upo wapi?

Unakumbuka taarifa za kila mwezi za BoT? Zimeishia wapi na kwanini?

Hapa nimechagua upande mmoja kwasababu hakuna upande wa pili. Unalinganisha vitu vinavyowiana, kwangu upande mmoja siwezi kuupa uhalali.

Hapana, nimetenga maeneo mawili serikali na Bunge.
Kama mswada uliwakilishwa ni wazi ulipitia ngazi zote na wataalam waliuangalia wakiwemo classmate wa Mzuvendi wanaoandaa Bajeti. Haiingii akilini kwamba hakuna aliyeona tatizo la specificity kwa project kama ile. Ni wazi kilichofanyika kilikuwa na hila unayoita confusion.

Kwa upande wa Bunge, ninapenda sana mchango wako. Inadvertently unatusaidia kuonyesha umuhimu wa taasisi imara, na jinsi gani Bunge letu lime deteriorate kama sikuwa defunct
Umesema hapa chini Ni kweli, Bunge halikutimiza wajibu wake kwasababu zile zile,taasisi iliyopoteza nguvu zake katika kusimamia serikali.

Hili la bunge kwa upande wako ni ''shoot oneself in the foot''.
Huko nyuma umechangia mada hii ukisema hatuhitaji vikao, maamuzi mazuri ni ya kiongozi na kwamba kiongozi awe ''daring and bold''. Kwa mtazamo wako huo, ili kiongozi aweze kufanya maamuzi inabidi kusiwe na kikwazo . Mkuu huoni tatizo la bunge lilivyo ''drop the ball''

Wengine tunaamini katika taasisi imara, Rev. Kishoka akauliza ''checks and balances'' ipo wapi ikiwa taasisi kama Bunge inatenda kama ilivyotokea?

We're on the same page, kinachotutofautisha ni ''cherry and pick''.
The process was flawed ab initio, and that has given the critics the leverage and legitimacy to raise genuine concern, for simple reason ''Huwezi kusema nguruwe ni haramu lakini mchuzi wake ni halali''
Nadhani wewe unasoma post zangu ukiwa na mindset fulani, hivyo kila wakati unazeielewa ambavyo sivyo. Nimeshapigwa msasa sana kuhusu "Respecting Your Neighbor" hasa kwenye mambo ya biases, stereotyping na generalizations, na ninaona kama una element fulani fulani za mambo hayo kwenye topic hii. Unaonekana kuwa mwepesi sana kuelewa jambo vinginevyo kwa sababu hutaki kulisikia lilivyo kihalisi.

(1) Watu wote tunaishi kwa kufanya choices, maisha siku zote ni mtililiko wa choices. Tangu asubuhi hadi jioni tunafanya choices mbalimbali; kwenda kushoto au kulia. Ila elewa kuwa kuna biased choices na kuna unbiased choices. Choices zako kuhusu hilo ni biased choices.

(2) Niliposema kuwa Magufuli ni decisive, which is true, kama ilivyokuwa Marehemu Sokoine, ni kuwa maamuzi yote ya serikali lazima yetekelezwa bila longolongo, na sheria zote zifuatwe kama zilivyoandikwa. Niliposema kuwa siyo kila jambo lifanyiwe vikao, sikusema kuwa vikao vya Bunge visifanyike bali nilizungumzia mambo yanayohitaji uamuzi wa kiongozi chini ya mamlaka yake; nikatumia mfano wa kijiji kinachotaka kijengewe kituo kidogo cha polisi. Hilo siyo jambo la kusubiri kikao cha cabinet. Wewe lile neno la vikao unatumia generalization ya vikao vya Bunge ambalo silo nililosema.

(3) Kuhusu taasisi nilikuuliza huko nyuma kwenye post #55 una maana gani lakini nadhani hukunijibu kwa kina. Kwangu mimi tasisi za Serikali ni zile zinazosimamia sheria na utekelezaji wa mambo ya kiserikali. Nilishawahi kulalamika huko nyuma kwenye mada ya Katiba mpya kutaka mahakama zisiwe chini ya Wizara ya Sheria, lakini pamoja na muundo mbovu huo, nimekuuliza tena iwapo Serikali ya sasa inashinikiza mahakama kutoa hukumu za kuifurahisha serikali kuliko ilivyokuwa ikifanya miaka ya nyuma, sijapata ushahidi wowote.

(4) Bunge siyo taasisi ya serikali, na nimeuliza iwapo serikali ya sasa inasimamia maamuzi ya Bunge kuliko serikali zilizopita, ukanijibu kuwa Spika huyu ni member wa NEC ya CCM ambayo mwenyekiti wake ni Rais. Sijaona uovu wa serikali hii kwa jambo hilo kwani mambo yamekuwa vivyo hivyo miaka yote tangu mwaka 1965 enzi za Adam Sapi Mkwawa; inawezekana unaihukumu serikali ya sasa kwa stereotyping tu kuwa serikali hii inafanya mabaya siku zote kwa hiyo hata hili ni wao. Zamani kidogo tulikuwa na wabunge wa kundi la 21 akina Njelu Kassaka na wenzao walikuwa ni wana CCM lakini walitekeleza wajibu wao kuisimamia serikali bungeni; kwa nini wa sasa washindwe. Bunge hili kushindwa wajibu wake siyo kosa la serikali.

Conclusion: Unaposema Magufuli ni bulldozer ana weakan taasisi za serikali, sitegemei uwe na maana ya kuwa ana weaken Bunge kwani hajabadilli muuundo na madaraka ya bunge. Bunge kama taasisi iko vile vile tangu mwaka 1995.

Jambo pekee tunaloweza kuilaumu serikali kwa pamoja ni hili la polisi kuwanyanyasa raia bila taratibu za kisheria kwani hilo ni jambo ambalo liko chini ya serikali. Ingawa tabia hizi hazikuanzishwa na serikali hii kwani pia zimekuwapo kwenye serikali zilizotangulia, nilitegemea serikali iwe inachukua hatua za maana kuboresha utendaji wa polisi kutoa haki kwa raia lakini sijaona juhudi zozote kuhusu hilo. Ingawa kuna maafisa wa polisi wanaosimamia sheria kweli, bado naona kuna maafisa wengi ambao hawatendi majukumu yao kufuata sheria.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Conclusion: Unaposema Magufuli ni bulldozer ana weakan taasisi za serikali, sitegemei uwe na maana ya kuwa ana weaken Bunge kwani hajabadilli muuundo na madaraka ya bunge. Bunge kama taasisi iko vile vile tangu mwaka 1995.
Mkuu, ni vema tukajadili hoja tukapingana na kukubaliana, I mean agree or agree to disagree without insinuation or words construe.

Hoja zikiwa nzito kuna option ya kuiacha lakini ni jambo baya sana kumwekea mtu maneno.
Tena unasema ''unaposema'' ukiwa na uhakika nilisema hayo.

Tadhali onyesha katika bandiko langu lolote ndani ya JF nililowahi kutumia neno Bulldozer

Pili, naomba waonyeshe wasomaji wapi nilipotumia neno 'Magufuli' katika mjadala huu

Tukiliweka hili sawa tutaendelea na mjadala wetu mzuri tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom