The Daring and Bold Magufuli

Title ya thread inahusu Magufuli; kwa hiyo hata kama hukusema neno Magufuli, the context is clear. Chanzo kikubwa cha upande huu wa mjadala tunakoelekea ni pale nilipo-question mchangiaji mmoja aliyesema ana weaken institutions na alichota fedha za hazina kujenga Uwanja kijijini kwao Chato bila kibali cha Bunge. Wewe umekuwa unachangia upande huo huo wa kussuport hilo. Ni kwa vile huwa sipendi kutumia majibu ya generalization, ndiyo maana ninapokujibu wewe ninakuaddress wewe tu bila kuhusisha wengine walio upande wako, kwa hiyo ndiyo maana sikusema kuwa "Mnaposema" bali nilisema "Unaposema." Ingawa hujaandika neno kwa neno kama nilivyo paraphrase kwenye conclusion hiyo, context ya michango yako ilikuwa hivyo kuhusu institutions. Upande wa Bunge ulifikia kusema kuwa Spika ni member wa NEC na hata hiyo post niliyoquote hapo inarudia hilo hilo "Inadvertently unatusaidia kuonyesha umuhimu wa taasisi imara, na jinsi gani Bunge letu lime deteriorate kama sikuwa defunct"

Nyuma huko nilikuambia kuwa Bunge lilikuwa hivyo siku zote tangu Uhuru, wewe ukasema hapana ni wakati wa utawala huu tu.

Kama unakana kuwa huo siyo mtazamo wako, na serikali ya sasa haijaweaken Bunge, basi ni vizuri, kwani ina maana kuwa tunakubaliana sasa kuwa ni kweli Bunge lina matatizo makubwa sana kiutendaji, lakini hayasababishwi na Magufuli..
 
Kwahiyo inabidi usome alichoandika mtu, siyo kutafsiri kwa mtazamo wako. Ni hatari
 
"Kichuguu, post: 32464455, member: 348"]Chanzo kikubwa cha upande huu wa mjadala tunakoelekea ni pale nilipo-question mchangiaji mmoja aliyesema ana weaken institutions na alichota fedha za hazina kujenga Uwanja kijijini kwao Chato bila kibali cha Bunge. Wewe umekuwa unachangia upande huo huo wa kussuport hilo.
Kama uli question mimi nilionyesha kwa uwazi kwanini kuna wanao doubt. Hoja yangu ilikuwa moja, kwamba, kulikuwa na tatizo kuanzia mwanzo jambo ulilokubaliana nami kwamba neno Geita ni tatizo

Tofuatisha kati ya kujenga hoja na ku support. Mimi najenga hoja hata kama hutakubaliana nazo. Kwa njia hiyo sote tunaona ''blind spot''.
Ni kwa vile huwa sipendi kutumia majibu ya generalization, ndiyo maana ninapokujibu wewe ninakuaddress wewe tu bila kuhusisha wengine walio upande wako, kwa hiyo ndiyo maana sikusema kuwa "Mnaposema" bali nilisema "Unaposema."
Watu wangapi wanajua hupendi generalization? Mtu aliyesoma bandiko lako bila kupitia huko nyuma angeelewaje kuwa sijasema maneno hayo?

Utetezi wako ni flimsy na lengo halikuwa zuri. Ilikuwa kufanya implication kwa kuweka maneno nisiyosema. Ni hatari sana na sijui kama unaelewa impact yake.
This was intentional, the best way is to say sorry!
Ingawa hujaandika neno kwa neno kama nilivyo paraphrase kwenye conclusion hiyo, context ya michango yako ilikuwa hivyo kuhusu institutions.
Unaweza kuwa na tasfiri yako ambayo tunaiheshimu. Huna haki ya kufanya tafsiri yako kuwa ni ya umma! Ni hatari sana
Kama unakana kuwa huo siyo mtazamo wako, na serikali ya sasa haijaweaken Bunge, basi ni vizuri, kwani ina maana kuwa tunakubaliana sasa kuwa ni kweli Bunge lina matatizo makubwa sana kiutendaji, lakini hayasababishwi na Magufuli..
Nani kasema ndiye anayesababisha? Unaweza kuliangalia tatizo kwa jicho la wasomaji na si kwa mtazamo wako binafsi

Kabla ya rasimu ya Warioba niliwahi kusema sana hadi kuitwa mzee wa Mfumo.
Nilisema mifumo yetu ya taasisi si imara, lakini kwasasa hali ni mbaya kuliko huko nyuma.

Uliniuliza Mahakama inashinikizwa kutoa hukumu?
Sikujibu kwasababu tunaposema udhaifu hutuangalii factor moja.

Wewe ulitaka hukumu wakati mfumo wa sheria una mambo mengi sana.
Bunge nimekuonyesha matundu ambayo umekubaliana nayo
NBS nikakuuliza, mswada wa dharura na nguvu kubwa ilikuwa ya nini? Huna jibu
Nikakuonyesha jinsi taasisi kama polisi ilivyokosa credibility na integrity, ukakubaliana nami

Hoja hapa si nani kashinda nani kashindwa bali tujifunze kwa hoja bila kuwa na vinyongo.
Tuwe honest and credible.
 
Mjadala huu umeanza kukosa mwelekeo kwani sasa mjadala unaanza kuwa na lugha ambazo siyo kiwango cha platform hii.

Ngoja nikumbushe tena kuwa mimi nilianza kwa kusupport decisiveness ya uongozi wake. Nina imani kuwa kiongozi shupavu ni lazima awe decisive na unapologetic kwa mambo anayoamini. Kuna wakati tuliwahi kusema rais ni Kikwete ni dhaifu tena hapa hapa JF kwa kuwa alikuwa indecisive katika mambo mbalimbali.

Baada ya hilo la decisiveness mada ikaishia kwenye hoja mbili kuu hizi:
(a) Magufuli kachota pesa bila idhini ya bunge kwenda kujenga uwanja kwao
(b) Magufuli anajiamulia mambo peke yake kiasi kuwa anaweken institutions mbalimbali za serikali (paraphrasing) . Imefikia kuwa institutions hizo zinashinikizwa kutoa data za uwongo ili kumfurahisha yeye tu. Ninadhani hii ndiyo pia uliyotumia kusema kuwa huamini data zinazotolewa na taasisi serikali. Na vile vile kuimply kwamba hata bunge linapitisha yale mambo anayopenda yeye tu, kwa vile (I guess) Speaker ni mjumbe wa NEC.

Majibu yangu yote yako focussed kwenye hizo hoja mbili tu na nilikuwa natoa vielelezo kwa nini ninazipinga.

Sasa kama wewe ulikuwa unazungumza mambo mbali mbali hata yaliyo nje ya hoja hizo mbili, basi it is very unfortunate, mimi nilikuwa ninatafsiri majibu yako yote along hoja hizo mbili tu. I am sorry, I was too focussed.

Kwa sasa inabidi tuishie hapo
 
Mkuu Kichuguu na Rev. Kishoka

The trouble is, western theories on leadership are based on western societies, not african, so they can not really work and they have not worked in last 50 years.

Ninachoona kwenye serikali ya JPM ni kuwa kuna mentality ya "Tanzania lazima ipige hatua" come what may. Kuna kuna genuine willingness. Lakini inasikitisha kuona kuwa kumbe kuna watanzania wenzetu wanapenda status quo, tubaki tunasota tu.

These things like Decisiveness, Awareness, Focus, Accountability, Empathy, Confidence, Optimism, Honesty, Inspiration, are very good in theory, and can work in Sweden, Japan Norway and Denmark, where most of people have same or similar culture, beliefs, education levels, lakini huku kwetu ambako mtu anataka mshahara bila kazi, umeme bila kulipa kodi. Na tusiangalie kiongozi kwa kumuangalia rais peke yake, what about diwani, mbunge, waziri, mwenyekiti etc etc....nadhani waafrika tunatakiwa kuwa na akili ya kujua kuwa ni lazima tuwe na njia inayoweza kutuendeleza
 
NI KWANINI WANAMTUKANA NA KUMSIFIA NYERERE HAPO HAPO?

Mkuu Rev. Kishoka
Katika mjadala huu naomba nizungumzie mada yako kwa namna nyingine ambayo kwa kiasi fulani inafedhehesha

Siku hizi imekuwa ni kawaida kusikia watu wakiongelea '' Awamu' hii imejenga vituo vingi vya afya kuliko Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwa pamoja.

Ni hoja inayoonekana kuwa ''zungumzo' na imepangwa izungumzwe hivyo.

Wanozungumza hoja hii ni watu wenye ufahamu na weledi na hilo linaacha mwaswali kama wanafanya kwa kutojua au kwa kujua hasa tukizingatia weledi wa wengi wa wananchi wetu.

Ni upotoshaji uliokithiri usiozingatia takwimu wala mantiki unaolenga hadaa na si ukweli.

Rais mstaafu Mwinyi aliwahi kusema '' yeye hawezi kuvaa viatu vya Mwl Nyerere'' na akasema pia ''Kila zama na kitabu chake'' Maneno haya yana maana sana na sijui wanaoeneza uvumi wa vituo vya afya wanayakumbuka au kuyajua.

Niongelee zama za Nyerere ambaye kwa mtazamo wangu kauli za vituo vya afya ni kumtusi hadharani

Mwl akichukua madaraka ilikuwa zama yake na kitabu chake.
Mwl hakuwa katika nafasi yoyote ile inayolingana na waliomfuata, alianza kujenga msingi si kuezeka paa.

1. Idadi ya watu wakati wa Uhuru ilikuwa milioni 9. Alikuwa na Daktari wa tiba mwenye sifa hiyo mmoja.

Sijui kama alikuwa na Engineer zaidi ya wawil. Hakuwa na mwanasheria hadi kuazima mwanasheria mkuu kutoka nje.

Mwl hakuwa na watalaamu wa kada za kati na chini. Nchi ilikuwa haina vyanzo vya nishati kama mabwawa ya umeme.

Hatukuwa na mfumo wa kusambaza maji. Mwalimu hakuwa na viwanda zaidi ya mashine ndogo ndogo.

Hakuwa na chuo kikuu hata kimoja. Barabara hazipitiki wakati wa masika. Reli iliyokuwepo ni ya kati na kaskazini

Orodha ni ndefu na inaweza kujaza kurasa na kurasa ikionyesha changamoto alizoanza nazo Nyerere akiwa na watu milioni 9, Taifa changa lililopata uhuru.

Taifa lilihotaji kuwekwa pamoja ili kuwa na utangamano kuelekea maendeleo.
Watu hawajui kwamba Mwl aliteua hata madereva kuwa wakuu wa Wilaya achilia mbali taasisi nyingi.

Katika changamoto hizo Mw alikuwa aanze na ipi?Mwl aliyachukua mambo yote kwa pamoja hatua kwa hatua

2. Nyerere alikuta chanzo cha umeme cha Pangani, akajenga Nyumba ya Mungu na Kidatu ili tupate nishati ya uhakika
3. Mwalimu akaanzisha vyuo vya elimu ili kupata walimu wa kuliemisha taifa. Mtakumbuka Ngumbaru ili at least watu waweze hata kuandika majina yao.
4. Mwalimu akajenga vyuo vya chini vya afya (RMA), Medical assistant, Assistant medical office (AMO)
5. Mwl akajenga vyuo vya chini na kati vya kilimo na ufundi
6. Mwl akajenga chuo kikuu cha kwanza nchini kilichotoa viongozi wengi sana wakiwemo wa Tanzania ya leo
7. Akajenga barabara kuu za lami kama Segera-Chalinze ili kurahisha usafiri
8. Ni Nyerere peke yake aliyejenga reli hadi leo(TAZARA). Hizi zinzokarabatiwa hazijengwi upya
9. Alijenga reli ya Mruazi-Ruvu kurahisha mawasiliano ya reli nchini
10 Akajenga viwanda watu walikwenda ''shift' kama nchi zilizoendelea si kukaa Bar ikifika saa 10 Jioni kama leo
11.Mwalimu akajenga Hospitali ya rufaa na kutafuta watalaam
12. Akajenga vyuo vya ulinzi na usalama kama Monduli n.k.
13. Mwalimu alitoa elimu bure hadi kulipia wanafunzi nauli. Hiyo ndiyo elimu bure aliyotoa Mwl
14. Mipango ya usambazaji maji ilikuwa inaendelea kote nchini( Someni mipango ya maendeleo 1963, 1967 n.k.)

Orodha inaendelea na hayo hapo juu ni kwa ujumla wake tu. Tukianza kuchambua kwa undani orodha itapanuka sana

Yote haya Mwl aliyafanya katika mazingira magumu sana, akiwa na watu milioni 9, watalaam 0

Laiti Mwl asingejenga reli ya Tanga au Tazara akaelekeza nguvu katika vituo vya afya basi tungekuwa na vituo vya afya kila nyumba 10.

Lakini Mwl alikuwa anawaza, je, ajenge vituo vya afya bila watalaamu na vifaa ?
Zama zake vituo vya afya vilikuwa na magari kwa ajili ya referal ikibidi. Je, ndiyo hali iliyopo leo?

Lakini pia lazima tuangalie mambo kwa kutumia akili.
Hivi wakati wa population ya milioni 9 kulikuwa na sababu ya kuwa na vituo vya afya 300 kama leo tukiwa na 55 milioni? Rationale ya kwamba alijenga vituo vya afya vichache inatoka wapi?

Vituo vya afya havijengwi tu kwasababu ya ku score political point, vinajengwa kutokana na mahitaji.
Hitaji la vituo mwaka 1961 ni tofauti na 1970 au 1980 au 2000 au 2019 kutokana na ongezeko la watu.

Hoja kwamba Nyerere hakujenga vituo kama leo ni tusi. Watanzania wanaomuenzi Mwl kwa dhati wakemee tusi hili.

Kazi ya Mwl Nyerere ilikuwa ngumu na nzuri bila kupepesa. Kumlinganisha Mwl na kiongozi mwingine ni kumtukana

Tena Mwl akawa ''Bold and Daring'' kwa kutaifisha Hospitali za watu na shule ili kujenga Taifa la pamoja na kuondoa matabaka. Leo hatuoni kazi hiyo. Mwl hakuwa na resource za kutosha akachukua maamuzi magumu kabisa.

Nyerere alikuwa bold and daring kwa kila kigezo. Nchi hii ilipotoka na ilipo leo si vitu vya kulinganisha hata kidogo.

Kinachosikitisha wanaomtukana Mwl Nyerere kwa vituo vy fya kama ilivyo leo bila mantiki ni hao hao wanaomsifia pale wanapotaka kuungwa mkono.

Tuache kumtukana Mwl Nyerere kwa hoja laini zisizo na mashiko za vituo vya afya.

Kazi ya Mwl ilikuwa kubwa, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Acheni kabisa kulinganisha kazi za Mwl, mnamtusi
Tukianza kuweka kazi za viongozi katika mizani. tutaishia kudhalilishana bila sababu.

Anayedhani kuwa ni wakati wa kumweka Mwl katika mizani na kiongozi mwingie tafadhali aje hapa tuongee!!!
 
Reverend,

Asante kwa kutuletea amani tena.

Magufuli ana mapungufu kadhaa katika uongozi wake lakini ni kiongozi thabiti anayejua kusimamia analoamini. Hiyo ni sifa nzuri sana. Kuwa kiongozi mzuri siyo lazima uwe unafanya yanayofurahisha wayu tu, wakati mwingine hata yale yasiyofurahisha watu mradi tu yana malengo mazuri. Zamani sana Nyerere alitoa mfano wa mgonjwa wa Malaria anayeota jua: ukilazimisha kwenda kivulini, atachukia lakini hiyo ndiyo hatua inayomsaidia mwili wake. Magufuli kwa kiasi fulani amelazimisha wagonjwa wa Malaria kwenda kivulini

Uthubutu ni jambo moja, lakini katika uongozi tunafahamu ya kwamba kila nafasi ina ukomo wake. Uthubutu unaoonyeshwa na Rais Magufuli katika mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa nchi na uelekeo wetu kama Taifa ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ambayo yatachukua si tu viongozi wenye uthubutu kufanikiwa, lakini pia muda mrefu na inawezekana kabisa kuwa kilele cha mafanikio hayo kitaonekana wakati wa vipindi vijavyo vya utawala.

Najaribu kuangalia 'continuity plan' ya uthubutu wa Mh. Magufuli na nabaki na jibu moja tu; safari ya kurudi pale tulipotoka kabla ya Magufuli. Wakati yeye anaonyesha uthubutu, asilimia kubwa ya waliomzunguka, wambao wanaandaliwa kuwa viongozi baada ya wakati wake kumalizika wamekuwa ni watu wa kutukuza tu yale yanayofanywa na Mh Rais lakini sio wafuasi wa falsafa za Jiwe.

Nani atathubutu baada ya Magufuli?
 
Du, nasikiwa watu sasa wana 'uthubutu' hadi wa 'kudukua' na 'kuiba' tarakilishi za DPP!
 
Mafunzo mazuri duniani ni ya vitendo; historia ya mapokeo ineonyesha kuwa wazee wa zamani walikuwa wakiwapokeza watoto wao kwa kuwaonyesha jinsi ya kufanya mambo, Watoto wenye akili walirithi, na watoto wasiokuwa na akili hawakuriti; kupokewa au kutopokewa siyo jukumu la mzee, bali ni jukumu la warithi. Kupokea huwa siyo 1-1, bali ni kuchukua mazuri yote na kuboresha yale yaliyokuwa na mapungufu. Tanzania tunajua kuwa waliomfuata Nyerere hawakutaka kupokea bali walianza yao, na waliofuata nao wakaanza yao, na ikawa vivyo hivyo; historia ina heshima yake katika jamii. Iwapo kiongozi atakayefuata ataamua naye kujianzishia ya kwake kama waliomfuata Nyerere basi, tatizo siyo la kiongozi aliyetangulia bali linakuwa ni la jamii yetu sisi wenyewe kutotaka uthubutu. Katzi ya kiongozi nji kuonyesha njia, siyo kufundisha watu jinsi ya kufuata njia hiyo.
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾
Hatari ni kuwa hana Muda wakujenga BOLD and DARING Institutions( Kitu nachoamini akitaka anaweza na akiondoka tutamkumbuka kwa kujenga strong institutions) , yuko busy Kujijenga yeye.
Muda utasema.
 
Unaweza ukawa na sifa hizo za uthubutu, kusimamia unachokiamini etc lakini katika muelekeo ambao sio.


Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa BOLD na kuwa RECKLESS.
Kuna uthubutu (Bold) na umbwiga (Coward)
Kiongozi anayethubutu ni yule anayetenda ndani ya ' uwanja' na kutibitisha (prove wrong) wanaomcharura
Hapa Mkapa alikuwa ni 'mwalimu' . Wapinzani wakileta hoja yeye alijibu kwa hoja

Huyu aliyeondoka hakupenda hoja na alizijibu kwa kukimbilia sheria (coward)
Mfano sheria ya utakatishaji fedha ilitungwa kuweka watu mahabusu bila sababu.
Hivi kuna money laundering ya sh Milioni 10 ambazo ni takribani dola 3500!
Sheria ya kuzuia baadhi ya viongozi wasishtakiwa ilikuwa woga (coward)
Sheria za takwimu ni woga tu
Orodha inaendelea na hakuna 'bold' yoyote

Mtu anatathminiwa kwa Utu siyo vitu.
Ukiyafanya hayo kama mizani, ilikuwa failure. Utu ulipotea katika jamii, mifarakano, migawanyiko n.k

Mzee Mwinyi anasema 'Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana na anapofariki inabaki hadithi basi hadithi hiyo iwe nzuri'' .

Sina uhakika na tathmini lakini nina nina uhakika na kitu kimoja ' watangulizi' hadithi haikuwa hivi
 
Alikuwa BOLD kwenye kufanya maamuzi lakini RECKLESS kwa kufanya maamuzi kinyume na sheria, kanuni na taratibu... matokeo yake kusababisha maumivu kwa wananchi mfano mzuri ni sakata ka korosho, vyeti feki etc.

Alikuwa BOLD kusimamia alichokiamini na kusema mambo bila kuficha lakini RECKLESS kwa kutokuwa na kifua cha kupokea criticism dhidi yake... kauli mbiu yake ya msema kweli ni mpenzi wa Mungu ilikuwa applicable pale tu yeye ndio anaesema ukweli na sio wakati yeye anaambiwa ukweli na katika hilo amekuwa nana simile wala huruma kwa wote waliojaribu kumkosoa.
 
Alikuwa BOLD kwenye kufanya maamuzi lakini RECKLESS kwa kufanya maamuzi kinyume na sheria, kanuni na taratibu... matokeo yake kusababisha maumivu kwa wananchi mfano mzuri ni sakata ka korosho, vyeti feki etc.

Alikuwa BOLD kusimamia alichokiamini na kusema mambo bila kuficha lakini RECKLESS kwa kutokuwa na kifua cha kupokea criticism dhidi yake... kauli mbiu yake ya msema kweli ni mpenzi wa Mungu ilikuwa applicable pale tu yeye ndio anaesema ukweli na sio wakati yeye anaambiwa ukweli na katika hilo amekuwa nana simile wala huruma kwa wote waliojaribu kumkosoa.
Hakuwa 'bold' hata kidogo. Alikuwa mbabe na mwoga asiyeweza kukabiliana na challenges (coward)

Ukisoma maandiko ya watu wengi ikiwemo waliomuunga mkono, jambo moja wanalalamika ni yeye kuua Taasisi

Hili jambo tulijadili sana miaka ya nyuma hapa JF na kwamba ni hatari sana kwa ustawi wa jamii yetu.
Hakuamini wala kuheshimu katiba na kwamba alitaka kuwa katiba , serikali na nchi.

Tunashukuru mungu kwamba ipo taasisi moja ambayo kwa ' rumours' imetusaidia sana katika kipindi kigumu

Tazama suala la kuugua hadi kufariki kwakwe lilivyo kuwa handled, ilikuwa reckless and chaos kwasababu hakukuwepo na taasisi bali inner circle yake tu iliyoamua mambo tu.

Taasisi na mihimili mingine nje ya ule 'uliojichimbia' chini zaidi imekufa.
Taasisi kama zile zinazotoa haki zinapopoteza imani kwa umma ni hatari

Kuua taasisi ikiwemo vyombo vya habari, kumiliki vyombo vya habari mwenyewe na kutengeneza monopoly katika utawala ni mambo yaliyodhoofisha sana Taifa.
 
Back
Top Bottom