The Daring and Bold Magufuli

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Kama kuna kitu cha wazi ambacho ni funzo kubwa kwetu Watanzania katika miaka minne hii ya Awamu ya Tano na "Utawala" (maksudi kabisa badala ya kutumia uongozi) wa Magufuli ni UTHUBUTU!

Uthubutu, ni uwezo wa kufanya mambo bila kuwa na kigugumizi au kujishuku. Ni kufanya mambo, kusimamia unaloliamini bila kujali au bila woga. Sasa kwa Magufuli ambaye tulijua akiwa waziri alikuwa ni mchapakazi mpaka kuitwa bulldozer, ilimaanisha alifanya mambo jinsi alivyoona ni sawa kwa nafasi yake na sasa kwa kupata Urais n kuwa Rais wa Jamhuri, basi Ari, Kasi na Nguvu zake za kuwa Bulldozer na uthubutu zimeongezeka maradufu.

Uthubutu si lazima tuutazame kwa matokeo chanya pekee, hata matokeo hasi yanaweza kutokea kutokana na mtu kuwa na uthubutu, kudhamiria na kufanya lile alilokusidia.

Rais Magufuli ametusaidia sana kutuonyesha kwa vitendo, na si semi, kauli au porojo kuwa kwenye nia pana njia.

Naam, kuna maamuzi mengi yaliyotokana na Uthubutu huu yameleta maswali mengi na hata matokeo ya "uthubutu" kuonekana kama hatua ambazo zilikosa weledi, busara, uhakika au hata hekima. Lakini cha msingi kwa andiko langu hili si kukosoa au kusifia mafanikio au kushindwa kwa maamuzi aliyoyafanya, la hasha... naangalia silika ya kibinadamu ya kuwa na uthubutu, Daring!

Nakumbuka miaka 10 ya Rais Kikwete, uongozi au utawala wake ulionekana umepwaya kwa kukosa Uthubuu wa ukali na kusimamia mambo yafanyike, bila kujali matokeo. Nakumbuka mgombea wa Urais 2015 Bwana Lowassa alinukuliwa mara kadhaa akisema Tanzania inahitaji mtu mwenye kufanya maamuzi magumu, na Watanzania ule u-soft soft wa awamu ya nne, ulitufanya tutake kupata mtu "Dikteta" kauli na nadharia ambazo kwa umoja wa Kitaifa bila hata chembe ya tofauti za kisiasa ai itikadi, ilikuwa ni "natural" kukubali uhitaji wa kuwa na Rais Mkali, Dikteta!

Magufuli kathibitisha katika uanadamu kuwa Uthubutu si jambo la kusadikika, bali li jambo la kweli, lina uhai na kila mtu akikusudia na kujiamini, anaweza kuwa na Uthubutu!

Nikiiangalia Tanzania ilipo leo hii, miaka 58 tangu tupate Uhuru ambapo bado tuko kwenye hatua za mwanzo za kujaribu kupiga vita Ujinga, Umasikini, Maradhi, Unyonge na Utegemezi (UUMUU)pamoja na kutamka kwa vinywa vyetu mahitaji ya maendeleo ya taifa kuwa ni Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, sifa, hulka na wajihi wa kuwa na Uthubutu bado ni mchanga sana na ndio chimbuko la kukosa kujiamini, kuwa wanyonge na waoga kufanya maamuzi magumu.

Kuna dhana na falsafa inayosema fanya jambo, lisipozaa matunda chanya au uliyotegemea-matokeo hasi yanakupa fursa kurudia mchakato na kujifunza pale ulipokosea na kurudia jambo kwa ubora na umakini zaidi. Cha msingi ni kujiamini na kuwa na uthububu wa kufanya mambo.

Sasa kwa Tanzania yetu ya leo "Ya Magufuli" ya "MATAGA" na "CCM Mpya" utegemezi wa mwenye kujiamini na mwenye kuthubutu kumebakia kuegemea na kumtegemea mtu mmoja, Rais Magufuli. Wengine wote wamekaa kando wakishangilia na kusifia lakini hawana Uthubutu wa kwao wa kujitegemea na kwa nafsi zao bila kutegemea na kuzengea Uthubutu wa magufuli ambao sasa umeambatana na mamlaka na dhama kubwa kama Rais wa nchi.

Tumeshuhudia watendaji wa Serikali na Wanasiasa ambao wana majukumu ya kuongoza nchi, wakigeuka kuwa Wanyapara, wasiojiamini, wakitegemea sana UDola wa Kimamlaka na zaidi turufu yao kubwa ni kusema "maagizo kutoka juu" wakimaanisha ni maelekezo na maagizo ya Magufuli, wakikimbilia kuutegemea Uthubutu wa Magufuli kama ngao na nguzo.

Nasi wananchi ambao hatuna mamlaka au dhamana ya kiuongozi au madaraka, nasi tumekaa kando kwa unyonge au kuachia kila kitu kifanywe na kuamini na kutegemea "ah Magufuli ni kiboko".

Leo haki ya mwananchi inakanyagwa na kupuuzwa, tunakosa Uthubutu wa kudai haki na kusimama imara kukataa kuburuzwa. Ndio kuna hofu na mazingira ya kutishiana ambayo yanatufanya kukosa kujiamini, lakini kwa nini hatumtazami Magufuli yule aliyekuwa Waziri ambaye alisimama na kupata alichotaka na kudhamiria mpaka tukamsifia kwa ujenzi wa miundo mbinu Tanzania?

Nimesema awali, Uthubutu si lazima uzae matoke chanya (ambayo yanaweza kuwa ni mtazamo wa mtu, kikundi au wa aina moja au nyingine) au matendo yanayotikana na Uthubutu yapokelewe kwa mikono miwili na kila mtu. Lakini laiti kama kila mmoja wetu kwa miaka 58 tangu tupate Uhuru wetu tungekuwa na utashi, uimara, ujeuri, kujiamini na uthubutu hata kwa asilimia 50% a uthubutu wa Magufuli, si ajabu Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye maendeleo yake ya uchumi, kupanuka na kukomaa kwa haki za watu na yote ambayo tunanung'unikia leo, si ajabu yasingekuwa manung'uniko au kero za kutukosesha raha.

Nikiangalia na kupima Uthubutu wa Magufuli, kuna mengi kafanya (kutenda si lazima kuwe ni sifa ya kufanikiwa jambo) kwa kuamua. Ama ni kutoa maagizo, kuamrisha na kusimamia kikafanyika bila kujali matokeo (consequences or final result) au kuangalia hisia za watu. Mfano, aliazimia kupanuliwa kwa barabara, kukafanyika ubomoaji ili kupisha upanuzi wa barabara hata njia ya reli ya SGR. Hakusubiri majadiliano ingawa yawezekana kukawa na gharama kubwa kwa maamuzi hayo hasa pale penye malalamiko ya fidia.

Akaamua kununua ndege kwa fedha taslimu, zimenunuliwa ndege 5 kwa mkupuo tena kwa fedha taslimu bila kuwa na ukiritimba ambao Serikali na ATCL walifanya kwa miaka 20 kabla ya Magufuli kuboresha au kuwezesha Shirika la ndege kuwa na ndege za kutosha (wengi mtakumbuka ndege za Mattaka). Akasitisha mazoea ya kusafirisafiri ya viongozi na watendaji wa Serikali bila kujali kama kulikuwa na umuhimu wa uwepo na uwakilishi wetu au la, lakini amri yake ilisikilizwa kwa kuwa alisema atatumbua. Leo tumeona Chato inajengwa kwa kasi kubwa; iwe ni maagizo, amri au watu "kujituma" kuhakikisha Chato inakuwa na hadhi kubwa na sasa inageuka kuwa kivutio cha biashara na utalii. Akasema kufanyike uhakiki wa vyeti, wa wafanyakazi wa Serikali, nayo yakatimia. Akasema lazima kila mtu apate stakabadhi akinunua bidhaa ili Serikali ipate mapato... leo kila mtu anahangaika kuwa na stakabadhi! Akasema lazima tuhamie Dodoma, iwe kumekamilika au la, watu wakahamia Dodoma, wengine ofisi ziko kwenye vibanda na wanakaa vyumba vya kupanga.. lakini Serikali imehamia Dodoma.

Sasa najiuliza, sisi kilitushinda nini miaka yote kufanya maamuzi kama haya?ni kigugumizi gani kilitushika kwa muda mrefu kufanya mambo na kuwa na uthubutu, bila kuwa na woga au kujiumauma? kwa nini tuliamini hatuna uwezo wa kufanya mambo kwa hiari lakini tunafanya sasa kwa kuamrishwa na ni sawa na kwamaba tunachapwa mijeledi, tunazinduka na kufanya?

Leo nina uhakika Magufuli akisema tunarasimisha Katiba ya Wananchi iliyotokana na Rasimu ya Warioba, litafanyika bila kupingwa au miguno. Sheria kadhaa na miswaada imepelekwa bungeni na "Chama tawala" ama kwa woga, unafiki au labda ukweli halisi kimepigia kura na kupitisha kila kilichopelekwa na Serikali ya awamu ya tano. Rais Magufuli leo akisema ni marufuku kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa, hakuna atakayebisha.

Sasa ni rahisi kusema yeye ana mamlaka makubwa na anatumia cheo chake, lakini ukweli unabakia kuwa anayafanya kutokana na Uthubutu, daring.. hata kama mara nyingine ni kiholela (reckless) au ni kishari (mercilessly), but he gets shit done regardless.

Je sisi wote tungeanza kujiamini na kuanza kuwa na uthubutu bila woga kufanya mambo tunayoamini ni haki yetu kikatiba, ni wajibu wetu kusimama kuyapigania. Iwe ni nyumbani, makazini, kwenye masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiuzalishaji na kila jambo, uwe ni mfanyakazi, mwajiri, mfanyabiashara, mwanasiasa.. tukiwa wote na uthubutu, na tukafanya maamuzi kwa umakini lakini tukisimama imara kwa uthubutu, basi Tanzania ya Viwanda na Gurudumu letu la maendelo litapiga hatua kubwa na za haraka sana.

Lakini tukiendelea kwua Wategemezi wa magufuli, siku anaondoka tutarudi kule kule, kukwama matopeni na hata kuwa na mawazo potofu ambayo yanajengwa sasa hivi kusema tunahitaji Magufuli akae zaidi ya muda ulioko kwenye katiba.

Namshukuru sana kwa kutuonyesha Uthubutu, tuungane, tusimame imara tufanye mambo kwa uthubutu kupata haki zetu na maedneleo ya kweli na endelevu.

Ahsante Rais Magufuli kwa kutufundisha Uthubutu! Daring, Boldness.. Get Shit Done attitude!
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
Hitler did all that bau because of lack of freedom of speech his personal were not happy. What Magufuli is doing a white man could have done better but we chose to be free. We don’t need to be oppressed now.
Comrade Mzuvendi,

It had been years since we enjpyed such discussions.

I have highlighted few things on your first paragraph and I am very much alarmed by your comments which comes across as adoration of the "strong leadership" even though in true essence it isnt leadership but a type of Ops Manager or the MBWA typw (management by walking around) which isnt leadership at all. What is evenscary is that at nearly 60 years of self independence, there is a desparate need ya the type of "hands on " leader which is a result of delegation of responsibility hasn't worked well.

The quesion is would this shaking up things would result to a new norm? ridding paying lip service, reversing micro management and allow delegation to take place? would the new day become self sustainable and durable to last at least3 to 4 future decades with leadership rotation to come afte Magufuli?

Lastly, why does Tanzania at 58 years old, needed to have a micro manager as president of the country? Why arent we self propelling to get things done and we had to require mkung'uto na virungu to get the gurudumu la Taifa move somehow from tope... regardless if its moving to the right direction or not?

Do we have a succession (successor) system that can carry one the tempo, zeal and attitude ya result orianted leadership.. au kama kawaida tutakwenda through phase ya "hebu tupumue kwanza'? and if as taifa we choose "hebu tupumue kwanza"... don't wea ll think its time to do soul search to how we got there?
Rev. Kishoka;

Let me put this way. I am desperate for results in some key areas such as transportation, efficient in delivering government services and energy. When you so desperate, you can easily overlook serious shortcomings of the individual and give the person the benefits of the doubts. So, to be honest with you I think that is what I have done with Magufuli. The relationship I have with his presidency is very transactional. Take my liberty, freedom of speech and in return build me the railways.

I supports some of his initiatives lukewarmly as I wait for the results. If he finishes the railway lines in timely fashion, I will be elated because a robust transportation system in the country will improve commerce greatly and empower our people than other government program. The same applies to the proper use of our energy sources the country us.

At heat I am a very liberal person. I love democracy, the rule of law, and personnel liberty. For example, it won’t offend me if the LGBT community organizes a parade in the streets of Dar Es Salaam. However, I have become a realistic. Now I believe that strong institutions of the country, strong democracy, and the rule of law aren’t the outcome of textbook exercise as many Tanzania think. Rather, they are the results of historical events which have happened in the country, some of them very painful. So, to me, Magufuli’s leadership style is an historical event which might help shape the way we view our leaders.

So in summary, I have decided to sacrify my values for results. I am gambling here that the good results in transportation, government services, and energy sector might be good for the country at least in a short term. However, in a long term, his leadership style might force the next generation create democratic and strong institutions rooted in the current historical events.
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
Hitler did all that because of lack of freedom of speech his people were not happy. What Magufuli is doing a white man could have done better but we chose to be free. We don’t need to be oppressed now.
Hitler was in a league of his own. So we shouldn't go there or try to equate German situation of 1930s to what we have in Tanzania. In Tanzania, everything you exercise is a textbook material. The freedom of speech, rule of law, and democracy are things we have learn from others or we have forced to learn. What the point of having democracy when the elected leaders can't take their responsibilities very seriously?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
This notion of weakening institutions is very conjectural because I see all institutions running smoothly. The Parliament, Ministries, Courts, National Defense and Security Forces and all organs are running as expected. Of course is not business as usual, they have to run at some standard; if the head of some institution cannot lead that institution at the expected standard, it is fine for the president to let him/her go. The days of business as usual are gone
Mkuu Kichuguu, nimesoma kwa mshtuko mkubwa habari hii!

Kwamba institutions zetu zipo strong and running smooth! real! seriously!

1. Parliament: Hivi hii ni taasisi unayoweza kusikiliza inasema nini zama hizi!
Kwamba, umekaa chini unasikiliza na kutafakari Bunge limefanya nini kama rubber stamp

2. Ministries: Hizi si taasisi tunazoweza kuziita si za maana, ni sehemu ya mkono wa siasa tu
Ndiyo maana kila siku kunaweza kuwa na mabadiliko ya kuvunjwa, viongozi n.k.

3. Courts: Tangu Uhuru hakuna wakati Mahakama zetu zimetiliwa shaka kuliko kipindi hiki
Ni kwamba, watu wanazitumia kwasababu kisheria ndizo zilizopo, otherwise huu mi mhimili unaopoteza sifa kila uchao! Huu si mhimili wa watu kama akina Nyalali n.k.

4. National defense: Hii ndiyo taasisi iliyobaki imara, ingawa kuna dalili za kuingiliwa kisiasa

5.Security Forces: Hapa ni Polisi, Usalama, Ofisi ya DCI na DPP n.k
Mkuu haya yanayoendelea katika namna zinazotatiza na ku disturb ndiyo running smooth!

6. Umesahau Media house ambayo ndiyo mwathirika mkuu wa deteriorations ya institutions

Kwa ufupi ni kuwa katika nyakati zetu hakuna kipindi institutions zimeonekana kupoteza nguvu kama zama hizi.

Hatuongelei viongozi wa hizo taasisi tunaongelea taasisi katika uhuru na uwajibikaji

Mkuu Kibanga Ampiga Mkoloni kasema kuhusu strong institutions. Hii imekuwa hoja yangu kwa miaka mingi hapa jamvini. Siamini katika uwezo binafsi, naamini uwezo ndani ya taasisi

Kama kuna jambo la hatari tunalofanya ni kudhoofisha taasisi tukitegemea watu
Nyerere alipofariki nchi iliendelea kwasababu ya strong institutions

India ilikaa miezi 3 bila PM, UK wiki 3 na nchi iliendelea
Sisi alipojiuzulu PM tukaambiwa nchi imetikisika. Hapa huoni tatizo kweli

Nchi haipaswi kutegemea personality, inatakiwa isimame katika strong institutions

Mkuu with all due respect I'm shocked to the core! I'm struggling to decipher your message
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Usifuate unaloambiwa na wanasiasa, wewe chukua muda usome documents halisi.

Soma hotuba za bajeti za wizara ya uchukuzi na Ujenzi zote kwa miaka hiyo minne, halafu pia usome ripoti za ukaguzi kwa miaka yote minne.

Soma mwenyewe, usipewe summary na mtu mwingine;
ukitegemea summary utalatewa summary ya William Barr kuwa there was no collusion!

Kama pesa zingekuwa zinachotwa kinyemela namna hiyo halafu kuna matokeo tunayoona, basi ni wazi kuwa serikali zilizopita zilikuwa zinachota kwa vifaru.
Mkuu kuna mahali unanichanganya kidogo labda kwa ubutu wangu wa kuelewa

Unasema tusiwasikilize wanasiasa kama Zitto bali tutafute nyaraka tusome
Nyaraka unazotuletea ni kama Bajeti ambayo imeandaliwa kwa msukumo wa wanasiasa
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Data utazitoa wapi hali watoa data wanabambikwa kesi? Kwa Mh.Kikwete tuliona kwa sababu watu waliruhusiwa kusema kile ambacho wewe unaona kilikuwa kibaya kwa wakati ule..hv sasa utapata habari kutoka serikalini tu hakuna chanzo chochote cha habari.
Maneno mazito haya!

Kwamba, tusome bajeti inayoandaliwa na wanasiasa lakini tusiwasikilize wanasiasa!!

Ukitaka kujua kuna jambo, fikiri kuwa Wapinzani hawatakiwi kuhoji kwa bajeti mbadala
Yaani Bajeti ya Wapinzani lazima ihaririwe na ofisi ya Bunge, hii maana yake nini!

Mkuu anatushauri tusome takwimu za serikali.
Uchumi unakuwa kwa asilimia 7, IMF wanasema unakuwa kwa asiilimia 5.

Kwavile vyanzo vya takwimu vina ''monopoly'' kwanini akitokea mtu akaweka data mbadala tuone kama anapotosha! Kwamba, Bunge ni la ndiyoo na huku mtaani tuishi kwa ndiyoo!
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32398457, member: 348"]
Unaweza kupinga jambo lolote lakini lipinge ukiwa na ushahidi wa kwa nini unapinga. Wengie wamekuwa wanalalamika hapa kwa kutumia data za Zitto ambazo na kujipikia.
Data za uhakika tunazipata kutoka wapi? Hapa ndipo hutuelezi na ningeomba utusaidie
Kitu ambacho watu wangelalamikia zaidi ni kuwa miradi yote ya ujenzi inayolipiwa na pesa za serikali iajiri watanzania wengi kwa malipo mazuri kusudi pesa hizo ziingine mitaani tena,
Mkuu kwa sisi wengi tumeona mengi. Ninakuhakikishia kuwa kuna ushahidi usio na shaka wa kwamba sisi hatuwezi. Wakati wa Mkapa dhana hii ilitumika, matokeo yake barabara zilijengwa kwa lami na mafagio. Contractor hana hata Lori ya kubeba lami!

Lakini pia utaajiri Watanzania wapi katika kazi zinazohitaji teknolojia na elimu?
Wakorea wanajenga daraja, wana tenda na wanataka faida. Utaajiri watanzania wapi zaidi ya wafunga nondo? Na huyo mfunga nondo unataka alipwe milioni 6! Please

Reli inajengwa na Waturuki,sababu ni moja sisi hatuna uwezo wa ufundi
Hii haina maana ni mazezeta, hapana, ni kwasababu ulaji umetangulia na kazi haitafanyika
Unaweza kushangaa mataruma ya mbao! ilimradi watu wote kuanzia juu wanapiga

Sasa sijui ni miradi gani ikiwa kule Songea daraja la miti limejengwa kwa milioni 7
Pitia kumbukumbu za JF utaona hilo, na huo ni mfano mzuri kwamba sisi bado. Matumbo tu
Mimi ninakumbukua kuwa miaka ya themanini wakati wa miradi ya Nyerere, wazungu kwenye miradi ile walikuwa ni wale mabosi wa ufundi tu, lakini watumishi wengine wote walikuwa watanzania, na pesa za miradi ile nyingi zilikuwa zinarudi mitaani.
Si kweli na nina mifano ya kutosha. Si kweli kabisa
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mkuu Kichuguu, nimesoma kwa mshtuko mkubwa habari hii!

Kwamba institutions zetu zipo strong and running smooth! real! seriously!

1. Parliament: Hivi hii ni taasisi unayoweza kusikiliza inasema nini zama hizi!
Kwamba, umekaa chini unasikiliza na kutafakari Bunge limefanya nini kama rubber stamp

2. Ministries: Hizi si taasisi tunazoweza kuziita si za maana, ni sehemu ya mkono wa siasa tu
Ndiyo maana kila siku kunaweza kuwa na mabadiliko ya kuvunjwa, viongozi n.k.

3. Courts: Tangu Uhuru hakuna wakati Mahakama zetu zimetiliwa shaka kuliko kipindi hiki
Ni kwamba, watu wanazitumia kwasababu kisheria ndizo zilizopo, otherwise huu mi mhimili unaopoteza sifa kila uchao! Huu si mhimili wa watu kama akina Nyalali n.k.

4. National defense: Hii ndiyo taasisi iliyobaki imara, ingawa kuna dalili za kuingiliwa kisiasa

5.Security Forces: Hapa ni Polisi, Usalama, Ofisi ya DCI na DPP n.k
Mkuu haya yanayoendelea katika namna zinazotatiza na ku disturb ndiyo running smooth!

6. Umesahau Media house ambayo ndiyo mwathirika mkuu wa deteriorations ya institutions

Kwa ufupi ni kuwa katika nyakati zetu hakuna kipindi institutions zimeonekana kupoteza nguvu kama zama hizi.

Hatuongelei viongozi wa hizo taasisi tunaongelea taasisi katika uhuru na uwajibikaji

Mkuu Kibanga Ampiga Mkoloni kasema kuhusu strong institutions. Hii imekuwa hoja yangu kwa miaka mingi hapa jamvini. Siamini katika uwezo binafsi, naamini uwezo ndani ya taasisi

Kama kuna jambo la hatari tunalofanya ni kudhoofisha taasisi tukitegemea watu
Nyerere alipofariki nchi iliendelea kwasababu ya strong institutions

India ilikaa miezi 3 bila PM, UK wiki 3 na nchi iliendelea
Sisi alipojiuzulu PM tukaambiwa nchi imetikisika. Hapa huoni tatizo kweli

Nchi haipaswi kutegemea personality, inatakiwa isimame katika strong institutions

Mkuu with all due respect I'm shocked to the core! I'm struggling to decipher your message
Maelezo yako ni sawa kabisa kuhusu weaknesses za hizo institutions, na kama nimekusoma vizuri ni kuwa ziko weak siku zote tangu Uhuru. Sasa kama ni hivyo, ndiyo maana napinga hiyo notion ya kuwa Magufuli ana weaken institutions ambazo sote tunajua kuwa ziko hivyo hivyo siku zote. Nilichotaka kusistiza ni kuwa institutions ziko kama zilivyokuwa siku zote, Magufuli hajaleta mabadiliko yoyote ya kuziweaken. Mawaziri kufukuzwa ndiyo niliyokuwa nasisitiza kuwa wasifanye bussiness as usual.

Swala la Rais kuwa na madaraka makubwa kikatiba ndiyo chanzo cha kuwa na institutions weak, na hilo tuliwahi kulipigia kelele sana hapa la kutaka Rais apunguziwe madaraka na waryoba katuletea katiba nzuri lakini kaishia kwenye droo. Kwa katiba iliyopo, mimi naona kila kitu kinakwenda sawa kikatiba, unless tupate katiba nzuri zaidi.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari sitaliongelea kwa kina kwani linauma pande zote mbili; yaani kuna makosa ya serikali na makosa ya vyombo vya habari vyenyewe. Sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 imekopi vifungu vingi kutoka kwenye sheria za zamani za 1976 na 1994. Sheria hizo zote zilikuwa za kikatili kwa vyombo vya habari na zimepitwa na wakati katika mazingira ya leo, na hapa ndipo linapokuwa swala la Bunge kuwa makini kupitisha sheria nzuri badala ya kuwa rubber stamp tu kama nilivyoeleza huko nyuma Serikali ililea mswada mbovu lakini ukapitishwa na bunge kuwa sheria. Hii ni pamoja na sheria ya mtandano ambayo tumeipinga sana humu. Sasa kwa upande wa vyombo inabidi vitambue kuwa vinafanya chini ya sheria zipi, siyo wazivunje tu eti kwa vile ni sheria mbaya. Ni lazima tuwe ni taifa linaloheshimu sheria zake.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Maneno mazito haya!

Kwamba, tusome bajeti inayoandaliwa na wanasiasa lakini tusiwasikilize wanasiasa!!

Ukitaka kujua kuna jambo, fikiri kuwa Wapinzani hawatakiwi kuhoji kwa bajeti mbadala
Yaani Bajeti ya Wapinzani lazima ihaririwe na ofisi ya Bunge, hii maana yake nini!

Mkuu anatushauri tusome takwimu za serikali.
Uchumi unakuwa kwa asilimia 7, IMF wanasema unakuwa kwa asiilimia 5.

Kwavile vyanzo vya takwimu vina ''monopoly'' kwanini akitokea mtu akaweka data mbadala tuone kama anapotosha! Kwamba, Bunge ni la ndiyoo na huku mtaani tuishi kwa ndiyoo!
Data za uhakika tunazipata kutoka wapi? Hapa ndipo hutuelezi na ningeomba utusaidie
Mkuu kwa sisi wengi tumeona mengi. Ninakuhakikishia kuwa kuna ushahidi usio na shaka wa kwamba sisi hatuwezi. Wakati wa Mkapa dhana hii ilitumika, matokeo yake barabara zilijengwa kwa lami na mafagio. Contractor hana hata Lori ya kubeba lami!

Mkuu kuna mahali unanichanganya kidogo labda kwa ubutu wangu wa kuelewa

Unasema tusiwasikilize wanasiasa kama Zitto bali tutafute nyaraka tusome
Nyaraka unazotuletea ni kama Bajeti ambayo imeandaliwa kwa msukumo wa wanasiasa
Bunge siyo serikali kuu, haliko chini ya rais; uzembe wa Bunge usichukuliwe kuwa ni Uzembe wa serikali kuu. Nnimeandika huko nyuma kidogo kuhusu uzembe wa Bunge katika kutunga sheria za nchi.

Bajeti za serikali huwa hazitayarishwi na wanasiasa, kuna jopo kubwa la wataalamu wa uchumi na uhasibu ndio hutayarisha bajeti zile kwa kushirikiana na wataalamu wa field nyingine mbalimbali kutoka mawizarani na tena baada ya kukusanya data za nchi nzima. Waziri anaisoma tu, halafu wabunge wetu wanasikiliza tu.

Kuhusu kumuamini Zitto hiyo ni haki ya kila raia kuamua wa kumuamini mtu wake. Najua Marekani kuna watu wanamuamini Trump hata kama anapoongopa waziwazi. Nimeshafuatilia sana malalamaiko ya Zitto na kuconclude kuwa mengi ni baseless. Anaposema kuwa pesa zimechotwa kinyemela wakati kweli bajeti inaonyesha kuwa zilipitishwa na bunge ni wazi kuwa kajitungia, na iwapo wewe hutapenda kusoma bajeti hiyo basi pia utakuwa ni victim wake na hiyo ni haki yako. Nimeonyesha huko nyuma kuwa manunuzi yote ya ndege yalikuwa kwenye bajeti lakini Zitto aliwahi kuibuka akidai kuwa Serikali ilichota hela hazina kwenda kununua ndege bila kupitishwa na Bunge. Kuna siku alidai kuwa ile Dreamliner ni terrible teen, nikamletea idadi ya ndege zote za Terrible teens na waliozinunua. Kuna mambo mengi yameibuliwa na Zitto na kuonekana kuwa siyo kweli; amekuwa conspiracy theorist mkubwa sana siku hizi. Inahitaji open mind kubwa kutafuta ukweli kamili uko wapi katika kila madai yake, ila ukisoma na confirmation bias in mind, basi utakuwa ni victim wake siku zote.

Kuhusu data mbalimbali za serikali zipo na ni accessible sana, ni kwa vile watu wengi hawataki kuzitafuta wanasubiri kuambiwa na wanasiasa kama Zitto na kumkubalia moja kwa moja hata kama anapotosha. Mimi niliweza kupata data za wizara ya Ujenzi Uchukuzi na mawasiliano (http://mwtc.go.tz/), Wizara ya fedha (http://www.mof.go.tz/), benki kuu (https://www.bot.go.tz/), national Bureau of Statistics (https://www.nbs.go.tz); nina imani unaweza kupata data za Wizara nyingine kwa njia hiyo hiyo kwani website za serikali ziko current sana sasa hivi kuliko zamani. Hata World Bank na IMF wanatumia data hizo hizo, hawana kitengo chao binafsi cha kukusanya data za nchi. Data za Uchumi kutoka World Bank ni hizi hapa kwenye excel file, na report ya NBS iko kwenye hilo faili la pdf. Zaidi zaidi ninataka uangalie hii page ya World bank ambayo ina visual aids nzuri kuliko kupitia namba za kwenye hilo excel file.

https://data.worldbank.org/country/tanzania
Weka mkazo kwenye hiyo Graph ya kwanza ya GDP uweke mouse yako mwisho kabisa itakuonyesha kuwa GDP ya mwaka 2018 ilikuwa ni $57.437b kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini
1565159855394.png

Halafu ukirudisha mouse nyuma kidogo, itakuonyesha kuwa GDP ya mwaka 2017 ilikuwa ni $53.321b kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini

1565159934154.png

Sasa wewe piga mahesabu ya growth rate kutoka 57.437 mwaka 2017 hadi 53.321 mwaka 2018 kama hutapa
{(57.437-53.321)/53.321}x100=7.72% tena ambayo ni zaidi ya ile iliyoko kwenye ripoti ya NBS na Benki kuu; inawezekana NBS wanatumia moving average method kuliko hiyo instantaneous value.

1565162359909.png

Hata hivyo, unaona kuwa hiyo ripoti ya 5.5% ni namba za kupikwa tu. Hata kama ingekuwa ni moving average ya miaka kumi kumi bado isingefika namba hiyo ya 5.5% ya IMF. Sijui motive ya IMF kupika namba hizo lakini data zinaonyesha kuwa utegemezi wa Tanzania kwa IMF umepungua sana kwa miaka ya hivi karibuni. Unlike World bank, hawana data za kina kuhusu Uchumi wa Tanzania; angalia hapa

https://www.imf.org/en/Countries/ResRep/TZA
Utasemaje kuwa data zao ndizo za kuaminika kuliko za Serikali na za World bank wakati wao wenyewe hawana database yoyote?

Lakini pia utaajiri Watanzania wapi katika kazi zinazohitaji teknolojia na elimu?
Wakorea wanajenga daraja, wana tenda na wanataka faida. Utaajiri watanzania wapi zaidi ya wafunga nondo? Na huyo mfunga nondo unataka alipwe milioni 6! Please

Reli inajengwa na Waturuki,sababu ni moja sisi hatuna uwezo wa ufundi
Hii haina maana ni mazezeta, hapana, ni kwasababu ulaji umetangulia na kazi haitafanyika
Unaweza kushangaa mataruma ya mbao! ilimradi watu wote kuanzia juu wanapiga

Sasa sijui ni miradi gani ikiwa kule Songea daraja la miti limejengwa kwa milioni 7
Pitia kumbukumbu za JF utaona hilo, na huo ni mfano mzuri kwamba sisi bado. Matumbo tu
Si kweli na nina mifano ya kutosha. Si kweli kabisa
Inawezekana wewe hujafanya kazi za kwenye construction projects; sehemu kubwa ya kazi hizo hufanywa na watu wasiokuwa na elimu ya juu kama unavyodhani. Kinachohitajia ni wataalamu wa kuwasimamia kuhakikisha kuwa kazi inafanyika vizuri. Project kubwa inaweza kuwa na mainjinia wawili tu pamoja na superintendents labda 10 tu kati ya wafanyakazi 300 wa project ile.

Mimi nilianza kufanya kazi kwenye ile miradi ya wakati wa Nyerere mara tu nilipotoka JKT; nilifanya kwa miaka miwiwli (tulikuwa na kitu kinaitwa Azimio la Musoma wakati huo). Nilianza kwenye mradi wa kujenga barabara kutoka Mororgoro hadi Dodoma iliyokuwa inafanywa na kampuni ya Kibrazili, baada ya hapo nikahama kutoka Dumila na kwenda Mororgoro Mjini na kujiunga na kampuni nyingine ya Kibrazili kujenga karakana ya reli, muda mfupi tu nikahamia mradi wa kampuni ya wakanada ya iliyokuwa inajenga Bwawa la Mindu kwa kuwa ilikuwa ikilipa zaid ya wabrazili, na mwishowe nikahamia kampuni ya Magunia kule Industrial Park kwa kupewa cheo cha Supervisor; dakika za mwishoni nikahamia kiwanda cha Canvass (kwa sababu za ujana tu kwa vile kiwanda kile kilikuwa na wasichana wengi wakati huo) kabla sijasepa kwenda Chuo Kikuu. Katika kampuni zote nilizokutajia, kasoro Canvass, wazungu au wabrazili walikuwa ni wale mabosi wa juu tu: Project Manager, Mainjinia, na Superintendents basi. Maofisa utawala wote, accounting, machine operators, madereva, mafundi, maforeman, vibarua, mesenja, wapika chai na kahawa, wafagiaji, walinzi na kila mtu wa chini walikuwa ni watanzania tu.

Siku hizi unaona kampuni ya nje inaleta hata vibarua kutoka kwao! Wachina walileta vibarua kibao kujenga uwanja wa taifa na baada ya project wakakwepa kurudi kwao, lao hii tunasuguana nao mitaani!

Unfortunately Jamiifurms hairuhus attachement za excel; hata hivyo unaweza kulipta kwenye hiyo website ya world bank niliyoweka link yake hapo juu
 
Attachments

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Bunge linatenga pesa halafu Wizara inasimamia; kwa hiyo madai ya kuchota pesa hazina kinyemela bila kupitishwa na bunge sasa tukubali siyo kweli.

Sasa zile operational procedures za utekelezaji wa miradi hilo ni jambo la Wizara husika, siyo la Bunge. Ijulikane kuwa Geita ni mkoa mkubwa na ile Regional Airport ingeweza kujengwa sehemu yoyote ndani ya mkoa huo kwa vile hakukuwa na airport yoyote ndani ya mkoa huo wakati huo; ndiyo maana appropriation inmonyesa kabisa kuwa construction of new airport. Inaonekana wazi kabisa kuwa kulikuwa na upendeleo wa kuchagua mahala pa kujenga airport hiyo kumpendeza Magufuli personally, lakini hilo halikiuki sheria yoyote ya bunge.
Unakumbuka Mramba na Yona walifungwa kwa kutumia hiyo ministerial discretion? I wasn't addressing sheria ya Bunge bali uhalisia kuwa hatuwezi kujifanyia vitu alimradi kuna "discretion"! Where are checks and balances? Je kuna tofauti gani ya ki-memo kwa Waziri baada ya pesa kupitishwa kikisema tumia huku na si pale palipopangwa?

Am I reading you right approving all inappropriate acts zilizofanywa tangu 2016 kisa labda unapendezwa na aliyeko madarakani?
 
Mzee hii topic ya uwanja wa Chato nimepata bahati ya kuijadili na rafiki yangu mmoja wa Bukoba ambaye alikuwa anasema uwanja ule ulikuwa ujengwe Bukoba lakini ukahamishwa kinyemela. Ni kutokana na mjadala ule ndipo tuliweza kuichambua bajeti niliyoweka hapo juu. Bajeti inasema Geita Regional Airport; sasa Geita ni ama mkoani, ama wilayani na ama mjini - yenyewe ilisomeka kuwa airport inajengwa mkoani Geita; haikuwa specific kuwa ni katika mji gani kwenye mkoa huo wa Geita. Kuna hisia kuwa ilikuwa ni Geita mjini, lakini bajeti haikusema hivyo; kumbuka kuwa hata uwanja wa Kilimanjaro Interational Airport hauko Moshi mijini. Kwa hiyo wakaamua kumpelekea mkulu.

1565215123065.png

Ni kweli kuna strong suspicion kuwa uamuzi ulifanywa kwa upendeleo lakini bajeti pia haikuwa specific. Je waliaacha bajeti iwe fuzzy namna hiyo kusudi pesa ikishapitishwa ndipo wapeleke uwanja kwa mkulu? you bet. Kwa yaliyoko vitabuni, hawakuiuka lolote kuhusu kuamua kujenga uwanja huo huko walikoupeleka. Kuna viwanja ambavyo walikuwa specific kama hiki
1565215315979.png

Msalato ni eneo specific point, wakati Mkoa wa Geiya ni eneo pana sana.

Anyway, you are free to read me the way it pleases you. Tujaribu kuishi kwa facts kuliko hisia; mimi ni shabaiki sana wa wa utawala wa sheria.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Mzee Rev. Kishoka na wote wanadhani kuwa uwanja umehamishwa kinyemela, je mmekubali kuwa waliopitisha bajeti ndio waliokosea kwa kushindwa kudai specificity? na hivyo basi kujengwa uwanja huo Chato siyo kosa kabisa kulingana na bajeti hiyo ingawa siyo picha nzuri? Huko nyuma nimesema kuwa wabunge wajitahidi kuwa wanasoma na kuelewa miswada inayoletwa kwao kabla ya kuipitisha. Zamani sana kulikuwa na mbunge mmoja wa NCCR Mageuzi kutoka mkoani Arusha ndiye aliyekuwa ananifurahisha kwa kusoma miswada yote mpaka full stop; sijui aliishia wapi?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32407956, member: 348"]
Maelezo yako ni sawa kabisa kuhusu weaknesses za hizo institutions, na kama nimekusoma vizuri ni kuwa ziko weak siku zote tangu Uhuru.
Hapana! sikusema hivyo na wala hiyo siyo maana yangu. Nilichosema ni kuwa institutions zetu zimekuwa defunct kwa sasa
Huwezi kulinganisha institutions zetu wakati wa Nyerere na sasa.
Hii ni mada ndefu sana, muhimu ni kuelewa kuwa institutions zetu zipo on the verge of collapsing. Taasisi zilivyo sasa ingalikuwa wakati wa Nyerere na waliofuata tusingekuwa tulivyo

Niambie katika miaka 3 iliyopita Bunge limefanya kitu gani chenye impact katika maisha ya kawaida ya mwananchi. Please show a piece of legislation unayoona haina masilahi na utawala bali wananchi.
Sasa kama ni hivyo, ndiyo maana napinga hiyo notion ya kuwa Magufuli ana weaken institutions ambazo sote tunajua kuwa ziko hivyo hivyo siku zote.
Haya ni maoni yako, tunayaheshimu. Tusichokubaliana nacho ni kuyafanya facts. ''sote tunajua'' ni ono lako si la kila mtu. Wapo wanaosema insitutions zetu ziko ''under siege''. Ni maoni yao
Nilichotaka kusistiza ni kuwa institutions ziko kama zilivyokuwa siku zote, Magufuli hajaleta mabadiliko yoyote ya kuziweaken. Mawaziri kufukuzwa ndiyo niliyokuwa nasisitiza kuwa wasifanye bussiness as usual.
Hatujui nani kaleta mabadiliko, tunachojua ni kuwa institutions zetu zipo weak, siyo independent and that is a precursor of unforeseen....
Kwa katiba iliyopo, mimi naona kila kitu kinakwenda sawa kikatiba, unless tupate katiba nzuri zaidi.
Inawezekana, tusaidie kidogo. Katiba inafuatwa kama ilivyo?
Malalamiko ya Wapinzani kunyimwa fursa za kufanya siasa ni malalamiko nje ya katiba?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32417036, member: 348"]Mzee Rev. Kishoka na wote wanadhani kuwa uwanja umehamishwa kinyemela, je mmekubali kuwa waliopitisha bajeti ndio waliokosea kwa kushindwa kudai specificity?
Hapa unatusaidia kueleza weakness za institution ya Bunge. Uwanja ulipoanza kujengwa hadi umekamilika si suala la siku moja. Kulikuwa na fursa ya kuhoji na kuna wabunge wa upinzani walitaka kuhoji, ''Bunge'' likawanyima fursa.

Pili, kutajwa Geita haikuwa bahati mbaya, ilikuwa politically calculated. Elewa hilo
Ukisema uwanja wa Morogoro kwa maana rahisi ni ndani ya Wilaya ya Morogoro

Ukiujenga Ulanga huwezi kusema Morogoro, utasema Ulanga Morogoro
Feasibility study ilipofanyika ilikuwa katika mtazamo wa ilani ya chama. Uwanja wa Geita
Inashangaza kidogo watu kuomba pesa bila kujua wanakwenda kufanya nini na wapi

Yaani watu wanaomba pesa kabla ya study, hesabu hizo sijui zinatoka wapi
Huko nyuma nimesema kuwa wabunge wajitahidi kuwa wanasoma na kuelewa miswada inayoletwa kwao kabla ya kuipitisha.
Unakumbuka wale wabunge wa Korosho.!!! Siyo kwamba hawasomi, siyo kwamba hawaelewi. Kinachotokea ni weakness ya taasisi ya Bunge, pengine kubwa kuliko wakati wa chama kimoja. Defunct house!
Zamani sana kulikuwa na mbunge mmoja wa NCCR Mageuzi kutoka mkoani Arusha ndiye aliyekuwa ananifurahisha kwa kusoma miswada yote mpaka full stop; sijui aliishia wapi?
Hata wakiona watasema vipi wakati wanapigwa stop na kiti?
Ndiyo maana Bajeti zao zinapaswa kusomwa na ofisi ya Bunge kana kwamba Wapinzani wamekuwa watoto wa sekondari wanaoandika risala na kuiplekea kwa Headmaster kwanza

Haya yote ni ushahidi kuwa mhimili wa taasisi hiyo ni defunct
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
"Kichuguu, post: 32408550, member: 348"]
Bunge siyo serikali kuu, haliko chini ya rais; uzembe wa Bunge usichukuliwe kuwa ni Uzembe wa serikali kuu.
Sikiliza ndugu, Spika wa Bunge ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM
Sasa sijui unataka watu waeleze nini zaidi. Huwezi kutenga Bunge na serikali kwa hali ilivyo sasa.

Bajeti za serikali huwa hazitayarishwi na wanasiasa, kuna jopo kubwa la wataalamu wa uchumi na uhasibu ndio hutayarisha bajeti zile kwa kushirikiana na wataalamu wa field nyingine mbalimbali kutoka mawizarani na tena baada ya kukusanya data za nchi nzima. Waziri anaisoma tu, halafu wabunge wetu wanasikiliza tu.
Again tusidanganyane hapa.

Bajeti huandaliwa kulingana na Ilani ya chama inayotarishwa na wanasiasa kukidhi ahadi za uchaguzi.Wataalam wanahusika sehemu za kiuchumi lakini mwelekeo mzima wa Bajeti ya Bunge letu ni siasa tu.

Hata wenyewe husema, wanatekeleza ilani ya chama na kwamba bajeti imelenga ''Wanyonge'' .

Wataalam hutengeneza bajeti kutokana na takwimu, si hapa kwetu.Sisi ni siasa
Sikuelewi kabisa, unaweza kuwa na mahaba na serikali lakini yasikufikishe hapo

Unaamini kwa dhati kwamba bajeti inaandaliwa na Watalaam na kwamba hakuna siasa! real, seriously. Hao watalaamu ndio waliosema Geita halafu wakaja kuomba pesa bila kujua wanajenga nini na wapi. Baada ya hapo wakahamisha uwanja kitalaamu. Please
Kuhusu data mbalimbali za serikali zipo na ni accessible sana, ni kwa vile watu wengi hawataki kuzitafuta wanasubiri kuambiwa na wanasiasa kama Zitto na kumkubalia moja kwa moja hata kama anapotosha. Mimi niliweza kupata data za wizara ya Ujenzi Uchukuzi na mawasiliano (http://mwtc.go.tz/), Wizara ya fedha (http://www.mof.go.tz/), benki kuu (https://www.bot.go.tz/), national Bureau of Statistics (https://www.nbs.go.tz); nina imani unaweza kupata data za Wizara nyingine kwa njia hiyo hiyo kwani website za serikali ziko current sana sasa hivi kuliko zamani. Hata World Bank na IMF wanatumia data hizo hizo, hawana kitengo chao binafsi cha kukusanya data za nchi. Data za Uchumi kutoka World Bank ni hizi hapa kwenye excel file, na report ya NBS iko kwenye hilo faili la pdf. Zaidi zaidi ninataka uangalie hii page ya World bank ambayo ina visual aids nzuri kuliko kupitia namba za kwenye hilo excel file.
Kwa hili, I rest my case.
Kwa faida ya wasomaji unachotaka kuwaaminisha ni kuwa data za kweli zinatoka serikalini.
Kwamba, watu wanaopika data leo wanageuka kuwa source.
Hivi unafikiri mswada wa takwimu, kwamba, zipatikane NBS ni bahati mbaya!
Utasemaje kuwa data zao ndizo za kuaminika kuliko za Serikali na za World bank wakati wao wenyewe hawana database yoyote?
Hivi unaijua IMF!
Hawa ni habari nyingine, hawasubiri kusoma data za NBS. Hawa ndio dunia siyo NBS, Please
Hao watalaamu wetu wanaweza kuitwa na kuambiwa waseme 9%. Nani atakataa!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Nguruvi3 Kuna contradiction ndogos katika katika post yako hiyo unaposema kuwa hujui ni nani ameweaken institutions hizo. na vile vile tunaweza kuwa tunaongea vitu viwili tofauti kwa kutumia maneno yale yale. Ukiacha la wapinzani kuzuiwa kufanya mikutanno ambalo nitalijibu hapa chini; Nisaidie kuelewa una maana gani unaposema wekende institutions, kwani mimi naweza kuwa naziona zinafanya kazi kulingana na wajibu wake lakini kuna yaliyoficha nyuma mabyo unayaelewa zaidi.

Angalia sehemu ya maoni yangu:

(a) Sijasikia kuwa Bunge lilishindwa kufanya kazi kwa kuzuiwa na Rais. Wabunge wote hawawajibiki kwa Rais kwa hiyo hakuna anayeweza kusema alisinikizwa kwa kuogopa kufukuzwa kazi na rais. Uzembe wote wa Bunge ni kazi ya spika na wabunge wake.
(b) Sijasikia Mahamakama inamwachia mtuhumiwa huru, halafu rais anasema lazima mtu huyo atiwe hatiani. Na vile vile sijasikia mahakama inamtia mtuhumiwa hatiani, halafu rais anasema mtu huyo aachiewe huru. Hivyo ninaona mahakama inafanya kazi zake sawasawa.

(c) Sijasikia polisi, takukuru au chombo chochote cha law enforcement kikamkamata mhalifu halafu Rais akawaamuru wamwache huru. Siku moja nimesikia Lugora anasema polisi imkamate mtu fulani- nadhani alikuwa ni Zitto, lakini Kamanda wa polisi akajibu wazi kuwa watafuata sheria, na ikawa hivyo. Raia kuitwa polisi kwa mahojiano kukiwa na tuhuma ni sehemu ya kazi za polis, kwa hiyo inawezekana Lugora akamtuhum mtu, polisi watamwita mtu huyo na kumhoji. Akionekana basi anaachiwa huru. Malalamiko ya polisi kudai rushwa kutoka kwa watuhumiwa siyasikii siku hizi kama ilivyokuwa zamani. Hivyo ninaona wanafanya kazi zao sawasawa

(d) Wapinzani kuzuiwa mikutano ni kosa kweli, na nadhani hilo nilishawahi kulipigia kele katka thread nyingine hapa. Lakini tabia za wapinzani kuzuiwa kufanya mikutano yao ni ya siku nying sana, haikuanza leo. Nadhani utakumbuka Slaa alivyokuwa akizuiwa kufanya mikutan yake eiti kwa sababu ya posli wamepta inteligensia, na kuna wakati yule mke wake akajeruhiwa na polisi uso mzima ukawa damu tupu. Huo ni udhaifu upo siku nyingi sana.

(e) Katiba iliyopo inampa rais madaraka mengi sana,sijuinisemeje. Kati ya madaraka aliyo nayo ni pamoja na kuwaadhibu watumishi wote wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania. hayo ni madaraka makubwa sana Public servants ni professionals ambao hawatakiwi waingiliwe kazi zao na viongozi wa kisiasa, lakini katiba ndivyo ilivyo. Kwa hiyo anapoamua kumfukuza kazi mfanyakazi yeyote wa serikali (tubmbua) ni kwa sababu katiba inamruhusu.
1565220242708.png

Sasa ili tusiwe tunazunguka zunguka, jaribu kuweka summary ya hizo hatua za kuweaken institutions hizo tuweze kujadili kwa mweleko mmoja..
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
Sikiliza ndugu, Spika wa Bunge ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM
Sasa sijui unataka watu waeleze nini zaidi. Huwezi kutenga Bunge na serikali kwa hali ilivyo sasa.

Again tusidanganyane hapa.
Ilikuwa hivyo tangu enzi za Adam Sapi Mkwawa

Bajeti huandaliwa kulingana na Ilani ya chama inayotarishwa na wanasiasa kukidhi ahadi za uchaguzi.Wataalam wanahusika sehemu za kiuchumi lakini mwelekeo mzima wa Bajeti ya Bunge letu ni siasa tu.

Hata wenyewe husema, wanatekeleza ilani ya chama na kwamba bajeti imelenga ''Wanyonge'' .

Wataalam hutengeneza bajeti kutokana na takwimu, si hapa kwetu.Sisi ni siasa
Sikuelewi kabisa, unaweza kuwa na mahaba na serikali lakini yasikufikishe hapo

Unaamini kwa dhati kwamba bajeti inaandaliwa na Watalaam na kwamba hakuna siasa! real, seriously. Hao watalaamu ndio waliosema Geita halafu wakaja kuomba pesa bila kujua wanajenga nini na wapi. Baada ya hapo wakahamisha uwanja kitalaamu. Please Kwa hili, I rest my case.
Imekuwa hivyo siku zote tangu enzi za Mkapa, ndipo tulipanza kuwa na hizo Ilani za Uchaguzi, kabla ya hapo chini ya chama kimoja tulikuwa na mpango wa maendeleo ya miaka mitano.

Halafu bajeti kuwa na siasa ndani yake ni mambo yanayofanyika duniani kote; wanasiasa wanaleta malengo yao, wataalamu wanapanga bajeti, halafu inawezekana wanasiasa wakachomekeza vitu vyao. Ndivyo ilivyo duniani kote; kwa Marekani nadhani unazijua hizo terms wanazoita pork barrel na earmarks kwa ajili hiyo.

Kwa faida ya wasomaji unachotaka kuwaaminisha ni kuwa data za kweli zinatoka serikalini.
Kwamba, watu wanaopika data leo wanageuka kuwa source.
Hivi unafikiri mswada wa takwimu, kwamba, zipatikane NBS ni bahati mbaya!
Hapo ndipo ninaposema kuwa usipoamini data za serikali basi usiamani data za institution yoyote. IMF hawana data collection system za uchumi wa Tanzania, World bank pia hawana, tena ukiwauliza wanakuambia wazi kuwa waazitoa hazina na BOT ambazo ndizo hizo hizo za serikali. Ukishakosa imani na data hizo za serikali basi achia hapo usingalie IMF wala World bank watakuambia nini. Kibaya ukishakuwa na mindest hiyo kuwa serikali inapika data basi huwezi kubadilika

Sijajua motive ya serikali kupitisha sheria ya takwimu, lakini nadhani pia ilikuwa ni kudhibiti watu kutoa namba zao zisizokuwa sahihi na kuzisambaza. Nadhani unajua kuwa hata marekani data za uchumi hutotolewa na institution moja tu; rais anaweza azakazimeza au akazitema hiyo ni shauri yake.

Hivi unaijua IMF!
Hawa ni habari nyingine, hawasubiri kusoma data za NBS. Hawa ndio dunia siyo NBS, Please
Hao watalaamu wetu wanaweza kuitwa na kuambiwa waseme 9%. Nani atakataa!
Nafikiri hapa mzee umekosea sana kuamini kuwa IMF ni kama Mungu anayeweza kujua jambo lolote bila kuwapo phyiscally; labda ni kutokana na kujua kuwa ni chombo cha mataifa makubwa. Elewa kuwa hawana makarani wakusanya data za uchumi wa nchi kutoka kila kona ya nchi; hawatozi kodi, hawana maofisa wa forodha kujua ni nini kimeingia nchini na ni nini kimetoka nje. Hupata raw data kutoka serikalini.

Halafu je umesoma zile website za World bank, na IMF nilzoweka hapo juu? Zina link mbalilbali zenye data kuhus uchumi wa Tanzania, ni nzuri sana.
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
Ilikuwa hivyo tangu enzi za Adam Sapi Mkwawa

Imekuwa hivyo siku zote tangu enzi za Mkapa, ndipo tulipanza kuwa na hizo Ilani za Uchaguzi, kabla ya hapo chini ya chama kimoja tulikuwa na mpango wa maendeleo ya miaka mitano.

Halafu bajeti kuwa na siasa ndani yake ni mambo yanayofanyika duniani kote; wanasiasa wanaleta malengo yao, wataalamu wanapanga bajeti, halafu inawezekana wanasiasa wakachomekeza vitu vyao. Ndivyo ilivyo duniani kote; kwa Marekani nadhani unazijua hizo terms wanazoita pork barrel na earmarks kwa ajili hiyo.

Hapo ndipo ninaposema kuwa usipoamini data za serikali basi usiamani data za institution yoyote. IMF hawana data collection system za uchumi wa Tanzania, World bank pia hawana, tena ukiwauliza wanakuambia wazi kuwa waazitoa hazina na BOT ambazo ndizo hizo hizo za serikali. Ukishakosa imani na data hizo za serikali basi achia hapo usingalie IMF wala World bank watakuambia nini. Kibaya ukishakuwa na mindest hiyo kuwa serikali inapika data basi huwezi kubadilika

Sijajua motive ya serikali kupitisha sheria ya takwimu, lakini nadhani pia ilikuwa ni kudhibiti watu kutoa namba zao zisizokuwa sahihi na kuzisambaza. Nadhani unajua kuwa hata marekani data za uchumi hutotolewa na institution moja tu; rais anaweza azakazimeza au akazitema hiyo ni shauri yake.Nafikiri hapa mzee umekosea sana kuamini kuwa IMF ni kama Mungu anayeweza kujua jambo lolote bila kuwapo phyiscally; labda ni kutokana na kujua kuwa ni chombo cha mataifa makubwa. Elewa kuwa hawana makarani wakusanya data za uchumi wa nchi kutoka kila kona ya nchi; hawatozi kodi, hawana maofisa wa forodha kujua ni nini kimeingia nchini na ni nini kimetoka nje. Hupata raw data kutoka serikalini.

Halafu je umesoma zile website za World bank, na IMF nilzoweka hapo juu? Zina link mbalilbali zenye data kuhus uchumi wa Tanzania, ni nzuri sana.
One of my classmate used to work for the IMF in one of African counties. They were only three IMF reps in the country and what they used to do was to collect data from the government agencies of the host country to forecast the GDP. So, there's not alot of science in IMF forecasts.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,447
2,000
One of my classmate used to work for the IMF in one of African counties. They were only three IMF reps in the country and what they used to do was to collect data from the government agencies of the host country to forecast the GDP. So, there's not alot of science in IMF forecasts.
The more I read the World Bank raw numbers, the more I become suspicious of their intentions in declaring a gdp of 5.2. I will those numbers when. I get back to my desktop
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
559
500
The more I read the World Bank raw numbers, the more I become suspicious of their intentions in declaring a gdp of 5.2. I will those numbers when. I get back to my desktop
IMF deals with risk management. So their main interest is to forecast the well being of the economy and then advise the government the best course of the action. Since, they are in the forecasting business, the past information has no value to them, unless that information is used to predict the future or manage the risk.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Mzuvendi na Kichuguu

Hizi taasisi za kimataifa na za magharibi si kama taasisi zetu hapa nyumbani
Kazi za IMF ni kubwa si uchumi tu inatumiwa katika usalama na ulinzi

Mzuvendi, hao classmate wake walitumika kama camouflage, kuna watu wanaijua nchi yetu na wapo kazini.

Kwa wale waliokuwepo, baada ya vita 1978 IMF ilieleza hali ya uchumi wa Tanzania miaka 10 inayofuata. Watu walidhani ni hadithi, walioishi nyakati hizo wanajua
Nakumbuka walisema hivi ''vitu vipo madukani kwa sasa, lakini baada ya muda hali itakuwa mbaya sana'' . Je hayakutokea?

Huwezi kufafananisha taasisi yoyote ya ndani na kazi za IMF hata kwa 10%

Baada ya shambulio la Dar na Nairobi, hakuna aliyejua nini kimetokea na nani walishiriki

Well, walikuja FBI ambao hata siku moja hawakuonekana, wakaenda kwenye nyumba hadi Bomu lililpotengenezwa. Apparently, hawakuwa na ''mwakilishi wala mkusanya data au taarifa''
Vyombo vyetu vya ndani vilibaki na mshangao tu bila kujua nini kinaendelea.

Kwahiyo mkae mkijua IMF na World Bank si wakusanya data za korosho, ni zaidi ya hapo na kwamba uchumi kwao ni security.

Hawa wanajua uchumi wa dunia miaka 2 au 3 ijayo, sisi hatujui hata ku forecast makusanyo ya TRA miezi 6 halafu mtuambie eti wanategemea data zetu, please
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom