The countdown: Updates kuelekea D9 special thread

The countdown: Updates kuelekea D9 special thread

Day 3 tunaifunga na huyu mzee

Tunamtangaza rasmi Mzee Butiku kuwa kati ya wazee wetu walioharibikia ukubwani.

Sisi hatuna cha kujadiliana na muuwaji aliyedhulumu uhai wa maelfu ya Watanzania.

Amepora utashi wetu. Na bado anatufokea na kutuchamba kama vijakazi wake.

Respectfully, retire, Mzee Butiku.
 
IMG-20251203-WA0042.jpg
 
👉Huyu ni shemeji yake na ABDULI,ni kaka yake na Mke wa Abdul...!
Huyu dogo kajazwa mihela na dada yake,Kodi za Watanganyika zinatumika vibaya sana aiseee🙌🙌
1764795234239.jpg
 
Day 4
#BREAKING: UN YAIKASHIFU VIKOSI VYA USALAMA TANZANIA KWA AMRI ZA ‘SHOOT TO KILL’ DHIDI YA WAANDAMANAJI
Umoja wa Mataifa kupitia wataalamu wake wa haki za binadamu umeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania kufuatia uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba 2025.

Katika taarifa yao, wataalamu hao wamesema kuna ripoti za mauaji ya kiholela kwa mamia ya watu, kutoweka kwa watu bila taarifa, na ukamataji wa kiholela kwa wingi dhidi ya waandamanaji, viongozi wa upinzani na wanaharakati wa kiraia.

Vile vile wamelaani vikali hatua ya vikosi vya usalama, ikiwemo polisi na jeshi, kwa kukumbatia amri za “shoot to kill” wakati wa amri ya kutotoka nje, huku maandamano yanayoongozwa na vijana yakilipuka kote nchini kupinga chama tawala.

UN imeitaka Serikali ya Tanzania kutoa taarifa za waliotoweka, kurudisha miili kwa familia ili kufanyiwa ibaada ya mamwisho ya heshima, na kuondoa vizuizi vya vyombo vya habari, ikionya kuwa udhibiti huo unakiuka wajibu wa kimataifa wa nchi hiyo.

Aidha, wataalamu hao wamefedheheshwa na hatua ya kuondolewa kwa wagombea wa upinzani, kukamatwa kwao kiholela, na mabadiliko ya kisheria yaliyopunguza uhalali wa mchakato wa uchaguzi.
1764899297728.jpg
 
Majibu


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea na kuzingatia matamshi na matamshi yaliyotolewa kwa nyakati tofauti wiki iliyopita na washirika wa maendeleo na serikali kuhusu Tanzania na matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025. Hizi ni pamoja na Ubelgiji, Canada, Denmark, Ujumbe wa Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ghana, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Slovakia, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Mataifa, Uswidi, Uswidi wa Amerika, na Wakfu wa Thabo Mbeki.

Tanzania imebainisha kwa kusikitishwa na yaliyomo katika taarifa hizo, licha ya mazungumzo ya wazi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wajumbe wa Kikosi cha Wanadiplomasia kilichoidhinishwa kuwa Tanzania, uliofanyika tarehe 28 Novemba 2025. Pamoja na kutambua nafasi ya jumuiya ya kimataifa katika kukuza demokrasia na maendeleo ya kijamii na kisiasa nchini, lakini pia inatambua umuhimu wa Tume ya Uwekezaji katika kuwekeza kwa usawa. vurugu za baada ya uchaguzi na kutoa ripoti.

Matokeo ya ripoti yataleta uelewa wa matukio ya bahati mbaya yaliyotokea na kuunda msingi wa ushirikiano wa kujenga siku zijazo. Tanzania bado ina nia ya dhati ya kujenga ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya amani na maendeleo na inatoa wito kwa wadau wote kuruhusu mifumo ya kitaifa ya kutekeleza hatua na hatua zinazochukuliwa na serikali.

Zaidi ya hayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuihakikishia jumuiya ya kimataifa na washirika wa maendeleo utayari wake na dhamira yake ya kuendelea kushirikiana katika masuala yote yenye maslahi kwa pande zote, kama washirika sawa.

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
 
LEO VIJANA WA UVCCM WATAKUWA DIAMOND JUBILEE NA KENANI KIHONGOSI, KAMA WATAPANGA UHALIFU DHIDI YA D9 TUTALETA AUDIO NA VIDEO ZA HUO MPANGO
 
TUELIMISHANE NA SIO KUTISHIANA KWA FAIDA YA WENGI

Nimesikiliza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi akisema maandamano ya tarehe 9 yamepigwa marufuku, akiyataja miongoni mwa sababu kuwa waandamanaji watakuwa na silaha za moto.

Swali la msingi ni hili: Jeshi la Polisi linathibitishaje kwamba waandamanaji watakuwa na silaha za moto, wakati wao ndio wenye jukumu la kuhakikisha hakuna silaha haramu nchini Tanzania? Madai hayo yanafichua udhaifu mkubwa wa polisi katika kulinda usalama wa taifa.

Zaidi ya hayo, polisi ndio wadaiwa wakuu katika malalamiko yanayotokana na maandamano haya: wanalaumiwa kwa utekaji nyara, ukatili, na hata mauaji ya maelfu ya watu. Sasa, yule anayelaumiwa ndiye anayezuia maandamano yanayodai haki na miili ya ndugu zetu. Hili haliwezi kukubalika.

Ni haki ya kikatiba kuandamana kwa amani. Badala ya kutoa marufuku, serikali na polisi wangepaswa:

  • Kutoa majibu ya wazi na yenye huruma kwa waathirika.
  • Kuruhusu maandamano na kuyasimamia kwa ustadi, sio kuyazuia kwa nguvu.
  • Wanasheria wafungue kesi mahakamani dhidi ya marufuku hii isiyo na msingi wa kisheria.

Rais anaweza kuwa na nguvu za kisiasa, lakini hana mamlaka ya kikatiba ya kuzuia haki ya wananchi kuandamana kwa amani. Marufuku hii inaonekana kama amri ya kisiasa, sio hatua ya kulinda usalama.

Ushauri wangu ni huu:
Badala ya kutumia nguvu, polisi waruhusu maandamano na wayasimamie kwa uangalifu. Maandamano si lazima yawe ya vurugu. Tukitumia akili badala ya jeuri, tutaepuka machafuko makubwa zaidi.

Wape wananchi nafasi ya kutoa maumivu yao.
Watumie akili, sio risasi.
Kwa sababu wananchi ni wengi – na wakati wanapofungua milango ya hofu, hakuna nguvu inayoweza kuwazuia.
1765039156037.jpg
 
 
VYOMBO VYA ULINZI RUVUMA VYAUNGANA KUHAKIKISHA JAMII ZINAENDELEA KUWA SALAMA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa Kushirikiana na maafisa na askari toka vyombo vya ulinzi na Usalama Ruvuma limefanya matembezi (Route match) na mazoezi ya pamoja kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri baina ya Majeshi pamoja na kuimarisha afya ya mwili na akili.

Matembezi hayo yamefanyika Disemba 04, 2025 katika maeneo yote ya Manispaa ya Songea na viunga vyake yakihusisha matembezi na kukimbia baina ya askari hao.

Mazoezi na kushirikiana baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma imekuwa ni desturi lengo likiwa kuwaakutanisha pamoja na kubadilishana mambo mablimbali ya kiutendaji na kuwa tayari kukabiliana na changamoto yoyote itakayotokea mbele

#halisimax #halisinewsflash
1765056213841.jpg
 
Day 7 matangazo ya police
 
Back
Top Bottom