Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 756
Dah this can be the post of the day, by the The Boss, Rejao na MTM mmezungumza Mambo ya Msingi sana Tuliowapa dhamana ya kuliongoza Taifa hili kwa Kipindi cha Miaka mitano 2010/15 wamwshaloose phocus na wako busy kwa Mbio za Urais inabidi kama Taifa hii Tabia Ikemewe kwa Nguvu zote. Tukiilea hii Tabia Tutakuwa kila Baada ya miaka Mitano tunachagua Viongozi ambao watakuwa busy na Urais ujao Matokeo tutakuwa ni taifa la uchaguzi tu
As long as viongozi wetu wanapatikana kwa mfumo wa kisiasa, ni lazima mwisho wa uchaguzi mmoja utakuwa ni mwanzo wa uchaguzi mwingine, kwa walioshinda kutekeleza ahadi zao ili wakubalike tena kwenye uchaguzi ujao, kwa walioshindwa kuangalia walipojikwaa, na kwa wenye ndoto za nafasi mbalimbali za kisiasa kuanza michakato mbalimbali ya kufanikisha ndoto zao kwenye chaguzi zijazo, hilo halizuiliki.
...Tunachopaswa kuboresha ni uhakiki wa vigezo tutakavyovitumia kumpatia mtu nafasi ya uongozi, umefika wakati sasa tuwe makini kuangalia fikra, uwezo na record za wagombea na vyama vyao ili kujiridhisha kama kweli wana uwezo na utayari wa kuzimudu changamoto tulizonazo kama Taifa, tusipoboresha hapa na kuishia kuimbaimba tu verse ole wetu..