TFRA kuna janja janja sana

Remoteque337

Member
Oct 14, 2023
18
41
Wakuu niende moja kwa moja kwenye hoja.

TFRA wanaendesha mafunzo kwa wananchi hapa mkoani Iringa kweye ukumbi wa Neema crafts kwa siku 2 yaani tarehe 30 January 2024 na tarehe 31 kwa mujibu wa tangazo lao walieleza mafunzo hayo ni buree.

Cha ajabu kufika ukumbini wanaanza kuwachangisha wakulima elfu 30,000 kila mmoja ili wakawaprintie cheti na kuwalazimisha wale chakula cha mchana na kupata kitini cha mafunzo, kwa hiyo pesa, upigaji.

Kwanini upigaji, kitini hakikost zaidi ya 3000, kuprint cheti haizidi 3000, chakula wakulima wamekula mara moja tu nani chakula kisichozidi elfu 3000 na hakikuletwa na mzabuni ni vile jamaa walimtafuta mama ntilie akawapikia wakafuata na gari ya serikali waliyokuja nayo, zoezi la kuwachngisha wakulima linaendelea na kama mkulima hajchangia hatopta cheti pamoja na tangazo kusema mafunzo ni bure.

RAI yangu takukuru iringa na ofisi ya mkoa kilimo walifuatilie ili na wahusika wawajibishwe.zaidi kama wanataka wakulima walipie utaratibu uwe wazi malipo yafanyike kwa control number na tangazo lieleze kwamba kuna gharama. Kiukweli wakulima wengi hawaelewi nini wafanye maana baadhi yao wametoka maeneo ya mbali na hawakujiandaa kwa hilo.

TFRA wawajibishe wahusika hali hii isiendelee.
 
Hii nchi imejaa upgaji mwingi saana,kila kitu kinaendeshwa kwa ujanja unjaunja tu
 
Wakuu niende mojakwa moja kwenye hoja.

TFRA wanaendesha mafunzo kwa wananchi apa mkoani iringa kweye ukumbi wa Neema crafts kwa siku 2 yani tr 30 january 2024 na tr 31.kwa mujibu wa tangazo lao walieleza mafunzo hayo ni buree,cha ajabu kufika ukumbini wanaanza kuwachangisha wakulima elfu 30000 kila mmoja ili wakawaprintie cheti na kuwalazimisha wale chakula cha mchana na kupata kitini cha mafunzo, kwa iyo pesa. upigaji.

Kwanini upigaji ,kitini hakikost zaidi ya 3000,kuprint cheti haizidi 3000 ,chakula wakulima wamekula mara moja tu nani chakula kisichozidi elfu 3000 na hakikuletwa na mzabuni ni vile jamaa walimtafuta mama ntilie akawapikia wakafuata na gari ya serikali waliyokuja nayo,zoezi la kuwachngisha wakulima linaendelea na kama mkulima hajchangia hatopta cheti pamoja na tangazo kusema mafunzo ni bure.

RAI yangu takukuru iringa na ofisi ya mkoa kilimo walifuatilie ili na wahusika wawajibishwe.zaidi kama wanataka wakulima walipie utaratibu uwe wazi malipo yafanyike kwa control number na tangazo lieleze kwamba kuna gharama.kiukweli wakulima wengi hawaelewi nini wafanye maana baadhi yao wametoka maeneo ya mbali na hawakujiandaa kwa hilo.

TFRA wawajibishe wahusika hali hii isiendelee.
Mkuu
Kwani kuna hasara gani ukitueleza what is the hell TFRA?
Punguza wenge la kuchangishwa, tulia andika nini maana ya TFRA, Nini dhima ya mafundisho hayo na kama ukiweza weka na kapicha ka hilo tangazo lao.

Tunaelimishana
 
TFRA ni mamlaka ya udhibiti ubora mbolea nchini tanzania.
Dhima ya mafunzo ni kuwafundisha wakulima na watu wenye nia ya kuwa wafanya biashara ya mbolea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom