Tff mkitaka soka la wanawake bongo liwe juu tengenezeni wachezaji kariba ya jezi namba kumi wa Yanga Princess

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,071
27,005
Nianze kwa ku declare interest, sijawahi kuwa shabiki wa soka la wanawake hata kidogo.

Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa nikiona wanawake wanacheza mpira nilikuwa nawaonea huruma kwa sababu nilidhani walikuwa wanaumia wakicheza.

Nimekuwa mtu mzima still bado sijawahi kuupenda mchezo huu kwa sababu moja tu, wachezaji wengi wanao ucheza mchezo huu wamekaa/ au wanajiweka kidumedume jambo ambalo linafanya mchezo huo ukose ladha kwangu.


Kwangu mimi "mpira wa wanawake " lazima uwa husishe wanawake walio kaa " kike" ( feminine women) na sio wanao jiweka kidume dume ( masculine women )

Wanawake ambao wanaupenda mchezo wa mpira wa miguu, Wana penda kuucheza, wanaweza kuucheza and yet still they want to remain in touch with their feminine side and not the otherwise.

Nataka nimuone mwanamke mrembo na anae jiweka kike mfano wa Hamisa Mobeto, Jokate Mwegelo, Wema Sepetu, Batuli, Kajala, Paula, Jacqueline (Mengi/Wolper), Uwoya etc akiwa anacheza mpira wa miguu kwa kiwango cha juu. Hii ndio ingeufanya mchezo wa mpira wa miguu wa wanawake kuwa na ladha ya mchezo wa wanawake.

Sitaki nimuone mwanamke anae jiweka kidume dume akiwa anacheza mpira wa miguu.. Kwangu mimi hii inaondoa ladha ya mpira wa wanawake kwa sababu I don't see women playing football. I just see the " men wannabes" playing football.

Nina sababu gani ya kutazama mpira wa watu ambao si wanaume lakini wanataka kuonekana kama wanaume wakati zipo timu za wanaume kibao tu . Ni kama vile nakuwa natazama mpira wa " wanaume fake '


Yani ni sawa uanzishwe mchezo wa netball kwa wanaume halafu wachezaji wawe akina Juma Lokole and co. Itakosa ladha. Ili iwe netball ya wanaume lazima wachezaji wawe vidume kwelikweli. Nataka nimuone pale Kalapina, Ney wa Mitego, Zola D and co wakicheza na sio akina Dokta Kumbuka.


Back to my topic. Jana nimetazama mechi ya ufunguzi ya Yanga Princess na Ilala Queens kuna mchezaji wa Yanga Princess anae vaa jezi namba kumi amenikosha sana ( ona sasa mimi shabiki namba moja wa Yanga lakini mchezaji kama huyo jezi namba kumi simjui hata jina simply kwa sababu si ufuatilii kabisa mchezo wa soka la wanawake)

Dada anaupiga mwingi kama Samia halafu amekaa kike, ana mapozi ya kike, ana kimbia kike, gestures za kike, amesuka kike, body language ya kike lakini anaupiga mwingi kweli kweli na yeye jana ndo alikuwa nyota wa mchezo akitupia kambani mara mbili.

Yani anavutia kutazama. Jinsi anavyo cheza mpira kwa madaha na urembo kumtazama ni kama natazama wanawake warembo wakinengua vile.

Dada yule amenifanya niupende mchezo huo na kuanzia leo nitakuwa nafuatilia mechi za Yanga Princess kwa ajili yake.

Nitaanzisha blog/website/ u tube channel/ instagram page kwa ajili ya kuandika habari za wachezaji wanawake wenye kariba yake.

Huyo dada angekuwa anacheza katika nchi ambayo soka la wanawake lipo juu angekuwa milionea in usds.

She deserves to be a millionaire.

Tff it's high time now anzeni ku tengeneza wachezaji wa soka wenye haiba ya kike kama dada huyo jezi namba kumi wa Yanga Princess.

Soka la wanawake litaanza kupata mashabiki wengi sana wa kiume kama ilivyo kuwa kwa netball miaka ya nyuma kabla CHANETA hajawaweka sheria ya kipuuzi ya kutaka wachezaji netball wavae mavazi sijui eti makufuli yao yasionekane.

Tff fanyieni kazi ushauri wangu soka la wanawake bongo ni njaa tupu jana uwanjani mechi ya wanawake imeisha wachezaji Yanga Princess wakaanza kuzunguka uwanja mzima mashabiki wanarusha sh hamsini hamsini na 200 wachezaji Wana gombania kuokota .

Ni taswira mbaya sana hiyo.

Inaonyesha wazi kabisa kuna ukata kwenye soka la wanawake.

Fanyieni kazi ushauri wangu muanze kupata gate collection
 
Mbna unaogopa sana afu unajistukia malizia hilo jina la co baada ya Juma lokole.

Hata kujiamini huwezi, nimecheka mbavu cna, kumbe huyo mtu unamuogopa eeeh???
 
Back
Top Bottom