TFF yajitenga na kauli ya Ndumbaro, yatoa hakikisho la usalama kwa timu zitakazokuja kwa ajili ya CAFCL na hakutakuwa na Ubaguzi kama ilivyodaiwa

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,728
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema hakuna shabiki atakayedaiwa pasipoti wakati anaingia uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns.

TFF imesisitiza kuwa michezo haisimamiwi na idara ya uhamiaji, hivyo imewatoa hofu wachezaji, mashabiki na uongozi wa Mamelodi na kuwahakikisha usalama muda wote watakaokuwepo nchini.

1000016170.jpg


Maoni Yangu: TFF wamechelewa sana kutoa tamko na waziri Ndubalo ajitokeze kutengua kauli yake na kutuomba Radhi mashabiki wa mpira wa miguu.
 
Toka mwanzo nilisema hii issue inahusiana na mechi ya Yanga kuliko hata ya Simba, mmeona sasa wenyewe kwenye barua ya TFF.

Inawezekana Serikali ilikuwa na nia njema kukataza jezi za Mamelodi ili kuepusha vurugu maana mechi ya Yanga itakuwa sensitive sana (wataumia sana wakifungwa halafu Simba ishinde) ila mtindo wa muda mrefu wa serikali kukimbia majukumu yake ya kutoa ulinzi na usalama badala yake kutafuta njia za mkato za makatazo huku wakibinya uhuru na haki za raia ndiyo matokeo yake haya. Naamini kuna kitu watakuwa wamejifunza.

Raia tuna sauti na nguvu tukiamua kuzitumia. Ni suala la kujitambua tu.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kuijulisha kuwa kuwa mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga dhidi Mamelodi Sundowans itachezwa kwa kufuata kanuni na taratibu za soka zilizowekwa.

Katika barua hiyo TFF imeihakikishia Caf kuwa mashabiki watapata fursa ya kuingia uwanjani kutazama mechi hiyo pasipo kulazimishwa kuonyesha hati ya kusafiria, kama ambavyo waziri wa utamaduni, sanaa na michezo, Damas Ndumbaro alisisitiza hivi karibuni.

“Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport (hati ya kusafiria) ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo ukifanya fujo Polisi watakuchukua ukapumzike kidogo utatoka baada ya mechi” alinukuliwa Damas Ndumbaro.

Hata hivyo katiba barua iliyoandikwa na TFF, imeijulisha kuwa taratibu zote za mpira wa miguu zitafuatwa katika mchezo huo na hakutokuwa na zuio lolote kwa mashabiki.

"Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalihakikishia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa mechi husika itachezwa kwa kanuni na taratibu zilizowekwa za soka na namna ya utaratibu wa kuingia uwanjani.

"Kwa hivyo, sio kwamba pasipoti (pasi za kusafiria) zitatumika kama kigezo cha kuingia uwanjani kwa mashabiki wa Mamelodi Sundowns na mtu yeyote kwa sababu mechi ipo kikanuni na taratibu za mpira wa miguu bali sio kwa Idara ya Uhamiaji.

"Timu ya Mamelodi Sundowns imehakikishiwa usalama wao kutoka kwa vyombo husika wakati wote ambao watakuwa nchini na kuheshimu taratibu za mechi yao dhidi ya Young Africans SC, na Dhamana hii pia inawahusu maafisa wa mechi, mashabiki wa Sundowns wanaosafiri pamoja na mashabiki wanaoishi Tanzania na anaetaka kuhudhuria mechi hiyo," ilifafanua barua hiyo.

20240323_120438.jpg


Kwahyo Kwa mujbu wa TFF sisi Mashabiki wa MAsandawana tunaoishi TZ tumeachwa huru kabisa
 
mkuu kajipakata , hekima ni kitu muhimu sana huwez ukawa mtu mkubwa kama waziri ukawa unaendeshwa na hype za kipimbi
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma barua CAF ya kulihakikishia shirikisho hilo la soka Afrika CAF kuwa mechi ya Yanga dhidi Mamelodi Sondowans itachezwa kwa kanuni na taratibu za soka zilizowekwa ya namna ya kuingia uwanjani, na kigezo sio passport...
TFF wameshtukia mtego ambao ungeenda kuigharimu nchi pakubwa tayari mashabiki ambao wangevaa jezi za mamelodi walishakubaliana kuwa chochote watakachofanyiwa na polisi au walinzi wa geti la kuingilia uwanjani wangekuwa wanarekodi moja kwa moja na kuzituma kwenye page ya CAF na FIFA
1711189166082.jpg
 
Back
Top Bottom