(TETESI)-MACHAME FAILURE MISSION

(TETESI)-MACHAME FAILURE MISSION

Nipo ndugu yangu.

Hii story inanishangaza tu, Mume wako unabadili umiliki wa mali wa nini?
Kuna jambo huwa napenda sana kuliongea hapa,85% ya wanawake wakishapata watoto wao kwa mume,mapenzi na kila kitu huisha na hupenda kuishi wao binafsi na watoto wao hujihisi kama wanabanwa fulani,kibaba jiongeze,kuwa bize na shughuli za mbali,kwani kumbana ni hatari mikononi mwako!
 
Mali ni ya mwanaume Ila watoto ni wa mwanamke. Wewe tafuta Mali na mwanamke azae basi. Mwanaume ahakikishe kuwa watt wake wote akiwemo na mkewe wanakula kulala kuvaa kufurahia kutibiwa basi na mwanamke ahakikishe anazaa na kulea watt.
Inaonekana Hawa wa Kilimanjaro wana ka tabia ka kutawala mwanaume.
Iyo kwangu hakuna
 
Kuna jambo huwa napenda sana kuliongea hapa,85% ya wanawake wakishapata watoto wao kwa mume,mapenzi na kila kitu huisha na hupenda kuishi wao binafsi na watoto wao hujihisi kama wanabanwa fulani,kibaba jiongeze,kuwa bize na shughuli za mbali,kwani kumbana ni hatari mikononi mwako!
Hili jambo kuna mtu aliniambia, ni mtu mzima nilitafakari sana. Na alisema mara nyingi kama umeshawasomesha watoto umemaliza.

Tatizo ninini? Kwanini wanawake hawataki kuishi na wanaume? Wanaume wanataka kuishi na wanawake?

Mambo yaliyotokea wiki hizi yananifanya nitafakari sana na niogope pia.
 
Em nisanue na serikali inahusika vipi? Niko kujifunza mdogo angu.
Familia ndo mjenzi mkuu wa taifa, na inatokana na ndoa.

Hivyo serikali imeweka sheria mbali mbali za kuongoza ndoa.

Sasa kwa huyu aliyeua mke wake anaweza akazuiliwa kabisa kuwaona watoto ikibainika anawaathiri kisaikolojia, hawezi kabisa kurithi mali za mke hata kwa wosia, mali zake zinaweza kutumika kufidia ndugu wa marehemu na kulea watoto.

Anateseka.
 
Hizo ni implications tu Coca, hazitoshi kufanya maamuzi. Ndio maana nikashauri nilichoshauri kwenye aya ya 3.

Huwezi ukaua tu, shida watu wanaamini ndoa ina stakeholders wawili tu(mume na mke), kumbe wapo wengi, mpaka serikali. Kwahiyo ukiwa unafikiria maamuzi magumu, fikiria juu ya hao wote.
Maneno ni rahisi sana kuongea lakini uhalisia haupo hivyo, ushawahi kuwa kwenye nafasi ya namna hiyo halafu ukafanya maamuzi ya kushirikisha hao the so called stakeholders wa ndoa?

Mkuu ni heri kukemea mzizi wa tatizo kuliko matokeo, wanawake wanatakiwa wajue wanaume sio robots, tunahisia pia kama wao. Muda mwingi tunatumia kupambania wenyewe na watoto huku tukijinyima kwa kiasi kikubwa lakini malipo yao kukosa shukrani.

Mtu anakansa ya utumbo, anayetegemea amuuguze ndio anamuongezea stress, unatarajia ni rahisi kuzihimili hisia hapo!
 
Hili jambo kuna mtu aliniambia, ni mtu mzima nilitafakari sana. Na alisema mara nyingi kama umeshawasesha watoto umemaliza.

Tatizo ninini? Kwanini wanawake hawataki kuishi na wanaume? Wanaume wanataka kuishi na wanawake?

Mambo yaliyotokea wiki hizi yananifanya nitafakari sana na niogope pia.
Kwa islam hawamalizani sana kama christian,ni kwa sababu ya uwezo wa mfumo wa kindoa!..../
 
Moja ya RED FLAG kwa mwanamke ni pale ambapo mmezaa watoto zaidi ya wawili ila utamsikia akikulazimisha umjengee nyumba ya kwake ili hali mnaishi katika nyumba ya familia ambayo hata mkifa warithi wa mali watabaki ni watoto wenu.

Vipi unalazimisha kujengewa nyumba ya kwako peke yako?

huwa inatuwazisha sana wanaume, tunahisi labda mna milango ya kutuua au kuachana!
 
This is true story;
Miaka ya 2000 Mwanandoa (Mama) kutoka Moshi alipanga mpango wa kumuua mumewe kwa kuwatumia vijana wa kazi ambao aliwapata kupitia mmoja wao hao vijana wa kazi.

Mpango ukapangwa wakakubaliana dau (adv) na kiasi kingine baada ya kumaliza kazi.

Wakati wa kuelekea utekelezaji wa dhuruma hiyo ya uhai, mmoja wa wale vijana wa kazi (waliotafutwa na yule master plan wao) nadhani nafsi ilimsuta kumbe anamfahamu yule Baba wanaetaka kukatisha Uhai wake. Siku chache kbl ya kutekeleza mpango wao alimtafuta yule mzee na kumweleza the whole plan na ushahidi wa pesa (partly) waliyopewa.

Mzee hakukurupuka akaenda polisi walat3ga Mtego wa kuwanasa wadhurumati wa Roho ya mzee kwenye moja ya kidaraja (by then) kidogo cha watembea kwa miguu eneo krb na shule ya msingi Mwere. Basi wakawanasa wale jamaa wakiwa full wamejikoki na siraha za jadi ambazo kimsingi ilikuwa ziishie kwa mzee wa watu anbaye alioa mke kwa mapenzi yake lkn mke akageuka jika na kutaka kumuua mzee wa watu.

Wauaji waliminywa na wakaweka wazi mpango mzima juu ya kumteketeza mzee ambapo kubwa kbs sababu ilikuwa ni kubaki na maki ambazo walikuwa wamezipata wakiwa kwenye ndoa.

Kwa hiyo hii kitu ni common sana kwa baadhi wa wanawake wa Kichaga hasa wamachame.

Kama uta observe sehemu kama Arusha wanawake wengi wanasukuma magari makubwa yale ya kupanda (sio kuingia) majority wanakuwa washapoka uhai wa wenza wao.

Mungu atusaidie kupata mwisho mwema, tamaa za mali zimekuwa nyingi na sasa si tu kwa wamachame ni wote kwa sbb ya hii wanasema usawa katika kila jambo which is not bad lkn wao wana transform in negative na ndo wanatuua kila kukicha.
maisha ya wanaume ni mafupi sana. Unakufa kwa stress za kuwatafutia wao wale na kuishi mazuri na unakufa kwa tamaa ya shetani unayelala nae kitanda kimoja.
 
Bella Urassa, ambaye ni dada wa marehemu Jenifer (Jeni) Urassa amesema hawezi kusema uongo, ni kweli mdogo wake alimweleza siku chache kabla ya kuuawa kuwa alikuwa na hofu kuhusu usalama wa maisha yake, akihusisha hofu hiyo na mgogoro wa umiliki wa nyumba yao iliyopo Bunju, Dar es Salaam. Hii ni baada ya Jane kubadilisha umiliki (hati) ya nyumba na kusoma jina lake na jina la watoto wake kinyume na matakwa ya mumewe Laurent Kweka ambaye kimsingi ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo.

Nisiwe muongo, ni kweli Jeni alinieleza kuwa ni kweli ameshughulikia hati na hati ya nyumba hiyo imetoka ikiwa na majina ya watoto wao wanne, na jina lake yeye akiwa msimamizi wao, jambo ambalo alidai lilipingwa na mume wake aliyekuwa akitaka hati hiyo iandikwe kwa majina ya wanandoa hao wawili.

Jeni kwa sababu zake binafsi hakutaka kabisa hati za umiliki wa mali ikiwemo nyumba hiyo yenye thamani ya inayopindukia milioni 350 viwe na jina la mumewe.

Kwa mujibu wa Bella, baada ya hati hiyo kutoka, Jeni aliwahi kusema anaamini mume wake angeweza kumuua kutokana na kitendo alichofanya cha kubadili hati hiyo ya nyumba bila idhini ya mumewe

Aidha Jeni alienda mbali zaidi akachukua mkopo bila ridhaa ya mume wake ba bila kumjulisha. Hata hivyo Mkopo alishindwa kurejesha, na walivyo mtafuta mume wake aka wajibu yeye hana pesa hivyo washughulike na aliyechukua mkopo.

Jeni, mzaliwa wa Nkuu Sinde, Kata ya Machame Mashariki, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, aliuawa kwa kupigwa risasi na mume wake alfajiri ya Alhamisi, Oktoba Mosi, 2026, nyumbani kwao Bunju, baada ya kutokea kwa tafrani ndani ya chumba walichokuwa wakiishi.

Akizungumzia mazishi, baba mdogo wa marehemu, Joseph Urassa, amesema familia ya kwao imeamua kumzika Jeni nyumbani kwao, kama alivyokuwa ameomba kuwa siku akifa asizikwe nyumbani kwa mume wake... Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ukoo wa familia alikoolewa, Mchungaji Tumsifu Kweka, amesema familia yao haitalumbana na familia ya Urassa na itaheshimu taratibu zitakazokubalika kuhusu mahali marehemu atakapozikwa.

NOTE:

1. Ni kweli 100% kuwa Jane alifanya hila na njama za kubadili umiliki wa mali ya mumewe kwa nia ovu ya kumdhulumu. Na hata Jane alijua si halali ndio maana alikuwa na hofu kuwa mwanaume asingechukulia poa huo upumbavu.

2. Ni kweli 100% kuwa familia ya Jane ilikuwa ina taarifa zote za nia ovu ya Jane ya kutaka kumdhulumu mwanaume mali zake ikiwemo nyumba lakini hawakumkemea wala kumshauri aache hiyo tamaa.

3. Ni kweli 100% kuwa Jane alishajipanga si tu kuachana na mumewe bali pia kumdhulumu mwanaume mali zake ikiwemo nyumba ndio maana alishawataarifu ndugu zake mapema kuwa hata akifa asiende kuzikwa nyumbani kwao mumewe.

4. Unawezaje kumtetea Jane kuwa hakupanga kumdhulumu mune wake mali na huenda hata alikuwa katika mipango ya kumuua mumewe ni vile tu amewahiwa. Kwa nini ahakikishe katika hati hiyo hakuna jina la mume wake? Si ni kwa sababu alijua mume wake atapoteza maisha siju za karibuni iwe kwa saratani au kuuawa?

Mwenyekiti mnanipa wakati mgumu sana kuwatetea ninyi wanawake.

Punguzeni tamaa! Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, nayo dhambi ikiishakukomaa huzaa mauti.

Si Jane tu alikuwa na tamaa bali hata ndugu zake walikuwa na tamaa ndio maana licha ya kuwa na taarifa za Jane kumdhulumu mume wake hawakumzuia wala kumshauri aachane na mpango huo hatari. Matokeo yake wamepokea maiti.

#C&P from well believed sources!

Kwahiyo kuua ndio solution?
 
Watu wanaendeshwa na mhemko kwenye hii issue.Kama ni kurithi bado mke au mume wote walikuwa na advantage 100% kisheria.

Hata watoto kama ingetokea wazazi wote wametangulia bado walikuwa na advantage 100% kisheria kwenye urithi.

Kuna siri nyuma ya pazia hatuijui kwenye haya mauaji coz kwa sasa mke, mume au watoto kudhulumiwa mali ni ngumu na siyo rahisi.

Unakuta mtu ana shahada halafu anashindwa kuhoji kuhusu mtiririko plus mchakato wa kubadilisha hati ukoje huku mwanandoa mmoja akiwa hai.Kaulizie hapo ardhi uone ugumu wake.

Nb: Tujifunze kutumia akili zetu hata kama ni za kuvukia barabara kuliko hii ya bendera fuata upepo.
kuna kitu kigumu mbele ya PESA?

Hujawahi kusikia kesi mtu amedhulumiwa eneo/nyumba ilihali ana document zote halali?
 
Mungu sazingine hutoa funzo kwa njia nyingi, hilo ni funzo kwa waliobaki! Kwani km issue ni kuwa mwanaume ana kansa ya utumbo na kwamba angeweza kufa si mali ingebaki ya kwao yeye na watoto wake? Halafu suala la kufikiria mwenzako atatangulia kufa iko nje ya uwezo watu, unaweza ukafa kwa ajali wakati wowote ukamwacha huyo anayeumwa!
wanawake huwa wanawaza kuwa wanaume ndio tunatangulia kufa kisha wao wanabaki na watoto. Ipo hivyo akilini mwao
 
Back
Top Bottom