(TETESI)-MACHAME FAILURE MISSION

(TETESI)-MACHAME FAILURE MISSION

Mkuu mada kama zipo above your level wewe kuwa msomaji tu. Jamaa anasumbuliwa na Cancer ya Tumbo. Mimi nimekaa nikihudumu sekta ya Afya kitengo cha kansa kwa miaka kadhaa, kwa hiko alichokifanya hatushangazwi, pia ndani ya ndoa hii inaonekana kuna mengi sana mwanaume alikuwa akiyavumilia, yamkini hata hiyo Kanisa aliipata kutokana na matatizo kadhaa kutoka kwa huyo mwanamke.
Nimewaza kama ni kweli haya yanayosemwa, na kama ni kweli jamaa ana kansa ya tumbo kwa asilimia 70% imetengenezwa na huyo bidada alikua akimlisha sumu taratibu
 
Je km Jane naye alikua na mipango ya kummaliza mumewe? Na angefanikiwa? Watoto wasingepata shida?
Hizo ni implications tu Coca, hazitoshi kufanya maamuzi. Ndio maana nikashauri nilichoshauri kwenye aya ya 3.

Huwezi ukaua tu, shida watu wanaamini ndoa ina stakeholders wawili tu(mume na mke), kumbe wapo wengi, mpaka serikali. Kwahiyo ukiwa unafikiria maamuzi magumu, fikiria juu ya hao wote.
 
Kuna vitu bado havieleweki kwenye hii story
Watu wanaendeshwa na mhemko kwenye hii issue.Kama ni kurithi bado mke au mume wote walikuwa na advantage 100% kisheria.

Hata watoto kama ingetokea wazazi wote wametangulia bado walikuwa na advantage 100% kisheria kwenye urithi.

Kuna siri nyuma ya pazia hatuijui kwenye haya mauaji coz kwa sasa mke, mume au watoto kudhulumiwa mali ni ngumu na siyo rahisi.

Unakuta mtu ana shahada halafu anashindwa kuhoji kuhusu mtiririko plus mchakato wa kubadilisha hati ukoje huku mwanandoa mmoja akiwa hai.Kaulizie hapo ardhi uone ugumu wake.

Nb: Tujifunze kutumia akili zetu hata kama ni za kuvukia barabara kuliko hii ya bendera fuata upepo.
 
Hizo ni implications tu Coca, hazitoshi kufanya maamuzi. Ndio maana nikashauri nilichoshauri kwenye aya ya 3.

Huwezi ukaua tu, shida watu wanaamini ndoa ina stakeholders wawili tu(mume na mke), kumbe wapo wengi, mpaka serikali. Kwahiyo ukiwa unafikiria maamuzi magumu, fikiria juu ya hao wote.
Em nisanue na serikali inahusika vipi? Niko kujifunza mdogo angu.
 
Bella Urassa, ambaye ni dada wa marehemu Jenifer (Jeni) Urassa amesema hawezi kusema uongo, ni kweli mdogo wake alimweleza siku chache kabla ya kuuawa kuwa alikuwa na hofu kuhusu usalama wa maisha yake, akihusisha hofu hiyo na mgogoro wa umiliki wa nyumba yao iliyopo Bunju, Dar es Salaam. Hii ni baada ya Jane kubadilisha umiliki (hati) ya nyumba na kusoma jina lake na jina la watoto wake kinyume na matakwa ya mumewe Laurent Kweka ambaye kimsingi ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo.

Nisiwe muongo, ni kweli Jeni alinieleza kuwa ni kweli ameshughulikia hati na hati ya nyumba hiyo imetoka ikiwa na majina ya watoto wao wanne, na jina lake yeye akiwa msimamizi wao, jambo ambalo alidai lilipingwa na mume wake aliyekuwa akitaka hati hiyo iandikwe kwa majina ya wanandoa hao wawili.

Jeni kwa sababu zake binafsi hakutaka kabisa hati za umiliki wa mali ikiwemo nyumba hiyo yenye thamani ya inayopindukia milioni 350 viwe na jina la mumewe.

Kwa mujibu wa Bella, baada ya hati hiyo kutoka, Jeni aliwahi kusema anaamini mume wake angeweza kumuua kutokana na kitendo alichofanya cha kubadili hati hiyo ya nyumba bila idhini ya mumewe

Aidha Jeni alienda mbali zaidi akachukua mkopo bila ridhaa ya mume wake ba bila kumjulisha. Hata hivyo Mkopo alishindwa kurejesha, na walivyo mtafuta mume wake aka wajibu yeye hana pesa hivyo washughulike na aliyechukua mkopo.

Jeni, mzaliwa wa Nkuu Sinde, Kata ya Machame Mashariki, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, aliuawa kwa kupigwa risasi na mume wake alfajiri ya Alhamisi, Oktoba Mosi, 2026, nyumbani kwao Bunju, baada ya kutokea kwa tafrani ndani ya chumba walichokuwa wakiishi.

Akizungumzia mazishi, baba mdogo wa marehemu, Joseph Urassa, amesema familia ya kwao imeamua kumzika Jeni nyumbani kwao, kama alivyokuwa ameomba kuwa siku akifa asizikwe nyumbani kwa mume wake... Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ukoo wa familia alikoolewa, Mchungaji Tumsifu Kweka, amesema familia yao haitalumbana na familia ya Urassa na itaheshimu taratibu zitakazokubalika kuhusu mahali marehemu atakapozikwa.

NOTE:

1. Ni kweli 100% kuwa Jane alifanya hila na njama za kubadili umiliki wa mali ya mumewe kwa nia ovu ya kumdhulumu. Na hata Jane alijua si halali ndio maana alikuwa na hofu kuwa mwanaume asingechukulia poa huo upumbavu.

2. Ni kweli 100% kuwa familia ya Jane ilikuwa ina taarifa zote za nia ovu ya Jane ya kutaka kumdhulumu mwanaume mali zake ikiwemo nyumba lakini hawakumkemea wala kumshauri aache hiyo tamaa.

3. Ni kweli 100% kuwa Jane alishajipanga si tu kuachana na mumewe bali pia kumdhulumu mwanaume mali zake ikiwemo nyumba ndio maana alishawataarifu ndugu zake mapema kuwa hata akifa asiende kuzikwa nyumbani kwao mumewe.

4. Unawezaje kumtetea Jane kuwa hakupanga kumdhulumu mune wake mali na huenda hata alikuwa katika mipango ya kumuua mumewe ni vile tu amewahiwa. Kwa nini ahakikishe katika hati hiyo hakuna jina la mume wake? Si ni kwa sababu alijua mume wake atapoteza maisha siju za karibuni iwe kwa saratani au kuuawa?

Mwenyekiti mnanipa wakati mgumu sana kuwatetea ninyi wanawake.

Punguzeni tamaa! Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, nayo dhambi ikiishakukomaa huzaa mauti.

Si Jane tu alikuwa na tamaa bali hata ndugu zake walikuwa na tamaa ndio maana licha ya kuwa na taarifa za Jane kumdhulumu mume wake hawakumzuia wala kumshauri aachane na mpango huo hatari. Matokeo yake wamepokea maiti.

#C&P from well believed sources!
Mungu sazingine hutoa funzo kwa njia nyingi, hilo ni funzo kwa waliobaki! Kwani km issue ni kuwa mwanaume ana kansa ya utumbo na kwamba angeweza kufa si mali ingebaki ya kwao yeye na watoto wake? Halafu suala la kufikiria mwenzako atatangulia kufa iko nje ya uwezo watu, unaweza ukafa kwa ajali wakati wowote ukamwacha huyo anayeumwa!
 
Kwa sasa ndoa imekuwa chanzo cha migogoro na vifo vingi sana wanandoa wamekuwa kama marekani na Irani kutafutana usiku na mchana, kiufupi Kanda ya kaskazini ni hatari sana kuoa huko na hao wanawake wa kimachame ni viumbe hatari sana kuwai kutokea hapa duniani.
Kuhusu wanawake wa huko tumeshaongea sana humu jamvini.
 
Je km Jane naye alikua na mipango ya kummaliza mumewe? Na angefanikiwa? Watoto wasingepata shida?
Bwana Kweka alimuwahi tu BI. Urassa ila huenda Jane angemtanguliza, kama move yake kweli ilikuwa hiyo manake kumuua ilikuwa moja ya mipango yake.
 
Watu wanaendeshwa na mhemko kwenye hii issue.Kama ni kurithi bado mke au mume wote walikuwa na advantage 100% kisheria.

Hata watoto kama ingetokea wazazi wote wametangulia bado walikuwa na advantage 100% kisheria kwenye urithi.

Kuna siri nyuma ya pazia hatuijui kwenye haya mauaji coz kwa sasa mke, mume au watoto kudhulumiwa mali ni ngumu na siyo rahisi.

Unakuta mtu ana shahada halafu anashindwa kuhoji kuhusu mtiririko plus mchakato wa kubadilisha hati ukoje huku mwanandoa mmoja akiwa hai.Kaulizie hapo ardhi uone ugumu wake.

Nb: Tujifunze kutumia akili zetu hata kama ni za kuvukia barabara kuliko hii ya bendera fuata upepo.
💯 Kuna mambo hayamake sense kabisa.
 
Bwana Kweka alimuwahi tu BI. Urassa ila huenda Jane angemtanguliza, kama move yake kweli ilikuwa hiyo manake kumuua ilikuwa moja ya mipango yake.
Kwenye hili napenda kusikiliza sana watu nione ufahamu wao, kulingana na maelezo ya dada wa Jane, ni wazi hawa walikua wanaliana timing, atakayewahi kabutua.

Matokeo yake Kweka kabutua.
 
Kuna tumbili zilinishanbulia humu, ndugu zangu nyie ni watu wazima unavadilishaje jina la hati bila idhini ya mume kwanini asinge mshawishi jamaa aridhie mwenyewe? Nyie mna shida sana na nimegundua humu wengi watoto hawawajui wanawake baba yangu mwenyewe Alisha wahi kuwa muhanga wa hayo mambo nilicho kiongea humu nakujua nje ndani nimekiishi
 
Hali ni mbaya sana wanaume wenzangu,shetani amewashika wanawake kwa mikono yote na ndiye anayewafanya wawe hivyo,tuishi na hawa watu kwa akili sana,wanawake wa sasa kwenye pesa huwaelezi kitu hawana huruma na wanaume kabisa kwenye hilo jambo,ndoa nyingi sana zinapumulia mashine kwa hii hali,upendo umekwisha inabakia tu mnaishi kama mtu na dada yake ndani ya nyumba...
 
Back
Top Bottom