Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Mkuu lile bomu lililipuka kwa bahati mbaya kutoka kwenye mtutu wa polisi na polisi aliyefanya uzembe huo geshi rya porisi rimemchuria hatua mazubuti za kisheria RPC kapelekwa makao makuu asubirie muda wa kustafu...

Source:- Tume ya mwema

Huyu tendwa naye aache ujinga, kumbe mtu akiwa na mwanya mkubwa sana ni dalili yakutokuwa na busara.
Anawezaje kusema mikutano ya CDM inakuwa na fujo wakati anajua kuwa kuna mikakati mahususi inayofanywa na Serikali kupitia CCM ili ionekane kuwa CDM ni chama cha kuhatarisha amani?

Hata kwa akili ya kawaida tu bila hata kuwa na elimu au ujuzi wa upelelezi utaona kuwa ni polisi ndio waliomuua Mwandishi maskini wa Channel 10. Askari alimuelekezea bunduki ya kufyatulia mabomu kwenye tumbo na akafanya kweli. Polisi wasiwe wajinga kwa kufikiri kuwa Watanzania wataendelea kuwa wajinga kama wao wa kudanganywa kwa mambo ya kinyama yaliyo wazi.

Marehemu alizungukwa na maaskari wapatao 6 wenye silaha na wengine walimuinamia huku yeye akiwa amekaa chini nadhani akiomba wasimuue. Hivyo kama lingetupwa bomu toka mbali kama hawa wauaji wanavyotaka Watanzania waamini, ni wazi maaskari wote hao wangekufa kwanza na si marehemu.

Kwa sura hii hakuna haja ya kuhangaika, ushahidi uko wazi. Polisi waseme tu kuwa walitumwa au waliagizwa waue basi. Kwani ilikuwa mbele ya RPC, killer namba 1. Vitabu vyote vitakatifu vinasema hakuna mji udumuo, na kila nafsi itaonja mahuti. Na adhabu ya binadamu ni hapa hapa duniani iko siku wenye furaha pia watalia. Ni suala la muda tu iko siku inakuja ambayo inatabiriwa kutokuwa mbali.
 
wa tz tena! mana akikifuta hamna action yyt tutayochukua zaidi ya kuja kulalamika jf tu, so asifanye uamuzi huo. mana tutakikosa bureee, na watu hawatokuwa na reaction yoyote, sisi wa tz mdomo mbele action nyuma
 
Tendwa amechelewa sana, watanzania wa leo sio wale wakufuata mtu,bendera au jina la chama,

Watanzania wa leo wanajua wanachokipigania, wako tayari hata kuongozwa na mbuzi kwenye kupigania haki zao.

Kwa sasa wanakiunga mkono
CHADEMA kwa sababu kimeonyesha mwelekeo wa kupigania haki zao, sio bendera wala jina la chama!!

kuongozwa na mbuzi? Me niko tayari kuongozwa hata na FUNZA kuliko Ccm(JK).
 
Mkuu lile bomu lililipuka kwa bahati mbaya kutoka kwenye mtutu wa polisi na polisi aliyefanya uzembe huo geshi rya porisi rimemchuria hatua mazubuti za kisheria RPC kapelekwa makao makuu asubirie muda wa kustafu...

Source:- Tume ya mwema

Huyu tendwa naye aache ujinga, kumbe mtu akiwa na mwanya mkubwa sana ni dalili yakutokuwa na busara.
Anawezaje kusema mikutano ya CDM inakuwa na fujo wakati anajua kuwa kuna mikakati mahususi inayofanywa na Serikali kupitia CCM ili ionekane kuwa CDM ni chama cha kuhatarisha amani?

Hata kwa akili ya kawaida tu bila hata kuwa na elimu au ujuzi wa upelelezi utaona kuwa ni polisi ndio waliomuua Mwandishi maskini wa Channel 10. Askari alimuelekezea bunduki ya kufyatulia mabomu kwenye tumbo na akafanya kweli. Polisi wasiwe wajinga kwa kufikiri kuwa Watanzania wataendelea kuwa wajinga kama wao wa kudanganywa kwa mambo ya kinyama yaliyo wazi.

Marehemu alizungukwa na maaskari wapatao 6 wenye silaha na wengine walimuinamia huku yeye akiwa amekaa chini nadhani akiomba wasimuue. Hivyo kama lingetupwa bomu toka mbali kama hawa wauaji wanavyotaka Watanzania waamini, ni wazi maaskari wote hao wangekufa kwanza na si marehemu.

Kwa sura hii hakuna haja ya kuhangaika, ushahidi uko wazi. Polisi waseme tu kuwa walitumwa au waliagizwa waue basi. Kwani ilikuwa mbele ya RPC, killer namba 1. Vitabu vyote vitakatifu vinasema hakuna mji udumuo, na kila nafsi itaonja mahuti. Na adhabu ya binadamu ni hapa hapa duniani iko siku wenye furaha pia watalia. Ni suala la muda tu iko siku inakuja ambayo inatabiriwa kutokuwa mbali.
 
msimshitue muacheni atekeleze inawezekana ndio mlango ambao Mungu atautumia kuleta ukombozi kamili wa nchi hii dhidi ya mafisadi.
 
Amechelewa kwa uamuzi wake wenye lengo la kukinusuru chama tawala, huu mwamko unaoendelea sasa ni vita ya kizazi mafisadi vs kizazi linda rasilimali, kazi hii sio lazima ifanyike kupitia cdm hata nje ya mfumo rasmi inaweza kufanyika na itawaumiza zaidi watawala maana katika mfumo wa sasa kuna ustaarabu.
 
Bure kabisa watanzania mikwala mingi mnaogopa hata kuzulia mandamano,. Heri mi murusha nimeshazoea siskilizagi amri za polisi naskilizaga lema au slss kasema nini
 
U-kichaa huja na hodi yake, naona huyu mzee tayari kaisha-data
 
Sasa yeye Tendwa analalama nini kama huo uwezo wa kukifuta CHADEMA? Nafikiri anatesti zali. Ajaribu kufuta Mkombozi wa Wanyonge ili aone uhondo na faida ya kutokuwa ethical leader. Kwa msemo wa Mzee Ojwang, akijaribu tu "ataona Kanga aliona" (with jaluo accent).

Kuna umuhimu gani wa kuunda tume wakati Jaji Tendwa ana hukumu mezani tayari? Yaani ukilewa madaraka kishikaji basi akili na busara nazo zinahamia masaburini...sorry but that's the fact.

mkuu bado nasisitiza mageuzi yako mioyoni.huyo tendwa afute hata leo tuone.
 
mijizee mingine hii nuksi kweli,limtu lilishastaafu linalazimisha tu vyeo,nyoooooooooooooooooooooooo
 
Chama cha demokrasia na maendeleo kimeamua kusitisha mikutano yake
ili kuepusha balaa nitakalo wakuta baada ya msajili wa vyama vya siasa John
tendwa kuvionya vyama vinavyosababisha mauwaji kwenye mikutano yake

mdau wetu alidokeza kuwa cdm sasa hivi wako kwenye mvutano mkali na wamesitisha
mikutano yao.

Mwandishi wetu alitaka mdadisi amwambie kwanini Zitto mara zote hajawai kushiriki hii mikutano ya chadema?
Alisema sasa hivi kuna mvutano mkali kati ya upande wa Zitto na upande wa Slaa na mbowe

Pata habari kamili kutoka HAPA
 
Hebu ajaribu tuone matokeo. Yaani nina hamu ya kuona matokeo yake baada ya kukifuta

Tatizo la viongozi wateule wa rais hapa kwetu ni unafiki,wanajua kabisa CDM kinamvuto mkubwa kiasi kwamba kinawanchama,wapenzi na mashabiki wengi ambao hawana dhamira mbaya ya nchi yao,ni wazalendo na wanapendana.Kitendo cha kulazimisha ccm itawale milele kitazalisha chuki mbaya miongoni mwa wananchi kuliko nyuki wanavyochanguka kwenye lundo lao.JOHN TENDWA AKEMEE POLIS TU MAANA NDIYO TATIZO KWA USTAWI WA DEMOKRASIA HAPA NCHINI,SIYO VYAMA VYA SIASA,vinginevyo afute CHADEMA ANUKISHE.
 
Hana ubavu huo. Hata akijaribu hatoweza na kama anajimini na ajaribu kufanya hicho anachofikiri ili ajionee mwenyewe nguvu ya umma inavyofanya kazi.

Kama huyu babu hajui kilichomtoa kanga manyoya au sababu ya maharage kuwa ni mboga na wakati huo huo ni futari na ajaribu kutekeleza hizo ndoto zake.Asifikiri anavyoifaidi nchi hii ndivyo watu wote wanavyoifaidi.

Wapo watu ambao kuishi kwao kumekula kwao kwa hiyo vurugu zinapotokea hawana wanachopoteza na ni wengi. Wakuu mkanyeni huyo babu amechoka na amani na sasa anataka kuwaangamiza kwa kauli zake za kuhamasisha vurugu badala ya kutumia hekima na busara.
 
Siasa za maji ya chooni zinawacost ccm.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wewe una nini wewe? wewe mwenyewe unaweza kufutwa wacha chadema. Cheza na sheria za nchi uone.

Sijakataa kuwa hawezi kukifuta CDM, ila nahitahi/napenda kuona matokeo ya kukifuta kwake... kwani kuna tatizo hapo Zomba?
 
Tendwa wafutie tu hicho chama, maana kila mkutano wao ni lazima watu wafe. Mie huwa nasema hiki ni chama cha wachawi wa ukweli, maana kila mkutano lazima watoe kafara ya damu za watu.
 
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

​Hakyanani humu duniani vilaza hawatakwisha. Hivi mtu makini anaweza kujipinga mwenyewe kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom