Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CHADEMA na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.

Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.

Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source: Habari - Radio Tumaini
 
Vipo vyama mbadala kibao ,nia na madhumuni ni kiondoa CCM na uhuni wake madarakani ,baadae tukimaliza kuiondoa tutagawana mbao na kuweka misingi mizuri tu ya kuendesha siasa zetu. Na vyama vilivyofutwa vitaruhusiwa kurudi ,Tendwa tutamfilisi kila kitu hata kama ana miliki baiskeli au paka.Kushinda azimio la Arusha.
 
Ngoja mie nipite tuu maana siasa si fani yangu na wala sijui cha ku-comment hapa!
 
Huyo ni kada tu hatuumizi kichwa!!! alafu mwambie awe makini asizeeke vibaya maana nchi inapaa kuelekea kwenye mageuzi yeye anaota ukada tu!! Shauri yake! by the way ukifuta Chadema umefuta mwamko wa watu?
 
Si ndio alibariki mauaji,kwa sababu yeye alitoa katazo kwa CDM lakini CCm kila mkoa walikuwa na shughuli ya hadhara kwa wananchi mwache ajidanganye ulivyosikiliza alilaani mauaji yaliyofanywa na polisi au amebariki polisi kupiga mabomu wananchi ndani ya ofisi ya vyama vyao na kuua waandishi wakitekeleza majukumu yao
 
Huyu naye kwa kujichanganya hajambo! Hawakumuuliza waliofanya fujo ni chadema au polisi! Kama ana hamu ya kufuta chama alete tupige kura kupendekeza chama gani kifutwe kama hatajikuta chama chake ndo kinatakiwakifutwe!

Nadhani anajiandaa kugombea ubunge kupitia CCM uchaguzi ujao.
 
Huyu baba naye atakufa vibaya, kwani amekuwa anatumika vibaya sana....!
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.
Itakua poa sana.
Tena nashangaa kwanini hakutoa tamko hili tangu mwaka jana.
 
Si ndio alibariki mauaji,kwa sababu yeye alitoa katazo kwa CDM lakini CCm kila mkoa walikuwa na shughuli ya hadhara kwa wananchi mwache ajidanganye ulivyosikiliza alilaani mauaji yaliyofanywa na polisi au amebariki polisi kupiga mabomu wananchi ndani ya ofisi ya vyama vyao

Katika mkutano wote yeye amelaani CDM kufanya vurugu kwenye mikutano yake.Inavyoelekea yuko pamoja na polisi.
 
Anazidi kuhalalisha kile nilichosema ktk ule uzi wangu wa sababu 3 zilizoko nyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema. Vifo hivyo, vinataka kuhalalisha jambo. Kama si kuchafua chadema, basi ni kuifuta chadema. Exactly, kama alivyosema rafiki yangu. Nijuavyo na niaminivyo, hilo halitawezekana.
Pili, kwa kuwa mjadala wote sasa umeelemea polisi kwa kubebeshwa lawama zote, Tendwa anataka kubadili mjadala uwe Chadema na vifo. Watz wa leo siyo wa miaka 50. Hawatafanikiwa.
 
Ngoja nipite kimya nisije nikaharibu siku yangu kwa kauli za hivi vizee
 
Ngoja mie nipite tuu maana siasa si fani yangu na wala sijui cha ku-comment hapa!
Dah!mungu akubariki sana mkuu.Ningekua kama wewe walahi ningenenepa balaa.
Anyway wewe pita hapa tuachie wenyewe tupambane lol!
 
Anazidi kuhalalisha kile nilichosema ktk ule uzi wangu wa sababu 3 zilizoko nyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema. Vifo hivyo, vinataka kuhalalisha jambo. Kama si kuchafua chadema, basi ni kuifuta chadema. Exactly, kama alivyosema rafiki yangu. Nijuavyo na niaminivyo, hilo halitawezekana.
Pili, kwa kuwa mjadala wote sasa umeelemea polisi kwa kubebeshwa lawama zote, Tendwa anataka kubadili mjadala uwe Chadema na vifo. Watz wa leo siyo wa miaka 50. Hawatafanikiwa.

Mungu amewaumbua.Kilichoikoa CDM ni zile picha zilizopigwa na waandishi kuonyesha yule polisi katili alivyofumua utumbo wa mwandishi yule masikini.Kwani siku ile tayari Chagonja alishasema CDM ndiyo walirusha kitu kizito kumuua yule mwandishi,kumbe walishajipanga kupiga propaganda na tayari Tendwa alishaandaliwa kuongea ujinga kama wa leo ili kuhalalisha kufuta CDM.Mungu ni mwema waandishi wamemuumbua Tendwa na wenzie.
 
Back
Top Bottom