Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Kama ni kweli he must be very sick. Narudia tena swali jamani Ni wapi CDM wamekwenda kwenye shughuli wakiwa na silaha? Hata Silaha wawe nazo polisi wazitumie kuua halafu huyu gamba Tendwa anasingizia CDM. Kwanza aifute CCM yenye serikali na jeshi la polisi linaloua wananchi kimkakati ili CDM ionekane wabaya. Aelewe kauli zake wananchi wengi wameshamstukia asipoteze muda labda kwa kuwafurahisha magamba wenzake na si kutishia watafuta haki.
 
Yaani wewe unatuelekeza kusoma toka habari leo? Kwani sisi ni akina Zomba? Hatusomi habari za propaganda bali zenye mashiko na huko huwa hazipo>>>>kaandike upya hilo rejeo labda utapata wafuasi

Kama u mwenyeji utajua Jey key ndiye malaria sugu
 
Last edited by a moderator:
Siasa zipo hizo? hapa ni msajili wa vyama kasema

HUKUMU ya kweli watatoa wananchi kwani wote wameona kwenye tv na magazeti.halafu tendwa ana haraka gani? na huyu ndio kiukweli kazi yake haijui kwani tume imeundwa na ndio itakayo leta ukweli tena ukweli tupu yeye ana haraka gani???
 
Anazidi kuhalalisha kile nilichosema ktk ule uzi wangu wa sababu 3 zilizoko nyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema. Vifo hivyo, vinataka kuhalalisha jambo. Kama si kuchafua chadema, basi ni kuifuta chadema. Exactly, kama alivyosema rafiki yangu. Nijuavyo na niaminivyo, hilo halitawezekana.
Pili, kwa kuwa mjadala wote sasa umeelemea polisi kwa kubebeshwa lawama zote, Tendwa anataka kubadili mjadala uwe Chadema na vifo. Watz wa leo siyo wa miaka 50. Hawatafanikiwa.

Lini tunaandamana kwenda polisi HQ? hatuogopi kutumbuliwa matumbo kwa ajili ya kutetea demokrasia hata kama sio wana-chadema....
 
Ccm mnang'ang'ania kuitawala tanzania ili muifanyie nini?
 
Mmh!wewe utakuwa:
1:-una mtindio wa ubongo,au
2:-ndo walewale wanaogomea sensa hadi nao pia walipwe posho..au
3:-Unafikiri kwa kutumia masaburi.

Chadema kimesababisha mauaji wapi?lini?
Uko kinyume na watz wote wanaolaani police kutumia nguvu kupita kiasi na kusababisha mauaji.

Wewe ni kenge......
 
Mijanaume mizima kila siku kutishia Tunia mara Misri na kila siku mara mnamwagwa ubongo mara utumbo hatuoni hiyo reaction yenu. Simjaribu basi hata siku moja?

ukiwa na mjinga hupati tabu kufanya mambo yako. Unamwambia naenda kusini, anatimua mbio ili akushinde, wewe unaenda mashariki, unaendelea na mupango yako.

Kalagabaho. . .
 
Nadhani kinachotakiwa kufanyika ni kugather evidence ambazo beyond reasonable doubt zinathibitisha kuwa viongozi wa CDM wamedhamiria kusababisha fujo, then viongozi hao wachukuliwe hatua stahiki, kwa sababu Tendwa hajasajiri viongozi amesajiri Chama. Sasa wa kuhukumiwa ni viongozi na si chama unless CDM iwe na sera rasmi ya kuchochea fujo, kitu ambacho hakipo.
 
Nyinyi ndio mnabaka demokrasia na utulivu wa Tanzania. Unaweza kunipa sababu za Daudi kumvaa mkubwa wa polisi wakati wameshatangaziwa watawanyike?

kwa maoni yangu,polisi na huyu tendwa watakuja kuiingiza NCHI hii kwenye matatizo. Tendwa huwa hafikiri anapotoa matamko yake mara nyingi hudhani yeye ni MUNGU ambalo ni kosa kubwa.asome alama za nyakati.kule MBEYA POLISI walishindwa kabisa kudhibiti mambo hali ilikuwa tete.
 
Nakuunga mkono kwa nguvu zote!! Hili pandikizi la ccm lifikishwe mahakamani mara moja!!!
 
Kauli ya tishio aliyoitoa msajili wa vyama vya siasa ikiachiwa bila kushughulikiwa itakuja leta balaa nchini, natoa rai kwa wanasheria mahiri wa chadema wakiongozwa na prof. Safari, Mabere marando, Tundu lisu, Halima Mdee N.K wamwandalie mashtaka huyu babu, afike kortini kuthibitisha kama chadema wamefanya mauaji ya raia, pia kumpiga pini ya mdomo asiingilie shughuli halali za vyama.

Naomba kuwasilisha.

Kichwa cha HABARI na HABARI au HOJA haviendani... Sasa ni kwanini UWAKILISHE habari POTOFU? Au ni Matatizo ya

UCHUNGUZI au UFINYU wa HABARI?
 
Enzi hizi za sayansi na teknologia kwa jinsi ilivyopiga hatua kubwa CCM na serikali yake ijitahidi kukubali ukweli wa mambo ili ibaki na heshima. Si rahisi leo kupinda ukweli hata kama wananchi kwa maksudi CCM imehakikisha wamekosa elimu ili ujinga wao uwe mtaji wa CCM kutawala. Wananchi si wajinga kiasi cha kushindwa kusoma picha. Teknologia imesaidia picha kuchukuliwa na kurushwa kwa umma wakati huo huo wa matukio kwenye mitandao mingi. Kusingizia na kupindisha ukweli inashusha hadhi ya mpotoshaji. Kazi kwenu magamba
 
Safari hii wameshikwa pabaya-ile picha imewaumbua-mgosi anaweweseka, hachomoki mtu
 
Iwapo huyo Tendwa ana mbavu aitishe kura za maoni kati ya CCM na CDM ni Chama kipi kifutwe!!
 
RPC kwenye shughuli ya CDM kijijini palipo tokea tukio-sikawaida-walikwisha amua liwalo na liwe
 
japo hajataja kuwa chadema ndio kitafutwa ila jicho la tatu limeona hicho..
so wasubiri mpaka pale mambo yatakapoiva kwani kwa sasa hoja ya mashitaka itakua haina nguvu sana
 
Huko mahakamani kuna nani? Sii hawa hawa wahuni wanaotuliia na kuwabambikizia kesi za uwongo ndugu zetu? Tutajaishia kuitupa mbali hii serikali kwa vingine matatizo yetu yanaongezeka. Huu ni uamuzi mgumu, lakini hatutakuwa na njia mbadala!
 
Back
Top Bottom