Tendwa na CCM yao wanahaha, watu wameshachoka huu mfumo na mambo 2015 yatakuwa mabaya sana kama wakingangania madaraka, mi nawashauri tu wasome alama za nyakati kwani kutumia jeshi la police kuvuruga mikutano ya CDM si njia sahihi ya kufifisha vuguvugu la mabadiliko, watu wameshaamua. kufanya hivyo basi jeshi hilo litakuwa linasafisha njia ya mabosi wao kwenda kwa MR. OKAMPO, watampoza JK bure, wamwache akabidhi nchi na astaafu kwa amani;
Wajibu wa chama chochote cha siasa ni kujinadi kwa wananchi wakati wote, sasa sijui walitaka CDM ijinadi hapo nje ya ofisi ya makao makuu kinondoni? naomba majibu ndugu msajili. Sababu hazina msingi, mara barabara nyembamba, mara sensa, mara msafara utapita, mara watu wanalima eti kilimo kwanza, mara kuna tetesi za al-shabab kuvamia mikutano: yote haya kuzuia CDM isinadi sera zake za kumkomboa mtanzania masikini.
Sasa hizi sababu ndizo zinafanya wananchi wachukie sababu hazina uzito wowote: Sasa hili la mwandishi ndiyo mmeharibu kabisa na mungu kasaidia kutoa ushahidi mweupe pee.
Huyu mzee naye ni gamba lililokomaa.