Tendwa, Marmo wala njama kuinyima usajili CCJ - hawana fedha ya uhakiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa, Marmo wala njama kuinyima usajili CCJ - hawana fedha ya uhakiki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 17, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakiondoa sababu nyingine zozote vi "nzi" vinaripoti kwa uhakika mkubwa kuwa Msajili wa Vyama vya siasa nchini Bw. John Tendwa na Waziri anayeshughulikia mambo ya siasa Bunge Bw. Phillip Marmo wameamua kuhakikisha kuwa chama kipya cha siasa nchini ambayo kinakuja na fikra mpya za kulirudisha taifa mikononi mwa wananchi CCJ hakipati usajili wa kudumu.

  Akizungumza mapema leo na vyombo vya habari Bw. Tendwa amezungumza kwa kejeli kuwa ofisi yake haina fedha za kwenda kufanya uhakiki wa wanachama mikoani kama sheria inavyotaka akidai kuwa kutokana na shughuli mbalimbali za uchaguzi haitowezekana kufanya hivyo kwa sasa.

  Hata hivyo, vi'nzi" hivyo vinadokeza kuwa msimamo huo wa Tendwa unatokana na maelekezo ya ushauri kutoka kwa Marmo ambaye kutokana na nafasi yake anatishiwa na mwanasiasa mmoja huko Mbulu ambaye ameonesha nia ya kutaka kugombea jimbo la MBulu kwa kupitia CCJ na ambaye tayari anaonekana kukubalika na hivyo, usajili wa CCJ utatishia moja kwa moja nafasi ya Bw. Marmo.

  Pamoja na hilo uongozi wa CCJ uliofanya mashauri masaa machache yaliyopita umeendelea kusisitiza kuwa hakuna jambo lolote ambalo serikali ya CCM itafanya litakalozuia CCJ kupata usajili wa kudumu kwani haki za maelfu ya Watanzania ambao wameamua kujiunganisha chini ya chama hiki kipya ni lazima zilindwe na hata ikibidi kuzuia uchaguzi mkuu kufanyika hadi CCJ nayo ipate usajili wa kudumu.

  Wakati huo huo CCJ inajipanga siku chache zijazo kutoa majibu kwa wazee wa Jiji la Dar kuhusu hotuba ya Rais Kikwete mbele ya wazee "wengine"; taarifa zaidi ya mkutano huo zitakuja mbeleni.
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tuko na CCJ kwa nguvu zote. Lazima wapate usajili
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo! Marmo is Marmo and is always Marmo. Kama kweli anafanya hivyo basi huyu bwana naona ile kazi ya kuwa "katsa" imempa fikra danganyifu kwamba he owns the destination of this country alone. Wahenga walituasa anayechimba kaburi lazima atangulie yeye kuliingia.
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Sijui Nijiunge na mimi?Nimeanza kupata matumaini ya kuona maendeleo yanakaribia kuja kwa taifa hili.

  Hivi kweli Ofisi hiyo haina pesa?Hilo si la kukubaliana nalo kabisa,waiitishe harambae wachangiwe..

  I love politics when it comes a time when things get hotter than before..

  Go CCJ..Ningeshauri wawaite walimu na siyo wazee..wazee wa nini hapa?
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna maana gani ya kuwa na utaratibu wa msajili kupewa jukumu la kuhakiki wanachama wa chama kinachohitaji usajili na msajili kwa upande wake kusema hana budget? Kama hana fedha anafanya nini ofisini?

  Huyo msajili alishawahi kusema kuwa CCJ hawataweza kushiriki uchaguzi mwaka huu. inawezekana ana maelekezo mengine nje ya utaratibu wake wa kawaida wa kiofisi. hatujui!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri hili.. we'll be considered.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ‘JK hawezi kuvunja sheria ya gharama za uchaguzi' (mwananchi) Monday, 17 May 2010 21:45

  Tumsifu Sanga

  MSAJILI wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema kuwa Rais Kikwete hawezi kuvunja sheria ya gharama ya uchaguzi mkuu baada ya rais kusema takrima ni ngumu kuzuilika.

  Tendwa alisema Rais Kitwete hawezi kubariki takrima na kwamba wakati akitoa kauli hiyo, alikuwa akitaniana na washiriki wa mkutano kati ya serikali na viongozi wa dini, uliofanyika hivi karibuni.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana Tendwa alisema sheria hiyo, hairuhusu kutoa kitochi isipokuwa alichomanisha yeye ni kwamba itakuwa ngumu kutekelezeka.

  "Hii sheria ni ngumu kidogo kwa sababu ni sheria ambayo wananchi wanapaswa kuifahamu hasa katika kipindi hiki kigumu. Tayari tumeanza kuzunguka mikoani kutoa elimu kwa wananchi,"alisema.

  Alisema ni vizuri kila mwananchi kufahamu umuhimu wa sheria hiyo kwa sababu inawahusu wagombea na wanasiasa.

  "Madhumuni ya kutoa elimu kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi ni kuondoa rushwa, lakini ngumu kutekelezeka kwa sababu chaguzi nyingi hutumia rushwa,"alisema Tendwa.

  Alisema sheria hiyo inatoa mamlaka na uwezo kwa vyombo vya dola na takukuru kuwakamata watu wanaotumia rushwa katika kampeni na chaguzi mbalimbali.

  Alisema kama uchaguzi uliofanyika mwaka 2005, watu wengi walitumia rushwa, lakini hawakuweza kukamatwa kutokana na ushahidi kukosekana.
  "Yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa hataruhusiwi kugombea ubunge ikiwa ni pamoja na chama chake kufutiwa usajili.

  "Tayari tumeshatoa elimu hii kwa vyombo vya dini na jeshi la polisi na hivi karibuni, tunajiandaa kuitoa kwa waandishi wa habari ili na wao wawasaidie kufikisha ujumbe kwa jamii," alisema Tendwa.

  Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu chama cha CCJ kushiriki uchaguzi mkuu ujao alisema bado hajajua kwa sababu bado hajapitia mafaili waliyoyapeleka ofisini kwake na pia hana bajeti ya kuzunguka mikoani kuhakiki wanachama wa chama hicho.

  "Walileta mafaili yao kwa maana kwamba kila mkoa na faili lake, lakini bado sijayapata,isitoshe sina bajeti ya kuzunguka mikoani kuhakiki kama kweli inawanachama zaidi ya 200 ama zaidi,"alisema Tendwa.
   
 8. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Tanzania Tanzania Nakupenda kwa Moyo wote....We have long way to GO
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i find this statement rather shabikilized kuliko kusaidia kutoa njia ya suluhu au utatuzi!!! mimi nadhani kuna mbinu zaidi ya moja kuzunguka adui kuliko kuimba pambizo tu...


  • huyo adui wa marmo akanushe ili kumpumbaza huyo mzee anayekwenda kuchukua ndumba kondoa
  • CCJ wapate power ya wakulu zaidi kuweza kubadili hali ya uwanja
  • tendwa aandaliwe zongo kama ambalo yeye anaandaa
  • CCJ waanze kujitokeza live na si kusimama kwenye virtual IDs ndani ya community
  • local presence ya CCJ iongozeke kwani hadi sasa wengi wa membaz wao nia wageni kwenye vijiwe vyetu ingawa ni wenyeji sana humu jamvini
  tanzania bila domokrasia inawezekana
   
 10. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkjj, I respect U so much and it pains me to have such a negative view on CCJ. I don't see what good can come from CCJ in 2010. Uchaguzi less than 5 months away, chama ndio kipate usajili, then kianze kunadi sera kitakuwa na wanachama wangapi kukipatia ushindi mwaka huu?? Chadema, CUF na wengine wako miaka 10+ na bado ni kazi mno kwao kushinda, hii CCJ itaweza vipi in uchaguzi yr and less than 5 months away??

  Narudia hii ni exercise ambayo haina TIJA, yaani chama ambacho as we speak kina less than 50,000 mbrs kinasumbua tume ya uchaguzi wakati wanadeal na mambo mengi muhimu kwangu mimi ni arrogance or at least poor planning and execution on the part of founding mbrs.

  Vyama vya upinzani tunavyo vya kutosha, kwa maoni yangu mkakati uwe kuunganisha nguvu na tuwe na at most vyama 2 tu vya upinzani, ili CCM iondolewe madarakani, otherwise tunaotaka mabadiliko tunakuwa weak and weak na ndio sababu watu wameshajichokea.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Moelex23,
  Sidhani kama utaeleweka na kibaya zaidi ni kutoelewa huko kunakoturudisha nyuma siku zote.
   
 12. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu kwa yeyote kwa sasa kuamini chama chochote kinaweza leta rapid changes.

  Hila ni muhimu ku-support anything against CCM safari ya maili elfu moja uanza na atua moja, who knows labda ukabila, udini na self glory zikishajulikana kuwa ni mbinu dhaifu. Labda watu wataanza kumuona adui kama alivyo na kujipanga kwa namna ya kumpiga pamoja kwa nia ya mabadiliko.

  It will take time but change is inevitable support change even if its not exactly to ur liking kumbuka CCM inalea wezi hivyo ni adui wa haki na ni adui wa Taifa letu.
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  tendwa alisema toka mwanzo kwamba anawashangaa hao wanaohamia CCJ kwani hakitosajiliwa mwaka huu.
   
 14. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ....Ikiwa chamacha CCJ kikinyimwa usajili wa kudumu kwa fitna, je wanaweza kwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi hadi kesi ya msingi isikilizwe? Tuna sheria hiyo?......
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,056
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  ELECTION 2010: CCJ locked out digg

  [​IMG]
  Registrar of Political Parties John Tendwa addresses a news conference in Dar es Salaam yesterday. With him is Deputy Registrar Ibrahim Mkwawa.

  By The Citizen Reporter

  The Registrar of Political Parties, Mr John Tendwa, said yesterday that his office does not have the money required to facilitate the swift registration of the newly formed Chama Cha Jamii's (CCJ).This has effectively sidelined CCJ from this year's General Election.

  CCJ submitted its documents to Mr Tendwa's office last Friday as part of the process of seeking permanent registration and making the party eligible for the October 31 polls.

  Mr Tendwa said yesterday his office does not have the budget to finance the verification of documents submitted by the opposition party. The process includes sending officials to ten regions where the party recruited its members.

  But CCJ secretary-general Renatus Muabhi said the party would consider all available options to ensure it was granted permanent registration.

  Section 10 (b) of the Political Parties Act Cap 258 requires a political party seeking permanent registration to obtain not less than 200 members from each of at least ten regions.

  The members should be people eligible to be registered as voters. Two of the regions should be in Zanzibar.

  Asked whether CCJ will participate in the General Election, Mr Tendwa was non-committal, saying he had not gone through CCJ's documents and there was money to verify all members recruited by the party.

  He said his office's priority this year was the Election Expenses Act, adding that they wanted to make sure that the public was conversant with it.

  Mr Tendwa said the Registrar's office would conduct public awareness campaigns on the newly enacted law as well as train journalists and other election stakeholders.

  He said his office has so far trained some members of the Police Force on the law, and was sensitising other key institutions such as the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB).

  This means that the office would not be able to work on CCJ's application before August, Mr Tendwa added.

  But Mr Muabhi told The Citizen by telephone that CCJ party had nothing to do with the availability of funds to facilitate the registration process.

  "We have fulfilled conditions within 180 days as required by the law for permanent registration after being granted temporary registration…it was not easy, but we did it," he said.

  He said Mr Tendwa was supposed to grant permanent registration to parties that fulfil all conditions without any delay.

  He reaffirmed his party's intention to participate in the October General Election, saying they were waiting for official communication from Mr Tendwa before they decided on their next move.

  When asked how the party would be able to participate following Mr Tendwa's pronouncement that he could not go through the CCJ documents before August, Mr Muabhi said:

  "We will look at other available options…we will decide on our next course of action after receiving official communication from the Registrar."

  Commenting on the development, Prof Mwesiga Baregu of St Augustine University of Tanzania accused the Registrar's office of denying the party its rights.

  He said such conduct had its roots in the transition from single-party rule to a multi-party democracy.

  "It was a controlled transition rather than a negotiated one where all players are involved in the process," he said.

  Elaborating, Prof Baregu said the transition was controlled by ruling party CCM, whose leaders appointed the Registrar of Political Parties, adding that this made him "the controller rather than Registrar of Political Parties".

  Another political analyst, Mr Ayoub Rioba, told The Citizen that reasons given by the Registrar were "flimsy".

  "I don't understand when the Registrar claims that he doesn't have money that he is supposed to have to do his work... it's irrational…what would happen if more than one political party applies for permanent registration?" he asked.

  He said CCJ had become a sensitive issue as the General Election neared because the party was seen as a ship into which CCM defectors were most likely to jump.

  Mr Tendwa told journalists if he found out that any of the members listed by CCJ was dead, he would immediately strike the party off.

  The Registrar said the process of registering a political party was not like instantly winning a World Cup lottery by opening a soda top.

  Mr Tendwa said he had in the past annulled provisional and permanent registration granted to political parties, and CCJ would not be an exception if it failed to fulfil legal requirements.

  On the Election Expenses Act, Mr Tendwa said if any person vying for a political post was arrested on corruption allegations, they would be immediately barred from elections.

  He said his office has already conducted seminars on the new law to religious institutions and the Police Force and now preparations were underway to do the same to journalists so that they help in disseminating the information to the public.

  According to Mr Tendwa, his office has already provided awareness in Dar es Salaam, Morogoro and Coast regions.

  He named other regions as Tanga, Arusha, Kilimanjaro and Manyara.
   
 16. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mkuu Hivi unawajua watanzania?

  Kwa nini CCM pamoja na majimambo yao wanashinda kila kukicha?

  Kuna mtu alisema asilimia 70 ya watanzania wanafuata mkumbo, watanzania hawaitaji kuimbiwa sana sera za chama maana huwa haziwasaidiii. Wanachohitaji ni matumaini kama vile techniques alizokuwa anatumia mrema mwaka 1995.

  Amini usiamini Chama kitakachoitikisa CCM ni chama kitakachoweza kuifunika kwa muda mfupi sana hasa hasa mida ya kuelekea uchaguzi mkuu.

  Kama utajipanga kwa muda mrefu itakuwa ni ndoto kuiondoa CCM madarakani. Kwa hiyo CCJ wakipata usajili usishangae muujiza utakao tokea.
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni ndoto nadhani ya kila mtanzania anayeitakia mema Tanzania kuona siku moja mabadiliko ya kweli ya utawala yanatokea. Mabadiliko ambayo yatamfanya mtanzania kurealize the dream ambayo tulikwa nayo just before and after uhuru. In reality mabadiliko haya inaonekana ni ngumu kutokea au haiwezekani kabisa chini ya CCM. The alternative therefore ni Vyama vya upinzani. Tukirudi nyuma kidogo ni ukweli usio pingika kwamba Tanzania haijawahi kuwa na the real momentum of change kama in 1995. Mrema alitikisa kila pembe ya Bongo na hata watawala walitikisika. Kiasi kwamba hata mwalimu alibidi anyanyuke Butiama kuja kuokoa jahazi. Baadae nini kilitokea? Migogoro isiyoisha na hatimaye a severely weakened opposition. Je momentum ile ilukwa ni kwa ajili ya itikadi nzuri ya NCCR ? sera nzuri za NCCR? Umahiri wa Mrema? I am sure you know the answer.

  Sasa tuje kwenye CCJ. Ni kweli umoja ni nguvu utengano ni udhaifu lakini kwa siasa za bongo na in reality si rahisi kuunganisha vyama vinavyotofautiana itikadi. Na hili suala la itikadi ndiyo linaloisumbua CCM kwani haijasimamia hilo hivyo ikishindwa uchaguzi ndiyo imetoka hiyo tunaweza tusiisikie tena. Kwa hiyo tunaweza jikuta tena mda si mrefu tuna lisisiemu lingine kama ilivyotokea Malawi na Zambia.

  Tukumbuke kuwa hata nchi tunazotamani mifumo yake say UK na US major parties ziko mbili lakini bado kuna utitiri wa vyama mfano as of 15 March 2010 (2010 -03-15), it shows the number of registered political parties as 367 in Great Britain. Marekani kuna vyama vingine vya siasa kama 30, can you imagine kuna mpaka Communist party of the united States? The only country in Africa so far to have at least achieved kuwa na vyama viwili vyenye nguvu karibu sawa na vyenye almost nafasi sawa kuweza kutawala ni Ghana.

  Having said the above si busara wala haki kuona kama CCJ imekuja kuvuruga upinzani au ndiyo inazuia muungano wa vyama vya upinzani, au ni vibaraka wa CCM. CCJ ipo kikatiba, wanachama wake ni watanzania na wana ajenda hopefully za kumkomboa mtanzania kama hatukubaliani nao tuwaache waplay their part. Na kama tuna amini they are part of the solution basi tujiunge nao.
   
 18. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni upungufu mkubwa wa fikra na akili mtu kama Marmo na nafasi aliyo nayo Kitaifa kufikiria kuwa anaweza kulinda nafasi yake ya Ubunge kwa kukinyima chama fulani usajili wa kudumu. Huo ni ubinafsi wa ajabu na inatoa picha halisi ya viongozi tulio nao hapa Tanzania. Inatia kero sana kuona watu ambao umri umeshagota ama kukaribia saa 12 jioni bado wanaamini kuwa wana hati miliki kwenye madaraka yao ama maeneo wanayoongoza hususan majimbo wanayowakilisha. Ushauri wangu kwa huyo mtu anayemfanya Marmo kuwa na kiwewe; Kama anakubalika huko Mbulu naamini hao Wambulu wanamkubali yeye na sio chama, muda anao wa kutosha kutafuta kivuko cha kumfikisha uwanjani ili ashiriki kwenye uchaguzi wa oktoba.
   
 19. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Wawaalike watu wa 'calibre' zote kwa maana ya wawakilish wao - wafanyakazi wa public sector, private sector, media, religious leaders, students including those of higher learing institutions, wastaafu hasa wale wa EAC, na wengineo. Marmo hamna kitu hata mwenzie Mrema anajua hili. Tendwa mwanzo alisema chama hiki ni hoax, kikasajiliwa kwa muda, sasa anasema hakuna fedha, kwa nini hakusema haya wakati wa kuwapa usajili wa muda?
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi hiyo ofisi ya Tendwa haina budget kwa ajili ya kuhakiki wanachama wa chama kipya? Navyokumbuka mwaka huu na hata mwaka jana sidhani kama kuna cham,a kipya kimesajiliwa, hela ya ya kazi hii wamepeleka wapi? Suppose ikatokea mwaka kuna vyama mia vinaomba usajili, vinaweza kunyimwa eti tu kwa sababu ofisi ya Tendwa haina hela ya kuhakiki wananchama?????? Nini hasa maana ya demokrasia? Na hata uchaguzi unaotugharimu mabilioni hauna maana kama argument zenyewe ndiyo hizi........ What for??????? nchi haina hela.

  Halafu kwa nini hao watu wake wanapokwenda kutoa semina hizo za sheria mpya ya uchaguzi wasifanye pia hili la kuhakiki wanachama wa CCJ?
   
Loading...