Diwani: Tembo wameua wananchi wangu

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
34
82
TEMBO WAVAMIA NA KUUA MTU LEO USIKU MNAMO SAA 6:30 AKIWA SHAMBANI KWAKE AKILINDA MAZAO YAKE .

Tukio hili limetokea leo hii usiku katika kijiji cha Ming'ongwa kitongoji cha Ipipililo. Diwani wa kata hii ndugu Emmanuel Maliganya Chenge anatoa taarifa hizi kwa masikitiko makubwa sana kwani amempoteza mwananchi wake ambaye alikuwa mzee maarufu katika eneo hilo .

Kitu kingine ambacho kinamfanya Diwani kuwa na masikitiko zaidi ni mfululizo wa matukio hayo katika kijiji kilekile, kitongoji kilekile ambapo mwananchi mwingine aliuliwa na tembo mwaka uliopita na pia mwaka huu kijana wa kijiji hichohicho na kitongoji kilekile alibamizwa na tembo na kuumizwa ingawa alitibiwa na kupona lakini hili la leo limeniumiza sana .

Sasa idadi ya wananchi wangu waliouawa tembo tangu mwaka jana wamefika watatu pamoja na madume mawili ya ng'ombe. Wimbi la makundi makubwa ya tembo sasa kila siku yanaingia kwenye vijiji vyote vilivyoko kata ya Sakasaka ambayo yanaendelea kuleta taharuki na usumbufu mkubwa kwa wananchi maana inalazimika kulinda mashamba yao pamoja na nyumba zao.Wadau wa habari pazeni sauti zenu ilii Serikali ione namna ya kuwasaidia wananchi walioko pembezoni mwa hifadhi .

Basi taratibu za mazishi tutaendelea kujulishana kutokana na mipangilio ya familia sasa tunaupeleka mwili wa marehemu mwanhuzi kwa ajili ya kuhifadhiwa tukiisubiiri taratibu za mazishi.
 
Back
Top Bottom