Pwani: Mtoto wa Tembo alivyonasa Kibindu, Halmashauri ya Chalinze

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Mnamo tarehe 11/09/2023 majira ya saa 2:22 asubuhi Ofisi ya Pori la Akiba Wamimbiki ilipokea taarifa toka kwa mwananchi aitwaye Manase Thomas Baha wa Kijiji cha Kwamsanja, Kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze. Taarifa ilisema kuna mtoto wa tembo amenasa kwenye shimo lenye tope na maji katika mashamba pori yaliyo jirani na hifadhi na tembo wenzake wamemtelekeza.

Hatua iliyochukuliwa
Askari wahifadhi 4 na Askari Mgambo 6 walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuokoa huyo mtoto wa tembo akiwa mzima japo alionekana kuchoka sana. Baada ya kuokolewa tembo mtoto alitokomea msituni kwa uelekea aliko wenzake. Jiranukta eneo la tukio ni 37M 0391937, UTM 9332982

Askari wahifadhi waliofanya kazi hii:
1. CRII Mushi I. O (I/C)
2. CRII Madaraka F. M.
3. CRII Mikomangwa D. M.
4. CRII Mutashyoba V. J.

Askari Mgambo na VGS ni;
1. VGS ISSA BIGO
2. MG 449455 RAJABU ALMASI
3. MG 493385 ANDREW HENRY
4. MG 581143 MRISHO RAJABU
5. MG 551826 IDD KAYANDA
6. MG 551814 FURAHA JUMA
 
Askari wahifadhi waliofanya kazi hii:
1. CRII Mushi I. O (I/C)
2. CRII Madaraka F. M.
3. CRII Mikomangwa D. M.
4. CRII Mutashyoba V. J.

Askari Mgambo na VGS ni;
1. VGS ISSA BIGO
2. MG 449455 RAJABU ALMASI
3. MG 493385 ANDREW HENRY
4. MG 581143 MRISHO RAJABU
5. MG 551826 IDD KAYANDA
6. MG 551814 FURAHA JUMA
:cool:
So what
 
Kama walimuweka makusudi walimpata wapi? Tabia ya tembo jike huwa hatekelezi/hamuachi mtoto wake mpaka kuwe hakuna namna yoyote ya kumsaidia mwanae pale anapopata shida.
Kwa wazo lako doesn't click my mind at all.
Kwa mwanadamu mambo ynte yanaweza kutokea mkuu,
Kama waliwasonga songa hao tembo na hatimae huyo mdogo akaingia kwenye tope?
Sikubaliani na jamaa 100% ila lolote linaweza kutokea.
 
Hakuna kiumbe kinachojali familia kama tembo, tembo huhakikisha mtoto anakuwa mbele au kama wako wakubwa wawili anawekwa katikati na haruhusiwi kuchepuka, lazima watamrudisha katikati. Tembo mmoja bila kujali umri akipata shida yoyote wataganya jitihada ya kumuinua kadiri wawezavyo na hawataondoka mpaka wathibitishe amekufa ndipo wataondoka lakini watarudi tena siku nyingine ili kuondoa mifupa na kuiweka ilipo mifupa ya tembo wengine, ni kama kaburi japo halijachimbwa!
 
Kumbe Vicky Kamata Amefichwa huko. Kama Afisa habari TAWA. Hii nchi, kazi bila Interview mwisho lini?
 
Mnamo tarehe 11/09/2023 majira ya saa 2:22 asubuhi Ofisi ya Pori la Akiba Wamimbiki ilipokea taarifa toka kwa mwananchi aitwaye Manase Thomas Baha wa Kijiji cha Kwamsanja, Kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze. Taarifa ilisema kuna mtoto wa tembo amenasa kwenye shimo lenye tope na maji katika mashamba pori yaliyo jirani na hifadhi na tembo wenzake wamemtelekeza.

Hatua iliyochukuliwa
Askari wahifadhi 4 na Askari Mgambo 6 walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuokoa huyo mtoto wa tembo akiwa mzima japo alionekana kuchoka sana. Baada ya kuokolewa tembo mtoto alitokomea msituni kwa uelekea aliko wenzake. Jiranukta eneo la tukio ni 37M 0391937, UTM 9332982

Askari wahifadhi waliofanya kazi hii:
1. CRII Mushi I. O (I/C)
2. CRII Madaraka F. M.
3. CRII Mikomangwa D. M.
4. CRII Mutashyoba V. J.

Askari Mgambo na VGS ni;
1. VGS ISSA BIGO
2. MG 449455 RAJABU ALMASI
3. MG 493385 ANDREW HENRY
4. MG 581143 MRISHO RAJABU
5. MG 551826 IDD KAYANDA
6. MG 551814 FURAHA JUMA
View attachment 2747073
mbona viaskari vyenyewe vinaonekana vizembe vinaogopa ogopa kitoto icho. hivi hawa kweli wamepita depo vizuri? hasa huyo wa kwanza aliyekuwa anakosea kupitisha kamba.
 
Back
Top Bottom