TCRA, Tunaomba ufafanuzi

Nakubaliana na wewe, serikali kilifanya kuwa ni mandatory kwa kila anarusha matangazo ya Tanzania, lazima anazirushe zile TV 5 bure!. Hata kama wanarushia matangazo Afrika Kusini, wana jinsi ya ku beam Tanzania ili decoder yoyote utakayonunua, iwe Zuku, DSTV au yoyote zile 5 channels ziwe mandatory!.
Kwa mfano kule Afrika Kusini, wazo baadhi ya lugha kuu ikiwezo Kizulu, Xhosa, Twasa na Sotho, sasa kila TV imelazimishwa kwa eneo la Wazulu, matangazo yote ya local, lazima yawe na tafsiri ya Kizulu for the locals japo wite wanazungumza lugha yao ya taifa ni Afrikaans na Kiingereza!.
Tungewalazimisha hata Isidingo itafsiriwe Kiswahi ndipo waruhusiwe kuirusha humu nchini!.

Pasco.
 
mkuu hapo issue ni antena tu... mimi TBC 1 na 2 ndo zina stack balaa ila hizo nyingine shwari kabisa.
 
kweli shibe mwana malevya!
Sina hakika kama uliwaelewa TCRA au unafanya makusudi kwa kuwa umelamba kibahasha.
Imagine mimi nitanunua ving'amuzi vitatu halafu kuna babu yangu pale kisarawe,kuna baba mdogo,wajomba n.k

hili zigo la gharama litanirudia mimi tu na bado uhuru wa habari utakuwa umeminywa!

Pasco fikra zako ni za ki TCRA au kimasaki masaki hivi!
 
Ni aibu kwa TCRA. Nchi hii bora liende! Local channels hazipatikani kwenye ving'amuzi, na hata zikipatikana baadhi zinakuwa hazina sauti. Shame on you!
 
kaka unaponiambia 'dish' nakumbuka nilivyokuwa naogeshwa na mama enzi hizo.fafanua kama wewe ni mtumishi wa TCRA.
Dish lipi?mbona mlituambia king'amuzi ?tuwe serious katika hili!

Uwe serious bwana acha u.se.nge!
 

Hili tangazo lako unatakiwa ulipie.
 
ITV na Star tv unazipata?

TBC1, STAR TV, ITV, EATV, CHANEL 10 chanel hizi zinapatikana bure kwenye kingambuzi cha star times nina zaidi ya mwezi sijalipia na nazipata
 
Ni aibu kwa TCRA. Nchi hii bora liende! Local channels hazipatikani kwenye ving'amuzi, na hata zikipatikana baadhi zinakuwa hazina sauti. Shame on you!

hivi TCRA wakufundishe mpaka namna ya kutune sauti kwenye kingambuzi? Kwenye rimoti kuna batani imeandikwa track hapo utamaliza tatizo la sauti,
 
Mkuu Meni', hivi si nimekujibu hivi?!,

Hii inamaanisha Kinga'amuzi kimoja tuu kinatosha!, na kwa ajili ya zile stesheni 5 basic ni bure!, zaidi ya hapo ni starehe!, starehe gharama!. Hivyo ving'amuzi vyako vitatu vya nini?, mimi nilijua hilo lalo ni jina tuu, kumbe ni kweli wewe una ...!. Tukija hili suala la bahasha, hii ndio kazi yangu inaendana na pakee ya bahasha, kama chef anavyoonjea jikoni, au mbuzi anayekula kwa urefu wa kamba yake!.

P.
 
Naangalia ITV na EATV zooote hazina sauti SHAME ON THEM sijui ni hujuma kwa IPPMEDIA kutoka kwa hawa TBC??? Maana Startime ni wadau wao?

Mkuu hii inarekebishika,kwenye remote ya Startimes juu karibia na kiwashio kuna button imeandikwa track ukishabonyeza nenda option ya pili(sikumbuki inaitwaje) chagua stereo alafu enter uone,ikikataa rudi tena jaribu right ikigoma jaribu center kama sikosei itatoa sauti tu.
 
TBC1, STAR TV, ITV, EATV, CHANEL 10 chanel hizi zinapatikana bure kwenye kingambuzi cha star times nina zaidi ya mwezi sijalipia na nazipata

kwa hiyo king'amuzi cha kununua ni star times!
Kwa hiyo lile dudu linaloitwa king'amuzi =star times?nielimisheni jamani!
 
Poleni sana wadau wenye tv...mi radio yangu mkulima aaah sina shida nasikiliza tu habari nimerudi enzi za mwalimu
 
Du misamiati imekuwa mingi, hizo red red nayo ndiyo mdudu gani? Mnatuchanginyi!

Kwa mujibu wa Baraza la Kiswahjili la Taifa (BAKITA) kisimbuzi ndiyo kiswahili sahihi kwa 'Decorder'. King'amuzi ni kiswahili sahihi kwa 'detector'
 
Pasco ,
heri ya mwaka mpya na HEKO sana kwa kutoa darsa kwenye hii mada........
Kama Serikali imeamua/imetamka kuwa local channel ziko tano (in my opinion huu ni ubabe kwa zile private TV Stations)....basi upatikanaji wa hizo local channels uwe across the board kupitia ving'amuzi vyote kwa wanaotoa service ya Television nchini kwetu.....with no exception........period
 
Last edited by a moderator:
Kwa TCRA

Kwanini gharama za simu Tanzania ziko juu sana kulinganisha na majirani zetu e.g Kenya

kwa mfano nikitaka kupiga simu nyumbani inanigharimu dola senti 18 hadi 40 kwa dakika......wakati nikipiga simu kenya inanigharimu dola senti 6 mpaka 10 kwa dakika.......
 
Haya yote tulipaswa kuyajadili kabla analogy haijazimwa.

mkuu yalijadiliwa hadi bungeni !sio mageni haya!
Nilivyowaelewa TCRA ni kwamba ifikapo jana kila mwenye TV apaswa kuwa na king'amuzi ili aweze kupata matangazo ya runingani.tena wakatufariji kuwa hakuna haja ya kutupa tv zetu na matangazo kutoka channel za nyumbani yatakuwa bure!na ving'amuzu vikaanza kushushwa bei!

Hivi kwa nini mnapenda kuwafanya watanzania ni mbumbumbu?

Message ya TCRA ilikuwa nunua king'amuzi utaziona hizo channel za nyumbani bure,kamwe sikusikia kuwa nunua 'dish' au 'king'amuzi cha star times' ili upate hizi local channels !

Juzi tulisikia ITV na Star Tv wanakuja na vinga'amuzi vyao....

Hapa nilipo nina Kinga'muzi cha zuku hakina ITV na star tv...ina maana ni suppliment kwa star times.

Mjadala ni mmoja tu ambao mpaka sasa sijaona aliyejibu....je mtanzania wa kisarawe anunue kinga'muzi gani aweze kujipatia habari 'bure' tena kutoka kwenye hizi local channels?

Kama hili 'dili' ni la star times tuwekane wazi.

Hivi ofisi za serikali zitatumia kinga'muzi gani....labda nirahisishe swali kwa namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…