TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

Braza kifurushi cha bomba ndio kile cha 19000? Mbona channel namba 224 (La Liga) ilikuwepo na ndio iliyokuwa inaonyesha EURO!
Haya...vipi kuhusu channel 481 Chinese Movie Channel?? Miaka yote naipata kwenye kifurushi cha Bomba 19,900 ghafla channel haipo

Kama sio uhuni wa DSTv ni nini???

Yapo mengi, TCRA angalieni jambo hili kama hawata pigeni marufuku nchi kwetu.

Msiruhusu kampuni zinazoibia wananchi wenu
 
Why unalazimisha upewe huduma haipo kwenye uwezo wako?

Tcra wafanyaje?Wakulipie kifurushi cha juu zaidi?

Wewe unajua wao wanalipia kiasi gani hiyo Olympic?

Hii tabia ya kulalamika vitu ambavyo vya gharama kwa kujipa haki mnaitoa wapi?

Nikienda Serena nikakuta mshikaki elfu tano.

Nilalamikie mamlaka ziwalazimishe?

We si utazame ndondo cup ya Azam?Lazima utazame olympic kama huna uwezo wa kulipia?
Yani Sasa hivi malalamiko ni mengi,itafika hatua mtu hapati haja na atataka wizara ya afya iingilie Kati.
 
Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini? Au kwasabb serikali yetu ni dhaifu ndiyo maana mnafanya mnavyotaka?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekan tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo alafu ghafla mnaondoa.

kipindi cha mashindano ya Euro walifanya huu wizi Kwa watumiaji wa kifurushi cha bomba Kwa kuwaondolea channel namba 224,tunawaomba TCRA waangalie haya manyanyaso ya hawa DStv.

Inakuaje Media zingine hawana wizi kama huu WA DStv? Kwann serikali wanashindwa kuwabana hawa makaburu ili waende sawa na media zingine?

Huu wizi wenu DStv ni kama mfano wa bus la kampuni Fulani ambalo walikuwa wakifikia Kwenye barabara ya lami wanatoza tena abiria kwasababu wapita Kwenye lami.
Mkuu sio ya makaburu dstv ni mbongo mwenzetu anaitwa balozi ami mpungwe ni mpogolo wa ifakara huko
 
Mkuu, unaposema wanavuruga signal unakuwa una maana gani?, kwamba wana temper na dish lako au king'amuzi?.

Maana dish ndilo hupokea signals na kuzipeleka kwenye king'amuzi/decoder na kuwa decoded. Dstv wana uwezo wa ku update ving'amuzi vyao kupitia satellite na hufanya hivyo mara nyingi, ila hili la kucheza na signal ili wakulipishe ndo kwanza nalisikia kwako.

Nina miaka 9 sasa tangu noamze tumia dish lao, na sijawahi hata siku moja ita fundi wao kuwa dish/decoder imeleta shida. 9 solid years
Hujui kwamba wanaweza kuingia kwenye akaunti yako na kushusha signal, unamaanisha kwamba hawawezi ku access account yako. Basi wasingeweza kukata huduma kwa wale ambao hawajalipa........jaribu kufuatilia kama hili haliwezekani.
 
Chukua Azam, dstv walikuwa poa sana miaka 3, 5 7 nyuma sio siku hizi wamekuwa miyeyusho sana.

“The devil is a joke!!!

Kwamba 3 years ago, ...premium , compact and prepaid “customers” walikuwako kwa standards za leo?

A lot has changed,it’s bitter to swallow, unfortunately it’s life!!!
 
Aisee uko sahihi. Nimewahi kulipia hicho kifurushi niliokota hela. Nili enjoy mwezi mzima. Saizi nimerudi kwenye 19000 yangu sioni faida yoyote baada ya kupata raha

Kuna channel za movie hzo wanawekaga movie mpya kali zipo channel kama 3 hv kwa ajil movie tu afu 4k sasa
 
Back
Top Bottom