DSTV mna nongwa na siasa siasa nyingi sana

Apr 16, 2021
83
118
Pindi kombe la Dunia likiendelea na sisi wapenzi wa mpira Duniani kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha hatupitwi na hii burudani ilioiteka Dunia tuliamua angalau mwezi huu tulipie angalau hata ving'amuzi vyetu vya DSTV malipo ya juu kidogo ili tuweze kuzitazama hizii mechi Mana Hali ya uchumi kwa sasa wote tunaijua

Anyway kufupisha stori mm nililipia kifurushi Cha sh 36000 kwa kutoka sh 10000 ninayolipaga kwa kila mwezi Ila ilimradi tu huu mwezi na mm kombe la Dunia niliangalie hata ghettoni Cha kusikitisha mechi zote zinazochezwa leo tar 23 - 11 - 2022 Kuanzia mechi ya MOROCCO NA CROATIA , JAPANI NA GERMANY, SIJUI KAMA HIYO HATA YA SPAIN NA COSTA RICA , BELGIUM NA CANADA Watazirusha kwa package ya kifurushi hiki, hakuna hata mechi moja inayooneshwa kwa channel za mpira zilizopo kwenye hiki kifurushi

Lakini Cha kushangaza zaidi wametuwekea channel namba 224 ( world cup fan Zone) wanatuonesha picha za mashabiki tu wakiwa jukwaani wakati mechi ikiendelea huku wachezaji hawaoneshwi kati,

Sasa DSTV hii channel mmeiweka kutukera sisi wateja WENU ama , yaani mm nilipie kifurushi kwa ajili ya kutuonesha vibe la mashabiki uwanjani, hivi mlikusudia Nini katika kuiweka chanell ya namna hii

Aisee yaani mechi inaendelea sisi tunaangalia mashabiki tu wanavyoshangalia uwanjani na mpira hatuuoni

LEO MMENIKERA SANAAAA
 
Lipia 56k..then kula maisha..tofauti na hapo endelea tu kuteseka..

Starehe gharama
Na ninateseka saana Kama leo sio powah ,mechi ya saa Saba, saa kumi na saa moja zote Holaaaa, sio powaah *****, nikasema ngoja nicheki TBC nako Holaaaa

Nikaamua Nile zangu tu series hapa yaTHE LAST SHIP, Nikisubiria mechi ya saa nne usiku labda wanaweza tukumbuka sisi wengineo
 
Mkuu acha kulalamika,DSTV walitangaza mechi zote ni kifurushi cha Compact ambacho gharama yake ni 56k,sasa wewe umelipia 36k unataka mpira?ndio maana vigezo na masharti...lipa 56k upate kuangalia mpira safi.
Wangejaribu hata kutubalansia mechi na WA package zingine, yaani mechi zote 4, zipo kwa package moja tu, wangetubalansia tu angalau mechi za Mchana moja iwe kwenye package za vifurushi vya chini na za usiku hivo hivo
 
Na ninateseka saana Kama leo sio powah ,mechi ya saa Saba, saa kumi na saa moja zote Holaaaa, sio powaah *****, nikasema ngoja nicheki TBC nako Holaaaa

Nikaamua Nile zangu tu series hapa yaTHE LAST SHIP, Nikisubiria mechi ya saa nne usiku labda wanaweza tukumbuka sisi wengineo

Msalimie kamanda Thomas CHANDLER

The Last ship
 
Wangejaribu hata kutubalansia mechi na WA package zingine, yaani mechi zote 4, zipo kwa package moja tu, wangetubalansia tu angalau mechi za Mchana moja iwe kwenye package za vifurushi vya chini na za usiku hivo hivo
Hawa ni wafanya biashara,wanacheza na fursa...wapigie huduma kwa wateja waambie wakuunge 56k,unaongeza pesa,wakibadirisha ,endelea kuangalia game wakati unajichanga kuitafuta 20k ya nyongeza.
 
Hicho kifurushi cha family wamefanya unyama Sana Kwa wateja haiwezekani waoneshe mechi moja Tu Kwa siku huu ni UJINGA ni Bora angalau wngefanya hata mechi mbili Kwa siku alafu nashangaa miaka hii kutazama kombe la dunia imekuwa anasa yaani hii Tanzania kila kitu ni yaani Tu.
Miaka ya zamani tulikuwa tunachek mechi zote bure Ila mwaka huu ni kufuru wanafanya
 
Mkuu we ni mgeni dstv au?

Mbona hata mpira haujaanza walishasema wataonyesha kuanzia kifurushi cha compact!!?

Ila bado una nafasi, jikaze ufanye top tup hiyo 20k ule maisha..
 
Pindi kombe la Dunia likiendelea na sisi wapenzi wa mpira Duniani kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha hatupitwi na hii burudani ilioiteka Dunia tuliamua angalau mwezi huu tulipie angalau hata ving'amuzi vyetu vya DSTV malipo ya juu kidogo ili tuweze kuzitazama hizii mechi Mana Hali ya uchumi kwa sasa wote tunaijua

Anyway kufupisha stori mm nililipia kifurushi Cha sh 36000 kwa kutoka sh 10000 ninayolipaga kwa kila mwezi Ila ilimradi tu huu mwezi na mm kombe la Dunia niliangalie hata ghettoni Cha kusikitisha mechi zote zinazochezwa leo tar 23 - 11 - 2022 Kuanzia mechi ya MOROCCO NA CROATIA , JAPANI NA GERMANY, SIJUI KAMA HIYO HATA YA SPAIN NA COSTA RICA , BELGIUM NA CANADA Watazirusha kwa package ya kifurushi hiki, hakuna hata mechi moja inayooneshwa kwa channel za mpira zilizopo kwenye hiki kifurushi

Lakini Cha kushangaza zaidi wametuwekea channel namba 224 ( world cup fan Zone) wanatuonesha picha za mashabiki tu wakiwa jukwaani wakati mechi ikiendelea huku wachezaji hawaoneshwi kati,

Sasa DSTV hii channel mmeiweka kutukera sisi wateja WENU ama , yaani mm nilipie kifurushi kwa ajili ya kutuonesha vibe la mashabiki uwanjani, hivi mlikusudia Nini katika kuiweka chanell ya namna hii

Aisee yaani mechi inaendelea sisi tunaangalia mashabiki tu wanavyoshangalia uwanjani na mpira hatuuoni

LEO MMENIKERA SANAAAA
Narudia

Tafuteni canal+ siyo world cup, EUFA wala EPL ambayo utaacha kuona
 
Back
Top Bottom