TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

Tulishalalamika sana kuwahusu hao dstv, inawezekana wapo juu ya sheria......wanavuruga signal ili uende na decoder halafu wanaishia kukwambia ni mbovu utoe elf 30 itengenezwe....TCRA fuatilieni hawa watu, iweje kila ukienda na decoder wakwambie ni mbovu na matengenezo lazima iwe elf 30?
Mkuu, unaposema wanavuruga signal unakuwa una maana gani?, kwamba wana temper na dish lako au king'amuzi?.

Maana dish ndilo hupokea signals na kuzipeleka kwenye king'amuzi/decoder na kuwa decoded. Dstv wana uwezo wa ku update ving'amuzi vyao kupitia satellite na hufanya hivyo mara nyingi, ila hili la kucheza na signal ili wakulipishe ndo kwanza nalisikia kwako.

Nina miaka 9 sasa tangu noamze tumia dish lao, na sijawahi hata siku moja ita fundi wao kuwa dish/decoder imeleta shida. 9 solid years
 
Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini? Au kwasabb serikali yetu ni dhaifu ndiyo maana mnafanya mnavyotaka?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekan tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo alafu ghafla mnaondoa.
Watu Masikini tuna taabu nyingi sana halafu kama ni Kipaji tulichonacho basi ni cha kupenda Kulalamika pasipo Kujiridhisha jambo fulani lenye Umuhimu na Utaratibu wake hasa Kibiashara.
 
Back
Top Bottom