TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

Why unalazimisha upewe huduma haipo kwenye uwezo wako?

Tcra wafanyaje? Wakulipie kifurushi cha juu zaidi?

Wewe unajua wao wanalipia kiasi gani hiyo Olympic?

Hii tabia ya kulalamika vitu ambavyo vya gharama kwa kujipa haki mnaitoa wapi?

Nikienda Serena nikakuta mshikaki elfu tano.

Nilalamikie mamlaka ziwalazimishe?

We si utazame ndondo cup ya Azam? Lazima utazame olympic kama huna uwezo wa kulipia?

Issue hapo sio gharama mkuu,kama channel ipo kwenye kifurushi cha bei ndogo kwanini mashindano yakiwekwa huko unaitoa hiyo channel wakati tangu mwanzo kabla ya mashindano ilikuwepo na inalipiwa kwa bei hiyo ndogo.
 
Dstv huwa Wanaota ofa ya channel, kila kifurushi kina channel zake za kudumu. Mfano, Ukiona kwenye bomba una angalia Epl fahamu kuwa hiyo ni ofa au Euro kwenye compact fahamu hiyo ni ofa.
 
Umekuja mjini juzi siwez kubishana na Fala,nimekuzidi Kwa kila kitu.
Bado ni mshamba Tu tena Sana kama bado unaona matusi ndiyo ujanja basi wewe uko nyuma Sana kimaisha hata jinsi unavyotukana inaonesha namna gani bado upo chini Sana kimaisha
Labda ulilonizidi hasa ni la Wewe Kukazwa sana tu.
 
Wametuondolea na channel 198 ambayo miaka yote tumekuwa tukitizamia Big brother Naija na kuanzia jumamosi Big brother inaenda kuanza msimu mpya. Dstv mnatukwaza sana
 
Nilishatupa vin'gamuzi mda sana. GB 1 Vodacom naangalia mechi live online dk 90. Dstv washawaona wabongo mnaishobokea ndio maana wanawapiga wabongo man'gombe. Nigeria premium wanalipia tsh 50,000 sawa na Naira 8890.
Hiyo inategemeana na sera za nchi, Mfano TZ kuna Kodi nyingi zinazpelekea gharama kuwa juu, Mojawapo ni Service leavy, Gharama za taka kila Mwezi, Kuna Brela, TRA, Leseni ya Biashara, Mazingira, yaani kiufupi mambo ni mengi sana mpka kupelekea gharama kuwa juu, Nigeria wao Mapato yao makubwa wanayapata kwenye mafuta, kwa hiyo huko pengine wananchi hawakamuliwi sana ndio maana kuna unafuu
 
Namaliza mzee, tena sasa hivi na airtel wamejiongeza nao unaangalia mechi dk 90 bila kukata GB 1. Ukiunga mechi ya pili inakata dk ya 21 au 22.
Mimi nina Aritel na Voda na zote GB 1 mechi haiishi hapo kama simu ipo 4G ikiwa 3G inamaliza ila buffering inatokea mara kwa mara
 
Natamani itokee siku moja Azam akapata rights za kuonyesha mechi za EPL hata kama sio zote lakin baadhi tuu

iyo siku ntajirekodi hadharani nikichoma moto decoder ya DSTV pamoja na dish lake kabisaaaaaa...

DSTV ni stupidy sanaaaa,nawavumlilia kwa sababu ya EPL tu,na si vinginevyo
Ni sh ngapi kwa mwezi ili kuangalia games za EPL?
 
Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekani tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo halafu ghafla mnaondoa.

Kipindi cha mashindano ya Euro walifanya huu wizi Kwa watumiaji wa kifurushi cha bomba Kwa kuwaondolea channel namba 224, tunawaomba TCRA waangalie haya manyanyaso ya hawa DStv.

Inakuaje Media zingine hawana wizi kama huu WA DStv? Kwanini serikali wanashindwa kuwabana hawa makaburu ili waende sawa na media zingine?

Huu wizi wenu DStv ni kama mfano wa bus la kampuni Fulani ambalo walikuwa wakifikia Kwenye barabara ya lami wanatoza tena abiria kwasababu wapita Kwenye lami.
Sio wizi hiyo chanel ya 224 ilikuepo kwenye bomba lakini wakati wa Euro ilipanda kwenda family kwa uamuzi wa uongozi huko SA lakini wakati wa Laliga unarudi From Bomba

Na kuhusu Olympics Mtaona kabisa kuanzia bomba wamecategorise kipi kinaonekana kuanzia bomba hadi kile kikubwa

Hii pia n kampuni ina gharama za uendeshaji jamanii
 
Issue hapo sio gharama mkuu,kama channel ipo kwenye kifurushi cha bei ndogo kwanini mashindano yakiwekwa huko unaitoa hiyo channel wakati tangu mwanzo kabla ya mashindano ilikuwepo na inalipiwa kwa bei hiyo ndogo.
Bora umefafanua vizuri maana wengine wanafikiri tunalalamikia gharama
 
Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekani tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo halafu ghafla mnaondoa.

Kipindi cha mashindano ya Euro walifanya huu wizi Kwa watumiaji wa kifurushi cha bomba Kwa kuwaondolea channel namba 224, tunawaomba TCRA waangalie haya manyanyaso ya hawa DStv.

Inakuaje Media zingine hawana wizi kama huu WA DStv? Kwanini serikali wanashindwa kuwabana hawa makaburu ili waende sawa na media zingine?

Huu wizi wenu DStv ni kama mfano wa bus la kampuni Fulani ambalo walikuwa wakifikia Kwenye barabara ya lami wanatoza tena abiria kwasababu wapita Kwenye lami.
Hao dstv Niliwaripoti TCRA kwa uhujumu waliofanya, kuondoa channel 224 bila taarifa na hivyo kunipunja kwa kunipa pungufu ya kile nilicholipia. Tarehe 16.07.2021 TCRA walitukutanisha mimi na DSTV kwa kikao cha usuluhishi pale Mawasiliano Tower. Mediation ilifeli, DSTV wakisema kuwa walitoa taarifa kuwa channel itahama hivyo hawakuwa na kosa lolote, mimi nikaendelea na msimamo wangu kuwa hakukuwa na taarifa za kuhama kwa channel, matangazo wanayoyasema yalikuwa ni ya vifurushi na sio uhamaji wa channel. Tumeambiwa bodi ya wakurugenzi wa TCRA watakapoketi kwa kikao, tutaitwa ili kusikilizwa suala letu na kutolewa uamuzi.

Mrejesho utafanywa humu. Tunachukua hatua.
 
Tuweke petition. Huwezi kunitaarifu huku mimi nilishalipa. Nani ana compesate, isitoshe FTA Chaneli ni kama za kulipia, yaani ukichelewa au usipolipa wanazitoa. Why?
 
Hao dstv Niliwaripoti TCRA kwa uhujumu waliofanya, kuondoa channel 224 bila taarifa na hivyo kunipunja kwa kunipa pungufu ya kile nilicholipia. Tarehe 16.07.2021 TCRA walitukutanisha mimi na DSTV kwa kikao cha usuluhishi pale Mawasiliano Tower. Mediation ilifeli, DSTV wakisema kuwa walitoa taarifa kuwa channel itahama hivyo hawakuwa na kosa lolote, mimi nikaendelea na msimamo wangu kuwa hakukuwa na taarifa za kuhama kwa channel, matangazo wanayoyasema yalikuwa ni ya vifurushi na sio uhamaji wa channel. Tumeambiwa bodi ya wakurugenzi wa TCRA watakapoketi kwa kikao, tutaitwa ili kusikilizwa suala letu na kutolewa uamuzi.

Mrejesho utafanywa humu. Tunachukua hatua.
Safi Sana mkuu....
Kuna watu wameniponda Ila najua nipo sawa pia Mimi sikulalamikia gharama za vifurushi Bali nimeshangaa kwann nimelipia channel ambayo IPO Kwenye kifurushi alafu ghafla wanaondoa eti Kwavile kuna Olympic
 
Wao dstv wakitaka usione vitu vipya, watengeneze channel maalumu waweke hayo mambo yao wanayoyaona ni premium lakini sio kuondoa channel iliyopo kifurushini, maana wanapoiondoa unakuwa umepata kitu pungufu ya ulicholipia.

Hii ya watu kukuponda ni kawaida tu mkuu, ni kawaida ya wapokeaji kubishana na hata kutetea vinavyofanyika isivyo halali. Yaani aliyefanya anaweza kukaa kimya na akaacha nyie wenyewe mjibizane, anajua wapo wataotetea upuuzi wake. Muhimu wewe amini kile unachoona kuwa ni sahihi na badilisha imani yako ikiwa utapewa maelekezo ukayapima na kuona ni sahihi ama sahihi zaidi.
 
Kwendeni zenu huko Azam DSTV mpango mwingine kabisa , kama mtu anapenda vya bure muacheni tu
 
Back
Top Bottom