TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
8,916
29,288
Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekani tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo halafu ghafla mnaondoa.

Kipindi cha mashindano ya Euro walifanya huu wizi Kwa watumiaji wa kifurushi cha bomba Kwa kuwaondolea channel namba 224, tunawaomba TCRA waangalie haya manyanyaso ya hawa DStv.

Inakuaje Media zingine hawana wizi kama huu WA DStv? Kwanini serikali wanashindwa kuwabana hawa makaburu ili waende sawa na media zingine?

Huu wizi wenu DStv ni kama mfano wa bus la kampuni Fulani ambalo walikuwa wakifikia Kwenye barabara ya lami wanatoza tena abiria kwasababu wapita Kwenye lami.
 
Why unalazimisha upewe huduma haipo kwenye uwezo wako?

Tcra wafanyaje? Wakulipie kifurushi cha juu zaidi?

Wewe unajua wao wanalipia kiasi gani hiyo Olympic?

Hii tabia ya kulalamika vitu ambavyo vya gharama kwa kujipa haki mnaitoa wapi?

Nikienda Serena nikakuta mshikaki elfu tano.

Nilalamikie mamlaka ziwalazimishe?

We si utazame ndondo cup ya Azam? Lazima utazame olympic kama huna uwezo wa kulipia?
 
Tulishalalamika sana kuwahusu hao dstv, inawezekana wapo juu ya sheria......wanavuruga signal ili uende na decoder halafu wanaishia kukwambia ni mbovu utoe elf 30 itengenezwe....TCRA fuatilieni hawa watu, iweje kila ukienda na decoder wakwambie ni mbovu na matengenezo lazima iwe elf 30?
 
Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini? Au kwasabb serikali yetu ni dhaifu ndiyo maana mnafanya mnavyotaka?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekan tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo alafu ghafla mnaondoa.
Usanii wao Mimi nauona kwenye kukosa kutupatia local channels.kwingine wako poa kulingana na matarajio yangu.
 
walizima siku ya fInal italy vs eng ni wahuni sana hawa hata hivyo nimeshaweka pemben kisimbiz chao falaaa san hawa
Bora kwako ulifika final mm waliitoa usiku game ya 3 ya makundi England vs Czech ghafla tu wakanipa kazi ya kuongeza pesa usiku
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom