TCRA Mmeshindwa kuzuia wizi unaofanywa na kampuni za simu kwa wateja wake ama na nyie mmeamua kuubariki

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Wakuu poleni na hili janga la Corona ni mda kidogo nilipotea humu hali yangu kiafya haikuwa nzuri kidogo,tuendelee kuchukua hatua stahiki za kujilinda na kuwalinda wengine,Si mzaha Corona ipo takribani siku 15 mpaka juzi zilikuwa siku za kifo kwangu hakika malaika wa mungu walikuwa upande wangu kwa Sasa hali yangu inatengamaa japo kwa taratibu

Turudi kwenye mada, Nikiri wazi hizi kampuni za mitandao ( Vodacom, Tigo, halotel na Airtel) wanatuibia sana sisi wateja wake nadhani ni kwa sababu ya ubovu na udhaifu wa taasisi zetu zinazohusika mimi natumia mitandao hii yote nitatoa mfano kidogo ambao kwangu umekuwa tatizo sugu kwa hii mitandao yote kila mara.

Nilikuwa naumwa na mda mwingi nilikuwa napigiwa kazi yangu ilikuwa kupokea pale ninapokuwa na unafuu wa kufanya hivo, Leo nilikuwa nina unafuu kidogo nikaomba nitumiwe vocha ya Tsh 10,000/= ya Vodacom ili nifanye mawasiliano nikatumiwa ilikuwa mida ya saa7 mchana kwa vile mwili ulikuwa umechoka baada ya kuhakikisha salio limeingia niliacha simu nikaendelea kupumzika nikiwa nimelala.

Saa 12 jioni naamka najiunga kifurushi Cha kiasi cha salio nililonalo naambiwa salio halitoshi na Sina deni lolote kuangalia salio nakuta Tsh 1,300/= imekatwa imebaki Tsh 8,700/= na sijajiunga na huduma yoyote ya makato ya pesa iwe kwa siku au kwa mwezi na simu yangu naishika Mimi tu , Ikabidi niwapigie simu Vodacom huduma kwa wateja nikiwa mkali kwelikweli.

Wamenijibu upuuzi sana, eti nimejiunga na huduma zaidi ya saba wakaniorodhoshea sijui hadithi, Mpesa app, na madubashwa mengine ya kipuuzi ambayo wametumia Kama kigezo Cha kuhalalisha wizi wao Cha kushangaza sijawahi kutumia hizo huduma hata siku moja nimeishia kumtukana yule dada wa huduma kwa wateja mpaka ikamlazimu akate simu na baada ya kukata zikaingia meseji kibao kwenye simu yangu zikionesha huduma nilizojiunga na kiasi cha pesa nilichokatwa kwa kila huduma na OPTION ya kujiondoa hapa wamenipiga changa la macho Baada ya kuwasiliana nao ili ionekane nimejiunga na nilikuwa natumia hizi huduma.

Hii kwangu sio mara ya kwanza, nilishawahi kuacha kuweka salio kwenye line ya Tigo kwa ajili ya upuuzi huu, nikahamia Airtel nako nikakuta huu upuuzi upo na si mara moja ni kila mara pale unapoweka salio na ukakaa mda mrefu bila kulitumia au kujiunga kifurushi kwa kiasi chote Cha salio kilichopo kwenye simu otherwise lazma kikombwe.

SWALI LANGU KWENU TCRA, ni kweli mmeshindwa kuzuia wizi unaofanyika kwenye hii mitandao? Pamoja na kwamba kumekuwa na malalamiko mengi dhidi ya wizi unaofanywa na hii mitandao kwenye account za wateja za pesa kwenye line au salio bila idhini yao mbona hamchukui hatua? nini wajibu wenu kwenye kumlinda mlaji dhidi ya uhuni wa hii mitandao au mpaka tuwaandikie kwa barua?

Hata pamoja na kusajili kwa alama za vidole, mmeshindwa kuwadhibiti hata wale wa tuma kwenye namba hii? TCRA mna miundombinu mizuri na ya kisasa kabisa na wafanyakazi wenu mnaajiri wale Division one/ first Class tatizo kwenu ni nini?

Tuchukueni hatua hii mitandao inatengeneza pesa nyingi kwenye huu wizi halafu wanarudi kuwapa hizo pesa kwa mgongo wa gawio ama misaada kwa jamii na nyie mnawachekea, wakati huu ni utakatishaji pesa kabisa.

N:B
Kuna member humu alianzisha uzi wa kusudio la kuzishtaki hizi kampuni amefikiwa wapi ili tumuunge mkono maana hawa jamaa ni wapuuzi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
537175.jpg

Tunashughulikia mkuu usihofu..😅
 
Voda kwa wizi wa kula muda wa maongozi wa wateja wao, wako vizuri. Ahueni kwangu wameacha kuniibia kwa sasa. Ilikuwa ukiacha hela tu ya muda wa maongezi, baada ya muda unakuta wameshaifyekelea mbali.
 
mimi siweki salio la vocha tena kwa jail ya huu wizi wao ni mwendo wa mpesa na tigo pesa au halo pesa majiungia kifurushi kutoka huko ja sio salio la kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu hivi nimeachana navyo nina kama miaka 5:
1. Kukwangua vocha.
2. Kuweka salio la kawaida.
3. Sina app yoyote ya kampuni za mawasiliano.

App niliyonayo ni crdb bank. Hii ndio kila kitu kwangu kwani ndio nafanyia utilities bills zooote:
1. LUKU
2. DAWASCO
3. DSTV/AZAM TV/STARTIMES
4. Vifurushi vya mitandao ya simu.

Dunia imeshakuwa ya kidigitali hii, usipoenda na uelekeo wa upepo utapeperushwa.
Unforgetable
 
Vitu hivi nimeachana navyo nina kama miaka 5:
1. Kukwangua vocha.
2. Kuweka salio la kawaida.
3. Sina app yoyote ya kampuni za mawasiliano.

App niliyonayo ni crdb bank. Hii ndio kila kitu kwangu kwani ndio nafanyia utilities bills zooote:
1. LUKU
2. DAWASCO
3. DSTV/AZAM TV/STARTIMES
4. Vifurushi vya mitandao ya simu.

Dunia imeshakuwa ya kidigitali hii, usipoenda na uelekeo wa upepo utapeperushwa.
Unforgetable
Kwani ni sheria kuwa na hiyo app ya CRDB? Mbna na wewe Kama unataka kuhalalisha huu wizi? Hapa TCRA imekosa weledi ipo kukimbizana na wanaocomment vibaya kuhusu serikali huko fb..kwa nchi zilizo makini huu upuuzi hamna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom