TCRA yataka wateja wa DSTV, AZAM na ZUKU waliolipishwa kuwasilisha taarifa zao

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
TCRA yataka wateja wa DSTV, AZAM na ZUKU waliolipishwa kuwasilisha taarifa zao

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewataka wateja visimbuzi vya DSTV, ZUKU na AZAM kutuma taarifa zao zinazoonesha na kuthibitisha kuwa wamekuwa wakilipia chaneli za ndani jambo ambalo ni kinyume na sheria.

TCRA imewataka wateja wa ving’amuzi hivyo kutoa taarifa juu ya majina yao kamili yaliyosajiliwa katika king’amuzi, aina ya king’amuzi anachotumia, namba ya kadi ya king’amuzi chake, eneo alipo, kiasi cha pesa ambacho amekuwa akilipia kutazama chaneli hizo na idadi ya miezi aliyolipia.

Taarifa hiyo ni maalumu kwa mtazamaji aliyekuwa anatozwa kutazama chaneli za televisheni ya TBC 1, ITV, STAR TV, CHANNEL TEN, EAST AFRIKA TV, na CLOUDS TV.

TCRA imewataka wahanga hao kutoa taarifa hizo ofisini kwao kupitia barua pepe au barua ya kawaida kwenye anuani yao ya dg@tcra.go.tz au kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano kwa sanduku la Posta 474.

Mnamo Agosti 7, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliziamuru Kampuni za DSTV, AZAM TV na ZUKU kuondoa cheneli za kutazamwa bila kulipia baada ya kukiuka sheria na masharti ya leseni zao kwa kuwatoza watazamaji ada za viwango mbalimbali kutazama chaneli hizo ambazo kisheria zinapaswa kutazwa bure.

2.jpg
 
usumbufu tu

Mimi nimeshangaa kidogo hapa, yaani utakua na udhibitisho gani kwasasa kwamba zilikua zinakatwa zote kama hujalipia? na kama zilikua zinakatwa TCRA si wanajua? kwani ilikua ikitokea kwa mteja mmoja mmoja?

Yaani hapa watusaidie tu hizo channel zirudishwe kule DSTV waache kututesa
 
Huku ni kutaka kutuibia tu,
Nimekua nikilipia vifurushi mbalimbali toka nimenunua miaka karibia mitatu iliyopita. Sometimes nalipia kifurushi kikubwa, cha kati au kifurushi kidogo.

Pia sometimes hulipia kwa wiki, mwezi au hata miezi miwili mpaka mitatu. Kwa hali hiyo basi, sina data kamili nimelipa kiasi gani toka nimekinunua.

Nachojua Azam watakua na taarifa sahihi na za kutosha juu ya nilicholipia.
 
kabisa mkuu
 
Simetimes ukitaka kukaa kwa furaha Jifanye kichwa nazi tu maisha yaende
 
Back
Top Bottom