TCRA acheni kushiriki kwenye wizi wa vifurushi unaofanywa na AZAM TV

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,678
22,266
Azam Tv imekua na tabia ya kutuibia wateja wa vifurushi vya Azam Tv, mteja ananunua kifurushi cha bei kadhaa na chaneli kadhaa kwenye kifurushi husika lakini kabla haujamaliza muda wa kifurushi husika Azam Tv wananyofoa baadhi ya chaneli ulizolipia, huu ni wizi na ni sawa na mwenye basi anayekatisha safari kwenye njia aliyopewa.

Nimelipia kifurushi cha shs.23,000/= kikiwa na chaneli nilizozihitaji 146 na 147 cha ajabu ghafla wahuni hawa wamezinyofoa! Tatizo hili lipo na tunapolalamika TCRA wanaziba masikio yao wasitusikie, kama kawaida mbele ya viongozi wetu mwarabu siku zote yuko sawa mbele ya mwafrika.

Licha ya wizi huu tumelalamika sana kuhusu uduni wa ving'amuzi na madishi yao lakini TCRA na Tume ya Ushindani hawachukui hatua yoyote kwani wanaona tunamsumbua mwarabu, sijui hali hii ya wizi itakwenda mpaka lini.
 
Sorry mkuu, hebu taja majina ya hizo chaneli
Chaneli 146 na 147 ni za filamu za Nigeria, wamenyofoa ziko kwenye kifurushi cha shs 35,000/=! Unyofoaji huu umefanywa wiki iliyopita kama sijakosea kwani ndipo king'amuzi changu kilipo update chaneli.
 
Chaneli 146 na 147 ni za filamu za Nigeria, wamenyofoa ziko kwenye kifurushi cha shs 35,000/=! Unyofoaji huu umefanywa wiki iliyopita kama sijakosea kwani ndipo king'amuzi changu kilipo update chaneli.
SIO KWELI!
IZO CHANEL ZIPO MPAKA KWENYE KIFURUSHI CHA 15000

RESERT KISIMBUZI CHAKO TU
 
Back
Top Bottom