TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

Hii ndio mana halisi ya karma, ulimwengu unakawaida ya kukurudishia kila unachokitoa ili kuweka msawazo katika asili.
Ukitoa upendo utarudishiwa upendo na ukitoa chuki basi chuki itakurudia.
 
Polepole alipokuwa anatunga hizi sheria kandamizi alifikiri kuwa ni kwa ajili ya kukomoa upinzani peke yake🐒🐒🐒

images (2).jpg
 
Hii ndio mana halisi ya karma, ulimwengu unakawaida ya kukurudishia kila unachokitoa ili kuweka msawazo katika asili.
Ukitoa upendo utarudishiwa upendo na ukitoa chuki basi chuki itakurudia.
 
kumbe ukiwa na Online TV hata kama wewe ni mwalimu ama mhasibu ukitaka kutoa elimu lazima pia uwe mwandishi wa habari....hatari sana.
 
Hii ni spinning tunafanyiwa nitaamini kuna ugomvi wakimuweka ndani!

Ila sheria hizi mbovu mbovu huyu alikuwa ni miongoni wa waliozipitisha.
 
Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.

Sasa kiki ya penalt tayari, mpira wetu Polepole ana hanjahanja, goli nani analifunga!

======

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji huku kamati hiyo ikisimamisha kipindi chake cha Shule ya uongozi na kumpa masharti ambayo anapaswa kuyatimiza ili kirudi hewani.


Akisoma hukumu hiyo, baada ya kusikiliza upande wa Kamati na Upande wa Utetezi, Mwenyekiti wa Kamati, Habbi Gunze amesema maudhui ya kipindi cha shule ya uongozi yalikuwa ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.

"Kuhusu kuwapanga wamachinga, Humphrey Polepole Online TV iliwatuhumu viongozi wa Serikali kuhusu kutofuata maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu ya kuwapanga vizuri wamachinga. Kituo hiki kimevunja kanuni na maadili ya uandishi na utangazaji kwa kutowapa nafasi viongozi hao kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma alizotoa.

"Polepole alitoa maneno ya uongo na udharirishaji kwa viongozi akisema ni waoga na hawajitokeizi kutoa ufafanuzi kuhusu deni la Taifa bila kuwapa nafasi viongozi hao kufafanua madai yake wakati viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Waziri wa fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba mwezi Juni alisema bungeni kuwa deni la taifa ni himilifu.

"Katika utetezi wake alisema amejikita katika utoaji wa elimu tu bila kuzingatia mizania na kwamba TV yake si kama vyombo vingine vya habari vinavyotoa maudhui ya habari, yeye anatoa elimu tu. Pia alidai kanuni hazijitoshelezi kwani hazielezi kwa mtu anayetoa maudhui ya elimu afanyeje, jambo ambaloi si kweli kwani kanuni zinajitosheleza na zinatoa mwongozo wote.

"Kamati imebaini kuwa Polepole TV haina waandishi wenye taaluma ya uandishi wa habari hivyo kukikua misingi ya uandishi na imemuelekeza ahakikishe anazingatia uchaguzi wa maneno yenye sitaha, kuzingatia misingi, kanuni na maadili ya utoaji maudhui mtandaoni.

Maamuzi ya Kamati

Kama imejiridhisha kuwa Polepole TV imekiuka shria za mawasiliano kwa njia ya kieletroniki, hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 44, kifungu kidogo cha kwanza, sehemu G cha sheria ya mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania, sura ya 172, na marejeo yake ya mwaka 2017, na kanuni ya 21, kanuni ndogo ya tatu na sehemu A ya kanuni tajwa hapo juu, Kamati inatoa adhabu zifuatavyo.

Kituo kinapewa onyo kali. Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole TV kusimamishwa kwa muda mpaka pale atakapofanya yafyatayo. Kuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi wa habari na utangazi na kuleta tija na ufanisi katika vipindi vyake. Kuhakikisha vipindi vyake vyote vinazingatia sheria, misingi na kanunia za uandishi na utangazaji wa habari pamoja na masharti ya leseni yake.

"Baada ya kuzingatia maelekezo hayo Kituo cha Humpohrey Polepole kitatakiwa kutoa taarifa TCRA ambapo TCRA ikijirishisha kuwa maelekzo yote yamezingatiwa kipindi cha Humphrey Polepole kitajrejea na kitakuwa chini ya uangalizi wa TCRA kwa muda wa miezi sita.

Uamuzi huu umetolewa leo jijini datr es Salaam, uamuzi wa kukata rufaa kupitia FCT upo wazi ndani ya siku 21.

Mwenyekiti wa Katai ya Maudhui ya TCRA, Habbi Gunze.
Haha, tutaelewana tu "polepole" na Watetezi wa Legacy😀
Ha ha ha!
Inaelekea kwa ukaidi wake, Polepole kesha kuwa kichwa cha msumari unaopigwa nyundo kuwatokomeza "waliounga juhudi"
 
Mchimba kisima kaingia mwenyew bhana
Raisi wa marekani Joe Barden aliomba aonane na mwanamziki Lady gaga baada ya kusema yeye hatochanja kwa kuwa rafiki wa binamu yake baada ya kuchanja amepoteza uwezo wa nguvu za kiume na kusababisha uchumba na mchumba wake kuahilishwa.

Sasa tanzania amabapo wamesema kuchanja ni hiali bado viongozi wanatuma TCRA kubana watu kwa hoja za hovyo na ni wasomi wanaotegemewa.

Unashangaa msomi gani anaweza kutoa hoja kama zile?
Viongozi wabadilike ni muda sasa wa kufanya mambo kwa kuheshimu watu na haki zao na pia kuheshimu nafasi walizonazo ili waweze kutumikia nchi kwa uzalendo.
 
Huyu akili yake ni mbilikimo
Najua huwezi kunielewa na wala siyo wewe tu ambae utashindwa kunielewa.

Sheria inapotungwa alietunga sheria ni pamoja na yule alieiunga mkono.Polepole alikuwa kinara wa kuunga mkono sheria kandamizi enzi zile za utawala wa Bwana Chato.

Ni matumaini yangu kuwa sasa umeelewa.
 
Tatizo kubwa la nchi hii ni watanzania wanaojiita wasomi na wataalum.
TCRA na wataalum wake sijui kama wanatambua thamani walionayo
Wasomi gani mtu anakalia ofisi kuuubwa anashindwa musoma statement huu upuuzi wa serikali utawagharimu
 
Back
Top Bottom