TCRA, hawa matapeli wa “TUMA KWA NAMBA HII” tutaishi nao milele?

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Ni kipindi kirefu sasa kumekuwepo aina hii ya utapeli tulioubatiza jina la “TUMA KWA NAMBA HII”. Wapo waliofanikiwa kukwepa na wapo waliolizwa, na bado kuna wahanga watarajiwa.

Haya yanatokea hata baada ya zoezi la usajili wa laini za simu ambao uliaminisha wengi ungekuwa suluhu ya jambo hili. Miaka inapepea na bado tunalijadili.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa utapeli huu unaratibiwa na watendaji wa makampuni ya mawasiliano na taasisi za fedha. Wengine wasema lawama zinapaswa kuvishwa kwa wahanga wenyewe kwa uzembe wao uliopitiliza, na wapo wanaonyooshea kidole Mamlaka yenye dhamana ya Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kushindwa kudhibiti tatizo hili.

Kuna wakati TCRA ilikiri ongezeko la matapeli hawa, mara baadaye tukataarifiwa kukamatwa kwa baadhi yao. Hata hivyo, bado watu wanalizwa tu. Kila leo wanaibuka na namba mpya na kutekeleza uhalifu wao kwa kujiamini. Tena wakikushindwa wanakuporomoshea matusi kadhaa ukae nayo kwa kutulia.

TCRA nipeni maelezo ya kunishawishi hapa. Mnashindwa kuratibu zoezi la kuwakomesha wahalifu ambao mna taarifa zao? Kukamata kadhaa kwa ajili ya publicity yenu ili muonekane mnatekeleza majukumu yenu bila kukomesha tatizo, ni kutotutendea haki - ni uhuni!

Sasa, tuendelee tu kuvumilia kwa imani ya kwamba jambo hili litafikia ukomo au tutulie tu tukijua “tutaishi nao”?
 
Ukifuatilia utaona hizi sms zinakufikia sana pale either ukiwa na hela kwenye simu au ukiwa umefanya miamala kadhaa which means mitandao ya simu kuna watu wasio waaminifu wanauza taarifa za wateja.
 
Siku moja niko hospitali moja ya rufaa nchini, nilimkuta mama mmoja ambae alipigiwa na mtu aliyejitambulisha kama mwalimu na kuhitaji hela mwanae yupo hospitali. Kama mjuavyo mtoto kwa mama, hakuwaza mara mbili akatuma pesa, akataarifu watu wa karibu na akaacha ratiba yake kumfata mwana hospitali, ilikuwa mshike mshike...

Zipo taarifa wananunua zile counter book za wageni zilizojaa kwenye mashule na taasisi nyingine..

Kama waliweza kupata sauti za Kinana/Nape wakitumia simu, Cyber wanashindwaje kuwapata hawa wasio na uzito wowote kwenye hii nchi?
 
Kuna siku nilikuwa nachat na mdogo wangu ,akaomba nimtumie hela ,nikamwambia badaye kidogo subiri.

Baada ya mda ikaingia msg " ile hela tuma kwenye namba hii".

Nilidhani ni mdogo wangu katumia namba nyingine maana ndo tumelewana kumtumia.

Mi nina desturi ya kufuta msg zikiingia so nikafuta hiyo namba . Baadaye nikampigia mdogo wangu kwamba nitumie ile namba nimefuta. Ndo akaniambia mi natumia namba yangu hiyo sijui.

Usipokuwa makini na umeongea na mtu kumtumia hela hiyo msg ikaingia unaweza ukamtumia kweli.
 
Nchi yetu na nyingi za ulimwengu wa tatu zina tatizo kubwa la kuruhusu jambo lililo kinyume na sheria ama uhuni tu kuendelea kwa muda huku taasisi zenye kazi ya kuzuia uhuni huo kukaa kimya.

Unaweza kusema huwezi kutapeliwa, lakini hiyo haina maana kuwa kinachoendelea kiendelee tu.

Nakumbuka tarehe 9 Mei 2022 majira ya saa 2.50 usiku nilipopokea ilikuwa simu ya ndugu yangu lakini alitumia namba ya mtu mwingine akiomba kiasi fulani cha pesa ili afanyiwe kipimo siku ya pili asubuhi (huyu alikuwa mgonjwa amelazwa katika hospitali fulani), katika mazungumzo nilimuuliza hiyo pesa nitume kwenye namba hii? akasema ndio.

Uzuri nilikuwa na hicho kiasi hivyo skupoteza muda, nikafanya muamala. Nikapiga kumueleza kuwa nimeshafanya muamala, naye akathibitisha kupokea.

Dakika chache baadaye ikaingia meseji kutoka namba 0733 584 129 iliyosomeka ''Nitumie tu kwenye namba hii 0716 135 528 Jina ni PAULO MAEMBE''

Hapa nikatafakari sana, kutapeliwa ni rahisi sana kwa sababu ya ''coincidence'', yaani kama ningekuwa sijatuma ile hela kwa ndugu yangu kulikuwa na nafasi kubwa sana kwa mimi kutuma ile hela kwa sababu ya mfuatano wa matukio na uharaka wa pesa husika.

Kwa kuwa nilikuwa na muda na kwa kuwa ni jambo rahisi kufanya uchunguzi mdogo, nikaamua kuanza kumtafuta huyu mtu anayeitwa Paulo Maembe.

Katika ulimwengu wa kidijitali, kupata taarifa ni jambo rahisi sana. Na wengi wetu tunaacha ''digital prints'' kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ''search engine'' jina la Paulo Maembe likatokea mara kadhaa, nikaanza kumtafuta kwenye mitandao, baada ya siku chache nikapata mpaka namba halisi ya simu na mahali anapoishi.

Baada ya mazungumzo nikagundua kuwa namba yake imesajiliwa mara kadhaa na yeye mwenyewe hajui. Kwa wepesi tuliweza kuthibitisha mpaka kijana aliyemsajilia line ya simu ambaye kwa makusudi alisajili namba za ziada kwa sababu hizi za utapeli.

Zoezi la yeye kuthibitiisha namba zake likafanyika na hatimaye ile namba ya utapeli ikawa ipo ''deactivated''.

Mambo machache niliyogundua kuhusiana na huu utapeli wa ''tuma kwenye namba hii''

1. Vijana wengi wanaosajili namba nje ya ofisi husika za mitandao ya simu, huwa wanasajili namba nyingi unapoenda kusajili.

Wakati wanakwambia network inasumbua huku ukiwa umeshaweka finger print jua amesajili namba ya kwanza, anapokwambia embu turudie jua hapo inasajiliwa namba ya pili. Baada ya hapo anakupa namba moja huku ukiwa umebakisha namba nyingine mezani kwake ambayo yeye ataiuza kwa wanaohitaji hiyo namba.

Hizi namba zinanunuliwa na watu wengi haswa hao matapeli lakini hata ambao sio matapeli wanapotaka kuficha identity zao.
Kwa mujibu wa hawa vijana hizi namba huuzwa kati ya 30,000 - 50,000/-

Wengine wanaonunua namba hizi ni wageni wanaoishi hapa Tanzania hasa hawa wanaotoka nchi za Kiafrika.

2. Watu wengi hawana muda wa kujiridhisha namba ambazo zimesajiliwa kwa majina yao ( Namba ya Kitambulisho cha Taifa) , wengi wanatembea mjini hapa lakini kitambulisho chake kimetumika kusajili namba nyingi bila wao kujua na hawataki kujua.

3. Mfumo wa TCRA wa kuwasilisha malalamiko na mitandao ya simu sio rafiki sana. Maana inabidi mara nyingi uanzishe kesi polisi, na kama mjuavyo Watanganyika na masuala ya polisi. Wengi huamua kuacha tu huku wakisubiri tukio lingine la utapeli.

4. Watu wengi hatuna muda wa kutaka kujiridhisha kuhusu mtu tunayetaka kumtumia pesa, inawezekana una ahadi ya kumtumia pesa mtu, yaani ukipokea meseji ya hivi huchukui muda kutaka kuthibitisha. Ni vyema tuwe tunathibitisha.

1653551263129.png
1653551263129.png
 
Chanzo cha haya yote ni makampuni ya simu yanayoruhusu usajili wa hovyo wa line za simu, na pia serikali kwa kutokuweka sheria kali za kuwadhibiti hawa matapeli.
 
Naona wamelitelekeza hili jambo kabisa. Sijui wanata tuishi nalo tu kama ilivyo malaria.
 
View attachment 2239057View attachment 2239057
Hapo mjibu hivi... Nshatuma katika Ile nyingine
 
Siku moja niko hospitali moja ya rufaa nchini, nilimkuta mama mmoja ambae alipigiwa na mtu aliyejitambulisha kama mwalimu na kuhitaji hela mwanae yupo hospitali. Kama mjuavyo mtoto kwa mama, hakuwaza mara mbili akatuma pesa, akataarifu watu wa karibu na akaacha ratiba yake kumfata mwana hospitali, ilikuwa mshike mshike...

Zipo taarifa wananunua zile counter book za wageni zilizojaa kwenye mashule na taasisi nyingine..

Kama waliweza kupata sauti za Kinana/Nape wakitumia simu, Cyber wanashindwaje kuwapata hawa wasio na uzito wowote kwenye hii nchi?
Watakuwa wana-enjoy tunavyopigwa.
 
Back
Top Bottom