TCRA fuatilieni tiGopesa, inakata mirija kwa mawakala

Haihitaji signals, wangetaka kukomesha wangezuia tu transactions za hivi.... yaani muamala usikamilike tu iwapo mpokeaji [kutoka kwa wakala] yuko nje ya eneo.
Yah! Systems ziwe zinareject miamala nje ya eneo husika hiyo ndo suluhisho pekee.
 
Ok. Nawaelewa mitandao wasipowalipa. Kwasababu ukimuwekea mtu wewe unapata gawio, na wao wanategemea uliomuwekea atume kwa mtu ili wao wapate hela. Sasa wewe ukimuwekea mtu wa Songea kwa kumtumia mtu wa Dar inamaanisha hawatapata hela kwasababu yule mtu hatumi anakutumia wewe kuweka bure.
Lakini je, unaona hilo suala liko ndani ya uwezo wa Wakala kujua eneo la alipo huyo anayemtumia ? Maana Kuna mteja anakuja na namba kichwani na haumfahamu. Kwa nini wao mitandao wasiweke utaratibu wa kureject hiyo miamala kwa Wateja waliopo nje ya eneo husika ili kumlinda huyu Wakala asifanye kazi bure ?
 
Wakala na mitandao wanajua makubaliano yao na jinsi ya kufanya hio kazi.
 
Mimi pia nafanya hii biashara mzee ukisema ufanye hayo yote uliyoyataja jiandae kupoteza wateja
Kweli kabisa, eti mteja aje uanze kumuandikisha majina, namba, kitambulisho. Si utajikuta unahudumia wateja 5 kwa siku. Haya Mambo yalikuwa yanatekelezeka zamani idadi ya watumiaji wa hizi huduma ilipokuwaga ni ndogo.
 
Eneo unalotolea huduma letsay unatoa huduma kata Fulani ukituma kwenda mbali na eneo hurejeshewi kamisheni , swali la kizushi kuna sheria iliyotungwa na kama IPO kwanini wasiweke kwenye matangazo yao ili wateja wajue?

Sent using Jamii Forums mobile app
Point!
Mitandao wahuni sana. Ni kweli mawakala wengi maskini wanakuta wanapata kamisheni ndogo sana bila kujijua. Ilibidi mitandao iwaweke wazi. Japo kna wakati zamani walikua mawakala wanakataa kumtumia mtu hela direct na hasa akiwa mbali.
 
Lakini je, unaona hilo suala liko ndani ya uwezo wa Wakala kujua eneo la alipo huyo anayemtumia ? Maana Kuna mteja anakuja na namba kichwani na haumfahamu. Kwa nini wao mitandao wasiweke utaratibu wa kureject hiyo miamala kwa Wateja waliopo nje ya eneo husika ili kumlinda huyu Wakala asifanye kazi bure ?
Mimi pia nna kijiwe changu maarufu mtaani cha hii mitandao, mwanzoni nilikuwa nawachaji kwa ambao wanatuma pesa nje ya mji, kuna siku mmoja akanichana ukweli kwamba mbona sehemu nyingine tukienda hatuulizwi maswali ya sijui 'unatuma kwenda wapi, ni hapa tu naona hayo maswali', na kabla jamaa hajanichana nilishagundua kuna upungufu wa wateja, maana siku za nyuma nilikuwa na wateja wengi sana. Nikapiga akili nikaamua niachane na hayo maswali, kila anayekuja namtumia for free, sahivi naona wateja wanaanza kurudi kama zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ya fedha ni ngumu sana. Ugumu umekuwa mkubwa zaidi pale line zilipoanzwa kuuzwa kiholela. Kama mtoa mada ungesoma sheria na taratibu za hizi mitandao kabla ya kuwa wakala Leo usingepiga kelele. Unacholalamikia ni issue ambayo wao wamekukataza na wewe kwa ukaidi wako umefanya. Ufahamu kwamba hiyo bypass inawapunguzia circulation na profit?

Najua utaniuliza kuwa we utajuaje kwamba muamala unaenda kwa mtu mwingine? Jibu ni kwamba sisi mawakala ndio tulikiuka taratibu. Wao taratibu zao zinataka mteja akupe kitambulisho hapo ndipo pa kutambua mhusika. Zilipoanza kuzagaa line baadhi ya mawakala wakapuuza kitambulisho, waliodai wakakimbiwa, kwenda na soko kila mmoja akapuuza.

Jambo la kushauri ni kwamba mitandao ifanye mabadiliko katika suala la uwekaji pesa. Iwe kama benki kuweka umwekee mtu yeyote bila kujali uwepo wake, sheria Kali ziwe katika kutoa ni lazima muhusika awepo ili kutoa ulinzi wa wizi.

Kingine hebu fanya research, tigo kila muamala wanakuonyesha commission yake, fanya kujumlisha commission za miamala yote ya siku kisha linganisha na commission watakayo kuonyesha kesho yake, kisha upate majibu halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Wakuu,

Binafsi na declare interest kuwa najihusisha na biashara za miamala ya mtamdao ya simu
Nimegundua, Mapema January baada ya Kamisheni Kushuka kwa ghafla.

Nilichogundua ni kutokulipwa kwa Mrejaa (kamisheni) pindi ninapo hudumia mteja anaetuma fedha kwa mteja alie nnje ya eneo, nilipoulizia kwa wakala mkuu nilijibiwa kuwa ukituma fedha direct kwenda kwa mtu aliye nje ya eneo hulipwi kamisheni/mrejaa hivyo unapaswa kumtumia mteja husika yeye ndio atume kwenda huko anakotaka kutuma, kama mjuavyo wateja wanakwepa makato lakini pia mteja anaweza akawa anataka kutuma fedha ila yeye hana laini ya Tigo.

Kilichonifanya niandike makala hii jikuwa wao TIGO wanakata makato kwa muamala husika lakini wakala harejeshewi kamisheni ya muamala husika why ?

Kama wanakata makato kwanini wasirejeshe? kwanini wao wanajipa? Na kwanini mitandao mingine wanatoa kamisheni hata utume popote?

Binafsi huu nauona kama wizi ambao umefumbiwa macho, nawasihi TCRA walifuatilie hili na wachukue hatua

NB: Nimewataja TIGO kwakua wao pekee ndio wanafanya hivi wengine hawana hii kadhia

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulivosaini ule mkataba wenye kurasa nyingiiiii, ulisoma kipengele kwa kipengele? au ulikimbilia tu kusaini bila kusoma mkataba wote? Kwa taarifa yako ikibainika umehudumia mteja ambaye hayupo mbele yako/mteja wa mbali adhabu yake ni kunyang'anywa uwakala. Kutokukulipa kamisheni n bado tu wamekufanyia huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa ni utaratibu mzuri, lakini kwa sasa umepitwa na wakati. Tunatumia hizi huduma kwa sababu ya upatikanaji wake uliopo kila Kona. Kwa hiyo nishindwe kupata huduma ya kutoa au kuweka kisa sina kitambulisho ? Huyo Wakala atahudumia wateja wangapi kwa siku kwa utaribu huo wa kuandika hizo taarifa.
Hapa bongo tanaishi kwa mazoea ndo maana ww unaona haiwezekani ila kuna nchi ni lazima kila mtu above 18 awe na id piga ua na kama huna ukikamatwa inakula kwako.
Pia hata hapa bongo kama serikali ikiamua hilo basi sio kazi ni rahisi sana.na sio kutembea nacho tu bali kila ofisi ama huduma utakayo hitaji basi ni lazma uonyeshe id yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hoja nyingine mwaka Jana kurudi nyuma walikua wanatoa kamisheni kwa miamala aina zote why walisitisha? tens kwa sisi mawakala ambao ndio tunafanya mitandao yao endelee kung'ara hawakutushirikisha, sasa sisi mawakala watu wamebaki wanagugumia ukiuliza kwa wakala mkuu anakwambia usitume pesa kwa mteja wa mbali huo ndio utaratibu, unajiuliza zamani tulituma pesa kwa wateja wa mbali na tulilipwa, sasa why now and why mitandao mingine inalipa? nimetumia fursa hii ambayo najua mawakala wenzangu hapa watatiririka na wadau wengine mtatiririka ombwe hili wahusika najua wataliona tena ikiwezekana mu watag huu ni ubabaishaji kama sheria IPO miamala I we rejected watu wanawekeza pesa mwisho wa mwezi wanaambulia 20k sijui 40k THIS IS BULL SHIT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia nna kijiwe changu maarufu mtaani cha hii mitandao, mwanzoni nilikuwa nawachaji kwa ambao wanatuma pesa nje ya mji, kuna siku mmoja akanichana ukweli kwamba mbona sehemu nyingine tukienda hatuulizwi maswali ya sijui 'unatuma kwenda wapi, ni hapa tu naona hayo maswali', na kabla jamaa hajanichana nilishagundua kuna upungufu wa wateja, maana siku za nyuma nilikuwa na wateja wengi sana. Nikapiga akili nikaamua niachane na hayo maswali, kila anayekuja namtumia for free, sahivi naona wateja wanaanza kurudi kama zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili suala ni gumu sana kwenye utekelezaji. Hata baadhi ya mitandao naona hata wao wanalijua hili. Ukienda kuchukua laini yako ya uwakala hawatakupa yake mavitabu ya kutunizia hizi taarifa sababu wanajua hayana manufaa. Mtu katoka zake site huko boss kamtumia hela kwa Tigopesa anakuja kwako achomoe japo nauli uanze kumuuliza sijui habari za kitambulisho atakuelewa kweli ? Hatokuja tena kwako siku nyingine.
 
acha uzandiki wewe kubaini umetuma hela kwa MTU alive mbali ni process unahitaji mahojiano na mteja dakika zisizo pungua mbili, pia kuna kudanganywa hivyo suala hili ama sheria hiyo imepitwa na wakati hai work now na mitandao husika itakosa mapato serikali itakosa mapato, na ukumbuke tunazungumzia issue ya kwanzia mwaka huu na sio siku za nyuma sasa huko nyuma walivyokua wanalipa hayo unayosema yalikua haypo? au hayajulikani?
Ulivosaini ule mkataba wenye kurasa nyingiiiii, ulisoma kipengele kwa kipengele? au ulikimbilia tu kusaini bila kusoma mkataba wote? Kwa taarifa yako ikibainika umehudumia mteja ambaye hayupo mbele yako/mteja wa mbali adhabu yake ni kunyang'anywa uwakala. Kutokukulipa kamisheni n bado tu wamekufanyia huruma

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa bongo tanaishi kwa mazoea ndo maana ww unaona haiwezekani ila kuna nchi ni lazima kila mtu above 18 awe na id piga ua na kama huna ukikamatwa inakula kwako.
Pia hata hapa bongo kama serikali ikiamua hilo basi sio kazi ni rahisi sana.na sio kutembea nacho tu bali kila ofisi ama huduma utakayo hitaji basi ni lazma uonyeshe id yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo yatawezekana endapo tayari Kuna mipango madhubuti tayari imeshawekwa mfano ikipitishwa hiyo Sheria ya kila raia kutembea akiwa ameivaa kitambulisho chake muda wote awapo nje ya makazi yake. Ila kwa sasa ambavyo ni watu wachache tu waliobahatika kuwa na hivi vitambulisho inakuwa ni uongo.
 
Of course hilo suala liko ndani yao, kwa kuwa wao ndio wenye uwezo wa kuthibitisha kuwa hiyo namba iko nje ya eneo husika, system yao ilibidi iwe na uwezo wa kureject hizo transactions kisha mteja aelekezwe utaratibu wa namna ya kutuma hiyo hela kwa kupitia namba yake, kuliko wao kumfanyisha kazi wakala pasipo kumpa mrejea.
Hii ni sahihi sana. Ila naona wangetaka kuweka mfumo wa kureject transactions wangeshafanya tangu zamani, labda kuna ulaji huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia nna kijiwe changu maarufu mtaani cha hii mitandao, mwanzoni nilikuwa nawachaji kwa ambao wanatuma pesa nje ya mji, kuna siku mmoja akanichana ukweli kwamba mbona sehemu nyingine tukienda hatuulizwi maswali ya sijui 'unatuma kwenda wapi, ni hapa tu naona hayo maswali', na kabla jamaa hajanichana nilishagundua kuna upungufu wa wateja, maana siku za nyuma nilikuwa na wateja wengi sana. Nikapiga akili nikaamua niachane na hayo maswali, kila anayekuja namtumia for free, sahivi naona wateja wanaanza kurudi kama zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
kama unafanya miamala ya kutuma mbali basi hapo hupati faidi unakua umewahudumia tu kwa kuwapa msaada wateja wako ila kamisheni hupati.

Kikubwa kwa mawakala kuwa na misimamo yenu eneo husika msikubali kufanya miamala ya kutuma pesa mbali.labda mteja akubali kukulipa chako kabisa.
Hata ukisoma log book ya m-pesa na tigo pesa wameweka baadhi ya kanuni moja ya kanuni ni muhudumie mteja unaemuona.

Tofauti na hapo msidhani kama eti kampuni siku moja zitakubali matakwa yenu nyinyi mawakala kwenye hili jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakala na mitandao wanajua makubaliano yao na jinsi ya kufanya hio kazi.
Ni kweli, taratibu ziko wazi kitambulisho ndio kinachokuwezesha kujua, na hata log book za uwakala zina column ya kujaza namba kitambulisho. Hali ilikuwa mbaya baada ya mawakala kuwa wengi competition iliwafanya wengine wapunguze masharti, waliozingatia masharti hawakupata wateja, na wao wakaamua kuacha kudai ID, Leo tunamlalakia tigo wakati tulikubali masharti na taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii sindano imeanza kuwaingia baarhi yao wameanza kuja kwenye huu Uzi wanajaribu kutoa majibu mepesi.... wenzeno wanalipa kwa fedha IPI halafu kamission huwa mnapandisha kiwango lakini mirejaa kwa mawakala inabaki ileile sana sana mwaka juzi mliipunguza huu nao niwizi mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yatawezekana endapo tayari Kuna mipango madhubuti tayari imeshawekwa mfano ikipitishwa hiyo Sheria ya kila raia kutembea akiwa ameivaa kitambulisho chake muda wote awapo nje ya makazi yake. Ila kwa sasa ambavyo ni watu wachache tu waliobahatika kuwa na hivi vitambulisho inakuwa ni uongo.
Mikakati iliyopo sasa ni ya kutoka huko kwenye kuishi kwa mazoea ndo maana kila mtu lazima awe na nida,na hiyo laini itakayohudumiwa iwe na jina la nida.yani majina ya nida na ya laini yafanane,hata kama ni mgeni awe na id au paspot.

Moja kati sababu nyingi zilizopelekea kuwekwa sheria ya kusajili laini kwa alama za vidole ni kuzuia utakatishaji fedha.
Na wakala anauwezo wa kutakatisha fedha kwa kufanya miamala haramu.
kutuma pesa kwa mtu wa mbali ni kosa,
kumuhudumia mtu bila kukupatia id ni kosa.
kumpa mtu wa mbali namba yako ya wakala ili atoe pesa ni kosa,
Kuvunja miamala ni kosa,
Kutokujaza log book na mteja kusaini baada ya huduma ni kosa,
Ila kwa sababu tunaishi kwa mazoea mambo yote hapo juu mawakala mnayafanya tena sana tu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom