Tozo za lipa kwa simu mitandao inakomesha wateja au mawakala

Mr. Marangu

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,565
1,516
Inavyo onekana mitandao ya simu haiko Regulated kumaintain balnce of fairness kati yake na mlaji pamoja na a mawakala (Agent)

Hivi siku za karibuni ukianzia Dec 2022, Mitandao ya simu imekua ikiongeza tozo(charges) kwenye kulipia huduma kwanjia ya simu

Kwa mfano kulipia Bidhaa yenye thamani ya Tsh 10,000 - 19,000/= makato yamekua yakipanda kutokea 180, 200+, 360 na Leo wamepandisha ni Tsh 700/= ukijaribu kuangalia hizi interval ya upandishaji ni karibu kila mwezi wanabadili makato kwa kuongeza charges

Sasa swali la msingi nani anabariki haya makato wanayoya yaongeza? Je, wanawakomoa mawakala waliohamishia huduma za kutoa fedha kwenye LIPA KWA SIMU.

Mitandao hii pia imekua ikipunguza kamisheni kwenye kila muamala anaofanya wakala, je nani anasimamia haki za mawakala ili hali hakuna chama cha MAWAKALA WA MIAMALA ?

Je, Serikali na Mitandao ya Simu wanacheza michezo ya Pledge Bargain???
 
Shida ni Wabongo tumekuwa wapigaji sana, kuna time lipa kwa simu ilikuwa ni free of charges, mawakala wakagundua mwanya wa kupigia hela sasa ikawa mteja akienda kutoa hela kawaida wakala anamwambia lipa kwa simu na anaambiwa aweke kiasi kile kile cha kutolea plus makato. Makampuni ya simu wamekuja kuligundua hilo na wao wakaanza kutembeza koleo.
 
Dah hii huduma changamoto wateja wamehama na kuanza kutumia huduma za Lipa as if ni halali mi naona Bora makampuni ya simu wafute huu utaratibu kwa muda
 
Back
Top Bottom