TCRA fuatilieni tiGopesa, inakata mirija kwa mawakala

Kama ni kweli wana nia ya dhati ya kuzuia watu wasitume pesa mbali direct kutoka kwa wakala, kwa nini wasiukomeshe huu mchezo kwa kuwapa signals mawakala kujua kama mteja huyu anajirushia yeye au anamtumia mtu wa mbali?

Haihitaji signals, wangetaka kukomesha wangezuia tu transactions za hivi.... yaani muamala usikamilike tu iwapo mpokeaji [kutoka kwa wakala] yuko nje ya eneo.
 
Yani ipo hivi, kazi hii ya uwakala kwa mtu anaekuja kuweka pesa kwa wakala haitakiwa atume bali aweke

1. kutuma ni kumrushia mtu pesa akiwa mbali na eneo hilo

2. Kuweka ni kujiwekea wewe mwenyewe mteja kupitia kwa wakala

Sasa wateja wengi hutuma kuliko kuweka kwa sababu mbali mbali, wengine hawana namba ya mtandao husika, pia wengine hawana elimu ya kutuma pesa kwenda mitandao mingine, wengine wanakwepa makato mara mbili.

Note
Mtoa mada analalamika kwa nini hii mitandao hususani voda na tigo haiwalipi mawakala kamisheni kwa wateja wanaotumiwa pesa wakiwa mbali, kwani ni vigumu mno kwa wakala kujua huyu mteja anaweka au anatuma, maana mteja mwingine anaweza kukudanganya kuwa anaweka kumbe anatuma

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa uemeendelea kuelekeza vyema mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huwezi kujua sana sana kesho yake ile mirejaa ulooneshwa haitalingana na kamisheni ya siku nzima itapungu Fanya utafiti utaligundua hili

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilifanya utafiti, kwa voda ndio wapo hivyo, ila tigo hapana hawafanyi hivyo labda kama wameanza siku hizi.

Kinachofanyika kwa tigo kama ulipata siku ya jana kamisheni jumla elfu 50, wao wanakupa 45k

Note.
Tigopesa kodi ya serikali wanaikusanya kwa kukata direct 10% kutoka kwa jumla ya kamisheni ya wakala ya kila siku, kamisheni ya mwisho wa mwezi inakuja kama ilivyo

M pesa wanakupa kamisheni yote mwisho wa mwezi halafu ndio wanakata 10% kodi ya serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumieni airtel money, kwani ni lazima kutumia tigo na voda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na airtel money kwa hapa dar atawashusha hawa tigo na voda, mimi kwenye laini zangu sasa airtel money anamkalisha huyo m pesa

Note
Airtel money ana udhaifu mkubwa wa network na huduma kwa wateja, akiliboresha hili atakuwa juu

Tigo ndio mwenye stable network ya pesa akifuatiwa na voda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haihitaji signals, wangetaka kukomesha wangezuia tu transactions za hivi.... yaani muamala usikamilike tu iwapo mpokeaji [kutoka kwa wakala] yuko nje ya eneo.
Hiyo ndio signal sasa, yan mteja akisema niwekee pesa, wakala ukiweka hapo hapo tu, transaction ifeli kwa kukupa ishara fulani,....

Nawe unamwambia mteja kama ana alternative afanye kama hana unamrudishia pesa yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii inachangamoto kubwa, wateja wengi sio wakweli. Mwingine anakwambia simu ameicha nyumbani kwenye chaji, mwingine kamtuma mtoto amemtuma aseme anayemtumia yuko nyumbani, mwingine anakuambia anayemtumia yuko ndani ya hilo eneo/mji, ukijifanya uko strict sana unapoteza wateja wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu, ukijifanya una sheria sana unapoteza wateja

Kuna jirani yangu kafunga ofisi kwa kujifanya anafuata utaratibu sana

Mara akija mteja amuulize kitambulisho na maswali kede kede, mwisho wa siku akawa anajihudumia mwenyewe na vitambulisho vyake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani ipo hivi, kazi hii ya uwakala kwa mtu anaekuja kuweka pesa kwa wakala haitakiwa atume bali aweke

1. kutuma ni kumrushia mtu pesa akiwa mbali na eneo hilo

2. Kuweka ni kujiwekea wewe mwenyewe mteja kupitia kwa wakala

Sasa wateja wengi hutuma kuliko kuweka kwa sababu mbali mbali, wengine hawana namba ya mtandao husika, pia wengine hawana elimu ya kutuma pesa kwenda mitandao mingine, wengine wanakwepa makato mara mbili.

Note
Mtoa mada analalamika kwa nini hii mitandao hususani voda na tigo haiwalipi mawakala kamisheni kwa wateja wanaotumiwa pesa wakiwa mbali, kwani ni vigumu mno kwa wakala kujua huyu mteja anaweka au anatuma, maana mteja mwingine anaweza kukudanganya kuwa anaweka kumbe anatuma

Sent using Jamii Forums mobile app
1 na 2 huwa Wakala anakatwa kwa kutoa huduma hio?
 
Hukatwi hata senti, ila hulipwi kama ukituma kwa mteja wa mbali ila ukiweka kwa mteja wa hapo hapo unapewa faida yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok. Nawaelewa mitandao wasipowalipa. Kwasababu ukimuwekea mtu wewe unapata gawio, na wao wanategemea uliomuwekea atume kwa mtu ili wao wapate hela. Sasa wewe ukimuwekea mtu wa Songea kwa kumtumia mtu wa Dar inamaanisha hawatapata hela kwasababu yule mtu hatumi anakutumia wewe kuweka bure.
 
Mimi pia nafanya hii biashara mzee ukisema ufanye hayo yote uliyoyataja jiandae kupoteza wateja
Airtel wanalipa hata halotel wanalipa hata kama ukituma pesa mikoa tofauti ila voda na tigo hawalipi hata sent tano sijui ni kwa nini.

Ila kama umepitia maswala ya utakatishaji fedha unaweza gundua ni kwa nn airuhusiwi kutuma pesa kwa mtu alie mbali,

Ukifata taratibu za wakala kumuhudumia mteja ni lazma akuonyeshe id yake yenye majina ya kufanana na namba unayo ihudumia iwe mteja anatoa pesa ama anaweka na lazma akuonyeshe kitamburisho na pia ww wakala ujaze taarifa za kwenye hicho kitamburisho kwenye log book na yy mtaja asaini kwenye log book.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vema mkuu,na hili lipo ndani ya uwezo wao,mbona wameweza kwenye vifurushi vya tigo rusha.siku ukiwa unadaiwa tigo wanakata juu kwa juu.na kwenye simu yangu naambiwa mteja atakatwa deni lake kwanini hili la tigo pesa washindwe??
Kutuma pesa mbali si hatari kama kutoa pesa mteja akiwa mbali.

Kama ni kweli wana nia ya dhati ya kuzuia watu wasitume pesa mbali direct kutoka kwa wakala, kwa nini wasiukomeshe huu mchezo kwa kuwapa signals mawakala kujua kama mteja huyu anajirushia yeye au anamtumia mtu wa mbali?

Mimi nadhani wanafurahia mchezo huo kwa sababu

Wanapata faida kubwa kwanza kwa kutomlipa wakala pili kwa kupata ada ya mteja atakaetoa huko mbali kwani uzoefu unaonesha wengi wanaotumiwa pesa wakiwa mbali, hutumiwa kwa lengo la kutoa hapo hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vema mkuu,na hili lipo ndani ya uwezo wao,mbona wameweza kwenye vifurushi vya tigo rusha.siku ukiwa unadaiwa tigo wanakata juu kwa juu.na kwenye simu yangu naambiwa mteja atakatwa deni lake kwanini hili la tigo pesa washindwe??
Yeah, wanaweza sana. Ila nadhani wanaacha hivyo makusudi ili waendelee kujineemesha kwa faida kitonga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok. Nawaelewa mitandao wasipowalipa. Kwasababu ukimuwekea mtu wewe unapata gawio, na wao wanategemea uliomuwekea atume kwa mtu ili wao wapate hela. Sasa wewe ukimuwekea mtu wa Songea kwa kumtumia mtu wa Dar inamaanisha hawatapata hela kwasababu yule mtu hatumi anakutumia wewe kuweka bure.
Lakini elewa pia wengi wanaotumiwa pesa mbali, ndio watoaji hao hao, hivyo faida yao ipo kwa anaetoa. Na kwenye miamala kutoa ndiyo ada inatozwa. Kuweka pesa ni bure ila kutoa ni ada inahusika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au pia waulize hivi: ww huwez kutrack hiyo no na ukajua kama unadanganywa au la kwann wao wasiukatae huo muamala ili hata ukikataa akienda kwa wakala mwingine iwe hivyo hivyo mpaka aje na simu? Mana wateja wengi ni waongo hawasemi ukweli
Eneo unalotolea huduma letsay unatoa huduma kata Fulani ukituma kwenda mbali na eneo hurejeshewi kamisheni , swali la kizushi kuna sheria iliyotungwa na kama IPO kwanini wasiweke kwenye matangazo yao ili wateja wajue?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom