TCRA fuatilieni tiGopesa, inakata mirija kwa mawakala

Habari Wakuu,

Binafsi na declare interest kuwa najihusisha na biashara za miamala ya mtamdao ya simu
Nimegundua, Mapema January baada ya Kamisheni Kushuka kwa ghafla.

Nilichogundua ni kutokulipwa kwa Mrejaa (kamisheni) pindi ninapo hudumia mteja anaetuma fedha kwa mteja alie nnje ya eneo, nilipoulizia kwa wakala mkuu nilijibiwa kuwa ukituma fedha direct kwenda kwa mtu aliye nje ya eneo hulipwi kamisheni/mrejaa hivyo unapaswa kumtumia mteja husika yeye ndio atume kwenda huko anakotaka kutuma, kama mjuavyo wateja wanakwepa makato lakini pia mteja anaweza akawa anataka kutuma fedha ila yeye hana laini ya Tigo.

Kilichonifanya niandike makala hii jikuwa wao TIGO wanakata makato kwa muamala husika lakini wakala harejeshewi kamisheni ya muamala husika why ?

Kama wanakata makato kwanini wasirejeshe? kwanini wao wanajipa? Na kwanini mitandao mingine wanatoa kamisheni hata utume popote?

Binafsi huu nauona kama wizi ambao umefumbiwa macho, nawasihi TCRA walifuatilie hili na wachukue hatua

NB: Nimewataja TIGO kwakua wao pekee ndio wanafanya hivi wengine hawana hii kadhia

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kazi mimi pia naifanya sana, yani sana

Tigopesa hapana unawaonea, wanalipa kila muamala unaoweka kwa mteja, hata awe kigoma wewe wakala upo dar, wanalipa.

Hako kamchezo ka kutolipa mawakala kwa direct deposit wanako Voda M pesa pekee na huwa wanasema kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr. Marangu ni kutuma au KUMUWEKEA mteja alioko mbali? Yaani nakuja kwako Wakala kakwambia niwekee 10,000 kwenye namba ****** ambae yuko eneo lingine(Simu siko nayo).

Kuweka naelewa mteja hakatwi, nyinyi huwa mnakatwa pindi mteja akiweka hela?
 
Of course hilo suala liko ndani yao, kwa kuwa wao ndio wenye uwezo wa kuthibitisha kuwa hiyo namba iko nje ya eneo husika, system yao ilibidi iwe na uwezo wa kureject hizo transactions kisha mteja aelekezwe utaratibu wa namna ya kutuma hiyo hela kwa kupitia namba yake, kuliko wao kumfanyisha kazi wakala pasipo kumpa mrejea.
Ni kweli kabisa mkuu, mimi naona hawa TCRA ni kama wamesinzia, hawawalindi mawakala kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je kama wewe ni wakala utajuaje kuwa mteja huyu anamtumia mtu aliye mbali?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni suala gumu ndio maana nasema, mtandao husika kwa kuwa wao wanajua hii hela inatumwa toka sehemu fulani kwenda sehemu nyingine ambayo ni nje ya eneo hela ilipotumwa. System yao ilibidi iwe inareject hizo transactions husika, Kisha mteja aelekezwe kuwa hela hiyo imegoma kwenda kwa sababu imetumwa nje ya eneo hivyo mhusika anapaswa aingiziwe hiyo hela kwenye namba yake kisha yeye ndo atume. Na hapo hata wao watakuwa wanamaximize profit kwa kuepuka hizo Bypass hapo.
 
Mr. Marangu ni kutuma au KUMUWEKEA mteja alioko mbali? Yaani nakuja kwako Wakala kakwambia niwekee 10,000 kwenye namba ****** ambae yuko eneo lingine(Simu siko nayo).

Kuweka naelewa mteja hakatwi, nyinyi huwa mnakatwa pindi mteja akiweka hela?

Akikujibu ukamwelewa nistue.
 
Mitandao ni wajanja sana, wao wanataka wapate faida hata isiyo halali yao, ndio maana huu mchezo wanaupenda sana. Huo mchezo hawawezi kuudhibiti, Mimi nalia na TCRA, ilibidi wao ndio wawabane hawa wa mitandao ili waweke utaratibu huo wa kuonesha namba kama ipo mbali au karibu, ili wakala usifanye kazi ya bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda pia hawakulipi kama ukituma pesa kwa mtu alie mbali.malizana kabisa na mteja anaetuma direct akupe chako kabisa.
lkn pia jua kwamba wakala ukituma pesa ww direct unawakosesha mapato. muwekee yeye mteja unaemuona alafu yy akituma anakatwa na ya kutumia kampuni inakua imeingiza hela.
Lkn pia kutuma pesa mbali ni hatari hasa kwa mteja ambae huja mfahamu vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutuma pesa mbali si hatari kama kutoa pesa mteja akiwa mbali.

Kama ni kweli wana nia ya dhati ya kuzuia watu wasitume pesa mbali direct kutoka kwa wakala, kwa nini wasiukomeshe huu mchezo kwa kuwapa signals mawakala kujua kama mteja huyu anajirushia yeye au anamtumia mtu wa mbali?

Mimi nadhani wanafurahia mchezo huo kwa sababu

Wanapata faida kubwa kwanza kwa kutomlipa wakala pili kwa kupata ada ya mteja atakaetoa huko mbali kwani uzoefu unaonesha wengi wanaotumiwa pesa wakiwa mbali, hutumiwa kwa lengo la kutoa hapo hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr. Marangu ni kutuma au KUMUWEKEA mteja alioko mbali? Yaani nakuja kwako Wakala kakwambia niwekee 10,000 kwenye namba ****** ambae yuko eneo lingine(Simu siko nayo).

Kuweka naelewa mteja hakatwi, nyinyi huwa mnakatwa pindi mteja akiweka hela?
Mfano wewe uko Dar mi niko Mbeya, kaja mteja na sh 100,000 ambayo anataka kukutumia wewe huko Dar, mi kwenye akaunti yangu itapunguzwa hiyo 100,000 kwa muamala nilikufanya, lakini kwa sababu uko nje ya eneo mimi sitapewa commission ( mrejea) kwa muamala nilioufanya Kama ambavyo ningepewa kwa mteja aliye eneo la karibu. Kwa hiyo nakuwa nimefanya kazi ya kanisa.
 
Hii kazi mimi pia naifanya sana, yani sana

Tigopesa hapana unawaonea, wanalipa kila muamala unaoweka kwa mteja, hata awe kigoma wewe wakala upo dar, wanalipa.

Hako kamchezo ka kutolipa mawakala kwa direct deposit wanako Voda M pesa pekee na huwa wanasema kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Fanya utafiti kwenye msg inayoonekana baada ya kufanya muamala huonesha umelipwa Ila kesho take ukiangalia unakuta kiasi kidogo sana ukiulizia unaambiwa ulifanya miamala nnje ya eneo, nimefanya utafiti na ni mganga, labda wewe unawateja wengi hivyo inakua ngumu kutrack sisi wenye wateja wwchache kila kitu kipo wazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
radicals hapa ndio simuelewi mleta mada
Yani ipo hivi, kazi hii ya uwakala kwa mtu anaekuja kuweka pesa kwa wakala haitakiwa atume bali aweke

1. kutuma ni kumrushia mtu pesa akiwa mbali na eneo hilo

2. Kuweka ni kujiwekea wewe mwenyewe mteja kupitia kwa wakala

Sasa wateja wengi hutuma kuliko kuweka kwa sababu mbali mbali, wengine hawana namba ya mtandao husika, pia wengine hawana elimu ya kutuma pesa kwenda mitandao mingine, wengine wanakwepa makato mara mbili.

Note
Mtoa mada analalamika kwa nini hii mitandao hususani voda na tigo haiwalipi mawakala kamisheni kwa wateja wanaotumiwa pesa wakiwa mbali, kwani ni vigumu mno kwa wakala kujua huyu mteja anaweka au anatuma, maana mteja mwingine anaweza kukudanganya kuwa anaweka kumbe anatuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr. Marangu ni kutuma au KUMUWEKEA mteja alioko mbali? Yaani nakuja kwako Wakala kakwambia niwekee 10,000 kwenye namba ****** ambae yuko eneo lingine(Simu siko nayo).

Kuweka naelewa mteja hakatwi, nyinyi huwa mnakatwa pindi mteja akiweka hela?
hizi kuali za kutuma au kuweka huwa inategemea na nani anaongea mteja akija akisema nitumia wakala kwake kitendo ni cha kuweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom