TBS mnaandaa mazingira ya rushwa ukaguzi wa magari?

Logic ya kukagua magari nje ilikua kuhakikisha magari yasiyo na viwango hayaruhusiwi kuja nchini. Yanabaki hukohuko. Sasa TBS imeamua yakaguliwe baada ya kufika bandarini...
TBS wanataka "kuvuta".

Naona TAKUKURU hapa waweke nyavu zao, watavuna wengi.

Naufanisi usipokuwepo, waweke njia mbadala ya kuwashitaki kwa ucheleweshaji magari mikononi mwao.
 
Kwa kweli Yani utakuwa mtihani mkubwa sana na utapelekea storage charges kuwa kubwa sana kwa mwananchi.
 
Tangazo la TBS lililotolewa majuzi, ati sasa ukaguzi wa magari used utafanyika hapahapa Bandarini linatia wasiwasi..
Mkuu seikali inapitia vikwazo vikali toka kwa wafadhili. Pesa hakuna. Huo ni ubunifu wa chanzo kimojawapi cha mapato ya Chato.
 
MAKUSANYO YA PESA TOKA TBC, MAKUSANYO YA PESA TOKA POLISI BARABARA, TUTAHESHIIANE KWA MIAKA 5 MINGINE
 
Tangazo la TBS lililotolewa majuzi, ati sasa ukaguzi wa magari used utafanyika hapahapa Bandarini linatia wasiwasi.

Huu utaratibu ulikuwepo zamani na uliondolewa kutokana na urasimu wake na uchelewashaji mkubwa wa kukaguliwa mali ya mteja.

Tukubali tusikubali palipo na urasimu na ucheleweshaji hapo tunakaribisha rushwa tu.

Gari lililokaguliwa Japan (na tunawafahamu wa Japan JAAI kwa umakini na weledi), halafu likaguliwe tena na TBS, mantiki ya uamuzi huo hauingii akilini.

TBS ni shirika la Umma, na tunaujua utendaji wake.

Kutoa vibali tu vya ukaguzi wa bidhaa za viwandani inachukua hadi miezi sita.

Kwa hili TBS, NO!
Hao JAAI wanakagua bure?
 
Yaa, uko sahihi huu uamuzi naona umesukumwa na lengo la kukusanya mapato. Gari linatakiwa likaguliwe huko huko kabla halijasafirishwa kuletwa nchini. Let say hao TBS wamekagua gari na kuona halifai, nani atawajibika kulisafirisha kulirudisha huko lilikonunuliwa au kuliteketeza.

Halafu kama sijasikia vibaya ada ya ukaguzi inafika mil. 3, hii haiwezi kuwa sawa kwa mtu ambaye ameshatumia pesa nyingi kulipia thamani ya gari na kulisafirisha jumlisha kodi ambazo ni maradufu ya bei ya gari.
Mitano tena
 
Bado sioni kama maslahi ya wananchi yamezingatiwa kwa kufanya ukaguzi wa magari baada ya kuwa yameingia nchini, bali kinachoonekana ni kuzidi kuweka ugumu wa maisha kwa wananchi hasa wanyonge. Namsihi Rais JPM aingilie kati jambo hili hata kabla halijaanza kutekelezwa.
 
Magari used hayato kosa kasoro
Mjitahidi sasa wabongo kununua magari brand new.....
Kama miaka ya nyuma

Ova
 
Serikali ya wanyonge hiyo twende kazi!
Saivi ni kwenda Rwanda tu kununua VW yaishe wana assemble apo Kigali
 
Mambo yamekuwa magumu sana

Bila kutoa kitu kidogo au connections basi salama yako itakuwa gari itakaguliwa hata miezi miwili na utaipata upande mwengine gari itakaa muda mrefu au mfupi na utaambiwa ni bovu ulipie gharama wanayotala wakurekebishie.

Na kadri mchezo utavyonoga basi hata gari likiwa zima halina tatizo utaambiwa tu ni bovu na utatoa hela ya matengenezo .

Mbaya zaidi mtu anaweza kuchomia spea ya gari yako ambayo haina tatizo lolote akaiweka kwenye gari yake au ndugu yake akakuwekea spea kuu kuu na bado ukalazimika kutengeneza gari kwa gharama kubwa

Usalama wa spea za magari yetu na spea utakuwa mdogo sana, hebu vuta picha mkaguzi au fundi anatesti gari yako akiigongesha je?, na huko gereji itapokuwa inalala kuna baadhi ya mafundi wezi hawa ulinzi wa spea zetu upoje?

Na usiombee uwe na adui hapo tbs, huchomoki, utapigwa hela ya matengenezo hadi akili ikae sawa.

Kwa hili linalotaka kufanyika kiukweli mnakatisha watu tamaa kuagiza magari kutoka nje, Yani sipendi gari nayoagiza kufunguliwa kwajili ya ukaguzi na wabongo maana tunajuana vizuri, Kwa hali hii ukiagiza gari tenga hela ya matengenezo kabisa lasivyo utaumizwa sana na gharama za kutunza gari gereji na hatimae kulitelekeza.

Tbs kwa hili mmekurupuka.
 
Huu uamuzi uangaliwe upya
TZ kuna mambo tunaenda mbele kuna mambo tunarudishana nyuma wakati huo huo
 
Laki 3 siyo m3!
Yaa, uko sahihi huu uamuzi naona umesukumwa na lengo la kukusanya mapato. Gari linatakiwa likaguliwe huko huko kabla halijasafirishwa kuletwa nchini. Let say hao TBS wamekagua gari na kuona halifai, nani atawajibika kulisafirisha kulirudisha huko lilikonunuliwa au kuliteketeza.

Halafu kama sijasikia vibaya ada ya ukaguzi inafika mil. 3, hii haiwezi kuwa sawa kwa mtu ambaye ameshatumia pesa nyingi kulipia thamani ya gari na kulisafirisha jumlisha kodi ambazo ni maradufu ya bei ya gari.
 
Mambo yamekuwa magumu sana

Bila kutoa kitu kidogo au connections basi salama yako itakuwa gari itakaguliwa hata miezi miwili na utaipata upande mwengine gari itakaa muda mrefu au mfupi na utaambiwa ni bovu ulipie gharama wanayotala wakurekebishie.

Na kadri mchezo utavyonoga basi hata gari likiwa zima halina tatizo utaambiwa tu ni bovu na utatoa hela ya matengenezo .

Mbaya zaidi mtu anaweza kuchomia spea ya gari yako ambayo haina tatizo lolote akaiweka kwenye gari yake au ndugu yake akakuwekea spea kuu kuu na bado ukalazimika kutengeneza gari kwa gharama kubwa

Usalama wa spea za magari yetu na spea utakuwa mdogo sana, hebu vuta picha mkaguzi au fundi anatesti gari yako akiigongesha je?, na huko gereji itapokuwa inalala kuna baadhi ya mafundi wezi hawa ulinzi wa spea zetu upoje?

Na usiombee uwe na adui hapo tbs, huchomoki, utapigwa hela ya matengenezo hadi akili ikae sawa.

Kwa hili linalotaka kufanyika kiukweli mnakatisha watu tamaa kuagiza magari kutoka nje, Yani sipendi gari nayoagiza kufunguliwa kwajili ya ukaguzi na wabongo maana tunajuana vizuri, Kwa hali hii ukiagiza gari tenga hela ya matengenezo kabisa lasivyo utaumizwa sana na gharama za kutunza gari gereji na hatimae kulitelekeza.

Tbs kwa hili mmekurupuka.
Kwani kuna tatizo gani kuhuisha huo mkataba mpaka kufikia maamuzi ghafi haya!? I hope hawataweka mafundi wezi wa vipuli vya magari, watuibie afu ionekane gari haikidhi viwango...maana uzoefu wangu unaonyesha vipuli vingi vya magari hunyofolewa bandarini na baadae kuuzwa kwa mhusika mwenye gari kwa bei ya kukomoa! Sasa hii hali ya kuwaruhusu waanze kukaa na magari ya watu na kuyakorokochoa mbona naona ni majanga kwa waahiza magari zaidi hata ya kule ukerewe afya!?
 
Back
Top Bottom