Mazingira ya rushwa uhamisho wa watumishi wa Umma

Kahindi95

Member
Mar 7, 2019
31
95
Habari za mchana wana jukwaa!

Nalipanda jukwaa hili na kero yangu kuu juu ya utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa umma!

Watumishi wa umma hasa kada ya elimu na afya tumekuwa wahanga wa migumo mibovu ya uhamisho! Mfano kada ya elimu.

Maafisa elimu na wakurugenzi wamekuwa miungu watu, mwalimu unafanya michakato yote tena uhamisho wa kubadirishana, afisa elimu anakataa kusaini barua. Mwalimu utahangaika huku na kule mpaka anasaini kwa shinikizo!

Hata baada ya barua hizi kutoka halmashauri na kwenda TAMISEMI bado nako kuna delays kupita kiasi! Wao wenyewe walitoa maelekezo ya kutoa vibali kila robo ya mwaka, lakini utekelezaji wake umekuwa tofauti sana jambo linaloendelea kutengeneza maumivu makali mioyoni mwetu watumishi! Ikumbukwe mpaka barua zinafika TAMISEMI huku chini mtumishi anakuwa kaumia sana kuzipitisha kwenye mamlaka za halmashauri zetu, kwanini nanyi TAMISEMI mnaendelea kucheza na tune zilezile? Mnakaaje na barua za mtumishi miezi sita bila kumtumia kibali chake aondoke jamaniiii?

Kazi kama ualimu ni kazi inayohitaji kujitolea sana, mnategemea mtu anyeishi na manung'uniko ataweza kufanya kazi kweli?

Mazingira haya ya ucheleweshwaji na sometimes upuuzwaji wa kutoa vibali kwa wakati yamechochea sana mianya ya RUSHWA watumishi wanarubuniwa kutoa rushwa ili wahame haraka kutokana na mchakato legal kuchukua mda mrefu sana na sometimes kupuuziwa na mamlaka (yaani barua zako zinaweza kufika TAMISEMI na usipate kibali cha kuhama) inalazimu watu kutumia njia zisizo halali (rushwa) kuhama.

Kama katibu mkuu TAMISEMI hayuko tayari kutoa vibali kwa njia halali kwa wakati kama walivyoahidi, ni vyema kuutangazia umma tujue! Familia zinaumia, watumishi tunapata msongo wa mawazo! Wanaotoa rushwa wanahama chap kwa haraka, tusio na connection tunaishia kutapeliwa. Yote hii ni kwasababu yenu TAMISEMI.

Huduma kwa wateja TAMISEMI (255 2621 60210) pia hawatusaidii chochote kujua progress ya mchakato.

Kwanini huduma muhimu kwa mtumishi wa umma kama uhamisho mnaiwekea mazingira ya rushwa?

Ni kweli nchi hii hata kuhama tu kituo cha kazi unahitaji connection (RUSHWA)?

Wanyonge tutaishije sasa?

Furaha yenu nikuona ndoa zetu zinasambaratika?

Furaha yenu nikuona familia zetu(wazazi, walezi,wategemezi wetu) zinateketea?

Mnafaidika na nini?

Kwa mambo kama haya mwalimu anakuwa na amani shuleni?

Naomba sana timizeni ahadi zenu mnazotuahidi, toeni vibali kila robo mhula kama mlivyoahidi, naamini itaongeza amani na ari ya utendaji kazi.

Kumbukeni asilimia kubwa ya watoto wa masikini huishia kuwa waalimu, pamoja na changamoto nyingi tulizonazo kwenye kada yetu, viongozi wetu mtutendee yaliyo mema ili tuwe na ari ya kufanya kazi.

Wakuu wa shule, maafisa elimu, wakurugenzi, katibu mkuu TAMISEMI mjitahidi kutatua changamoto hii kwa uharaka unaohitajika. Mnatuumiza vibaya sana hamjui tu!

Waalimu tunatapeliwa sana na vishoka wa hapo TAMISEMI kwasababu yenu!

NAOMBA KAMA MNAHITAJI PESA KUTOA VIBARI BASI ITOLEWE CONTROL NAMBA AMBAYO MWALIMU UKILIPA UNAKUWA NA UHAKIKA WA KUHAMA KWA WAKATI.
 
Nikuombe kitu kaka, hiyo kazi achana nayo Mungu atakusaidia mbele ya safari halafu wewe wasamehe Kwa moyo mweupe

Nilikuwa na kaka angu mmoja alikuwa anafundisha shule ya sekondari BAHI alihangaika sana na uhamisho arudi kwao songea lakini alipoona dalili hakuna akamwambia mkurugenzi mm hii kazi ya ualimu naona nikuachie tu sio mbaya kuliko kunitenganisha na Familia yangu, Familia ni bora zaidi kuliko hii kazi

Saiz ana maduka kumi ya hardware na supermarket saba songea mjini
 
Nikuombe kitu kaka, hiyo kazi achana nayo Mungu atakusaidia mbele ya safari

Nilikuwa na kaka angu mmoja alikuwa anafundisha shule ya sekondari BAHI alihangaika sana na uhamisho arudi kwao songea lakini alipoona dalili hakuna akamwambia mkurugenzi mm hii kazi ya ualimu naona nikuachie tu sio mbaya kuliko kunitenganisha na Familia yangu, Familia ni bora zaidi kuliko hii kazi

Saiz ana maduka kumi ya hardware na supermarket saba songea mjini
Et supermarket 7 songea hahahaha
 
Et supermarket 7 songea hahahaha
Kataa sio lazima, shida yenu mnaona kazi ya ualimu ni alpha na omega lakini kila siku mnanuka madeni mpaka kwenye mavuzi , hapo kinachokuchekesha nini sasa kwamba haiwezekani au?? Ebu nitajie hata mwalimu mmoja tu mwenye supermarket ya kueleweka hapa bongo mm kesho nitakuwa shoga
 
Dawa ni moja tu, kuwashitaki kwa mungu ili wale viboko vya mungu. Sema hivi na muumba wako:

Eeh Mungu muumba wa mbingu na ardhi nihukumie wanadamu wako wanaojifanya kukuabudu lakini hawakuogopi wewe uliewaumba kila siku wanawatesa watu walio chini, wanakalia haki zao na kununua vipando na kufurahia maisha na familia zao eeh mungu shusha moto katika maisha yao ili nao waone machungu wanayopitia watu wa chini yao. Amen.
 
Habari za mchana wana jukwaa!
Nalipanda jukwaa hili na kero yangu kuu juu ya utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa umma!
Watumishi wa umma hasa kada ya elimu na afya tumekuwa wahanga wa migumo mibovu ya uhamisho! Mfano kada ya elimu.
Maafisa elimu na wakurugenzi wamekuwa miungu watu, mwalimu unafanya michakato yote tena uhamisho wa kubadirishana, afisa elimu anakataa kusaini barua. Mwalimu utahangaika huku na kule mpaka anasaini kwa shinikizo!

Hata baada ya barua hizi kutoka halmashauri na kwenda TAMISEMI bado nako kuna delays kupita kiasi! Wao wenyewe walitoa maelekezo ya kutoa vibali kila robo ya mwaka, lakini utekelezaji wake umekuwa tofauti sana jambo linaloendelea kutengeneza maumivu makali mioyoni mwetu watumishi! Ikumbukwe mpaka barua zinafika TAMISEMI huku chini mtumishi anakuwa kaumia sana kuzipitisha kwenye mamlaka za halmashauri zetu, kwanini nanyi TAMISEMI mnaendelea kucheza na tune zilezile? Mnakaaje na barua za mtumishi miezi sita bila kumtumia kibali chake aondoke jamaniiii?

Kazi kama ualimu ni kazi inayohitaji kujitolea sana, mnategemea mtu anyeishi na manung'uniko ataweza kufanya kazi kweli?

Mazingira haya ya ucheleweshwaji na sometimes upuuzwaji wa kutoa vibali kwa wakati yamechochea sana mianya ya RUSHWA watumishi wanarubuniwa kutoa rushwa ili wahame haraka kutokana na mchakato legal kuchukua mda mrefu sana na sometimes kupuuziwa na mamlaka( yaani barua zako zinaweza kufika TAMISEMI na usipate kibali cha kuhama) inalazimu watu kutumia njia zisizo halali (rushwa) kuhama.

Kama katibu mkuu TAMISEMI hayuko tayari kutoa vibali kwa njia halali kwa wakati kama walivyoahidi, ni vyema kuutangazia umma tujue! Familia zinaumia, watumishi tunapata msongo wa mawazo! Wanaotoa rushwa wanahama chap kwa haraka, tusio na connection tunaishia kutapeliwa. Yote hii ni kwasababu yenu TAMISEMI!.

Huduma kwa wateja TAMISEMI (255 2621 60210) pia hawatusaidii chochote kujua progress ya mchakato.

Kwanini huduma muhimu kwa mtumishi wa umma kama uhamisho mnaiwekea mazingira ya rushwa?
Ni kweli nchi hii hata kuhama tu kituo cha kazi unahitaji connection?
Wanyonge tutaishije sasa?
Furaha yenu nikuona ndoa zetu zinasambaratika?
Furaha yenu nikuona familia zetu zinateketea?
Mnafaidika na nini?

Naomba sana timizeni ahadi zenu mnatuahidi, toeni vibali kila robo mhula kama mlivyoahidi, naamini itaongeza amani na ari ya utendaji kazi.

Kumbukeni asilimia kubwa ya watoto wa masikini huishia kuwa waalimu, pamoja na changamoto nyingi tulizonazo kwenye kada yetu, tutendeeni wema ili tuwe na ari ya kufanya kazi.
Wakuu wa shule, maafisa elimu, wakurugenzi, katibu mkuu TAMISEMI mjitahidi kutatua changamoto hii kwa uharaka unaohitajika. Mnatuumiza vibaya sana hamjui tu!

Waalimu wanatapeliwa sana na vishoka wa hapo TAMISEMI kwasababu yenu!

NAOMBA KAMA MNAHITAJI PESA KUTOA VIBARI BASI ITOLEWE CONTROL NAMBA AMBAYO TUTALIPA ILI TUHAME KWA WAKATI.
Vile vile nenda kwa wataalamu pasua chungu kwa kunuia yote mabaya wanayokufanyia
 
Nenda kwa shehe soma kitu inaitwa Al badeer nenda kanisani ungama utaona Moto utakavyowaka kwa kila anaekunyanyasa
 
Back
Top Bottom