TBS mnaandaa mazingira ya rushwa ukaguzi wa magari?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
9,342
2,000
Tangazo la TBS lililotolewa majuzi, ati sasa ukaguzi wa magari used utafanyika hapahapa Bandarini linatia wasiwasi.

Huu utaratibu ulikuwepo zamani na uliondolewa kutokana na urasimu wake na uchelewashaji mkubwa wa kukaguliwa mali ya mteja.

Tukubali tusikubali palipo na urasimu na ucheleweshaji hapo tunakaribisha rushwa tu.

Gari lililokaguliwa Japan (na tunawafahamu wa Japan JAAI kwa umakini na weledi), halafu likaguliwe tena na TBS, mantiki ya uamuzi huo hauingii akilini.

TBS ni shirika la Umma, na tunaujua utendaji wake.

Kutoa vibali tu vya ukaguzi wa bidhaa za viwandani inachukua hadi miezi sita.

Kwa hili TBS, NO!

Pia soma>
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
6,318
2,000
Yaa, uko sahihi huu uamuzi naona umesukumwa na lengo la kukusanya mapato. Gari linatakiwa likaguliwe huko huko kabla halijasafirishwa kuletwa nchini. Let say hao TBS wamekagua gari na kuona halifai, nani atawajibika kulisafirisha kulirudisha huko lilikonunuliwa au kuliteketeza.

Halafu kama sijasikia vibaya ada ya ukaguzi inafika mil. 3, hii haiwezi kuwa sawa kwa mtu ambaye ameshatumia pesa nyingi kulipia thamani ya gari na kulisafirisha jumlisha kodi ambazo ni maradufu ya bei ya gari.
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,241
2,000
Matokeo ya kuishi in a shithole country ,hii ni kazi ya traffic maana bila ya kuwa na roadworthy certificate huwezi kusajili gari !mfumo wote nchini hapa ni wa kimizengwe tu kisheria ilitakiwa gari inayotoka nje ya nchi ije na roadworthy certificate yake na ikifika hapa mwenye gari apeleke kwenye roadworthy stations zetu ikafanyiwe Nyingine.

Na usajili wetu ungekuwa utegemeane na maeneo ilipo gari,mtu anayeishi Tanga aweze kusajili gari lake pale tanga na apewe number plate ya pale,tbs they got nothing to do na issue hii na ndio maana nchi imejaa vitu feki vingi.
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
12,898
2,000
Logic ya kukagua magari nje ilikua kuhakikisha magari yasiyo na viwango hayaruhusiwi kuja nchini. Yanabaki hukohuko. Sasa TBS imeamua yakaguliwe baada ya kufika bandarini.

Yani ukiagiza gari Japan hata kama ni "mkweche" una uhakika litafika Dar. Na baada ya kukaguliwa na kuonekana ni "mkweche" utaambiwa ukalipie kwenye karakana ya UDA litengenezwe.

UDA watakutengenezea kwa gharama wanazotaka. Umenunua $2,000 unaambiwa matengenezo ni TZS 5M, hapo bado TRA hawajakutandika kodi ya 7M. Kama huna hela za matengenezo unalidump gari lako na kuondoka. Kwa kifupi tumeamua kuwa dampo.

Kwanini magari yasikagukiwe hukohuko nje ili kupunguza mlundikano wa magari mabovu nchini? Kwanini tunalazimisha kukagua magari hapa nchini? Tuna wataalamu wa kutosha? Teknolojia ya kutosha? Vitendea kazi vya kutosha? Bandari ya Dar inaingiza karibu magari 5000 kila wiki. Je tutaweza kukagua yote kwa wakati?

Je tumeamua kukagua magari yote nchini ili kuongeza mapato? Kwa kuwa karakana zitakazotengeneza ni za serikali hivyo serikali itajiongezea mapato?

Kwa sasa ukiagiza gari dogo (Saloon, SUV au Hatchback) unalipia ukaguzi karibu $300. TBS wanagawana pesa hizo na ma-agent wanaowasaidia kukagua kwenye nchi magari hayo yanapotoka. Je kwa sasa TBS wanataka kuchukua "mzigo wote" wenyewe bila kugawana na ma-agent hao ili kuongeza mapato? Je tumeruhusu nchi iwe "dampo" for the expense ya kuongeza mapato?

Serikali inapaswa kujitafakari upya juu ya uamuzi huu. Ukaguzi uendelee kufanyika hukohuko magari yanapotoka. Ikionekana hayana viwango yabaki hukohuko.

Rafiki yangu aliwahi kulipia $5,500 Japan lakini baada ya ukaguzi gari ikaonekana ni chini ya kiwango. Akapewa option ya kuchagua gari jingine kwa pesa hiyohiyo. Akapata gari zuri. Lakini kwa utaratibu mpya wa TBS gari ingefika Dar ndo aambiwe ni chini ya kiwango. Halafu ipelekwe garage ya UDA apewe "invoice" ya kulipia mamilioni. Kama hawezi aitelekeze gari.

Ameandika Malisa GJ
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,148
2,000
Hili jambo linaweza kuwa ni zuri,lakini naona tangazo limetolewa ila halina ufafanuzi wa jinsi uafanisi wa hili jambo utakavyokuwa,mi nadhani mpaka wamefikia uamuzi huu sidhani kama watakuwa wamekurupuka ni lazima watakuwa wamejipanga,kwahiyo sioni pia kama kuna ubaya wakilitolea ufafanuzi ili kuwaondolea watu sintofahamu...
 
Kwa TBS hii tunayoifahamu?
Ni kutegemea maziwa kwenye bomba la DAWASA!
 
MESHACK WARIOBA

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
892
1,000
Hili jambo linaweza kuwa ni zuri,lakini naona tangazo limetolewa ila halina ufafanuzi wa jinsi uafanisi wa hili jambo utakavyokuwa,mi nadhani mpaka wamefikia uamuzi huu sidhani kama watakuwa wamekurupuka ni lazima watakuwa wamejipanga,kwahiyo sioni pia kama kuna ubaya wakilitolea ufafanuzi ili kuwaondolea watu sintofahamu...
Achana na Magari, Ulizia Shehena zingine ambazo huwa zinategemea Uhakiki wa TBS zinachukua Muda gani, Halafu ongezea na Magari takribani 5000+ ambayo yanaingia kwa wiki moja.
 
Assalafiyyu

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,816
2,000
Hivi hawa viongozi wa sasa huwa wanafikiri kwa kutumia kiungo gani...?

Mbona tunaofikiri kwa kutumia ubongo hii kitu hata haiingii akilini?
 
secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
4,753

Kweli kabisa.

biashara ya kununua magari nje itaathirika..

hakuna mtu atakuwa tayari kutoa mamilioni ya shilingi.

kwa gari ambalo hana hakika likifika tz atalipata kwa muda muafaka tena bila figisu.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
117,381
2,000
Logic ya kukagua magari nje ilikua kuhakikisha magari yasiyo na viwango hayaruhusiwi kuja nchini. Yanabaki hukohuko. Sasa TBS imeamua yakaguliwe baada ya kufika bandarini.

Yani ukiagiza gari Japan hata kama ni "mkweche" una uhakika litafika Dar. Na baada ya kukaguliwa na kuonekana ni "mkweche" utaambiwa ukalipie kwenye karakana ya UDA litengenezwe.

UDA watakutengenezea kwa gharama wanazotaka. Umenunua $2,000 unaambiwa matengenezo ni TZS 5M, hapo bado TRA hawajakutandika kodi ya 7M. Kama huna hela za matengenezo unalidump gari lako na kuondoka. Kwa kifupi tumeamua kuwa dampo.

Kwanini magari yasikagukiwe hukohuko nje ili kupunguza mlundikano wa magari mabovu nchini? Kwanini tunalazimisha kukagua magari hapa nchini? Tuna wataalamu wa kutosha? Teknolojia ya kutosha? Vitendea kazi vya kutosha? Bandari ya Dar inaingiza karibu magari 5000 kila wiki. Je tutaweza kukagua yote kwa wakati?

Je tumeamua kukagua magari yote nchini ili kuongeza mapato? Kwa kuwa karakana zitakazotengeneza ni za serikali hivyo serikali itajiongezea mapato?

Kwa sasa ukiagiza gari dogo (Saloon, SUV au Hatchback) unalipia ukaguzi karibu $300. TBS wanagawana pesa hizo na ma-agent wanaowasaidia kukagua kwenye nchi magari hayo yanapotoka. Je kwa sasa TBS wanataka kuchukua "mzigo wote" wenyewe bila kugawana na ma-agent hao ili kuongeza mapato? Je tumeruhusu nchi iwe "dampo" for the expense ya kuongeza mapato?

Serikali inapaswa kujitafakari upya juu ya uamuzi huu. Ukaguzi uendelee kufanyika hukohuko magari yanapotoka. Ikionekana hayana viwango yabaki hukohuko.

Rafiki yangu aliwahi kulipia $5,500 Japan lakini baada ya ukaguzi gari ikaonekana ni chini ya kiwango. Akapewa option ya kuchagua gari jingine kwa pesa hiyohiyo. Akapata gari zuri. Lakini kwa utaratibu mpya wa TBS gari ingefika Dar ndo aambiwe ni chini ya kiwango. Halafu ipelekwe garage ya UDA apewe "invoice" ya kulipia mamilioni. Kama hawezi aitelekeze gari.

Anyway, tuendelee kuchangia matibabu ya mtoto Aryan aende India kutibiwa. Kumbuka safari ni ijumaa na tayari ameshakata ticket.

Tuma mchango wako kwenda (MPESA) 0763223388, Glory Makuka (mama mzazi wa Aryan). Mungu akubariki sana.!

#RudishaTabasamu #LetLoveLead #MalisaGJ

1611237419001.jpeg
 
View attachment 1682672
Umeongea vizuri sana kwa logic..
viongozi wa serekali muwe na aibu....!!!
apply proper reasoning......
otherwise hata biashara ya magari itakuwa disrupted.....
mtakosa hata hiyo kodi kubwa mnayoipata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom