TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

mh kweli mwisho wa ubaya ni aibu je jeshi la police lipo tayari kwa aibu hii?
 
SAKATA LA MURO: KESI YA PANYA KAPEWA PAKA.
SAKATA la madai ya kuomba Rushwa ya shilingi Mil.10 linalomkabili mwandishi wa shirika la Habari la TBC, Jerry Muro linahitaji uchanganuzi wa Kina, na fikra yakinifu zitakazokidhi haja za watanzania wanaofuatilia swala hili, na kuondoa utata unaoonekana wazi.

Suala la Muro limejaa utata na halieleweki wazi si tu kwa wananchi wanafuatilia, bali hata yeye nadhani hajui kunachoendelea.

Utata huu unatokana na mambo makuu mawili. Kwanza ni mazingira ya kukamatwa kwa hicho kinachodaiwa “Rushwa” na pili ni wahusikakatika Kesi yake.

Mazingira ya Kesi tangu kukamatwa kwake hadi kufikishwa kituoni yanaibua maswali mengi kwa kila mwenye fikra hai. Murro alikamatwa Jumapili ya tarehe 31/01/2009 akiwa katika gari lake aina ya Cresta GX100 lenye namba za usajili T 545 BEH na kufikishwa katika kituo kikuu cha Polisi Mkoa wa Dar; kwa madai ya kuomba rushwa ya Sh. Million 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Bw. Michael Wage.

Bw. Wage anadai kwamba aliombwa rushwa hiyo na Muro siku mbili kabla ya kukamatwa, walipokutana na Muro katika Hotel moja jijini Dar. Hivyo Muro alipofikishwa kituoni hapo alitakiwa kutoa maelezo kuhusu tukio la siku mbili zilizopita.

Haingii akilini mtu kuomba rushwa leo halafu eti akamatwe siku mbili baadae; Lazima Umma uelezwe kwanini hakukamatwa siku hiyo hiyo alipoomba rushwa? Au labda makachero wote wa Polisi walikuwa wameenda likizo hivyo ilibidi kusubiri hadi siku mbili baadaye watakaporudi kutoka huko walikokuwa wameenda kula “good time”.

Lakini pia ni kwanini Bw. Wage hakuripoti Sakata hilo TAKUKURU ambao kisheria ndio wanaoshughulikia rushwa? Angeenda TAKUKURU angepewa noti zilizojizolea umaarufu kama “Pesa za moto” ambazo zingetumika kama ushahidi mzuri wa kumtia Murro hatiani. Je, Wage hafamu kuwa TAKUKURU ndio wenye dhamana ya madai yote yanayohusu rushwa? Kama anafahamu hilo, alienda Polisi kufanya nini?

Kwanini alikimbilia Polisi badala ya TAKUKURU? Huko polisi alikuwa anamfuata nani? Lazima swali hili lijibiwe kwa ufasaha na uyakinifu.

Lakini cha kuchekesha ni kwamba alikamatwa bila ushahidi wowote uliohusu Rushwa. Si “noti za moto” za TAKUKURU wala sarafu za Polisi alizokutwa nazo Murro.

Badala yake Polisi waliibua madai ya kukutwa na pingu ambayo hayana uhusiano wowote na kesi ya msingi ya Rushwa.

Lakini hili la pingu nalo linahitaji mjadala mpana. Mjadala huu ni kutokana na mazingira ya kukutwa kwa Pingu hizo. Gazeti la Nipashe la Jumatatu February 1/2010 liliripoti kuwa Murro alipofikishwa Kituoni hapo alipelekwa sehemu ya juu (Ghorofani) ya kituo kwa ajili ya mahojiano. Wakati Murro akiwa kwenye mahojiano gari lake lilikuwa likilindwa na askari kanzu.

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, siku hiyo alipoombwa rushwa Wage alidai kuona Pingu ndani ya gari la Muro. Hivyo Muro alipokamatwa gari yake ikalazimika kupekuliwa. Lakini funguo zikapotea katika mazingira yaliyojaa utata hapohapo kituoni. Hivyo Muro kulazimika kupiga simu nyumbani kuomba funguo za akiba.

Lakini kabla funguo za akiba hazijafika, zile zilizopotea zilipatikana na pingu hizo kukutwa ndani ya gari la Jerry; Je, nani alikuwa na funguo hizo?? Je, nikisema kwamba kuna askari alipoka fungua hizo na kwenda kuweka Pingu kwenye gari la Muro nitakuwa nimekosea?? Au nikisema wale makachero walioachwa kulinda gari wakati Muro akiwa kwenye mahojiano walitumia mbinu zao za “Kimafya” kutumbukiza Pingu katika gari la Muro nitakuwa navunja kifungu gani cha Sheria??

Lakini Wage, (mhasibu aliyesimamishwa kazi na waziri Mkuu kutokana na shutuma za ubadhirifu) akaibua hoja nyingine mufilisi. Eti alipokuwa kwenye gari ya Muro (wakati Muro akimuomba rushwa) alisahau miwani yake ambayo baada ya upekuzi ilikutwa kiti cha mbele wakati wa upekuzi.

Binafsi sidhani kama kukutwa kwa miwani kinahusika na sakata la msingi la Rushwa. Bali kwa kutumia ushahidi wa miwani kwa mbaaali kunaweza kutusadikisha (japo si sana) kuwa Wage alipanda gari ya Muro. Lakini je, kila anayepanda gari ya Muro anaombwa rushwa? Kama kila anayepanda gari ya Muro huombwa rushwa basi madai ya Wage yatakuwa na msingi; vinginevyo hizo ni fikra kurupushi tu.

Katika gari ya Muro kulikutwa vitu kadhaa, vikiwemo vifaa vyake vya kazi. Lakini pia ilikutwa miwani, boksi mbili za tissue na pingu za mkononi.
Viwili kati ya hivyo yaani miwani pamoja na tissue, Wge alidai ni mali zake na alizisahau aliposhuka. Kama amekiri kumiliki miwani na tissue na kwamba alivisahau aliposhuka, basi yawezekana hata hizo pingu yeye ndiye mmiliki wake na alizisahau tu, kama alivyosahau hivyo vingine. Kama aliweza kusahau miwani (anayoitumia kila siku), kwanini tushindwe kuamini kuwa hata hizo pigu alizisahau??.

Baada ya kuona namna MAZINGIRA ya Kesi yalivyojaa utata hebu tuangalie WAHUSIKA katika Kesi hii.

Michael Wage ambaye ndiye mlalamikaji mkuu katika Kesi hii ni “mhanga” katika “bomoabomoa” iliyofanywa na waziri mkuu mhe.Mizengo Pinda ambapo watendaji wa juu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo walisimamishwa kazi.

Lakini ikumbukwe kuwa hadi waziri mkuu kufikia hatua ya kuwasimamisha watendaji hao kazi inadaiwa Murro ndiye aliyefichua ufisadi uliokuwa umeighubika Halmashauri hiyo. Kwa tafsiri hiyo Muro ndiye “aliyewachomea utambi” watendaji hao, na kwa maana hiyo wana hasira nae. Hivyo nikisema Kesi hii ni ya kupikwa sidhani kama kimantiki itapingika.

Lakini hata jeshi la Polisi nao si marafiki sana wa Muro maana nao walishajeruhiwa na makucha yake.

Akiwa ITV Muro aliwahi kufichua rushwa iliyotolewa kwa trafiki katika maeneo ya barabara ya Dar – Moro. Habari hiyo ilirushwa na kituo cha televition cha ITV kupitia kipindi cha Ripoti maalum haikufurahiwa sana na Polisi maana Askari polisi 13 walisimamishwa kazi kwa tuhuma hizo za rushwa. Lakini pia hivi majuzi Murro alishiriki kuandaa kipindi cha Usiku wa Habari kilichorushwa na TBC -1 ambapo askari wa Usalama barabarani Mkoa wa Iringa walionekana wakipokea Rushwa.

Hili nalo liliongeza idadi ya maadui wa Muro na labda pia liliibua mbinu za namna ya kumzima. Ndio! Hatakiwi kuendelea kuumbua wakubwa kwa kile anachokiita “Habari za Uchunguzi”. Nani ana uhakika wa kupona kama akiachiwa aendelee kufichua? Yeah! Lazima azimwe maana fichua fichua yawezekana akafichua pasipofichulika.

Lakini jumatatu tarehe 1/February/2010 Kamanda wa Polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam; Selemani Kova aliongea na waandishi wa habari kuelezea tukio la kukamatwa kwa Muro. Pamoja na kuongea sana (kama kawaida yake) alinukuliwa na vyombo vya habari akisema “…..hapa namsaidia Wage kusema; maana haya alipaswa kuyasema yeye”.

Kauli hii inaibua utata kwa kila mwenye akili timamu. Wage ni nani hadi aajiri Jeshi la Polisi kumsemea? Kwa lipi hasa? Na kwa ujira wa shilingi ngapi?

Baadhi ya watu wenye fikra finyu walimsifu RPC Kova kutoa tamko bila kujua kuwa Kova alikuwa anajishtaki mwenyewe. Kwa kukiri kwamba anasema kwa niaba ya Wage; ina maana kuwa Wage ndiye aliyemtuma aseme. Swali. Tangu lini Kamanda Kova amefanyika kuwa Afisa habari/msemaji wa Wage??

Napotafakari kauli ya Kova (Kwamba alimsaidia Wage Kusema) naanza kupata majibu kwanini Wage hakwenda TAKUKURU na badala yake akakimbilia Polisi.

Kutokana na kauli hii uhusiano baina ya Kova na Michael Wage unapaswa uchunguzwe ili tujue msimamo wa RPC wetu. Ikiwezekana achague moja kama ataendelea kuwa RPC au ataacha kazi yake ya upolisi abakie na hiyo mpya ya kuwa Afisa habari wa Wage.

Kwa ujumla mlalamikaji katika Kesi hii Michael Wage pamoja na wanaoendesha kesi hii Jeshi la Polisi wamewahi kuwa “majeruhi” wa Muro kwa nyakati tofauti. Halafu eti leo ndio wanaongoza upande wa mashtaka katika Kesi ya yuleyule “mbaya wao”. Halafu tunategemea haki itendeke. Thubutu!! Hicho ni kichekesho. Tusishangae kuona Muro akipokwa HAKI yake waziwazi maana Kesi ya Panya kapelekewa Paka. Ni uzandiki.

Niachie ujumbe:
0715-187677



Bravo Malisa!!!
 
KOVA...aibu....aibu.... aibu .....aibu.... aibu ...aibu.... aibu- Chini ya kiwango...mngesubiri....aaah....*****shit Leta Bunduki ******* shit.....

Nani ana chungulia? sh**** wote turudi nyuma tuwaangalie wanacho fanya...
 
Mh mode
natumaini huu mzima wa afya
tunaomba msaada tuunganishie story za jerry muro
kwa uwepo wangu nimeona kama threads 7 za jerry na uchunguzi aujakamilika mpaka ukikamilika kila sehemu ni jerrymuro ....
tutashukuru kwa msaada wako
 
risiti hutengenezwa mtaani tu....tusubiri zithibitishwe then tuanze kuhoji
 
Bunge la jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar limeambiwa leo hii na waziri mkuu wake mh pinda
swala la jerry muro wameomba watashugulikia kwa umakini zaii na haraka zaidi huku riport ikiwa wazi kwa kila mtanzania...

Kazi kubwa hongera jerry hata ukifa leo umeingia kwenye
kumbukumbu ya hoja za bunge kukujadili;ilikuwa patashika walipoanza kumjadili....
Kila la kheri haki itaonekana br kuwa mpole
 
Bunge la jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar limeambiwa leo hii na waziri mkuu wake mh pinda
swala la jerry muro wameomba watashugulikia kwa umakini zaii na haraka zaidi huku riport ikiwa wazi kwa kila mtanzania...

Kazi kubwa hongera jerry hata ukifa leo umeingia kwenye
kumbukumbu ya hoja za bunge kukujadili;ilikuwa patashika walipoanza kumjadili....
Kila la kheri haki itaonekana br kuwa mpole

Hiyo Jamhuri iko maeneo gani?
 
Mh, sasa naona kama hii movie inatumika ku-diverte attention ya mambo mengine mazito yanayowashinda kama msukumo wa chama, miswada nk
 
mh kweli mwisho wa ubaya ni aibu je jeshi la police lipo tayari kwa aibu hii?

......Au jery Muro. Kama kumiliki Pingu kwa uhalali sawa Hakuna kesi, lakini hizi stori nyingine zinachanganya,Aidha ni mwenzao? au si mwenzao!, Na kama si mwenzao yuko upande gani? na wenzake ni kina nani? Na hizo pingu? na hiyo Bastola? Kuna nini Hapoooooooooooooooo?
 
mh mradi mwingine huo hapo lazima tume iundwe fasta watu wale pesa jamani tanzania rahaa
 
Nashindwa kuelewa uchunguzi ni wa rushwa,kumiliki pingu au kutaka rushwa ambayo kwa haraka ya polisi wetu hakuwahi hata kukutana na mtoaji,big up Jerry
 
Jerry akitoka blanc kama la neige atakuwa akaula,ila ila akitoka mchafu itakuwa kazi kweli kweli maana yeye ndo alikuwa anawafichua baadhi ya walarushwa polisi
 
hili Sakata kwa sasa lipo lipo tu ..Bunge ,Police ,Takukuru hata halieleweki
 
Nipashe imefanikiwa pia kuona risiti aliyopewa Muro kama ushahidi wa ununuzi wa pingu hiyo, ikiwa na namba 34357310. Stakabadhi hiyo ni mali ya serikali pia.
Risiti hiyo iliyotolewa Mei 20, mwaka 2008, inaonyesha kuwa Muro alinunua pingu kwa Sh, 25,000. Muro ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, Jumapili iliyopita alikutwa na pingu katika gari alilokuwa akilitumia mara baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kutaka fedha kwa njia ya vitisho kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.


kesi bado inautata kutokana na haya.
-.kova inaonesha hajui sheria za nchi kutokana na kwamba duka linalo uza pingu lipo nchini na mtu unaweza kununua na sio kama kova alivyosema raia haruhusiwi kuwa na pingu na hamna duka linalo uza pingu.


-kwa upande wa jerry muro kama nilivyonukuu alisema kwamba anamiliki bastola na pingu kwa kipindi cha miaka minne sasa.kama nilimnukuu hivyo na wenzangu mnaweza kunisaidia labda nilimsikia vibaya,kwanini risiti inaonesha may 20 2008 wakati yeye alikuwa anamiliki pingu kwa miaka minne? 2008 mpaka leo miaka minne bado hijafika.


kidogo hapo imenichanganya kwahio wakuu walioelewa zaidi yangu nitafurahi kufahamishwa zaidi la sivyo kuna mengi zaidi yana kuja kwenye kesi hii.
 
Back
Top Bottom