TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Inawezekana ni uvivu wangu wa kusoma pages za nyuma- aksante kwa kunitoa tongo tongo machoni.

So kama ni fisadi so na y anayo kesi ya kujibu- si ndio?

Kifupi huyo Michael Wage, alikuwa Mhasibu wa halmashauri ya Bagamoyo kabla ya kutimuliwa na Pinda mwanzoni mwa mwaka huu kwa tuhumu za ubadhilifu wa fedha za halmashauri.

Huyu jamaa, mjini Morogoro anamiliki lodges na mahotel (zinaitwa GWAMI) ambayo idadi yake wengi hatufahamu, pia anafanya finishing ya jengo la ghorofa sita pale maeneo ya Msavu, just adjust to kituo kikuu cha mabasi ya mikoani.....!

Inawezekana mali hizo kazipata toka kwa ndugu zake au alicheza kamari, lakini serikili ilitakiwa ijiridhishe na vyanzo vya mali zake baada ya kumtimua....sasa wao wanaconcentrate kny Jerry vs Kovu sagga.... tuuuuuuuu! cheap cheap cheap things........! MM is right!
 
Jamani hili jambo sio jepesi kama tunavyolijadili.Hoja ya Hamad ni kuwa waandishi wa Tanzania wakifichua maovu huwa wanafuatiliwa sana,tumeiona kwa Kubenea na Ndimara na wengine wengi huko nyuma na sasa ni kwa Muro.Na kwa jinsi hii nchi ambavyo haina haki na hasa kwenye vyombo vya dola ndio maana imeonekana ni bora kumkaba Waziri Mkuu ingawaje naye amejibu kisanii as always.Tusiposimama kidete kutetea waandishi wetu tutpataje kufahamu mabaya yanayoendelea hapa nchini?where is the freedom of press?

........... Gender Sensitiv hapa hatutetei ila tunajiuliza wanadiscuss nini wakati kesi yenyewe bado iko jikoni? Watasema Jerry anaonewa kwa kuwa anafichua maovu, what if baadaye ikigundulika ana hatia? Wangesubiri kwanza hatma ya kesi na ikigundulika kuwa kahujumiwa basi wana haki ya kulisema na kukemea police.
 
Wengi tunaliona Bunge letu kama sehemu ya maongezi, mipasho, majigambo,....Lakini hali ni hiyohiyo maofisini, kwenye vikao vya vyama vyetu vya siasa, polisi nao sasa hivi wanashindia kwenye TV, hapa JF ni mipasho tu, kuwalaumu Wabunge wetu ni kuwaonea tu.
Nchi imegeuka ya majungu, kusengenyana, kutapeliana, kuongopeana,....bora kunakucha!
 
headline_bullet.jpg
Aliinunua Shirika la Mzinga mwaka 2008
headline_bullet.jpg
Kama raia akitaka anaruhusiwa kuinunua
headline_bullet.jpg
Yabainika bei yake ni poa tu, ni Sh. 25,000



Pingu.jpg

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akionyesha pingu anazomiliki mwandishi wa habari za uchunguzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro.



Kadhia anayoendesha kwa mbwembwe Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuhusu mwandishi wa habari za uchunguzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro, imezidi kumweka pagumu baada ya risiti ya pingu anayotuhumiwa nayo mwandishi huyo kupatikana.
Hali hiyo inajitokeza baada ya kile alichoapa Kova kwamba hakuna raia anayeweza kumiliki pingu, na kwamba alikuwa na hakika kwamba Muro asingeweza kupeleka risiti hiyo.
Juzi akiendelea na juhudi zake za kuwakamata watuhumiwa na kuwahukumu huku akisema wengine ni “matapeli sugu”, Kova alisema kwamba Muro aliyekamatwa Jumapili iliyopita na kuachiwa kwa dhamana, alikuwa hajawasilisha risiti hiyo.
Uchunguzi wa Nipashe umebaini kwamba Muro alinunua pingu hiyo kihalali kutoka duka la kuuza silaha la Shirika la Mzinga. Shirika hili ni mali ya serikali.
Nipashe imefanikiwa pia kuona risiti aliyopewa Muro kama ushahidi wa ununuzi wa pingu hiyo, ikiwa na namba 34357310. Stakabadhi hiyo ni mali ya serikali pia.
Risiti hiyo iliyotolewa Mei 20, mwaka 2008, inaonyesha kuwa Muro alinunua pingu kwa Sh, 25,000. Muro ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, Jumapili iliyopita alikutwa na pingu katika gari alilokuwa akilitumia mara baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kutaka fedha kwa njia ya vitisho kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.
Wage pamoja na maofisa wa juu wa Halmashauri hiyo mwezi uliopita walifutwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa tuhuma za ufisadi wa kutisha. Bado wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Miongoni mwa rushwa ambazo Muro alizifichua ni zile zilizohusu askari wa usalama barabarani kupokea rushwa.
Kwa mara ya kwanza Muro alifanya kipindi maalum akiwa mfanyakazi wa ITV na kuwanasa askari hao katika barabara kuu ya Morogoro, kati ya Dar es Salaam na Morogoro.
Mara ya pili alifanya kipindi cha usiku wa habari katika barabara kuu mkoani Iringa na kilionyeshwa na TBC1 anakofanya kazi Muro kwa sasa.
Mwaka jana Muro alishinda tuzo ya mwandishi bora wa mwaka na kipindi cha ITV ambacho kilisababisha askari kadhaa walioonekana wakipokea rushwa kufukuzwa, ndicho kilimpandisha ngazi.
Kadhalika kipindi cha TBC1 nacho kimepeleka kilio kwa askari waliomulikwa, na sasa wanachunguzwa kabla ya kufukuzwa kazi kwa kula rushwa.
Kamanda Kova tangu kuibuka kwa kadhia ya Muro ambayo imeacha maswali mengi kutokana na kuendeshwa mno kwa mizengwe, amekuwa akikanyaga sheria ambazo kama kiongozi wa juu wa Jeshi la Polisi anapaswa kuzisimamia.
Kwa mfano Jumatatu Kova alionyesha hadharani bastola anayomiliki Muro kama ambavyo polisi wengi wamekuwa wakionyesha silaha walizokamata kwa watu wanatuhumiwa kwa ujambazi.
Ingawa Kova alikiri kwamba Muro alikuwa anamiliki bastola hiyo kihalali, hakueleza umma ilikuwa na umuhimu gani basi kiutaalam na kiusalama kutoa taarifa za kina za silaha ya raia, ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kubeba risasi na ilikotengenezwa.
Kadhalika, Kova alionekana akijenga hoja kwamba pingu aliyokuwa anamiliki Muro ilikuwa inatiliwa shaka na kukiwa hakuna sheria yoyote Tanzania inayomzuia mtu kumiliki pingu, kifaa hicho si silaha wala hakina ukiritimba wowote wa kukimiliki.
Kova pia anadaiwa kuvunja sheria ya Takukuru ya mwaka 2007 kwa kuwataja watu waliotoa taarifa za rushwa, hivyo kuweka suala zima katika mtihani mkubwa wa kisheria.
Kifungu cha 51(1) (a) cha sheria hiyo, kinazuia kutajwa kwa jina, makazi na anuani ya mtu aliyetoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa au aliyesaidia mamlaka inayohusika kufanikisha kukamatwa kwa mhusika.
Juzi Kova aliwaanika watu wengine wawili aliodai kuwa ni washirika wa Muro katika kutenda uhalifu, na aliwatangaza kwamba ni “mapateli sugu wasiostahili kupewa dhamana”. Kova aligeuka kuwa Polisi na Hakimu wa kuhukumu papo hapo.
Kadhia ya Muro imekuwa ikibadili mwelekeo kila uchao, awali polisi walikuwa wanamtuhumu kwamba alidai rushwa ya Sh. milioni 10, lakini wameshindwa kueleza ni kwa nini hawakuweka mtego ili kumshikisha na pia ni kwa nini suala hilo halikupelekwa Takukuru ambao kisheria ndio mahali hasa pa kushughulikia makosa ya rushwa.
Jana nipashe iliwasiliana na uongozi wa Shirika la Mzinga ambalo linauza pingu hapa nchini, na ulisema upo tayari kumuuzia hata mwandishi kama anazo fedha.
"Wewe kama una hela njoo tutakuuzia pingu, haina shida tatizo lipo katika silaha," alisema Mary Peter, mfanyakazi wa shirika hilo alipoulizwa na Nipashe, jana jioni.
Mary alipoulizwa kama anakumbuka Muro aliwahi kununua pingu kwao, alijibu kwa kifupi kuwa yeye sio msemaji wa shirika hilo.

KATUNI(111).jpg


CHANZO: NIPASHE
 
Sasa hivi kwenye kipindi cha maswali na majibu ya kawaida wanajadili mechi za Simba na Yanga!
 
Lile sakata la Jerry Muro, limetinga rasmi bungeni asubuhi hii kwenye kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo.

Sakata hilo limeshushwa bungeni na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (Pemba), alimuuliza Waziri Mkuu, katika nchi nyingi, waandishi wa habari wanaokuwa mstari wa mbele kufichuo vitendo viovu dhidi ya dola, dola huwa inawashukia, kama polisi wanavyomshukia Jerry Muro, baada ya kufichua rushwa yaTraffic?

Pinda alijibu, Jerry Muro ni binadamu kama binadamu wengine, hivyo anaweza kufanya makosa, na polisi nao vile vile ni binadamu, hivyo alisema anasikitika jinsi suala hili linavyoshupaliwa kwa kutumia vyombo vya habari, amesema polisi wanatumia vibaya vyombo vya habari, na Jerry nae anatumia vyombo vya habari kuendeleza malumbano.

Pinda amesema anashauri polisi kutimiza wajibu wake kwa kutumia zile zile standard procedures sio kutumia media.Rashid Mohamad akauliza swali la nyongeza, kwa kumtaka Pinda kuingilia mchakato ili kuharakisha na haki, itendeke. Pinda akajibu, hana sababu ya kuingilia uchunguzi wa kipolisi, japo kuna public interest lakini hebu kwanza viachiwe vyombo husika.
Kamanda Kova ni kawaida yake kutumia vyombo vya habari toka yupo Mbeya.Na ndivyo vimempandisha chati na kuchangia kwa asilimia kubwa hayo mafanikio yake mpka hapo alipo.
 
kuumbuka kwa kamanda Kova hakupo mbali, kweli haiitaji unajimu kuliona hilo.
 
Taarifa za CCTV za Jerry Muro Kamanda Kova vipi au bado wanatengeneza wataalam wake mwenye taarifa tunaomba atueleze wamefikia wapi...................
 
Muro muro muro
muro muro muro
muro muro muro
muro muro muro
 
Kifupi huyo Michael Wage, alikuwa Mhasibu wa halmashauri ya Bagamoyo kabla ya kutimuliwa na Pinda mwanzoni mwa mwaka huu kwa tuhumu za ubadhilifu wa fedha za halmashauri.

Huyu jamaa, mjini Morogoro anamiliki lodges na mahotel (zinaitwa GWAMI) ambayo idadi yake wengi hatufahamu, pia anafanya finishing ya jengo la ghorofa sita pale maeneo ya Msavu, just adjust to kituo kikuu cha mabasi ya mikoani.....!

Inawezekana mali hizo kazipata toka kwa ndugu zake au alicheza kamari, lakini serikili ilitakiwa ijiridhishe na vyanzo vya mali zake baada ya kumtimua....sasa wao wanaconcentrate kny Jerry vs Kovu sagga.... tuuuuuuuu! cheap cheap cheap things........! MM is right!

Ni kweli Next Level kwa sababu wanadai mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana makosa . Ingawaje mtoa rushwa hapa alitoa taarifa mapema kwa police (na siyo TAKUKURU) haimuondoi kwenye hatia ya kutaka kutoa rushwa kwa kuwa sababu za yeye kutaka kutoa hiyo rushwa hazieleweki. Afadhali ingekuwa kwamba kuna service ambaye Bwana Jerry alitakiwa kumpa Wage (Service ambayo ni haki yake Wage) na akaambiwa huipati hadi utoe rushwa, yaani hiyo favor hataipata hadi atoe rushwa) na Bw. Wage kwa kujua kuwa service hiyo ni haki yake kwa nini ailipie ndo akaendatoa taarifa.

But kwa jinsi hadithi ilivyo hakuna favour hiyo iliyowekwa bayana. Wanadai kuwa Bw. Wage alitaka Jerry asimtoe hadharani kama fisadi (meaning kuwa may be Jerry alikuwa na information kuwa huyu Bw. ni fisadi na anavyo vielelezo) Na hii information anayo Jerry Muro peke yake kama mwandishi wa habari otherwise angehonga waandishi wote walio na vielelezo hivyo.

So hata kama aliombwa rushwa alitakiwa aeleze kwa ufasaha ilikuwa rushwa ya nini na why alikubali kuitoa kama hakuwa na hatia.

Bora wangemchomekea ya ujambazi pengine wangetuokota.
 
Wengi tunaliona Bunge letu kama sehemu ya maongezi, mipasho, majigambo,....Lakini hali ni hiyohiyo maofisini, kwenye vikao vya vyama vyetu vya siasa, polisi nao sasa hivi wanashindia kwenye TV, hapa JF ni mipasho tu, kuwalaumu Wabunge wetu ni kuwaonea tu.
Nchi imegeuka ya majungu, kusengenyana, kutapeliana, kuongopeana,....bora kunakucha!

Nakubaliana na wewe katika suala la kupenda cheap cheap...umbea ni cheap sana!

Lakini sikubaliani na wewe kabisa unaposema tusiwalaumu wa bunge kwa kufanya mipasho bungeni. Mipasho watuachie sisi wa vijiweni, wao wamepewa dhamana na wananchi kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake. Hawa wanalipwa mishahara na marupurupu kibao kwa kazi hiyo kutokana na kodi zetu mzee! Nalipa kodi kny gari, vyakula, vinywaji, PAYE, wtax, importation taxes.....sehemu ya kodi hizo wanalipwa hawa jamaa! kodi zetu hazilipwi ili wafanye mambo ya mipasho bungeni mkuu.....!

Mi nikifanya mipasho silipwi kodi yako, ila tu naweza pewa penalty ya kutoperfom vizuri kwa mkoloni wangu......!

Wabunge lazima wawe serious kwenye issues zenye maslahi kwa taifa sio mipasho unayoisupport......!
 
Kamanda Kova ni kawaida yake kutumia vyombo vya habari toka yupo Mbeya.Na ndivyo vimempandisha chati na kuchangia kwa asilimia kubwa hayo mafanikio yake mpka hapo alipo.
Sio yeye tu. Hata EL alikuwa hivo, Mzee Makamba, JK mwenyewe anakwenda kuhani misiba, kuona wagonjwa kwa TV, Mzee Mengi na ITV yake ndio hivo, Magufuli ndio hafanyi kitu bila kamera kummulika,......Hii sasa ndio fashion na sehemu muhimu ya utendaji kazi.
 
Nawashukuru sana Polisi kwa walichomtendea huyu dogo Jerry Muro

a) Wamemwongezea sana umaarufu wa kuwa mwanahabari shujaa
b) Wamesaidia kumweka mdogo wangu katika orodha ya akina Ken Sarowiwa, Katabaro na Rutayasingwa

b) they have made Jerry a much more popular investigative journalist in east africa

thank you very much our police force
 
Nimejiuliza sana, nikaona sio vby kuja kuomba msaada hapa;

Hivi nini kifanyike ili mapoloce wetu wafanye kazi kwa standadi na maadili ya jeshi??
 
Nimejiuliza sana, nikaona sio vby kuja kuomba msaada hapa;

Hivi nini kifanyike ili mapoloce wetu wafanye kazi kwa standadi na maadili ya jeshi??

Tuandamane- hii ni issue pana si suala la police peke yake. Katika nchi yoyote ambapo police inakuwa na 'mahusiano' ya karibu na wakuu na viongozi wengine inakuwa ngumu kuirekebisha. Inapofikia police wa barabarani anapangwa barabara flani kwa miadi ya kupeleka kiasi kadhaa mwisho wa siku kwa Bosi wake- hapa atakamata wahalifu na kuchukua rushwa kwa nguvu zote kwani anatakiwa apeleke akiba kwa bosi il kesho tena apangwe.

police wanapofikia hatua ya kushirikiana na wakuu katika kulinda ufisadi kwa nguvu za dola e.t.c. Kitakachotuokoa ni kubadili system nzima na si kutarget police mmoja mmoja
 
Bastola na pingu vyote vinamilikiwa kihalali. Limebaki lile la rushwa sasa ambalo Kova ameshalikoroga hata kulipeleka mahakamani itakuwa vichekesho.
 
........... Gender Sensitiv hapa hatutetei ila tunajiuliza wanadiscuss nini wakati kesi yenyewe bado iko jikoni? Watasema Jerry anaonewa kwa kuwa anafichua maovu, what if baadaye ikigundulika ana hatia? Wangesubiri kwanza hatma ya kesi na ikigundulika kuwa kahujumiwa basi wana haki ya kulisema na kukemea police.

Nimesema kwamba vyombo vyetu vya dola sio vya kuaminika hata kidogo.Hivyo kuwaachia wao inatia shaka bota tu kuwa pre empty kwenye mihimli mingine ya nchi kama vile Bunge.
 
Haya kale karisiti ka ile pingu kamepatikana na wananchi mnakaribishwa kujipatia pingu zenu kwa Tshs 25,000/= tu.Kova leta sinema nyingine maana wewe na cheo chako hata hujui sheria za nchi sijui cheo hiki ulukipataje.Kama kuna fisadi alikutuma umnyamazishe Jerry Muro amechemsha na wewe unadhlilsha cheo hicho unastahili kuwa mkuu wa mgambo kule Manyoni.Nenda shule angalau ujuejue sheria acha longolongo ulizozoea kule Mbeya.
 
Aleluyah!

Ni Imani yangu kuwa kwa mapenzi yake Mungu wetu Muumba sote tuanendelea vema. Nikaona ni vema nami lau kwa mstari mmoja nami nichangie swala hili ambalo kwa hakika limegusa mioyo ya wapenda maendeleo na haki katika nhi yetu ya Tanzania.

Sina sababu yoyote ya kuhumu kati ya Polisi na JM, ninachotaka kuwaambia wapendwa tujipe muda na Mungu wetu aliye hai tunaye muomba usiku na mchana atayaweka haya wazi hadharani.
JM jipe moyo umeingia katika kumbwa na impact yake ni kumbwa lakini Mungu atakuinua na ushinde, huu ni mtihani wako wa kwanza. Polisi nawatakia kila la kheri muwezi kuupata ukweli halisi ulio nyuma ya JM kwa manufaa ya taifa letu. Nakemea kila mpango wa kuzimu na hila yoyote amaboyo imeandaliwa kuuficha ukweli katika Jina la Yesu Kristo wa nazareti! Mungu na awabariki sana!
 
Back
Top Bottom