TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

JAmani sasa wewe unaomba rushwa halafu unatumia nguvu (kumfunga pingu ili atoe rushwa si kutumia nguvu?) huo ni ujambazi sasa si kuomba rushwa . Nafikiri hii ni hadithi ili k


uhalalisha uwepo wa pingu ndani ya gari la Muro


Hercule Poirot
The man above can solve this mystery no one else can connect the dots

1) pingu kwenye kuomba rushwa,
2) miwani kusahauliwa kwenye gari polisi
3) kumshika kabla ya kupokea hela
4) suspect kutosema kama anazo au hana hizo hela alizoombwa
5) and lastly kutotolewa hela za mtego na PCCB aka TAKUKURU na au
polisi
 
tuwasikiliza Polisi kama wana kesi yenye ushahidi utakaoweza kusimama mahakamani; kama hawana na wameboronga wawe tayari kuomba msamaha.

I agree with you. Ila ningependa kuona kwamba wachangiaje waache emotions na ku-focus kwenye issue. Pamoja na kwamba Muro ameonekana kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa tusifikiri kwamba hawezi kupokea rushwa, la hasha. Vita dhidi ya rushwa ni very complicated hasa ukizingatia baadhi ya watumishi wa vyombo vinavyosimamia maadili kama polisi, media, mahakama, nk wanajulikana wazi kuwa wanakiuka maadili ya kazi zao kwa kudai na kupokea rushwa.
Ukiachilia mbali issue ya Jerry, sekta ya habari hasa ninaongelea waandishi hawaja-address issue ya rushwa ipasavyo ndani ya taaluma yao. Ni nadra kabisa kuona kuwa vyombo vya habari vinaongelea tatizo lililo ndani yao kwa nia ya kuwa mfano bora kwa jamii. Ninashukuru kuwa walau hapa JF tunaweza kuandika kwa ajili ya wachache waweze kusoma tatizo lililopo la rushwa ndani ya media ya Tanzania.
 
Hapa ndani kuna waandishi wa habari ..nendeni mkaisake habari hii mtuletee ikiwa complete hata mambo ya kutiana mashaka mala tuwaze hili mala lile

Please give us full and complete report on this issue
 
Na kuwa kuna watu wengine watajitokeza leo kutoa ushahidi jinsi jamaa alivyowatoa hela.

Vitha ni vitha Mura


Sawa Mura,

Kwa nini walingoja Geshi la Polisi limwekee mtengo mura? Siyo michezo ya kuigiza kweli? Jamaa ametengeneza maadui wengi kwa "kazi nzuri" aliyoifanya na ndiyo maana huko nyuma niliwahi kusema kuwa amejipa jina jipya lakini la hatari sana, 'ENEMY OF THE PEOPLE"!
 
"Muro alikuwa ameahidiana na mfanyabiashara mmoja kuwa angepewa Sh10 milioni kama hongo, lakini mfanyabiashara huyo alitoa taarifa polisi na ndio leo (jana) wamefanikiwa kumkamata. Walimkamata mara baada ya kupokea fedha hizo," alisema mtoa taarifa

....hii kitu is much confusing, wengine wanasema alitaka kupokea rushwa from mfanyakazi alitimuliwa kazi na Pinda huko Bagamoyo.....huyo hapo juu anasema ni mfanyabiashara.......???????which is which......?
 
Akifikishwa mahakamani leo au lini sijui ndipo tutafahamu nini kilijiri kwa uhakika. Vinginevyo waandishi wa habari za uchunguzi tulionao na hasa wale ambao wamekwisha jitengenezea majina ndio zao hizo. Nasikia hata wale wanaoonekana kwenye kipindi cha Jambo Tanzania wanalipa kitu kidogo kwa waandaaji na waongozaji wa kile kipindi! Tuna safari ndefu kwenye mapambano haya.
 
Mzee Mwanakijiji;

Kuna vitu havi TALLY hapo.

1. Pingu ya nini kwa mtu kama yeye??
2. Kama alipigiwa simu na kwenda eneo la tukio, Je alipokea hiyo hela?
3. Kwanini hela itoke polisi na sio TAKUKURU?
4. Wage alijuaje Jerry ana pingu kwenye gari lake?


Kuna dots zina miss kwenye hii movie..

FP

Mkuu kama ukimsoma vizuri MMM, unaweza kugundua kwamba Jery pengine alijiandaa na team yake pamoja na wanausalama kucover a compherensive thing. Hivyo kwenye gari lake pengine aliwabeba wana-"usalama" or sth. So pingu nk zaweza kuwepo.

Again kama upande mwingine tena yaani takukuru na wanausalama waliokuwa nao ambao walimkamata Jerry bila kujua yuko kazini, walifanya kazi yao sawa ndo mana wakamtia nguvuni.

Hii ni kama habari hizi ni sahii kadiri watoaji walivyotuletea...anyway time will tell.
 
kama kakamatwa na Polisi ni HUJUMA! KUMDHOOFISHA KIKAZI. It is a plot planned by the corrupt officers!
 
Duh hizi nyeti ni za kweli? Manake tusije anza kuchangia story za kusadikika au zile za kutumiana meseji katika simu!?
Hivi kuna mtu asiyeamini mwenzake humu? ni kweli tukio hili limetokea
 
Nilihisi tu some trouble is on his way na akiweza kupenya kwenye hili tope zito jina litakuwa limetingwa na tetemeko la ardhi, let's see what happens next.
 
taarifa nilizopata muda si mrefu mwandishi wa habari aliyejipatia umarufu kwa kufichua rushwa za trafiki naye amekamatwa kwa kuomba rushwa ya milioni 10

Ninachojiuliza zaidi ni kama huyu bwana alijidhatiti kwa mbinu za medani jinsi ya kukwepa mitego ya rushwa na mingine inayoweza hata kuhatarisha uhai wake. Kama sivyo, basi ni jambo la kushangaza sana. Huwezi kufanya kazi ya aina hiyo kirahisirahisi tu hasa katika nchi kama hii ambayo rushwa na ufisadi vimekuwa taasisi inayobebwa na watawala. You need to be really smart.

I'm inclined to believe the guy is innocent but, MAYBE just MAYBE, very naive!
 
Source: Daily News 01 Feb 2010:
POLICE in Dar es Salaam are holding a journalist with the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), Jerry Muro, on allegations of corruption involving millions of shillings.

The Dar es Salaam Special Police Zone Commander, Mr Suleiman Kova, confirmed the arrest of the TBC journalist, saying he allegedly solicited 10m/- bribe from former Bagamoyo District Council Accountant, Mr Michael Wage.

Mr Kova said Muro posed as an official with the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) and attempted to extort the money from Mr Wage.

Police told reporters at Central Police Station in Dar es Salaam that Muro was brandishing a pair of handcuffs when threatening to arrest Mr Wage in Bagamoyo.

The former district accountant reported the matter to police leading to Muro's arrest. Police found the pair of handcuffs and a pistol in his car during a search.
 
I've to do some work now - nimesoma weeee hii thread (for almost an hour) lakini sikupata chochote! Kila post inanukuu nukuu iliyonukuliwa!

Hei - mchana mwema
 
Kwenye gari lake alikuwa na Pistol na pingu. Na amethibitisha kuwa anamiliki pistol na pingu. Hapa inaonekana kuna kitu inapikwa na nadhani polisi wanataka kumnyamzisha au ili akiwa anasafiri atoe taarifa ili wawataarifu waokota rushwa wao wawe makini barabarani!!!!!!!!!
 
Hakika Muro ataweza kutumabia mwenyewe ile miwani na pingu zilikuwa za nani. Polisi ndio wenye pingu.Au unaweza kunuanua ya kwako Kariakoo?

Ndio maana wamemwachia maana wanajua wameboronga big time. Maigizo hayaachi kuwa maigizo hata ufanye nini.
 
Ninachofahamu, PCCB ndiyo wakamataji. Mtego unawekwa, mtu unapokea na muda mfupi jamaa wanakutokea na kukutia mbaroni. Haya hii tena inakuwaje, eti polisi mnamkamata Jerry kwa madai kuwa ameomba rushwa. Kwani ilitolewa? mbona hili halizungumzwi? Jana tunaijua...ALUTA KONTINUA. TBC fanyeni kazi tuko nyuma yenu.
 
Tshala, 1975, allanafricanboy, Askofu, Azikiwe, Bavuvi, Binti Sayuni, Brooklyn, Buchanan, Bwassa, Bweha mweupe, D5, Dina, Dogo Tundu, Drifter, drphone, FairPlayer, FDR.Jr, gkundi, hsbaky, JoJiPoJi, Kaitaba, KakaJambazi, Kimbweka, kisikichampingo, Konaball, Kwetunikwetu, Liz Senior, Magezi, Maverick, Mburahati, Mfamaji, Mfuatiliaji, Miwani, mkongojoli, monie2009, msaragambo, MwanajamiiOne, Mzawa Halisi, ndundu, Nonoo, Nyambala, nyaunyau, PJ, Pundamilia07, Sabasaba, safariwafungo, Shagihilu, Shedafa, Tristan, umbopa, Watu


Mpaka Kieleweke leo, lol
 
mapambano ndo yameanza, vita haikwepeki, na twendeni mstari wa mbele basi.
 
Back
Top Bottom