TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Jamani mi nafikiri hapa kuna maelezo zaidi yanatakiwa hapa.....maelezo ya Jerry Muro hayaeleweki....UPDATES please
 
Source: Daily News 01 Feb 2010:

Mr Kova said Muro posed as an official with the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) and attempted to extort the money from Mr Wage.

Police told reporters at Central Police Station in Dar es Salaam that Muro was brandishing a pair of handcuffs when threatening to arrest Mr Wage in Bagamoyo.

The former district accountant reported the matter to police leading to Muro's arrest. Police found the pair of handcuffs and a pistol in his car during a search


Huyo mshtaki naye wa ajabu sasa wewe ulitishiwa kuwa usipotoa rushwa utakamatwa na kufungwa kwa pingu ya Jerry- ukamatwe kwa kosa gani?-la kukataa kutoa rushwa au kuna tusilolijua hapa???

Rushwa iliyoombwa hapa ni kwa ajili ya nini? Bado haieleweki bana - mi ctaki
 
Jerry pingu unasema ni zako???? mwandishi wa habari au kuna kingine tusichokijua babangu?


naomba anaejua sheria za tz anifahamishe,mtu wa kawaida haruhusiwi kumiliki pingu,maana kuna baadhi ya nchi pingu,na hata nguo bandia za polisi sio kosa kuwa nazo.vilevile naamini sheria inaruhusu mtu binafsi kumiliki bastola.....hivyo kukutwa na bastola sio issue kama anaimiliki kihalalai,pingu sijui naomba mnifahamishe
 
Tatizo la Watanzania ni kwamba hatuna standard moja inapokuja kwenye uhalifu. Tunatetea/kupinga kulingana na mhusika ni nani.

Kama Muro amechukua rushwa inabidi ashughulikiwe sawa na raia mwingine yeyote bila kujali yeye huko nyuma kafanya nini.

Masaula ya kwamba kwanini polisi na si TAKUKURU naona ni kutafuta mchawi bure.

Muhimu ni kusubiri ukweli wote ujulikane.

Kilicho wazi ni kwamba kwa tanzania waandishi wa habari huwa wanachukua rushwa ili waandike habari nzuri au wamtetea mhusika.

Mkulima hakuna anayeleta double standards hapa ila tatizo liko kwenye hadithi yenyewe- haijakuwa na convincing power ya kutosha kumwingiza Jerry matatani hasa ukizingatia kuwa wakamataji wenyewe wametoka kuumizwa juzi juzi na Jerry -kidonda hata hakijapona- wangeipika vizuri hii hadithi huwenda tungeelewa zaidi.
 
Kama Jerry angeomba rushwa si angewekewa mtego na PCCCB? Lakini ikumbukwe kuwa wanasema yeye ameomba rushwa akijitambulisha kuwa in officer wa PCCCB, hii hapa imekaaje? Yamkini kuna kitu hapa, either ka ukweli fulani au malipuano.
http://issamichuzi.blogspot.com/2010/01/jerry-muro-akiwa-kituo-cha-kati-cha.html.
Ninahisi kuwa Jerry anaweza pia kuwa intelligence agency na polisi hawafahamu. Maana yuko equipped kuliko nilivyomdhania.........Let give it time, we will soon learn something from here.

Kwa ni mtambuavyo Mr. Muro siwezi kumdhani kabisa kwamba anaweza kujipachika kesi ya jinsi hii..!! Ukisikia mtu anajitangaza yeye ni afisa Usalama au PCCCB na kadhalika jua dhahiri kwamba mtu huyo ana hitilafu kichwani kwani hata sheria za kazi zao hazi waruhusu kujitangaza. Na hili silitegemei kutokea kwa Mr kwa kipindi cha sasa.
 
kwani bado kamanda wa kanda maalumu yule mpenda magazeti na TV hajatoa taarifa maana aliahidi leo mchana huu lazima aseme kwa kina nini kilijiri kwenye sakata zima.
 
naomba anaejua sheria za tz anifahamishe,mtu wa kawaida haruhusiwi kumiliki pingu,maana kuna baadhi ya nchi pingu,na hata nguo bandia za polisi sio kosa kuwa nazo.vilevile naamini sheria inaruhusu mtu binafsi kumiliki bastola.....hivyo kukutwa na bastola sio issue kama anaimiliki kihalalai,pingu sijui naomba mnifahamishe

Nchi yetu ina mambo mengi sana kabisa, hasa unapoingia kwenye anga za hawa wa heshimiwa, Wana mbinu nyingi kabisa ambazo wanaweza kuzitumia ili kukushusha chini na kukushikisha adabu kwa lugha wanayo tumia wao.

Polis wa Kitanzania wakiamua kukushikisha hata wizi wa kuku wanaweza, Sipendi kuliongelea sana hili,bali kwa wale walio kwisha pitia matatizo ya jinsi hii watakueleza, JARIBU KUFUATILIA KISHA CHA KIFO CHA KOMBE KULE MAILI SITA MOSHI.!!!

 
[/COLOR]

Mchezo ndipo ulipoanzia hapa- mpigie simu jifanye kuna habari- akija tu we tuachie kazi. Jerry unayo namba ya simu uliyopigiwa -atafutwe huyo mpigaji wa simu then tujue kama ni kweli kulikuwa na habari au ndo ulikuwa unaambiwa 'baby come?'

[/COLOR]

Nauliza tena hapa Jerry angesaidia namna gani?-Kumrudisha kazini au?

[/COLOR]
Kwa nini akimbilie kutoa ushahidi wa vitu alivyovikuta kwenye gari mapema hivi? Je Jerry wakati unatoka nyumbani kwako uliviona vidhibiti hivi garini kwako?



Jerry wakati wa kukamatwa hakukuwa na purukushani yoyote iliyowapa nafasi police kupossess ufunguo wako wa gari? Ulipopatikana mara ya pili ulipatikanajepatikanaje? sio kuwa waliuchukua na kwenda kuplace hivyo vidhibiti?

ah geshi ra borisi mnabaka haki yangu ya kuwaamini, mi ctaki kabisa bana


Wakati mwingine najaribu kuifananisha Tanzania na Urusi au labda niseme pamoja na nchi yetu kuwa ya utawala wa Kidemokrasia bado asilimia KUBWA imetawaliwa na Nguvu za kijeshi ukianzia kwa Mgambo,Magereza,Polis na Hata Jeshi.

Hawa watu bwana wacha kabisa kabisa, hata kama wangeamua kutumia funguo zao zingine bado wangeweza kuingia ndani ya hiyo gari bila hata Mr Muro kujua na kuweka hiyo pingu na fedha pia bila tatizo lolote, Kesi za jinsi hii nilisha ziona nyingi sana.
 
Nchi yetu ina mambo mengi sana kabisa, hasa unapoingia kwenye anga za hawa wa heshimiwa, Wana mbinu nyingi kabisa ambazo wanaweza kuzitumia ili kukushusha chini na kukushikisha adabu kwa lugha wanayo tumia wao.

Polis wa Kitanzania wakiamua kukushikisha hata wizi wa kuku wanaweza, Sipendi kuliongelea sana hili,bali kwa wale walio kwisha pitia matatizo ya jinsi hii watakueleza, JARIBU KUFUATILIA KISHA CHA KIFO CHA KOMBE KULE MAILI SITA MOSHI.!!!

Tobaa!!! Yarabi, tumefikia kulinganisha kifo cha Kombe na soo la Muro!!! Sasa tunaenda mbali kwa kutaka kumtetea mwandishi. Jamani suala la Kombe kwa sasa sio siri tena lakini kwa vyovyote haliwezi kulinganishwa na suala la Muro. Jamani, huyu ni mwandishi wa habari ambaye amekuwa celebrity kwa kiasi fulani kwa sababu ya kazi yake ITV. Kombe alikuwa nafasi nyeti sana na ni kwa sababu hiyo aliuawa (eti alifananishwa na mwizi wa magari!!)
 
Hii inaweza kuwa skandeli nyingine kwa jeshi la polisi na kuwafanya kupukutika zaidi kama haki ingefuatwa. Mtiririko mzima wa tukio hili unaonyesha misuko ambayo haikukamilika iliyofanywa kama kwa maksudi vile (mtizamo wangu).

Nini hatma yake? Polisi ikikosa mashiko katika suala hili, IGP ataliambia nini taifa? Yuko tayari kuendelea kuwawajibisha vijana wake kama waliotimuliwa kwa kuonekana wakipokea rushwa?
 
Hapa kuna nini? Mbona habari hazitiririki jamvini kama tulivyozoea???

Wakuu Kova si alisema ataitisha press conference saa sita mchana?? Bado kimya???

Maswali ni mengi kuliko majibu.....
 
SAKATA la Jerry Muro limetolewa ufafanuzi na kamanda Kova muda mfupi uliopita kuwa faili lake limepelekwa kwa mwanasheria Mkuu kwa uchunguzi zaidi ili kuona kama anastahili kupelekwa mahakamani au la. Kwa sasa Jerry, ambaye yuko nje kwa dhamana, anatakiwa kutulia wala kutoongea chochote kwa faida yake. Imeonekana mlungula hakuchukua ila alikuwa anaandaliwa mazingira ya kushikishwa rushwa...

i1575_1265018018jerry33.jpg


Source: gonga hapa
 
SAKATA la Jerry Muro limetolewa ufafanuzi na kamanda Kova muda mfupi uliopita kuwa faili lake limepelekwa kwa mwanasheria Mkuu kwa uchunguzi zaidi ili kuona kama anastahili kupelekwa mahakamani au la. Kwa sasa Jerry, ambaye yuko nje kwa dhamana, anatakiwa kutulia wala kutoongea chochote kwa faida yake. Imeonekana mlungula hakuchukua ila alikuwa anaandaliwa mazingira ya kushikishwa rushwa...

Source: gonga hapa
Jerry naamini kama mwandishi makini wa kizazi kipya atakua humu akisoma na kutafakari ushauri huu anaopewa na Watanzania wenzake, ushauri murua Pape.
 
Pole Jerry kwa yaliyokukuta. Kama ni ya kweli haya unapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kama ni ya uongo hao waliokuzushia wapelekwe kwenye vyombo vya sheria pia.
Lakini kuna kitu kinanitatanisha hapa ukijaribu kusoma kwenye vyanzo vya habari kuna vitu vinajicontradict hebu angalia hapa
"Habari zaidi zinasema kuwa Muro, ambaye alishinda tuzo ya Mwanahabari Bora wa mwaka 2009 kutokana na habari yake ya rushwa inayofanywa na askari wa usalama barabarani, alikumbwa na mkasa huo jana majira ya saa 6:00 jijini Dar es Salaam.
Alikamatwa wakati akiwa hoteli ya Sea Cliff.
Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Muro alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na polisi mara baada ya kuarifiwa na mfanyabiashara mmoja, ambaye jina halijawekwa bayana na polisi, kuwa mwandishi huyo amedai rushwa ya Sh10 milioni.
Habari zinadai kuwa mwandishi huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha hizo.
"Muro alikuwa ameahidiana na mfanyabiashara mmoja kuwa angepewa Sh10 milioni kama hongo, lakini mfanyabiashara huyo alitoa taarifa polisi na ndio leo (jana) wamefanikiwa kumkamata. Walimkamata mara baada ya kupokea fedha hizo," alisema mtoa taarifa".
source Mwananchi news paper

"Jerry alimuomba rushwa mhasibu huyo ili habari ile isirushwe hewani kwenye kipindi chake cha ‘Usiku wa Habari’, kitendo kilichomfanya awape taarifa maofisa wa TAKUKURU kuhusiana na suala hilo,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, baada ya mhasibu huyo kutoa taarifa TAKUKURU na kuweka mtego, mhasibu huyo na Muro walikubaliana kukutana katika Hoteli ya City Garden iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam ili achukue pesa hizo.
Wakiwa katika hoteli hiyo ndipo maofisa wa TAKUKURU walipofika na kumtia mbaroni mtangazaji huyo majira ya saa nne asubuhi na kumpekea Kituo Kikuu cha Polisi ambako alihojiwa kabla ya kuachiwa huru jana jioni". source: Tanzania Daima news paper.

Tuamini source ipi ya habari kati ya hizo mbili ? Waandishi wa habari wa Tanzania kuweni makini wakati wa kutoa kazi zenu. Kumbukeni mnawapotosha watu kwa kutoa habari zenye utata
 
SAKATA la Jerry Muro limetolewa ufafanuzi na kamanda Kova muda mfupi uliopita kuwa faili lake limepelekwa kwa mwanasheria Mkuu kwa uchunguzi zaidi ili kuona kama anastahili kupelekwa mahakamani au la. Kwa sasa Jerry, ambaye yuko nje kwa dhamana, anatakiwa kutulia wala kutoongea chochote kwa faida yake. Imeonekana mlungula hakuchukua ila alikuwa anaandaliwa mazingira ya kushikishwa rushwa...

Source: gonga hapa
Inategemea hilo faili limeandikwa tuhuma gani na kivipi.
 
Mtu mwenye akili zake akijaribu "kuunganisha doti" kwa kweli mambo yako ndivyo-sivyo. Inaonekana polisi wametumia hasira kumlipiza kisasi huyu Bwana mdogo na this is a pre-mature move. Wangesubiri kidogo. Muro is one of the most famous fellas in the (former) republic of tanganyika at the moment. Mahakama yeyote itachukulia kwa makini sana tuhuma dhidi yake kwani kwa nafasi yake he is stepping on the toes of big potatoes. Ni lazima asingiziwe mengi. jaji makini ataona hizi doti haziunganishiki na kumuachia kijana achape kazi. Those are my two cents!
 
Kula nyuzi hapa:

i1583_12650252423.jpg


[ame]http://www.youtube.com/watch?v=cl2Ow-Goxvc&feature=player_embedded[/ame]

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=pbTK9XVL84o&feature=player_embedded[/ame]

Kova kasema kumbe Jerry alikuwa anamiliki silaha bila hata kuwa na risiti ya kununulia....

Huyu jamaa sijui kama atatoka salama kweli...

Source: hapa
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=cl2Ow-Goxvc[/ame]
haya sheshe ndo hilo,na jamaa kakutwa na pingu na bastola risiti hana,watu wengine unawaona kama watiifu kumbe ni majambazi na waporaji,sasa hii unaweza sema polisi walimbambikia lakini inaonekana jamaa nae kabugi mahali,naona polisi wameamua tu kumshtua kama anajisahau kama na yéye mchafu vilevile.
 
Back
Top Bottom